The Political Economy of the investment climate in Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The Political Economy of the investment climate in Tanzania

Discussion in 'Great Thinkers' started by mwanza_kwetu, Jun 29, 2011.

 1. m

  mwanza_kwetu JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 684
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wakuu,

  Isomeni hii nondo iliyo attached

  [​IMG]
   

  Attached Files:

 2. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2011
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
 3. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  thanks itanisaidia kiasi chake ila ile yenyewe haipatikani, raia mwema walisema wana copy, cant we get that document kweli mafisadi wameificha haippatikani
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,548
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Slaa afufua upya ufisadi
  Mwandishi Wetu
  29 Jun 2011
  Toleo na 192
  Raia Mwema


  [​IMG]
  • Asema hadanganyiki na kesi za dagaa
  • Wazungu watoa ripoti kwa donors inayotaja ufisadi
  • Wawataja Lowassa na Rostam
  • Rostam aitwa mtengeneza viongozi – kings maker
  WAKATI wafadhili wakikabidhiwa ripoti inayoonyesha bado Tanzania kuna ufisadi, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ameibuka na kusema hatorudi nyuma katika mapambano dhidi ya rushwa kutokana na serikali kuwaogopa wala rushwa na mafisadi wakubwa.

  Akizungumza katika mahojiano maalumu na Raia Mwema, jana, Jumanne, Dk. Slaa amesema wakati wote ambao yeye na wenzake katika Upinzani wakipigania hatua kuchukuliwa dhidi ya mafisadi na wala rushwa wakubwa, serikali imekuwa na kigugumizi katika kuchukua hatua; huku ikitumia mbinu za kuwafunga midomo.

  Akitoa mfano wa kesi mbalimbali zikiwamo za wizi katika akaunti ya madeni ya nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (EPA) kupitia kampuni ya Kagoda Agricultural Limited na kashfa ya rushwa katika ununuzi wa rada ya kijeshi, Dk. Slaa amesema serikali inawalinda wahusika wakuu.

  "Kampuni kama Kagoda wahusika wanajulikana lakini hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi ya wahusika. Hii si dalili nzuri maana inaashiria kwamba wakubwa wanahusika ama wanawaogopa wahusika. Hatudanganyiki na hatunyamazishwi, tutaendelea kusema na kutaka hatua zichukuliwe," anasema na kuendelea;

  "Kashfa ya rada ni aibu kusikia serikali inadai fedha za rada wakati ilikuwa na kigugumizi wakati Uingereza wakichunguza wahusika wa rada na walishindwa kutoa ushirikiano kwa wachunguzi, lakini sasa eti wanasikia kuna fedha ndio wanazitaka. Kwa nini walikataa kushughulikia wahusika kwa sheria zetu za Tanzania na kuachia Waingereza kila kitu?" alihoji Dk. Slaa.

  Alitoa mfano wa kashfa ya Meremeta inayohusiana na kampuni iliyohusishwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ); huku kukiwa na wanasiasa nyuma ya kampuni husika akisema fedha zilizopotea katika kashfa hiyo zingeweza kutumika kusomesha walimu 19,000.
  Dk. Slaa amesema sasa ana muda zaidi wa kupambana kwa kufanya utafiti wa kina na kwamba atahakikisha wananchi wote wanaelimika na kufahamu haki zao. Amesema amekua akifanya ziara vijijini kukutana na wananchi mara kwa mara na kuzungumza nao juu ya mustakabali wao.
  Wazungu wawasilisha ripoti kwa donors
  Wakati huo huo ripoti iliyoandaliwa na waandishi wawili wa Kizungu, Brian Cooksey na Tim Kelsall, yenye jina "The political economy of the investment climate in Tanzania", imekabidhiwa kwa wafadhili wakuu wa Tanzania.
  Baadhi ya mambo muhimu kuhusu uchumi wa Tanzania yameanishwa katika ripoti hiyo, ambayo Raia Mwema lina nakala yake, ikiwa ni pamoja na mifano hai ya rushwa kubwa kubwa inayogusa wanasiasa.
  Waandishi hao waliandaa ripoti hiyo kwa niaba ya taasisi ya kimataifa ya Africa Power and Politics Programme (APPP) ya Uingereza. Uandaaji wa ripoti hiyo umefadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID) na Shirika la Misaada la Ireland (Irish Aid); licha ya kuwa taasisi hizo zimejipembua kwenye utangulizi wa ripoti hiyo kwamba si lazima mawazo ya waandishi hao yafanane na ya kwao.

  Katika ripoti hiyo, waandishi hao wameonyesha wazi kwamba bado Tanzania inaathiriwa na mabadiliko ya kisiasa na ufisadi unaowahusisha wanasiasa pamoja na kuwa imekuwa ikipokea wawekezaji wengi kutoka nje katika kipindi cha miaka kumi na tano iliyopita.

  Lowassa , Rostam watajwa kwenye ripoti
  Ripoti hiyo imewataja kwa majina wanasiasa ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao chama hicho kimewataja kuwa chanzo cha kushuka kwa umaarufu wake mbele ya umma kikielezea kuhusishwa kwao na kashfa mbalimbali, baadhi zikiwa zinatajwa hadharani kwa mara ya kwanza.
  Wanamtaja Waziri Mkuu, aliyejiuzulu, Edward Lowassa, wakianzia na wakati akiwa Waziri wa Ardhi na baadaye Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo, wakimuelezea kuwa alitumia madaraka kwa maslahi binafsi. Wameorodhesha mifano.

  Ripoti hiyo yenye kurasa 96 imemtaja pia Mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz, wakimuelezea kuwa mmoja wa wanasiasa walioonyesha umahiri mkubwa katika kutengeneza viongozi na kupewa jina la ‘king-maker' akihusishwa kikamilifu katika kampeni za urais wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete hata kabla ya kuingia rasmi katika Kamati Kuu ya chama hicho akiwa Mweka Hazina nafasi aliyodumu nayo hadi mwaka 2007.

  Katika ripoti hiyo, Rostam anatajwa kuhusishwa kwake na sakata la Richmond lililomgharibu marafiki zake, Lowassa, Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha, ambao kwa pamoja walijiuzulu nafasi zao za uwaziri mkuu (Lowassa) na Wizara za Nishati (Karamagi) na Madini na Afrika Mashariki (Dk.Msabaha).
  Ripoti hiyo, ambayo imetolewa Juni 2011, imetolewa katika kipindi ambacho nchi wahisani zimeonyesha kutoridhishwa na hatua zinazochukuliwa dhidi ya watuhumiwa wakuu wa ufisadi pamoja na kuwapo kesi kadhaa za rushwa zilizofikishwa mahakamani na nyingine kuwa katika hatua za upelelezi.

  Tayari Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imekuwa katika wakati mgumu kukabiliana na changamoto hizo, huku kukiwa na kampeni za kisiasa za kuzima hatua kadhaa zinazofanywa na taasisi hiyo ambayo kwa sasa imepanua matawi yake nchi nzima.

  Vyanzo vya habari mjini Dodoma vimeeleza kwamba watuhumiwa wakuu wa ufisadi wamemwaga mamilioni ya fedha kuendesha kampeni za kuzuia uchunguzi dhidi yao ikiwa ni pamoja na kuwatisha watendaji wa TAKUKURU akiwamo Mkurugenzi wake Mkuu, Dk. Edward Hosea, wakitaka ang'olewe katika nafasi yake.

  "Baada ya kuona kwamba kuna majalada yameanza kukamilika, baadhi ya watuhumiwa wanaendesha kampeni za kutaka Hosea ang'olewe ili kesi hizo zisimame na wao wapate kujipanga upya. Inabidi wabunge wetu wawe macho na watuhumiwa hao ambao wamekwishafikia Dodoma kuendesha kampeni hizo wakishirikiana na wenzao walioko huko," anaeleza mtendaji mmoja serikalini.
   
 5. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Kagoda, richmond,.....hata watu walio nje ya Tz wanayajua haya vizuri tu. Lakini Mkama amesema wale mafisadi ni rafiki zake wa karibu, japo atajitahidi eti kuwachukulia hatua!
   
 6. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nafikiri tutaweza kuidownload
  s sasa thanks ngoja nipande mlimani nipate kuisoma. Bubu umepotea sana mkuu karibu tena
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,548
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Ahsante Mkuu nimeshakaribia..labda tunapishana mitaa tu Mkuu maana JF sasa imekuwa kubwa mno ila nipo sana tu.
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,307
  Trophy Points: 280
  Siku zote naingana na Dr. Slaa na Chadema kwenye single hii ya "Vita dhidi ya Ufisadi" ila kwa sasa lazima Chadema wajikite kwenye kutafuta single hit nyingine itakayo hit top of the charts za siasa mpaka 2015 na kuisambaza single hiyo mpya mpaka ground zero kwenye level ya common man.

  Nahofia CCM kung'amua single hit ya "Vita Dhidi ya Ufisadi" ambayo Chadema wanaitumia kama mtaji wake kwa kuwekeza mtaji mkubwa kwenye single hit moja, hivyo kuamua kujivua gamba kiukweli kwa kuwatosa mafisadi na kuwafikisha mahakamani kabla ya 2015!.

  Politics jamami its a dirty game, kama ni kweli ni ufisadi ndio uliopelekea CCM kupata kipigo ilichokipata 2010, then kuna uwezekano CCM ikawa tayari kufanya lolote legal/illegal kuhakikisha kipigo kile hakijirudii.
   
 9. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 643
  Trophy Points: 280
 10. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  PJ, CCM wakijifanya wanavua magamba kikweli kweli ndio watakuwa wamejikaanga kwa mafuta yao wenyewe! Magamba yaliyovuliwa yataamua kumwaga mboga na hapo ngoma itakuwa imeanza upyaaa! Alternatively, CCM wataamua kukomaa na magamba yao ambapo kitaendelea kuporomoka kwa kasi hadi ICU! Kwa vyovyote vile, CCM ina hali mbaya sana!
   
 11. T

  Technology JF-Expert Member

  #11
  Jul 1, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 733
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  Dr Slaa ile habari kwamba unakwepa kodi TRA ulishaijibu ??? what did you say/admit?
   
 12. h

  hans79 JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  sheria z wazi kwa akwepae kodi,tra huwa hawatangaz kuwa mkwepaj amelipa kod ila kama tongotongo zinakubana nenda tra utapata ulohitaj,zaid ya ubeya huna hoja.zungumzia matatizo utawala tz yanayoleta umaskin sababu utendaj u dun serikalin hilo nalo hulion mchumia tumbo!
   
 13. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #13
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kama posho zinakatwa kodi TRA waanzie kwa Wabunge pale Dodoma!
   
 14. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #14
  Jul 1, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu nianze kwa kusema ninawaunga mkono CDM kwa asilimia zote. Upinzani ni muhimu pale chama tawala kinashindwa kutatua matatizo yaliyopo.

  Sasa basi, kama CCM wakijivua gamba ki-ukweli na wakashughulikia kero mbalimbali zilizopo kisawasawa, basi na waendelee kutawala. Kwa maana nyingine, CDM hawana haja ya kutafuta single wala nini, tuendelee kupigia kelele matatizo sugu yaliyopo maana ikiundwa single mpya inamaana ufisadi umeisha?

  Tuko pamoja
   
 15. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #15
  Jul 1, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Mkuu Pasco, the good thing about hii single ya ufisadi ni kwamba in full context JK ni muhusika tena on the top of the list. Sasa hata ikichezeshwa kwa namna unayosema kitachofuata ni yeye kuumbuliwa and the guy is just neva ready on this . Otherwise ungewaona Kagoda mahakamani siku nyingiiiiii hata kwa kudanganyishia tu. Infact inasikitisha maana hela inayopotea kwa ufisadi kwa mwaka ingeweza kutimiza ile dream ya kuunganisha makao makuu zote za mikoa kwa lami in say 3 years.

  Hii single of course ni kama vile zilizoimbwa na Jim Reeves, Bob Marley na MJ hazichuji ati.
   
 16. M

  Mzee Madoshi Senior Member

  #16
  Jul 1, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  [FONT=&quot]Click on the link provided in the Raiamwema online article titled 'Slaa afufua upya ufisadi', you will be able to read and print this report[/FONT]
   
 17. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #17
  Jul 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  I updated the 1st post, sikujua kama hii haikuwekwa JF last week.
   
 18. m

  mwanza_kwetu JF-Expert Member

  #18
  Jul 1, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 684
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Done; Thanks very much wazee karibuni muone mambo hizi ndizo habari achaneni na akina MS/Magamba/et al. Tusome report tuwe na hoja
   
 19. m

  mwanza_kwetu JF-Expert Member

  #19
  Jul 1, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 684
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Thanks Invisible; Pls these are the documents elites reads; once you have one le us get update will help shape our knowledge further kuliko kukaa na hoja zisizo na mashiko. Invisible you have make my day and this firday karibu kapripoint kupata nyama choma nikperuzi taratibu report hii
   
 20. popiexo

  popiexo JF-Expert Member

  #20
  Jul 6, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 743
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tunapoelekea kusheherekea miaka miaka 50 ya uhuru wa Tanzania, nimeipata report hii ambayo nimetumiwa na mmoja wa jamaa zangu. Ni nzuri inaweza kukupa historical perspective ya political economy ya kanchi ketu. Ni kareport karefufu kidogo na kanacover picha nzima ya kwanini Tanzania iko hapa sasa:
  - It shed light on the path our nation took since independence
  - It calls a spade a spade (as it mentions corrupt leaders by names, etc)
  - It's written by a foreigner who has nothing to loose (I wonder if a Tanzanian living in Tz would do such a report)
  - It is a technical report written in layman language (anybody can read and understand the content)
  - It's well researched with a lot of undeniable facts
  - It's very current ( releeased June 2011)
  - etc
   

  Attached Files:

Loading...