The People's Bank of Zanzibar mjitathmini kitengo chenu cha usalama

LICHADI

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
4,145
11,191
Juzi nilikuwa hapo tawi la kariakoo shimoni kufuatilia fedha, nilichokiona mnatakiwa mbadilike mara moja kwenye masuala kiusalama.

Ni hivi, ukiingia kwenye hilo tawi, hakuna katazo lolote la matumizi ya simu wateja wakiwa ndani yani watu wanajiachia kwa ku-chat wanavyotaka, mpaka kupokea simu watu wanapokea na kupiga yani kama watu wapo nyumbani vile.

Kuwaacha watu watumie simu ndani ya benki ni hatari kwa wateja wenu, mnahatarisha usalama wao hasa kwa wanaotoa fedha nyingi, kuna watu wengine sio wema wanaweza kuchoresha wateja wanaotoa fedha nyingi kwa majambazi mwishowe wakavamiwa na kuibiwa.

Igeni mfano wa benki nyingine zote ni marufuku mtu yeyote kutumia simu akiwa ndani ya benki, kwa ajili ya usalama.

Mtu akiporwa mamilioni yake nnje huko akirudi humuwezi kumuelewa, eneo lenyewe ni Kariakoo.
 
Yakhe sie hatuna shida labda Nyie wabara.

Ukifika hapa wewe bonyeza kizenji hiyo simu yako yaheeeee ulongeee weee Hadi uchoke mwenyewe
 
Sheikh wangu hapana kuogopa. Hizi benki zimeshaombewa kwa dua hivyo usiwe na woga kuwa mtulivu, usalama ni mkubwa
 
Hilo la kukataza matumizi ya simu ndani ya Bank wala halisaidii kwenye kuzuia uhalifu wa kupanga(organised crime). Mipango ya uhalifu haipangwi hapo bank bali nje ya hapo

Unashangaa kukatazwa kutumia simu na ufanisi wa mabenk yetu upo chini sana. Waweza tumia hata saa mbili ukiwa ndani ya bank hujapata huduma na muda wote huo usitumie simu!!! Eti ukitaka kuongea utoke nje!!! Sasa hapo unakua umezuia nini? Sana sana unakua umesaidia camera zisipate footage ya anayetumia simu
 
Back
Top Bottom