The Pentagon (BCBG)

Midnight

JF-Expert Member
Apr 24, 2021
229
675
Ni saa saba na nusu sasa, wakati hivi leo nyie mmelala sisi bado hatujafikilia hata kurudi nyumbani kujificha . Tafadhali kama mlisema sheria ya kufunga ma-bar mida hii ipo hai chonde chonde nawaomba makamanda wa mama mje mtufulushe huku, maana tunakamuliwa sana, ni bora pulukushani na maafande kuliko hawa viumbe aliowashinda baba muumba na kijana wake Adam.

Tuwiane radhi kwanza, maana mara nyingi kutokana na haya mavilevi yetu na maisha ya ma-corruption corruption inafika wakati tunashindwa kusalimiana. Nawasalimu katika jina la jumuhuri, wenzangu hapa meza ya jirani wanaitikiaga bière ziendelee.. sasa ni mwendo wa kuviziana round azungushe nani!!? Na kwa hali ilivyo sasa naskia ma-bar yanafurika haswaa..... ni kama vimlijaa vimeshaanza kutililisha fedha jamuhurini, ila ngoja tusubili tuone.

Ukweli ni kwamba mara nyingi nyakati za usiku hasa nikiwa maeneo yangu pendwa poteza mawazo huwa napata wasaa kidogo KUANDIKA chochote hapa jamvini. Na huwa mara nyingi najitahidi walau ifike usiku sana hivi ndipo nianze kuandika chochote ninachojisikia kuwashirikisha ninyi jamaa zangu tusiojuana, sijui ndugu gani sisi¿ Sasa leo kidogo sina la maana saaana ila nataka niwagusie kidogo maana hapa nilipo nimeluka mabolingo sio ya kigogo. Ohhh sorry ni kitoto na sio kigogo, DJ chokambaya na bia za offer katulusha sana leo, ulikuwa ni mwendo wa bolingo tu hapa, kiutani utani nimejikuta nimeselebuka Albamu nzima ya Wenge musica BCBG wenyewe kuanzia ngoma ya kwanza hadi mwisho, leo nimekumbuka mbali sana, unakumbuka jinsi Wenge musica na Albamu yao ya Pentagon katika nyingo yao moja wakiwa jijini Paris n'a jezi za PSG Paris Saint-Germain kipindi hicho wamechukua ubingwa club bingwa ulaya mwaka 1996 kuelekea 97 hivi, enzi hizo hadi ya miaka ya 2000 na kuendelea hivi mliokuwepo Tanzania mnasema ukipanda basi la mkoa mnakula bolingo mwanzo mwisho na sio nowdays mnaangalizwa na kusikilizishwa bongo hood flavors.
Hawa jamaa wanatisha aisee maana wamemtoa machozi njemba yangu moja hapa na ile nyimbo yao ya No comment schengen, sasa sijui ni pombe au utamu wa nyimbo au analia na hawala na hasala za fedha za umma tulizo zichoma hapa kuanzia jioni....???
Yaani leo pesa yangu haijaenda bure kabisa maana kama jasho limetutoka kisawasawa na kilingala tumekiimba ki pombe pombe hivyo hivyo...

Yote kwa yote nipende kuwatia moyo tu ndugu zangu wanachama wenzangu wakujitapikia wenyewe bila kuumwa malaria wala ugonjwa wowote zaidi ya kuzidiwa na maji ya dhahabu ya kuwa milija iliyoziba imeanza kuachama na sisi waumiza viungo vyetu vya ndani tusihofu maana muda wa ukombozi na kulala kaunta umekaribia. Big up kwa DJ choka mbaya kwa hamasa yako na kutufanya tujiulize tutaanzaje kurudi makwetu usiku huu, huku tukitambua fika vijana waliojiarili wameshaingia mzigoni now.

Big up wahudumu wote mnaopenda mitelemko, na kutugonganisha na kuwasubili hadi nyakati hizi za lala Salama na bado mnatutoloka.

Bila kuwasahau member wenzangu wazungusha round kama mpo humu big up sana kwa kuwafanya wachaga waendelee kufanya uwekezaji kwenye ma-bar na kutufilisi taratibu taratibu.

Kuna watu niliwasahau hapa, japo nimeskia tetesi zenu mnapanga kutuachia jahazi la ulevi peke yetu, na wahakikishia kwa jina la kanisa la MC pilipili Siku moja mtarudi kundini wanakondoo waasi ninyi na Big up kubwa itawahusu wasaliti wakubwa wa kunyanyua uchumi wa nchi yetu kupitia kitengo cha pombe na anasa.

Kumladhi, kuna wengine wamesahaulika huku. Tafadhali ndugu zetu mamenager hawa mabaunsa na wapambe mnaowajaza kama walinzi wa magereza muwaambie watupe pumzi kidogo, vibomu vimezidi na tukiacha vitu vyetu mtuhifadhie maana kesho nayo siku tutarudi kuvichukua sio mnagawana kama mavazi ya mkombozi na Big up kubwa kwenu pia kwa kuwa madalali wa malaya na mapaka shume yasiyokuwa na mfugaji.
 
Hujaietendea haki pombe mkuu!! Yani umelewa halafu una uwezo wa kuandika maelezo marefu hivi? Kulewa gani huko? Acha kujipunja
Siku hizi tukiwa bar za mbali hatulewi sana. Si unajua tena vijana wapo kazini!!
 
Sasa ww unataka tuisifie timu moja tu, juve kaishapewa sifa zake anakaa kando, psg nae anakula zake.. Na kama si nzuri kwako, nzuri kwa wengine.
Hujanielewa mkuu what is was intending is
Juve was the champion during the said 96/97 season
Relax dude
 
Mambo ya biere bwana, bora hata hiyo PSG, hatiati ilikuwa niitaje utopolo FC
 
Back
Top Bottom