"The Party Must Serve the People":An Unpublished Speech By J. K. Nyerere | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"The Party Must Serve the People":An Unpublished Speech By J. K. Nyerere

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 19, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alitoa hotuba hii huko Kingston, Jamaika katika maadhimisho ya miaka 50 ya chama People's National Party (PNP) ambacho kilikuwa ndicho chama cha kwanza cha kisiasa nchini Jamaika. Hii ilikuwa ni June 4th, 1988.


  "In poor countries, honest political activists are not rewarded for their efforts by becoming materially wealthy. Indeed, they may suffer undeserved disrepute, abuse, and poverty. But, political activists, working together peacefully, can make a very important contribution to the well-being of the people, and to the freedom and development of their nation." - Julius Nyerere


  "A Basic Needs and Self-reliant Strategy is not an easy one to follow. The poor people are the best-organized people in any nation, but they are not the most vocal. An emphasis on their needs, and on the work of developing their capacity, will not be popular with the Middle Class, who in a poor country, may in any case not be living very well by developed country standards. It will be definitely unpopular among the wealthy and economically powerful in a nation, who are used to receiving first consideration from their governments. The policies aimed at implementing a ‘Basic Needs Strategy’ will, therefore, be mocked and distorted by people with influence; they may be made very difficult to implement. The party has to remain firm, and help its government!" - Julius Nyerere

  This is one of the most reflective speeches by Father of the Nation Mwl. J. K. Nyerere. Hotuba hii ni kama mwendelezo wa hotuba nyingine aliyoitoa mid 1960s huko Sudan ambayo ilikuwa na jina tofauti "The Party Must Speak for the People". Siwezi kushangaa basi kuwa hii ya mwaka 1988 katika fikra za Nyerere yumkini ilikuwa inaendeleza wazo hilo alilolitoa Sudan.

  Ni hotuba ambayo kiongozi wa chama chochote cha kisiasa anapaswa kuipitia kwani inadokeza misingi mbalimbali ya kiuongozi ambayo yaweza kufuatwa katika kuunda aidha chama kipya au kuboresha chama cha zamani.

  a. Kwa upande wa CCM je ni kwa kiasi gani chama hiki kinaendelea kuwatumikia wananchi?
  b. Kwa upande wa Upinzani ni kwa kiasi gani wamejipanga kuwa watumishi wa wananchi?
   

  Attached Files:

 2. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  a. Kwa upande wa CCM je ni kwa kiasi gani chama hiki kinaendelea kuwatumikia wananchi? hawa wameshaprovefailure kwa kuendekeza wafanyabiashara na kutoka kabisa kwenye misingi yao
  b. Kwa upande wa Upinzani ni kwa kiasi gani wamejipanga kuwa watumishi wa wananchi? sera na ahadi zinazotekelezeka tu . nia ya dhati ya wanasiasa wetu ndio inatia shaka sana ukombozi wa nchi hii.
   
 3. S

  Sheba JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 210
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji,

  Nakupongeza kwa post hii. Haya ndio mambo yanayostahili kujadiliwa humu kwenye Jamiiforums na sio kujadili watu. Nimeisoma hotuba hii vizuri. Hiki ndio tunachokikosa leo kwenye vyama vyetu vya siasa. Hata kwenye hotuba yake ya mwaka 1962 inayoitwa TANU na Raia, Mwalimu anasisitiza juu ya Chama cha siasa kujihusisha na shida za watu wake. Katika hotuba hiyo, amekemea tabia ya Viongozi kujisahau na kuanza kuwa busy kujishughulisha na Masuala ambayo hayana mahusiano na shida za watu wanaowazunguka. Mfano, Viongozi kujadili marupurupu na posho zao, hadhi na kinga zao nk.

  Vilevile nimewahi kusikia hotuba yake nyingine akifafanua kwa nini aliamua kutoa nguvu zaidi kwa Chama na si Serikali katika kile kilichokuja kujulikana kuwa ni "Chama kushika Hatamu". Katika hoja zake, Mwalimu alisema kuwa kwa asili yake Serikali ni chombo cha mabavu, hivyo siku zote ni combo kandamizi na ni rahisi sana kwa chombo hicho kulinda maslahi yake na watumishi wake zaidi kuliko maslahi ya wananchi. Hivyo, kikiachiwa dhamana ya kusimamia maslahi ya watu, maslahi ya watu wa chini na ya wananchi wengi yatakuwa mashakani. Badala yake, Chama ni chombo cha umma chenye uwakilishi na kilicho karibu na wananchi. Chama kina uwezo mkubwa wa kusikia maoni na maslahi ya watu walio wengi kwa kuwa msingi wa kazi za vyama ni "interest aggregation and interest articulation". CCM kupitia Azimio la Arusha lilitoa uongozi makini. Chama hutoa uongozi wakati Serikali hutawala.

  Tatizo tulilo nalo leo ni kupwaya kwa vyama katika kutoa uongozi. Serikali kwa maana ya dola(civil service) imeandelea kutawala kama inavyotegemewa. Kwa kuwa imekosa wasimamizi makini au uongozi makini, imekuwa ikijifanyia mambo yake kwa kuyumbishwa na wanasiasa ambao wamepotoka kimaadili. Matokeo yake ndio haya tunayoyashuhudia.
  M
  Swali kubwa la kujiuliza ni kuwa, je, tunaona uongozi katika Vyama vilivyoko sasa? Binafsi, SIONI.
   
 4. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mwanakijiji thanx kwa thread nzuri zenye mantiki na zinazoitaji tafakuru ya kina. Nyerere kweli was a great leader. Laiti serikali ya CCM ingemuezi kwa matendo hakika nchi ingejaa neema. Mawazo ya Mwl. Nyerere yamepuuzwa sana, nowdays Chama ndio kimekuwa Adui wa wananchi badala ya kuwa mkombozi wa wanyonge. Chama kimewasaliti waasisi wake na kimekuwa zigo kwa wanachama na wananchi. Hali kama hii inahitaji mabadiliko!
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Oct 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Sheba umetoa point nzuri sana ya suala la "chama kushika hatamu". Katika mawazo ya Nyerere chama kilikuwa ni cha 'watu' yaani yawananchi. Kwa hiyo kwa chama kushika "hatamu" aliamini kuwa ni nafasi ya wananchi kushika hatamu ya uongozi. Aliona mstari ulionyoka kutoka kile kinachosemwa kwenye Ibara ya 8 ya Katiba kuwa "madaraka ya kutawala yatatoka kwa wananchi" hadi kwenye "chama kushika hatamu" na "serikali kuongozwa na chama".

  Chama cha kisiasa kinapoacha kuwa chama cha watu (wananchi) kinaanza kuwa chama cha kikundi cha wanufaika wachache (an elite group) na hapa ndio huwa mwanzo wa maangamizi ya vyama vyote vikongwe. Ilitokea kwa chama cha Kaunda na cha Chiluba. Sata anajaribu kufuata hii kanuni ya chama kusikiliza wananchi na kutenda kwa ajili yao.

  Kwa mfano, katika nchi yetu CCM ingekuwa ni chama ambacho kweli kinasikiliza, na kinawakilisha mawazo ya wananchi serikalini kusingekuwa na madudu haya yote. Ni kwa sababu chama siyo tu kimepoteza mwelekeo bali pia kimepoteza ile clout (ujiko) iliokuwa nao; CCM imeacha kuzungumzia watu na imeacha kuwatumia watu na sasa inatumikia serikali. Fikiria kwa mfano, tukisema tuondoe ruzuku kwa vyama vya siasa ni chama gani kitaathirika zaidi?
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Bila kupoteza muda sana, hivi vikundi mbalimbali vinavyotumia 'brand name -ccm' haviko kutumikia wananchi, badala yake vinatumia wananchi na rasilimali zinazowazunguka wananchi kwa manufaa yao. Tukija kwa vyama vya upinzani, huko nyuma vyama vya upinzani vilishindwa kabisa kujipanga kutumikia wananchi kwa sababu kila juhudi waliyofanya (upinzani) ilivurugwa na ccm (wakati huo ccm wakiwa wamoja). Lakini sasa tunaanza kuona dalili za vyama vya upinzani kuanza kujipanga au/na kuongea mambo yanayowagusa 'poor people' kwa sababu ccm wamejikita zaidi kwenye 'civil war' na hivyo kukosa mwanya wa kumshughulikia jirani. Na hii ndio salama wa watanzania kwamba ccm watoboane macho kabisa kabisa, wawe vipofu na kama mungu anasikia sala za wanyonge basi awageuze viziwi pia ili wasisikie mipango ya kuwaokoa 'poor people'.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Oct 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Lakini vyama vyetu vya siasa vinagombania nini hasa?

  a. madaraka
  b. kuwatumikia wananchi
  c. Nafasi ya wao kutawala
  d. x?
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Collectively, naweza kusema chama chochote kinagombania nafasi ya 'kutawala'. Hivyo hata hivi vyama vya upinzani wanagombania hicho hicho. Likini ukiwa na mfumo mzuri wa 'checks & balances' basi kutawala kutaambata na kutumikia wananchi. And all you need ni kuwa na mtu mmoja tu pale juu (top person) ambaye ana nia ya kutumikia wananchi then everything else falls into place. Mfano, ccm siku zote wanataka kutawala, lakini Baba wa Taifa Mwl Nyerere alitaka kutumikia wananchi na kwa sababu alikuwa kwenye nafasi ya ushwawishi na usimamizi aliweza kufanya (walau kwa % fulani) kufanya ccm ionekane wako kuwatumikia wananchi. Kuondoka kwake kumefunua 'true colours' za ccm. Now, kwenye vyama vya upinzani the story inaweza kuwa similar kama unakuwa na kiongozi weak. Ndio maana ni muhimu sana kuangalia nia na uwezo wa kiongozi wa juu katika kusimamia na kushawishi direction ya kutawala/kutumikia wananchi.
   
 9. S

  Sheba JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 210
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni kuwa hata vyama vya upinzani navyo ni sehemu ya tatizo. Si kweli kuwa vinajihusisha na shida za watu. Ninachokiona Mimi ni kuwa vimeamua kuwa wajasiriamali wa shida za watu. Wanatumia shida za watu wetu kama mtaji wa kutafutia wapiga kura na kupandikiza chuki dhidi ya CCM( cheap political strategy).
   
 10. S

  Sheba JF-Expert Member

  #10
  Oct 19, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 210
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0


  Tatizo ni kuwa hata vyama vya upinzani navyo ni sehemu ya tatizo. Si kweli kuwa vinajihusisha na shida za watu. Ninachokiona Mimi ni kuwa vimeamua kuwa wajasiriamali wa shida za watu. Wanatumia shida za watu wetu kama mtaji wa kutafutia wapiga kura na kupandikiza chuki dhidi ya CCM( cheap political strategy).

  Tujiulize, mgogoro wa Halmashauri ya Arusha unahusika na maslahi gani ya wananchi? Je, kwa kususia vikao na kudhoofisha shughuli za Halmashauri za kuendeleza miundombinu na kutoa huduma za afya kunasaidiaje wananchi wa Arusha? Je, kutoshiriki kwa wajumbe wa upinzani kwenye vikao vya Halmashauri hakuwanyimi watendaji wa Halmashauri fursa ya kupata mwongozo katika utekekezaji wa majukumu Yao?

  Lengo langu hapa si kuuponda upinzani bali ni kuweka mizania sawa na kujenga hoja kuwa vyama vyetu vyote vya siasa vinatuangusha na vina ombwe la uongozi. Iko mifano michache michache inayoonyesha kuwa katika baadhi ya ngazi za madaraka na baadhi ya Viongozi wangali wanatekeleza wajibu wao vizuri. Mfano, Halmashauri ya Karatu pale imejitahidi kujishughulisha na shida za watu na hatimaye wananchi pale wameipa CHADEMA uongozi kwa kuwa imefanya ya vizuri katika ngazi ya Halmashauri kujishughulisha na shida zao. Hivi majuzi nilimuona Mhe.Mnyika akijishughulisha na wananchi wake, alishirikisha Viongozi wa kata zake na baadae kuambatana nao hadi DAWASCO kwenda kutafuta ufumbuzi wa tatizo la maji. Wako pia Wabunge wengi wa CCM ambao pia wanafanya hivyo na zipo ngazi nyingine za uongozi kwa CCM nao wanafanya hivyo.


  Katika kujumuisha, nachelea kusema kuwa kama alivyohoji Mwanakijiji, hata katika upinzani hili la kutojihusisha na shida za watu Kama alivyoliona Mwl. Nyerere lipo. Ni tatizo la kiuongozi ambalo linapaswa kurekebishwa ili nchi isonge mbele. Tutafute majawabu NJE ya vyama. Vyama vya siasa sio mwarobaini wa matatizo yetu.
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Oct 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Chama kisichotumikia wananchi kinatumikia nini basi?
   
 12. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #12
  Oct 20, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ivi to what extent did Nyerere contribute to our current state of affairs? Mtu kutoa speech nzuri sio kipya, lakini implementation ya hizo speech kwa watu wake aliweza? He had the opportunity to steer the ship in the right direction, did he?
   
 13. M

  Mr.Right JF-Expert Member

  #13
  Oct 20, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 408
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MYTH za UHURU wa TZ

  Historia feki ya Nyerere kwamba ndiye aliyekuwa muasisi wa Taifa so called "Baba wa Taifa?"

  Nyerere katoka ktk ELITE family, baba yake alikuwa CHIFU; lakini ktk historia tunaambiwa alikuwa "mlalahoi"

  Nyerere alitumiwa na Wakatoliki Wazungu lakini tunaambiwa alikuwa hapendi "Wazungu?" kwa sababu alikuwa na msimamo mkali kuhusu Ubepari.

  Lakini wamesahau Nyerere alipelekwa kusoma ktk shule za ELITE huko ULAYA lakini tunaambiwa alikuwa hataki kitu chochote kutoka kwa Wazungu.

  Najua wadau mnazo MYTH nyingi sana za Nyerere na UHURU.
   
 14. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #14
  Oct 20, 2011
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,650
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Ni muhimu kutathmini kauli kama hizi za JKN in their proper political-historical context ya enzi zile za "Kidumu Chama", "Zidumu fikra za Mwenyekiti", "Chama kushika hatamu" and whatnot.

  That being said, kwa mazingira ya sasa, kauli kama "The Party Must Serve the People" sound not only irrelevant, outlandish, and outmoded, but also serve to render relatively ancient political concepts like "The Party" and "The People" both semantically meaningless and non-existent.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Oct 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  ni kweli kabisa kwa sababu kauli hiyo ilizungumzwa katika context yake. Hata hivyo, Nyerere anapozungumzia "The party" hazungumzii chama chochote tu anazungumzia chama ambacho kimeshika madaraka na by extension chama ambacho kinataka kushika madarka ya kuongoza taifa. Haiwezekani kuwa na chama cha kisiasa ambacho kimeshika madaraka ambacho hakiwatumikii watu. Chama cha siasa ambacho kimeshika madaraka lakini hakiwatumikii watu - ambao ndio asili ya madaraka hayo - chama hicho kinapoteza uhalali wa kuwepo madarakani na wananchi wakipewa nafasi wana haki ya kukiondoa kwani wanahitaji kuwa na chama chenye kuwatumikia wao. Vin

  Vinginevyo, chama cha siasa kisichowatumikia watu na kimeshika madaraka kinamtumikia nani?
   
 16. F

  FJM JF-Expert Member

  #16
  Oct 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  @Sheba,
  Natofautiana na wewe kuhusu issue ya Arusha. Ni rahisi sana ku-misjudge nini hasa kilitokea Arusha. Tukumbuke, chanzo cha mgogoro wa Arusha ni ukiukwaji wa taratibu za kupata kiongozi/viongoizi wa kuwatumikia wananchi. Mayor wa jiji la Arusha hakupatana kihalali, ila wako watu walilazimisha ili ionekane kapatikana kihalali. Hii nafananisha na 'forced marriage', ambayo it is not only illigal, but a breach of fundamental human right. Na angalia karibu Africa nzima huu mtindo wa kupata viongozi ki-ujanja ujanja halafu wanakuja na 'solution' za kugawana vyeo mezani -ndio unauwa uwajibikaji.

  Kama unaowaongoza wanakuwa 'alienated' from the process of electing you ni vigumu sana wananchi hao hao wakaamini kuwa you have thier best interest in your heart. Kwa bahati Tanzania ya sasa is a classic example ya viongozi walipachikwa na madhara yake tunaona. Hapa Dar kama ilivyo sehemu nyingi tuna mkuu wa mkoa tuna wakuu wa wilaya tuna Mayor wa jiji na ma-mayor wa Ilala, Temeke & Kinondoni, lakini wote kwa ujumla wao haonekani hata kuliongelea tatizo la usafiri, mifereji ya kupitisha maji n.k. Ni vigumu kujuwa nani anaongoza juu mkoa!

  Kuhusu hiki unachokiita miradi ya maendeleo ya Arusha, hii miradi ipo regardless ya kuwa na mayor wa kupachikwa au wa kuchaguliwa. Na kumbuka hela nyingi za hizi miradi zinatokana na bejeti kuu ya serikali inayoipa kila Halmashauri fungu. Na kwa ufahamu wangu huko Arusha Kanisa linatoa almost 50% ya huduma muhimu za jamii i.,e shule, hospitali, maji etc.

  Tukirudi kwenye mada ya hii thread naweza ku-argue kuwa unless unakuwa na mfumo wa kumpata kiongozi kupitia kwa ridhaa ya wananchi ni vigumu sana kuwa na kiongozi wa kuwatumikia watu! There was/will always be one Mwl Nyerere! Hivi kama Mayor kawekwa na watu fulani atawajibikaje kwa wananchi na sio kwa hao waliomuweka.


   
 17. S

  Sheba JF-Expert Member

  #17
  Oct 20, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 210
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Swali lako zuri sana. Ni vyema sana tukanyambulisha kuwa watu katika siasa(polity) sio homogeneous. Watu katika siasa wanatafsiriwa katika muktadha(context) kama mchangiaji mmoja alivyosema. Katika muktadha wa Mwalimu, watu kwake wa ikiwa ni peasants na urban dwellers (baba kabwela) ambao ndio wa ikiwa wengi. Hakumaanisha wafanyabiashara ambao kimsingi walikuwa wachache sana na tayari wamekuwa priviledged. Ndio maana Azimio la Arusha na Sera nyingi katika utawala wake zililenga sana kundi hilo.

  Baadae na kufuatia Azimio la Zanzibar, focus ya watu ikabadilika. Uongozi wa CCM ukatwaliwa na kundi lenye mtazamo kuwa watu muhimu zaidi katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ni kundi la wafanyabiashara, wenye mitaji na tabaka jipya la Kati ambalo lilijumuisha Viongozi na wale waliofaidika na Mfumo. Kuanzia hapo, ukiangalia mwelekeo wa sera na utekekezaji wake utagundua kuwa WATU ambao CCM inajishughulisha nao ni wakina nani.

  Kwa bahati mbaya, WATU hawa wapya wana hulk ya kutoridhika na kupenda makuu tofauti na peasants na walalahoi. Wana hulka ya kupe, mahitaji yao yanatanuka(dynamic), wanapenda fursa na haki zaidi kuliko wajibu. Hivyo, wamefilisi uwezo wa CCM kiuongozi bila ya kuleta matunda yale yaliyotarajiwa kupatikana kutokana na CCM kuwekeza kwao. Matokeo ya chaguzi za hivi karibuni yamekmbusha CCM kuwa ipi umuhimu mkubwa wa kuwarudia watu wake wa zamani maana ndio wameendelea kuwa watiifu na waaminifu kuipata kura CCM. Tumeona katika uchaguzi mkuu uliopita na hata ule wa Igunga jinsi ambavyo CCM ilivyokosa kura maeneo ya Mijini.

  Katika Miaka ya karibuni kumetokea mabadiliko makubwa katika mizania ya siasa Tanzania. Tabaka la waishio mijini limepanuka sana, na ushawishi wake katika siasa umekuwa mkubwa zaidi ikilinganishwa na nguvu ya idadi yao. Tabaka hilimkwa sasa ndio movers and shakers wa siasa za nchi. Kila Chama kinajitahidi sana kulikamata tabaka hilinkwa ahadi lukuki. Kwa kusoma upepo, CHADEMA inaonekana kumudu siasa za tabaka hili. Kwa kufanya hivyo, kumeipa CHaDeMA nguvu ya kisiasa. Kwa maoni yangu, mtihani mgumu walionao CHaDeMA ni kuendelea kulidhibiti kundi hili maana kwa kifupi "halibebeki" na kukuponyoka dakika yoyote ni rahisi sana. Ukijishughulisha sana na shida zao unapoteza focus ya kudeal na shida za walio wengi.p ambao ndio wapiga kura wa dhahiri. CCM wamegundua hilo na sasa mwelekeo wa sera zao unaanza kujikita zaidi kujishughulisha na shida za vijijini ambako makelele ya mgao wa umeme huko hayana nafasi.

  Nataka kuhitimisha kwa kusema, kwa sasa vyama vyetu haijishughulishi vya kutosha na shida za watu. CCM imegubikwa na kilema cha migogoro ya madaraka na makundi maslahi. Hali kadhalika CHADEMA nayo imegubikwa na kiu Kali ya kukamata dola kiasi kwamba iko tayari kubeba lolote ambalo inahisi litaipeleka kwenye dola. Vyama vyetu kwa sasa vinajishughulisha zaidi na haja ya kugawana madaraka na sio shida za watu.
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Oct 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Chapakazi, ukweli wa nadharia fulani hautegemei kama aliyeitoa ameitimiza kwa asilimia mia moja. Plato aliandika kitabu kinaitwa "The Republic" ndani yake alijaribu kuelezea nadharia mbalimbali za utawala na mahusiano kati ya watawala na watawalia na humo tunalielewa zaidi wazo la Demokrasia. Plato hakuimplement nadharia alizoziandika humo lakini leo hii miaka zaidi ya 2000 baadaye kitabu chake kinaendelea kusomwa na mawazo yake kunyambulishwa.

  Martin Luther King hakuwa kiongozi lakini ukweli wa nadharia zake juu ya usawa na haki za watu weusi hautegemei wala haukutegemea yeye azisimamie. Sasa kufikiria kuwa the validity of an argument, theory or proposition depends on the person who propose them ni makosa. Kwa sababu, kichaa akisema nyumba yako inaungua ukweli wake hautegemi kama yeye ni kichaa au timamu. Nyumba itakuwa inaungua au haingui.

  Leo hii, watu wanawasoma kina Adam Smith na kina Friedman na wanauchumi wengine lakini haina maana kuwa waliotoa nadharia hizo walihitaji kuzisimamia na kuzikamilisha as a matter of fact ni dalili ya usomi kupitia nadharia zilizotangulia, kuzikosoa kisomi, kuziboresha na hata kuzikataa. Nyerere aliukosoa ubepari jinsi ulivyo na kwa kwa kweli alikuwa mbali sana ya muda wake kwani ukosoaji wake ambao ulikataliwa na wasomi wa zama zake leo hii unakuwa sahihi. Na cha kusikitisha ni kuwa hatuna wasomi wenye uwezo wa kuzipitia hizi nadharia na kuzitetea katika ulimwengu wa sasa na badala yake mtu anatoka na kusema tuzikatae. Ukiulizwa kwanini - unasema kwa vile Nyerere hakuzitekeleza. Na hili ni jibu ambalo mtu anafikiria amelitoa kwenye usomi.

  Nikuuliza: kuna tatizo gani katika kufuata the First Basic Needs Strategy?
   
 19. M

  Maga JF-Expert Member

  #19
  Oct 20, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 325
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Ya kwanza (a) kwa 99.5%, 0.5% iliyobaki ndio inaenda C na B
   
 20. Z

  Zanaki JF-Expert Member

  #20
  Oct 20, 2011
  Joined: Sep 1, 2006
  Messages: 544
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35

  Sasa kama alikuwa anachukia wazungu, mbona mshauri wake wa karibu alikuwa mama wa kizungu.

  Lazima kuna mtu popote ukienda, aliyeongoza uanzishwaji wa Taifa, no matter how far back in history you have to go back. Sasa uli suggest mwanzishi wa Taifa hili awe nani?

  Aliyekwambia Nyerere alikuwa hataki chochote cha wazungu ni nani? Kwani Nyerere alienda ulaya kwa mtumbwi? Alitembelea gari zilizotengenezwa na Nyumbu? Alivaa nguo za Kiwanda cha nguo cha Urafiki?
   
Loading...