The Open University of Tanzania

KASEHUYE

JF-Expert Member
Mar 11, 2014
299
59
Habari,
Naomba nifikishe ujumbe huu kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Mjaliwa na Waziri wa Elimu wa Tanzania Mh. Profesa Joyce Ndalichako, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ni jipu kubwa sana lililoiva na linalohitaji kutumbuliwa haraka iwezekanavyo. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kina matatizo makubwa sana ya Uongozi, Viongozi wa Chuo Kikuu hiki wanafanya wanavotaka wao na wengi wao wako after money tu na si kuwahudumia walengwa. Kwa mfano, Mimi na wenzangu tumemaliza Certificate ya ICT mwaka 2013 lakini cha ajabu mpaka sasa 2016 hatujapewa vyeti vyetu na hatujui tutapewa lini maana tumekuwa tukipewa ahadi zisizo na mwisho. Lakini pia, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kina tendency ya kuajiri Walimu wenye vigezo hafifu. Kuna watu wana GPA zisizo wapa sifa ya kufundisha Chuo Kikuu.
Mwiosho, naomba Mheshimiwa Waziri Mkuu pamoja na Waziri wa Elimu mfike Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kushuhudia uozo uliopo hapo hasa katika hii taasisi ya IEMT iliojaa watu mizigo wasiojua majukumu yao.

Barnaba Paul - Mbeya
Ahsanteni sana.
 
Hii umechoma kibanda naona sms sent ngoja tuone
Kuna majipu mengi sana hapo Mkuu, Waziri wa Elimu hana budi kwenda OUT kutumbuwa majipu sugu. Watu wanfanya kazi kwa mazoea kana kwamba wao ndio watu pekee wanaoweza fanya shughuli hizo.
 
Back
Top Bottom