The Only Thing We Have to Fear is Fear itself

Mimi nakukaribisha mheshimiwa Mbowe kujichanganya nasi ili upate na uchangie mawazo mbalimbali kutoka katika majadiliano haya.

Lakini mimi sioni tatizo kama sisi tunaochangia mada hatuoneshi majina yetu.

Tayari katika nchi kama Uchina na Zimbabwe kwenye serious oppressive regimes, raia huwa wanakuwa monitored wanapokuwa online kwa kutumia special software zinazoweza kutoa report kuhusu source ya material na intended destination ambayo mara nyingi ni IP address na namba ya simu.

As a result watu kibao wamesumbuliwa na mamlaka mbali mbali iwe za intelligence au wanamtandao.
Pia katika kudhihirisha hilo wote tumesikia jasusi wa zamani wa KGB alivyouawa kinyama akiwa ndani ya nchi nyingine.

Kwa sababu hio mawazo au makala ambazo mimi huziandaa huwa nakuwa nimezifanyia utafiti wa kina. Huwa pia nafanya tafiti kupitia source mbalimbali ambazo nyingine huwa ni za kulipia.

Kuna masuala mengi ambayo wewe mheshimiwa Mbowe inabidi utueleze kuhusu nia yako ya kutaka kuwa uraisi nchini Tanzania.

Kwanza je,ni nani anakufadhili au amekuwa anakufadhili katika kampeni zako za kutaka uraisi.Kwa kuuliza swali hilo ninamaanisha kwamba serikali iliopo madarakani hivi sasa imefadhiliwa na wafanyabiashara wakubwa na watu wengine wa nje ya Tanzania kwa minajili ya kutaka kufanikisha malengo yao binafsi na kuhujumu uchumi wa Tanzania.

Pili,je unafikiri ni kwa nini upinzani Tanzania na Afrika kwa ujumla huwa unashindwa kufanikiwa,kwa sababu hata hayati Mwalimu wakati wakupigania uhuru wetu wa bendera chama chake cha TANU kilikuwa kikifadhiliwa na chama cha labour cha Uingereza hivo kuwa na nguvu kifwedha hata kuweza kwenda New York na hiyo watanzania wengi wa leo hawajui,kwani tunaambiwa kulichangwa fwedha za harambee.

Tatu je,una mawazo gani kuhusu suala la uzalishaji umeme katika nchi yetu na una masuluhisho gani ya muda mfupi na muda mrefu?

Nne je,nini strategy yako kwa uchaguzi ujao na nani ni strategist wako.Nakuuliza swali hili kwa sababu ma-strategists wa chama cha Democrats pale Marekani waliingia na strategy ya kukata na shoka kuchukua viti kwenye bunge la Congress.

Mwisho nakukaribisha mheshimiwa Mbowe na nnataka niwe mwanachama wa behind the scenes ili tubadilishe nchi yetu.
 
Dr Who: That is a tall order question. What do you expect in a politician? Do you believe that a politician can be positivist or empiricist? I don't! The only perspective for a politician is to be either idealist or realist or both. Of course, he has to have empiricists and positivists around to move his idealistic agenda forward. And this is the mistake we may have made for electing JK; he is not an idealist; he can't come up with big ideas.




Mwanasiasa,

First of all I have a confession to make.I have always thought you were Mr Mbowe but your web name is mwanasiasa

That said, my answer to is not what i expect from a politician to be either Structuralist,Realist or Liberlist but when it comes to Mr Mbowe he seems to be far from the first two and this leaves me with an option of whether by chance he might be a liberalist especially after his quote from FDR and this scares me greatly as this is the man that 40 million Tanzanians will put their faith to protect them in other words National Security should be the centre of his plans but he doesnt come across as such and it would have been better at least he could have confessed to be a neo-realist.

And he scares me more when he quotes FDR

but i hope he will be back to clarify this matter
 
Mh. Mbowe,
Bravo brother Bravo!
Maanake hivi ndivyo inavyotakiwa kwa KIONGOZI.....
Tunakuomba tu uwe na mtu wa kuweza kuhifadhi baadhi ya mwasali yetu wengine maanake sidhani kama utaweza kurudi nyuma na kuyaorodhesha kirahisi.
Forum hii imekuwa sawa na ule mkutano wako ulioufanya kule machimbo ya Tanzanite.. That's the way to go brother!
Karibu uwe karibu nasi na sisi tujisikie kuwa wewe ni mwenzetu!
Hizi ndizo sifa za - Mtu wa Watu.
 
MUH. MBOWE

Ninakushukuru sana Muh.Mbowe kwa ujasiri wako kujiunga na watanzania wenzako bila woga na kujitambulisha katika forum hii kuwa wewe ni nani ,mimi nilikuwa msomaji tu katika chombo hichi cha habari ,sikuwa mchangiaji vile vile sikuju kama watu wakubwa kama RAIS, WABUNGE,MAWAZIRI,RC.DC,PS,na wengine wengi mlikuwa mnaingia huku nakufuatilia kile kinacho endelea humu ndani.

Ninatunaini chombo hichi kimekuwa cha pekee kwa sababu hata mtu mdogo kama mimi, sauti yangu sasa inasiki popote duniani ninatunaini kila mtu huku aliyezaliwa na mwanamke anamapungfu yake hakuna aliye kamilika.

Mimi ninapenda kuchangia na watanzania wenzangu mambo ya msingi yanayohusu taifa letu changa Tanzania, labda niseme hivi hii ndunia kwa sasa imekuwa kijiji kimoja kupitia tekinolojia hii ya habari na mawasiliano, mimi sioni sababu ya wakubwa kununua vyombo vya habari au kugombani cheo katika chama cha wanahabari ili mazambi yao yasiandikwe.

Watu hao kutokana nauwezo wao mdogo wa kufikiri walifikiria kwamba vyombo vya habari vitabakia kuwa MAGAZETI ,TV na RADIO tu milele sasa Tekinolojia ya habari na mawasiliano ina wanyima usingi kutokana mazambi yao,.sisi wanaforum na wanablog tunawaambia hichi,ndicho kipindi habari imekuwa bure haiuzi ,utajikuta wewe na familia yako uko kila mahali katika mitandao.

Utakuta maelezo na picha kama vile mastaa wa Hollywood huko marekani ukielezewa kwa kile kizuri ulicho kifanya katika jamii au kibaya ,kutokana na uwezo na nguvu walizo nazo hao watu, sasa nina wambia muda umekwisha tafuta kazi nyingine ya kufanya huu ni muda wetu kukuelezea ni nini chanzo cha mafanikio yenu au umasikini wenu na nini kinacho wakufanya muwe na kiburi,na matisho ya kila aina,

Jingine kwa nyiye wakubwa wa wadogo nina towa ushauri wa bure ukiona unaandikwa katika mitandao na umeandikwa vibaya sana ,roho inauma na umeandikwa kwa kitu cha kweli ulicho kifanya na ukapata faida sasa ni muda wa wewe pia kutoa kidogo mambo yaendelee mbele, pia wala msipaniki mnapo andikwa sana mlisha kula faida.

Ni waambie kitu chakufanya katika mitandao hii kuna watu wanao wajua kwa undani inawezekana mligombana au wivu pia kuna digirii za chuki binafisi zina uzwa na Osama na Bush. Sasa basi tafuta watu humu ndani au nje ya forum hii,unda timu yako ndani ya mtandao huu waku wajibu mashambulizi uwape pesa kidogo wa wajibu wale wanao waandika vibaya. (WESTERN UNION)

Lakini ukisema unaanza matisho kwenye forum na watu wakikujua ni wewe wanakumaliza, jibu kama vile siyo wewe kaa kimya wacha watu wako wafanye kazi hii pia ni sehemu ya sera ya CCM ajira kwa vijana ,maisha bora kwa kila mtanzania na ndiyo mchezo unao endelea kwenye forum nyingi duniani wachani jaziba , hasira na matisho,

Ninatumaini wazee wengi duniani hawajui haya mabadiliko ya kitekinoljia yaliyo tokea yana wapa shida sana wengine wana shikwa na presha na magonjwa mengine , kusikia wameandikwa kwenye mitandao ya Internet, kwahiyo nilazima muende na wakati hii tekinolojia ndiyo sehemu ya maisha ya watu kila siku katika maisha yao, ni kama kuvaa nguo,au kupiga mswaki,

Mimi ni kiwa kama msomajina mtafiti katika forum hii nilivutiwa sana baada ya Muh.Mbowe kuingia humu ,nimesoma habari nyingi sana nyingi nimezikopi .

ninazifanyia kazi nitazirudisha katika forum hii kwa sura nyingine, kwa kumbukumbu zangu, mimi pia ninafanya utafiti kuhusu jinsi watanzania wananyo pata maendeleo na kuboresha maisha

jinsi wachache wanavyo ujumu uchumi wa nchi hii jinsi wachache wanavyo ishi vizuri na wengi shida ,jinsi mtu mmoja anavyo weza kuchukua riziki za wengi.

Mimi ninafanya utafiti kuhusu suala la muheshimiwa MENGI na MANJI chanzo cha matatizo ni nini kwa matajiri hawa, ninaandika ripoti, itakayosaidi kamati ya bunge ndugu zangu wana forum hizo articles sizioni katika forum hii ninaziomba nimalizie kazi ripoti hiyo itawekwa katika mtandao huu.

Muendesha mtandao huu tunaomba hizi artcles za MENGI na MANJI zirudishwe au aliyenazo aziweke huu ni uhuru wa maoni ,kama Rais JK,EL,wanaandikwa humu kwani hao wawili, ni nani hao ,kwa taarifa zisiporudi tuna anzisha WEBSITES NA BLOGS alafu tunaweka LINK katika forum hii ili watu wasome ,mnaweza kununua MAGAZETI,TV,naRADIO tu ,sasa tuna wapa muda nyiye mnao endesha huu mtandao hizo articles zirudi.

Naomba kutoa hoja

by King
 
Ahaaa, Dr Who I am not Mbowe, not at all. I am just mwanasiasa. I just happened to believe in the course advanced by CHADEMA and Mbowe. Given time, I will come back on the issue of liberalism, realist, FDR quote, etc. We may wish to have a topic of its own on this.
 
William King


Waswahili walisema tugange yaliyopo yaliyopita si dwele.

Wewe unafanya utafiti kuhusu whom whatsoever tuletee issues tutadiscuss without kuwatazama usoni ni wakina nani?

Anzisha thread usitoe vitisho visivyokuwa na msingi - hatupo hapa kutetea wala rushwa


Wacha
 
DrWHO,
What was wrong with FDR? Wamarekani walimpenda mpaka wakampa 4 terms.
 
Mwanasiasa & Jasusi I will come back baada ya kama saamoja hivi niwajibu kwa undani

lakini kukuweka sawa bwana jasusi ni kuwa hapa hazizungumwi nani mbaya au mzuri lakini tunazungumzia the whole concept of International Relations na nafasi gani bwana mbowe ambaye anaweka akawa rais wa nchi yetu sasa hiii inamaana hata private life yake itakuwa open kwenye public domain maana ndio inakuja na package nzima ya siasa hiyo

Nilifikiria niianzishie separate thread lakini i will keep this option open

ttl
 
DrWHO,
Kwa sababu linahusiana na hii topic, na thread yenyewe aliyoianzisha Mhe Mbowe ni maneno aliyotumia FDR basi naona iendelee hapa hapa.
 
Ok

Nasikitika kuwa mwenyewe hajaja kuweka mambo sawa humu but i will continue this discussion na Mwanasiasa who seem to be more intouch with Chadema and so on lakini jibu langu litamsubiri atakayoyasema
 
NAshukuru sana bwana Mbowe, kwa ujasiri wako wa kuweza kujiunga na jambo forum, ingawa sina uhakika kama ulichokiongea hapo juu ndio itakuwa mara yako ya mwisho au la!

Vilevile mie naweza kusema wewe unaonekana kama utakuwa ni mchangiaji zaidi wa kuangalia kuliko kutoa hoja hasa zile 'zisizo na uoga' kutokana na wadhifa wako kama chama chako, jamii na kibiashara.

Sidhani kama kuna siku tutasoma makala yako yeyote humu ndani ambayo intakuwa inabainisha kwa mfano majina ya wala rushwa serikalini kabla ya wao kukamatwa au mahakama kuwa imewahukumu, kwa sababu ambazo kama unajua sheria za nchi na utaratibu wa sheria unaweza kufanya. Hivyo umejiwekea kikwazo wewe mwenyewe kwa kutaja jina lako kamili.

Hii forum sio ya kusema kuna rushwa nyingi serikalini, au viongozi wanakula sana rushwa bila hata kugusa ni nani na yuko kitengo kipi, kwa namna hiyo mchango wako siku zote utakua wa juujuu tu, kwa sababu za uoga wa yatakayofuata kama utakuwa umetaja majina ya watu.

Hivyo kuficha ID kunasaidia watu kusema bila woga kama ulivyosema wewe, ingawa huna uhakika kusema hivyo vitu bila kutumia jina na kweli unafikri kwamba ni uoga. Mimi nafikri kwamba wewe ndio umejiondolea uhuru wako wa kuweza kutaja majina ya watu wanaotuhumiwa kuvunja sheria bila hofu ya kushitakiwa au kusumbuliwa na watuhumiwa.

Nafikiri ulitakiwa uulize swali ni kwanini watu wengi humu ndani mnaficha majina yenu ya kweli, bila kurukia kwenye uoga. Sheria ya nchi tu zilizoendelea zinavipengele ambavyo vinawalinda walipua skendo 'whistleblowers' kwa kutowataja hadharani, na wakati mwingine kuficha hata ID zao. Hata polisi na vyombo vya usalama wana sheria zinawalinda watoa taarifa za maovu 'informers'. Sasa kwanini humu iwe tofauti na sehemu nyingine za kutoa habari nyeti?

Na fikiri ni mapenzi ya mwanachama wa forum kuona kama anaweza kutumia jina lake halisi au lingine lolote.
 
Bila kurudiarudia yaliyosemwa, nadhani Mheshimiwa umeteleza. Katika uwanja kama huu ni hatari na huenda makosa kwa wadhifa wako kujiweka wazi kama ulivyofanya. Ni rahisi kubomolewa kuliko kujijenga. Sasa angalia hapa ndani unavyosakamwa! Na kumbuka kadri unavyojibu au utakavyojibu ndio watu watakuja na maswali. Elewa kuwa humu ndani hatufuati kanuni kama za mjadala ulio wazi na wenye kusimamiwa na kuratibiwa vizuri. Hapa kila mtu anatoa mhemuko wake kulingana na anachokijua, alichokisika, na hata kama ni majungu. Kumbuka siasa za Bongo ni mchezo mchafu.

"It was too high a risk on your side to have made yourself public in this forum. Otherwise, it was a gimmick that was geared towards gaining cheap popularity...and I don't think you need that."
 
Duuuuh, Mada hii imeisha tazamwa na watu elfu 4 na upuuzi... ama kweli Mbowe anauzika bob sikutegemea...
Mbowe mkali sanaaaaaaaaa! kapandisha chati kijiwe chetu within one week it's a best seller..
 
Vigogo' Chadema wamwaga misaada KKKT

Na Ally Sonda

MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mbunge wa Viti Maalum wa chama hicho, Grace Kiwelu wametoa msaada wa Sh 4,200,000 ili kusaidia miradi ya ujenzi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Majengo mjini hapa.

Mbowe, kwa upande wake alichangia Sh 2.5 milioni na Mbunge Kiwelu akatoa Sh 1 milioni kwa ajili ya maendeleo ya miradi kanisani humo.

Aidha, mwanasiasa huyo (Kiwelu) alitoa msaada wa Sh500,000 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa choo cha shule ya awali ya kanisa hilo.

Akizungumza mjini hapa baada ya kukabidhi sehemu iliyobaki ya misaada hiyo, Kiwelu alisema kuwa, ili kuhakikisha kuwa waumini wanakuwa na maendeleo kiuchumi, amejitolea Sh 200,000 ili kutunisha mfuko wa Ushirika wa Akiba na Mikopo (Saccos) unaojulikana kwa jina la UWAMKI ulioanzishwa na waumini wa kanisa hilo.

Kwa mujibu wa mbunge huyo, fedha hizo zitatumika kununua baadhi ya samani muhimu za ofisi ya ushirika huo ambao unatarajiwa kuwa mkombozi kwa waumini wa kanisa hilo na wa kata za jirani.

Kwa upande wake, Mbowe alisisitiza kuwa viongozi wa chama hicho, wataendelea kuwasaidia waumini wa madhehebu ya dini nchini ili kujenga taifa la watu waliobobea kwenye imani ya kumjua Mungu kwa kufuata maagizo yake.
 
Mkandara.
unapenda kijinga sana hilo sio debe bali unapiga deki. kule Chifupa vs Mbowe kuna elfu mbili ndani siku tatu atauzika zaidi.

Es.

Huyo jamaaa anafanyiwa Course work na kina Balile hana anachosoma nimesema sana hilo, wewe muulize Mwanasiasa ambaye anasoma kweli kama muda huu mwanafunzi aliyeanza masomo october 2 anaweza kuwa na muda wa kupoteza tena anafanya digrii 2 in a time.
kazi kwenu, sisi tumeng'amua zamani.

hiki chama ni cha wakristu na hata misaada yenyewe inapelekwa huko huko Kilimanjaro, anayetoa ni Kiwelu (mchaga) na Mbowe (mchaga) huku akina Mwanasiasa wanasema chama kina sura ya kitaifa. msiba mkubwa.
umeona hapo wanawasisitiza wawe na saccos iwe kama yao, ulikuwa hujui chadema ni saccos?
 
chinga una akili ya kuku ,bill amepost hiyo text hapo anasema grace ametoa michango lakini nilivyoelewa ametoa pia kwa niaba ya mbowe ,chairman wake thats not abnormal,alafu acha ukabila ,so unataka hata jk wakwere aogope kuwachangia .

kaka mkandara kasema freeman anauza na thats is true kwasababu thread aliyoanzisha wameangalia watu elfu nne, ile yako wameshea na amina ina watu elfu mbili you know why thread ya mwanakijiji ilikuja hapa inamuhusu amina peke yake wlichangia watu hata mia hawakufika kwa siku tatu ikahamishiwa na adm kule kwenye vibweka ndio kidogo ikagain ,nafikiri hapo kidogo umeelewa
inaonekana wewe una malengo yako huku naunatuharibia kweli.
 
Philimon mikael.
mwenye akili za kuku unamjua alitakiwa awe shule muda huu ametoroka yuko Moshi.
nimewasiliana na university registrar on +441482465136 kasema undergraduate wote wanatakiwa wawe shule.
 
Okay, so Mbowe yuko Moshi, anafanya degree mbili, ametoa misaada etc etc. etc
What the hell does it have to do with Christianity or tribalism? jeeez! aren't we mentally mature?
 
Back
Top Bottom