The Only Thing We Have to Fear is Fear itself

Bravo Mwanasiasa,

Point well said, na umekuja across kama wewe ndiye mwenye kiti wa Chadema, badala ya Mzee Freeman na JJ, isipokuwa tu hebu fafanua maana ya militarism ndani ya CCM na Upinzani, hapo sijakupata?

Mzee Freeman,

Respect kwamba finally, baada ya kuangalia kila siku kwa pembeni, umeamua kuja mwenyewe, off course ninajua kuwa siku zote ulikuwa upo hapa maana watu wako fulani ninawajua wapo hapa kila siku haiwezekani kuwa hukuwepo, anyway heshima mbele kwa kujitokeza kwenye hii forum, hii inapaswa kuwa ni clear message kwa bwana Ukimwi kwamba hii forum inafanya kazi yake inavyotakiwa ingawa katika maizngira magumu lakini, hey! it is better than noithing,

Mzee Freeman,

I have a problem na ujumbe wako kuhusu majina ya bandia ninaona unataka kupoteza lengo pamoja na nia yako njema ya kuja hapa, do not tell us what to do bro!, wewe jibu mapigo tu, tena please we have nothing to apologize for kwa kutotumia majina yetu, wote hapa tunajua what time is hatuhitaji kukumbushwa na mtu yoyote, kilichokuleta hapoa na sio forum zingine ni kwa sababu the message is powerful na clear understandable, njia zote tunazozitumia humu ndio hasa nyinyi politician wa bongo mnazozielewa vizuri, na ndio maana hata magazeti mnayoyamiliki, on this I mean wote CCM na Upinzani huwa hamuaandiki majina, WHY? take this thing ya majina back bro! no more lectures kwenye hilo, next time you come just deal with the message,

But baada ya kusema yote hayo, ninasema heshima yetu kwako kwa kukubali hatimaye kuingia kama ulivyo kwenye hii froum, na ninakuomba uendelee kuwepo hapa ili tufundishane siasa na tuulizane maswali ya kweli kwa faida ya taifa letu, taifa letu liko njia panda, we know that, sasa hii sio forum ya upinzani kama some of us walivyoshauri, hapana hii ni forum ya wananchi wanaoelewa ukweli wa kinachoendelea bongo, na wangependa kusikia majibu au marekebisho, sasa tunategemea wewe na wenzako mje hapa mtupe majibu mnayoyafahamu, bila siasa nyingi tumesikia siasa za kutosha sasa tuongee majibu tu bro, hizi habari za majina ni irrelevant,

hebu tulonge issues Mzee Freeman wote hapa ni watu wazima, tuseme issue, na the hot one sasa hivi ni Richmond na IPTL, hebu tuwekee msimamo wa chama chako, utakapoingia tena, pia kama unaweza hebu gusa kuhusu hii NONESENSE ya unga? Halafu hebu gusia kuhusu elimu yako mpya, maana kuna tunaoiona kama kuna u-KIHIYO! kihiyo! ndani yake, hebu tuwekee usawa?

Wasaalaam wazee wote wa hii forum, na karibu wazee wa Chadema Freman na JJ, na we are ready for you ila please do not tell us how to write, Thank you! na Forum idumu!
 
Mbowe Karibu sana, katika hii Forum.

Kuna watu humu wamekuwa wakitoa masomo mazuri na ya maana kwa taifa letu na pia ushauri mzuri TENA WA BURE KWA VIONGOZI WA UPINZANI KAMA WEWE KWA KUWA NYIE MNA JUKWAA.

KARIBU SANA UJIFUNZE TOKA KWETU NASI TOKA KWAKO. hONGERA SANA KWA KUAMUA KUNOA UBONGO ZAIDI.
 
Mzee Es
Ninatumaini kwamba Muh. mbowe hayuko hapa kufundisha mtu yeyote jinsi ya kuandika katika forum hii jambo la kwanza nikumkaribisha kama kiongozi wa kitaifa pia ametoa ushauri kwa wana forum.

kwa mimi binafsi nina mkaribisha Muh. Freeman katika forum hii ambayo ilianzishwa makusudi kabisa na shirika moja lisilo la kiserekali kwa watanzania kutoa maoni yao kupitia njia ya INTERNET na kuwashauri viongozi wetu wanapo kosea au kulewa na madaraka.

Muh. Mbowe ni kiongozi wa kwanza katika afrika kuingia katika Mtandao wa Internet na kuongea na wananchi kwa karibu na kusikiliza maoni yao, Muh. Mbowe amekuwa akitumia vyombo vya habari mbali mbali kama TV,RADIO,MAGAZETI na kukutana na wananchi uso kwa uso au ana kwa ana kwa kuonyesha upeo wake mkubwa wakufikiri ameamua kutumia Tekinolojia ya Habari na Mawasiliano ya Komputa kufikishia wananchi ujumbe kwa MTANDAO WA INTERNET amboa utamsaidia sana katika chama chake.


Muh. Mbowe hongere sana na hapa unaongea na wasoni , wa Bunge, Ma Balozi RC,Ma DC, Mawaziri, Usalama wa taifa, Polisi, Jeshi,watanzania, Viongozi wa vyama ,wadau na watu walioko ndani ya sisitimu na watu wenye ufahamu kama wewe watakao kushauri nini chakufanya katika chama chako, makosa yaliyotokea na mengine mengi sana. mimi ni mwana CCM halisi sasa muh.mbowe karibu

Muh. Mbowe sasa sauti za wapiga kura wako zina sikika moja kwa moja [LIVE!!!!!!]Pia ninaamini utajizolea wanachama wengi sana 2010
 
Nimekusikia mkuu, haya tukate issues! issues! issues jamani kukaribisha imetosha issues! kabla Mzee Freeman hajawa na shughuli nyingi!
 
Ndugu Mheshimiwa Freeman,
KARIBU... karibu saaana na kiti cha ugeni tafadhali kipokee utupe habari zitakazo tupa moyo na matumaini.... karibu sana.

Hapa ndio JAMBO..na hakuna maskhala kabisa na viongozi ndugu yangu ila tunazungumzia sana hoja ambazo ni MATOKEO ya uongozi.
Pili, Sii kweli kwamba hatufuatilii kwa kina utekelezaji wa hawa viongozi wetu kabla hatujatoa hoja zetu na mara nyingi sii rahisi kwetu kutoa malalamishi kabla kiongozi hajaifanya kazi yake.
Mathalan swala la Richmond limeongelewa sana humu baada ya tender zimeisha tolewa.
Ebu tuambie kweli Tender ya mradi wa huduma ya Kitaifa kama UMEME kweli inaweza tolewa kupitia board za ULAJI wala sii bungeni?... Umeme ni commanding heights ya uchumi wetu imekwenda pewa watu kwa utaratibu wa kihuni na visingizio vya Tender ya kitaifa, hali viongozi haohao wanakwenda nchi za nje kuomba misaada ya kujengewa madaraja na shule za msingi.
Tena kibaya zaidi hawa hawa viongozi wanakwenda nchi hizo na kuitangaza nchi yetu ktk Uwekezaji hali nchi haina Umeme masaa 12 na zaidi kwa siku.
Sii haki yetu kuuliza kwa nini:-
Umeme unawashwa USIKU wakati uzalishaji umesimama na kuzimwa MCHANA kutwa wakati wa uzalishaji! ... nani kweli ataweza ku invest ktk mazingira hayo?
Sii haki kuuliza UMEME kukosekana kwa zaidi ya MIAKA wala sii tatizo la siku moja!.na ahadi zinazidi kusogeza kalenda mbele. Je, hao viongozi kweli wanaweza kusimama hapa na kutuambia kwa nini umeme umekuwa GONJWA SUGU hali altenatives zipo wazi kabisa?...
Hao Richmond wamepewa deadline sijui April 2007! Hivi kweli viongozi wetu wapo serious na tatizo hili ama hawafahamu umuhimu wa umeme ktk uzalishaji?...
Mengi yapo ndugu Freeman karibu tena!... hayo yanayokuhusu wewe mshikaji yakubali na - Yatafutie ufumbuzi. Kama ulivyosema ktk healing process inabidi kwanza mtu akubali makosa yake kisha kutafuta mbinu hata therapy katika kutafuta mwanzo Mpya.
KARIBU.
 
chinga unataka wabunge wa chadema waige mfano wa amina,well unatofauti na icon wako amina ,mnafanana sana.
changamoto.
tuanzeni kupitia ahadi alizotoa jk kwenye kampeni so as to establish perfomace and percentage of the promises fullfilled.ili tujikite zaidi kwenye kukumbusha ahadi za wananchi,kama ni kulala wamelala wabunge wa ccm ambao EL aliwabana wasiongelee issue ya energy,demokrasia imedumazwa sana bungeni ,hakuna afadhali!!!!!!!!!!!!! pia kuna issu ya uchache wa wapinzani....
 
Naona post No.1 ziko nying leo, I expect more to come, but watch their deeds (lips)!
Bravo Jambo Forum, when I open Jambo forum nowadays at leat 20 people on line sometimes 40; versus 1 to 3 in the past months!!

Bring them all, I expect ........ more!

By the way you may also explain in details about your majimbo politics! By the way how do you combine business and politics together?
 
Mikael
napitia ndoa ya Chadema na David Cameron kwanza nenda kwenye tamko la chadema. hapa tusipachafuwe ni kumkaribisha mheshimiwa tu Mbowe mkwewe Mzee Mtei(wakamua maziwa) na kule ninajadiliana na Mnyika(mshika mapembe)
 
data za Chadema na Conservatives ninazo na sidhani kama hapa ni mahapa pake unless kuwe na different thread itakayo explore the links btn Chadema in Tanzania,Conservatives in Uk na kwa mbali na hao Republicans in the states


Faili la Mbowe pia hali kadhalika lipo lakini sioni sababu gani kuanza character assassinations humu na pili sioni chochote kinachomlink yeye au maisha yake binafsi na siasa za humu ndani lakini ita better to keep it for future reference wakati inthe meantime tuna hili la muhimu zaidi la kudiscuss policy za chama chake
 
Chinga nani kakutuma kuharibu hii bodi ?

Nimefarijika kusoma habari za Mheshimiwa Mbowe kuingia katika forum hii. BIla shaka lipo lililomvuta. Na kweli amevunja rekodi, maana wanasiasa wa calibre yake hawaingii kwenye vitu hivi. Sijui wanavidharau au hawavijui? Ukweli ni kwamba hata baadhi yetu tunaompinga Mbowe na Chadema kisera, tunamheshimu kwa baadhi ya vitu vyake; na ndiyo maana tumekuwa tunamfuatilia kwa kila hatua anayochukua. Katika mazuri anayofanya, kama lile la elimu, hatuna sababu ya kumbeza. Tunabaki kutafuta mahali pa kumchallenge, maana inavyoonekana huyu jamaa si mwepesi kama watu wengi tulivyodhani huko nyuma. Anaonekana simple, lakini binafsi nimemfuatilia sana. He is serious. Karibu Mheshimiwa.

Naamini kwa kuingia kwake hapa ataweza kutoa baadhi ya majibu ambayo kamwe hayawezi kujibiwa na mtu mwingine, hasa kama yanahusu harakati za chama chake, kinachoonekana kuwa juu sasa kichati.

Tungependa na wanasiasa wengine serious wa vyama vingine wajitokeze, si kwa kushawishiwa, bali kwa kujituma wenyewe. Tukiwa nao tutakuwa na fursa ya pekee inayowezeshwa na mtandao huu. Wanaharakati wa kisasa lazima watandae kisasa.

Lakini nina changamoto. Inapoletwa hoja MAKINI tuijadili hiyo kwa UMAKINI; maana naona wapo baadhi yetu wanatanguliza ama utani au vijineno visivyojenga hoja. Sijui kama ndivyo walivyo, au wanatumiwa kuvuruga hoja zinazoletwa. Sihitaji kutoa mifano hapa, lakini wadau mnaona kwamba kwa jinsi hii ya watu kuacha hoja na kuingiza vijineno vinavyotoka nje ya mantiki, tunaweza kujadili porojo badala ya hoja. Sidhani kama hilo ni mojawapo ya malengo ya forum hii.

Ninavyoona - sijui wengine mnaonaje - ni kwamba forum hii ni ya watu serious. Watu serious huanza na serious issues, hawatangulizi trivial issues. Vinginevyo, sasa tutakuwa kama wale wale tunaotaka kuwakosoa.

Jambo mojawapo ambalo limekuwa linatutafuna baadhi yetu ni kukaa katika mfumo uliofungwa na wazee waliouasisi, usio na mahali pa kutokea, usio na nafasi ya mambo mapya, unaopenda usanii badala ya ubunifu, unaotanguliza hadaa badala ya ukweli hata kama unauma. Hiki ndicho kilichotugawa sasa wana CCM, ambao sasa hatuko wamoja tena, na tunatafuta mlango wa kutokea.

Sitaki kutoa lecture hapa, lakini nina usongo na issues. Nasikitika ninapokuta watu watatu mfululizo wanazama kwenye character assassination juu ya vitu vidogo vidigo na hawatoi proof. Sawa tuko kijiweni, lakini kwa nini tusi-improve kijiwe chetu? Nadhani hali hii ndiyo imesababisha mwenzetu mmoja akahoji kama kuna mtu katumwa kuharibu forum hii! Ndiyo tuwe huru, lakini tuwe serious...
 
Bwana Freeman karibu sana ndani ya forum and I hope you'll be a regular contributor.
 
Wanaforum, Salaam sana!

1. Nawashukuru sana kwa makaribisho.Ukaribisho uliotoka kwa "Senior Members" kadhaa na wengine wote naupokea kwa heshima kubwa.
2. Nimesoma dhamira yenu thabiti ya kupenda kuendelea kutumia "pen names". Hoja zenu zina msingi na sina sababu ya kuendeleza mjadala wa somo hili.
3. Nitashiriki kadri fursa zitakavyoniruhusu, hata hivyo, mniruhusu nisijiingize kwenye malumbano yasiyo na "substance."
4. Nategemea hoja kadhaa zinazohusu Chadema na hata viongozi wake, zitaibuliwa. Ni lengo langu zijibiwe zote. Sisi kama chama hatuendeshi siasa za kificho na woga. Mimi na timu yangu yote tunaamini katika kujenga Chama Taasisi. CHADEMA siyo mali ya Mbowe na viongozi wenzake, ila Mbowe ni kiongozi wa taasisi hii. Uongozi ni dhamana na naheshimu na kulisimamia hili.
5. Kila taasisi makini ina taratibu zake za ki-utawala sambamba na mfumo wa utoaji habari. Naheshimu forum hii kama chombo kamili cha habari chenye haki ya kuhoji na kujua chama hiki kinachangia nini katika mustakabali wa Taifa letu. Kama tulivyo tayari wakati wowote kuhojiwa na chombo chochote cha habari, tutakuwa tayari kujibu hoja yeyote yenye mantiki. Hivyo basi, itawezekana baadhi ya hoja zikajibiwa na watendaji wa chama na nyingine nikajibu mimi.
6. Pale hoja itakapokuwa imepewa majibu rasmi ya chama, watendaji wa chama watatumia majina yao halisi na nafasi zao ndani ya chama zitawekwa wazi. Lengo hapa ni kuepuka majibu yasiyo rasmi yakapewa tafsiri potofu kuwa ni majibu rasmi ya chama.
7. Sina hakika kama utaratibu huu utaendana na azma ya forum hii. Aidha, si kusudio langu kugeuza forum hii jukwaa la siasa la Chadema, ila naamini jamii na wanaforum wana kiu ya kuelewa vyama vinasimamia vipi maslahi ya Taifa.
8. Wanabodi na wanaforum, kama uelewa wangu ni sahihi, naomba ushauri ili hoja zianze kujibiwa.
9 .Sitasita vilevile kutoa maoni yangu binafsi inapobidi.

Nawashukuru kwa kunisoma

Freeman Mbowe
 
You still havent answerd my question Mr Freeman hoping that you are not into "punch and judy" politics of DC & TB.Its a pretty m much straight question that i asked you and i can repost what i asked you earlier:

As much as i have my objections with Politicians but i have to admit that you sure have some "guts" and secondly i got abit curious with your FDR quote...i dont have any particular problem with it but i have some serious objections with FDR's liberalism in IR which in 2006 is disgused as Realism

Now my question to you Hon Mbowe,Are you by any chance a REALIST?
 
Mbowe,
Yes, nakubali wewe mkali... na moto wa kuotea mbali!
Nadhani tunaweza kuanza na maswala yanayowatatainisha wengi ikiwa ni
1. UDINI...
Je, Chadema inajihusisha vipi kuepuka watu wenye nyadhifa ktk dini kuwa viongozi wa Chama. Kuna msemo usemao ni vigumu mzazi kumhukumu mwanao, nikiwa na maana - Kiongozi wa dini siku zote hawezi kuwa Kiongozi mtetezi mzuri serikalini bila kuiweka dini yake mbele. hata kama makosa yamefanyika.
2. Swala la Majimbo..
Hili swala limekuwa na ugumu sana kwetu kulikubali kwa sababu tumeona harufu ya Utengano na sii kwa sababu ya madai ya CCM. Baadhi tunakubali majimbo ya kiuchumi yaani Special Economic Zones jambo ambalo CCM wameisha lifanyia kazi. Je, hii ndiyo ilikuwa azma ya Chadema toka mwanzo na ikatafsirika vibaya ama ni kweli Chadema inapendekeza majimbo yajitegemee kama ilivyo ktk nchi za Magharibi na hasa Marekani.
 
I have so many questions for him but i wont until he answers what i asked him and i am trying to think he is either deliberately dodging my question or he hasnt got anything to say at this moment but at least he should be honest about it
 
Mzee Freeman,

Utakapo pata nafasi naomba uguse suala la Ditopile kwa ujumla na respect kwa the rule of law katika nchi! au taifa letu!

Lakini so far heshima mbele kwa kurudi na kuendelea kuwepo, SALUTE bro!, ila soon tuta-get into real business hapa hapa!
 
Back
Top Bottom