The New York Times lasambaza uongo Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, ladai haukuwa huru na wa haki. Je, ni kweli tunyamaze, au uongo tukanushe?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,571
Wanabodi,

Hili ni bandiko la Swali, Gazeti la The New York Times, la Marekani, ambalo ni la tatu duniani kwa ukubwa, lasambaza uongo kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, ladai haukuwa huru na wa haki. Je, ni kweli tunyamaze tuu au ni uongo tukanushe?

Kwenye bandiko hili, natumia kanuni ya samaki kwenye tenga la samaki, hata ukiwa na samaki 100 kwenye tenga la samaki, wengine walivuliwa asubuhi, wengine mchana na wengine jioni, ukawaweka kwenye tenga moja, yule samaki mmoja wa asubuhi akioza, then samaki wote wanakuwa wameoza, hata wale wa mchana, hata wale wa jioni, Wazanaki wana msemo wa Kizanaki usemao "wote manzi ganyanza"

Vivyo hivyo ndivyo uongo ulivyo, ukisema vitu vya kweli 99, halafu ukachomekea kitu kimoja tuu cha uongo, huo uongo mmoja, unabatilisha zile kweli zote 99, na zote kuonekana ni uongo mtupu!

Kabla ya kuanza makala yangu hii, naomba ku -hare info kuhusu magazeti makuu 10 ya dunia hii yanaongozwa na gazeti la The Guardian la UK, likifuatiwa na The Wall Street Journal la USA, gazeti la The New York Times la USA ni la tatu, mengine ni 4. The Washington Post (USA) 5. China Daily (China) 6. The Times of India (India) 7. The Sydney Morning Herald (Australia) 8. The Asahi Shimbun (Japan) 9. Dawn (Pakistan), 10. Zaman (Turkey)

Gazeti la The New York Times, la nchini Marekani ambalo ndilo gazeti kubwa la 3 duniani, limeanza kueneza uongo kuhusu uchaguzi Mkuu wa Tanzania, kwa kuiambia dunia kuwa uchaguzi mkuu wa Tanzania haukuwa huru na wa haki.

Katika toleo lake la leo, gazeti hilo limechapisha makala kuhusu Tanzania, kwenye makala hiyo, wamesema mengi mabaya kuhusu uchaguzi mkuu wetu, japo kuna mengine ni kweli yalitokea, na kuna mengine ya kuibiwa kura yanasemwa tuu lakini hayana ushahidi, lakini kuna mengine yamesemwa ni uongo mtupu wa mchana kweupe!.

Gazeti hili limefanya mahojiano na Mtanzania mwenzetu mmoja, naomba nisimtaje humu maana huyo jamaa ni kipenzi cha baadhi ya watu humu JF, na ana followers wengi kwenye mitandao ya kijamii, hadi wengine ni kana kwamba wanamuabudia, hivyo ukimkosoa tuu jamaa huyo, kuwa vitu vingine, jamaa anawadanganya wazungu kupitia media zao za kibeberu, watu wake watakushukia kwa matusi as if umemkufuru mungu wao!.

Naomba kwanza nikuwekee makala yenyewe, na wewe ujisomee uone tunavyoanza kusingiziwa uongo, na kwa faida ya wale wenzangu na mimi ambao hizi kwao ni lugha za watu, nitawachambulia huyo samaki aliyeoza katika tenga hili ni yupi.

Tanzanian Opposition Leader Leaves Country After Police Bar Protest​

Tundu Lissu, an opposition leader, had called for protests after the country’s October presidential election was marred by allegations of fraud.

merlin_179204742_a154a57a-e3b8-46b6-ba9b-77171a4c9a7a-articleLarge.jpg

Tundu Lissu casting his vote last month in the town of Ikungi, in the Singida Region, of north Tanzania.Credit...Associated Press
By The Associated Press
  • Nov. 10, 2020
DODOMA, Tanzania — Escorted by Western diplomats, Tanzania’s main opposition candidate left the country for Belgium on Tuesday after rejecting a presidential election he asserted had widespread irregularities.
“I am not fleeing the country,” said the candidate, Tundu Lissu, who was escorted at the airport by ambassadors from the United States, Germany and Belgium. “I am only going to explore different platforms to reclaim justice, democracy and dignity of Tanzanians.”
Mr. Lissu survived an assassination attempt in 2017. He returned to Tanzania this year from Belgium to challenge the country’s president, John Magufuli, a populist who won a second term in October.
Mr. Lissu and other opposition leaders had urged citizens into the streets for an “endless peaceful demonstration” over the Oct. 28 election, in which widespread fraud was alleged and many observers were barred. But police blocked the protest.

The opposition leader had been housed at the German embassy since Nov. 2, when he was released by police after hours of interrogation.

The United States and others noted credible allegations that called the vote’s results — and the East African country’s democratic ideals — into question. Allegations included the rejection of thousands of election observers, a massive slowdown in internet and text-messaging services and ballot box stuffing.

Several opposition leaders were arrested or beaten or both around the vote. The chairman of the Chadema opposition party, Freeman Mbowe, and two other Chadema leaders were charged with “terrorism-related offenses.”
Mr. Magufuli later noted “a few challenges” around the election but called it generally peaceful. The government has denied any cases of intimidation.

On Tuesday the United Nations human rights chief, Michelle Bachelet, said in a statement that she was “disturbed by reports of continued intimidation and harassment against opposition leaders and members in Tanzania” after the vote.
The statement added: “Reports indicate that at least 150 opposition leaders and members have been arrested since 27 October in mainland Tanzania and in Zanzibar. While most have been subsequently released, at least 18 reportedly remain in custody.”
She said those detained for exercising their human rights should be released.
Tanzania’s Election
Hii ni story ya pili kwa The New York Times kuizungumzia Tanzania within one week, story ya kwanza ni hii
As Tanzania’s President Wins a Second Term, Opposition Calls for Protests
Oct. 31, 2l020


Uongo katika story ni kuhusu kufungwa kwa SMS, japo ni kweli wakati wa kipindi cha uchaguzi Mkuu wa Tanzania, kutokana na Watanzania wengi kuwa na simu janja na kila mwenye simu janja akanunua bundle ili kufuatilia uchaguzi kwa kutumia simu yake kwa mtandao wa internet, masikini mtandao wa internet ghafla ukaelemewa hivyo ukawa slow na sometimes ukawa haupatikani, hivyo watumiaji wa WhatsApp, Facebook, Twitter, YouTube etc ikawa haipatikani kirahisi, lakini SMS zilikuwa zinapatikana kama kawaida kwasababu SMS hazitumii internet hivyo mtu huhitaji kuwa na bundle kutuma au kupokea SMS!, hivyo walioathirika na go slow hiyo ya internet ni Watanzania matajiri na vipato vya kati wenye uwezo wa kumiliki simu janja, na huduma zilizotegemea internet ya mitandao ya simu, lakini kwa taasisi zinazotumia private network, VPN, hazikuathirika, na Watanzania walio wengi wanaotumia simu za vitochi, wao waliendelea kudunda tuu as if nothing happened!, hivyo hawa New York Times ni waongo!. Uongo ndio huo mmoja tuu!.

Aliefile hii story kutoka Tanzania ni shirika la habari la AP. Kwa vile mimi ni mwandishi, na kwenye uandishi tulifundwa darasani ukipata story from a single source, kabla hujai publish, editor unapaswa kui verify kwa kufanya kitu kinachoitwa double checking na cross checking kwa watu wengine zaidi ya huyo single source wao, and it was as simple as ABC, unampigia mtu mwingine yoyote aliyeko Tanzania, una verify uliyoambiwa na source wako, jee ni kweli internet was down? Je, hata SMS? Wangepata majibu!.

Uongo kuhusu kutopatikana mawasiliano ya SMS ndio samaki mmoja aliyeoza, katika hili tenga la samaki wa story ya The New York Times kuhusu uchaguzi Mkuu wa Tanzania.

My Take
Kwa kawaida siku zote mimi huwa nashauri uongo ukisemwa na kuachwa kurudiwa rudiwa bila kukanushwa, siku moja utageuka ukweli, lakini kwa makala hii, sishauri tukanushe uongo huu mdogo kuhusu SMS tuu, huu ni wa kuu puuzia tuu, maana kukanusha uongo wa gazeti kama The New York Times, ni kama kufungua the Pandora Box, kunaweza kufumka mavitu ya ajabu!.

Don't underestimate the powers of media, magazeti ya Marekani!. The Washington Post, limewahi kuandika story ya kashfa ya Watergate, ikampopoa rais wa Marekani toka White House, ikulu akaiona chungu, akabwaga manyanga na kuachia ngazi!.

Hata magazeti yetu, japo mengi ni ya kufungia samaki, lakini kwa mahitaji yetu ya Tanzania na uzalendo!, hakuna gazeti Tanzania linaweza kusema uchaguzi Mkuu haukuwa huru na wa haki, kwa mujibu wa magazeti yetu, uchaguzi mkuu wetu, licha ya kukabiliwa na dosari ndogo ndogo, uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, walioshinda wameshinda kwa haki na kihalali, walioshindwa wameshindwa kwa haki na kihalali, wakubali matokeo, uchaguzi sasa umekwisha , kazi iliyo mbele yetu ni kazi moja tuu, kuijenga Tanzania.

Namalizia na lile swali la msingi la bandiko hili kuwa Gazeti la The New York Times, la Marekani, ambalo ni la tatu kwa ukubwa wa kusomwa sana duniani, lasambaza uongo kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, ladai haukuwa huru na wa haki!, Je ni kweli tunyamaze tuu au ni uongo tukanushe?.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
 
We jamaa hata utumie miaka 100 kusifia uongo na udikteta, kamwe hautapata uteuzi hata kuwa balozi wa nyumba 10.

Na watu kama nyingi ndio mnaompoteza kaisari kwa kusifia hata visivyosifika, hata mambo anayoamini mabaya kwa taifa nyinyi ndio mnamfanya apoteze dira na kuona mazuri. Kwasababu ya tamaa ya kupata uteuzi.

Kwa mtu yoyote mzima wa akili anajua uchaguzi huu haukua wa haki, hata kwa wana ccm wenyewe (Wakiongozwa na "Mnadhimu Mkuu Wa Uongo, Unafiki & Uzandiki - Prof Polepole") na vyombo vya usalama wanajua uchaguzi haukua wa haki.

Na hata Rais mwenyewe anajua uchaguzi huu haukua wa haki.

Uchaguzi kama ulikua wa "HAKI & MLISHINDA KWA KISHINDO" kwanini mlifunga "INTERNET" na "SMS KUWA SENSORED (Zenye neno Lissu/Tundu Lissu)"? Mlikua mnaogopa nini?

Mshindi anaanzaje kuogopa?Mtenda haki anaanzaje kuogopa?
 
Fanya kazi mzee kwani ushasikia Biden anafuatilia kilichoandikwa na Mwanahalisi...Kikubwa cha kujifunza ni kusimamia tunachoamini ...kelele za chura haziwezi mzuia tembo kunywa maji
Sisimizi aliweza kumuua tembo. Sisimizi alichoshwa na uonevu wa kukanyagwa na tembo. Aliingia kwenye mkonga wa tembo na kuanza ziara zisizo rasmi. Ziara hizi zilimkera sana tembo.Katika harakati za kumtoa sisimizi tembo alijipiga kwenye mwamba na kudhurika vibaya.
 
Sisiminzi aliweza kummua tembo. Sisiminzi alichishwa na uonevu wa kukanyagwa na tembo. Aliingia kwenye Mekong’s wa tembo na kuanza ziara sisizo rasmi. Ziara hizi zilimkere sana tembo.Katika harakati za kumtoa sisiminzi tembo alijipiga kwenye mwamba na kudhurika vibaya.
Hivi hii ndo ile kanuni ya dua ya kuku sio ah ah.
 
Siku zote nimekuwa natetea sisiemu huwa hawaibi kura.

ILS huu wa wakati huu kitendo cha kuona karatasi nyeti kama ya kura kwenye clips za video mitaani nimeogopa sana.

Kama zinatengenezwa na wapinzani kwa ajili ya propaganda, basi TISS ilipaswa iundwe upya kwa kushindwa kukusanya intelligence na kuzuai hilo. Kitendo cha licha ya kuonekana mitaani na hakuna hata mtu aliyekamatwa na kushtakiwa, tena clip moja mlalamikaji akiwa ameshika hayo makaratasi ya kura zilizopigwa mbele ya Polisi zimenifanya niogope siasa na utaratibu wetu wa kutoa haki.

Kikubwa naomba Amani ktk ya dhuruma
 
Kuzima internet
Kamatakamata ya wapinzani
Kuwazuia mawakala wa vyama pinzani
Kupita bila kupingwa

Kufanana kwa matokeo ya majimbo
Ccm kushinda majimbo yote Hali walikuwa wakipiga magoti kuomba kura

Ushiriki wa polisi kuisaidia ccm
Kuuwawa kwa watz Zanzibar, Tarime, Tunduma, Rorya, nk.

Kuzuia vyombo vya habari visiripoti upinzani
.nk
Hizi ni kasoro za uchaguzi
 
Back
Top Bottom