The New Tanzania "SHADOW CABINET"

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
Mawaziri kivuli watangazwa

2008-02-15 09:21:20
Na Frank Mbunda, Dodoma


Kufuatia Rais Jakaya Kikwete, kulivunja Baraza la Mawaziri wiki iliyopita, Kambi ya Upinzani Bungeni nayo imetangaza majina ya mawaziri vivuli wanataoshirikiana na serikali.

Hayo yalielezwa na Kiongozi wa Kambi hiyo Bungeni, Bw. Hamad Rashid Mohammed, alipozungumza na waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa Bw. Hamad, Bw. Shoka Kahmis Juma, atakuwa waziri kivuli Ofisi ya Rais Utawala Bora, wakati Bi. Grace Kiwelu atakuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Bw. Chacha Wangwe ataongoza wizara ya Mazingira katika Ofisi ya Makamu, wakati Bi. Riziki Omar Juma atakuwa waziri kivuli (Muungano).

Kwa mujibu wa Bw. Hamad, Dk. Ali Tarab Ali atakuwa waziri kivuli wa Afya na Ustawi wa Jamii akisaidiwa na Omar Ali Mzee.

Bw. John Cheyo atakuwa waziri kivuli wa Ardhi akisaidiwa na Bw. Ali Said Salim na Bw. Suzan Lyimo akipewa kazi za kusimamia kazi kama waziri kivuli wa wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, akisaidiwa na Bi. Nuru Awadh Bafadhil.

Kutokana na mabadiliko ya wizara yaliyofanywa na Rais Kikwete, kambi ya upinzani bungeni pia imemteua Bw. Said Amour Arfi, kuwa waziri kivuli wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, wakati Bw. Zitto Kabwe ameteuliwa kushika wizara ya Miundombinu akisaidiwa na Bw. Kabar Shamis Faki.

Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo itaongozwa na Bi. Mwanawetu Said Zarafi, akisaidiwa na Mohamed Ali Said, wakati Bw. Salim Abdulla Khalfani, atakuwa waziri kivuli wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana.

Wizara ya Maji na Umwagiliaji itaongozwa na Bi. Mhonga Said Ruhwanga akisaidiwa na Bi. Mkiwa Adam Kiwanga, wakati Bw. Salim Hemed Khamis atakuwa waziri kivuli wa Kilimo, Chakula na Ushirika akisaidiwa na Bw. Juma Said Omar.

Kwa mujibu wa Bw. Hamad, Bibi. Maulidah Anna Komu atakuwa waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia na watoto, wakati Bw. Mwadini Abbas Jecha, ataongoza wizara ya Mifugo na Uvuvi, akisaidiwa Bw. Ali Khamis Seif.

Wizara ya Maliasili na Utalii itasimamiwa na Bi. Magdalena Sakaya, atakuwa waziri kivuli wa Maliasili na Utalii, wakati Muhammad Ibrahim Sanya, atakuwa waziri kivuli wa Mambo ya Ndani ya Nchi na wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa ikiachwa kwa Bw. Khalifa S. Khalifa.

Wizara ya Nishati na Madini itasimamiwa na Bw. Mohamed Habib Juma Mnyaa, akisaidiwa na Bi. Savelina Mwijage, wakati Bi. Fatuma Maghimbi, akipewa kazi ya kusimamia wizara ya Katiba na Sheria.

Katika hali hiyo Bw. Masoud Abdula Salim, amepewa kazi ya kuwa waziri kivuli wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, wakati Bw. Abuubakary Khamis Bakari, atakuwa waziri kivuli wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Bi. Lucy Owenya atakuwa waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko akisaidiwa na Bi. Khadija Salum Alli.

Kwa mujibu wa mabadiliko hayo, yeye mwenyewe ataongoza wizara ya Fedha na Uchumi, akisaidiwa na Bi. Fatma Fereji, wakati Dk. Wilbrod Slaa, atakuwa waziri kivuli ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, akisaidiwa na Bi. Ania Chaurembo.

Kwa mujibu wa Bw. Hamad, Bi. Halima Mdee, atakuwa waziri kivuli Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge.

Wakati huo huo, Bw. Hamad aliiomba serikali kuiongezea uwezo kambi hiyo ili iweze kufanya kazi zake kwa ufanisi.

Kulingana na Bw. Hamad, kazi za kambi hiyo kwa sasa zinakwamishwa na uchache wa vitendea kazi na kukosekana kwa ofisi kwa mawaziri vivuli wa kambi hiyo.

``Kama mnavyofahamu hawa muda wote wapo hapa katika ofisi ya Dk. Slaa, au pale kwangu, hivyo ni vigumu kufanya kazi zao kikamilifu, tunaiomba serikali kupitia ofisi ya Spika kutambua hali hiyo,`` alisema Bw. Hamad.

SOURCE: Nipashe
Source link: IppMedia.

SteveD.
 
Hapa naona wameamua kumweka Zitto miundombinu ili akapambane na Chenge na hapo patawaka mioto bila shaka.

Nawatakia kila la kheri na naamini kuwa wataendelea kutoa changamoto kwa ajili ya ujenzi wa taifa hili.
 
Hapa naona wameamua kumweka Zitto miundombinu ili akapambane na Chenge na hapo patawaka mioto bila shaka.

Nawatakia kila la kheri na naamini kuwa wataendelea kutoa changamoto kwa ajili ya ujenzi wa taifa hili.


Fedha kapewa nani? Pale nako kuna issue nzito pale .Huyu jamaa sijui Makullo huyo anapashwa kukabwa koo all the time
 
Lunyungu.Fedha yupo Hamad Rashid.nafikiri yeye alishafanya kazi wizara ya fedha...kama kuna comments zozote Zitto anaweza kutuambia..
Sina Hakika kama Hawa mawaziri vivuli wanalipwa posho au ni sehem tu utamaduni wa kuwa na Vivuli...
Kwa maoni yangu ni kuwa LETS WORK as a TEAM...
 
Back
Top Bottom