The most educated tribe

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Nilikuwa na tafuta taarifa fulani kuhusu Mkoa wa Ruvuma kupitia mtandao nikakutana na tovuti zaidi ya tatu zinaelezea kabila la watu wasomi zaidi hili:
<H1 class=firstHeading>Ruvuma


Ruvuma is a region in Tanzania. Ruvuma has a lot of tribes. The most educated is the Wanyasa from Mbamba Bay along Lake Nyasa, especially from Linda Village.

Tovuti husika ni:
  1. http://www.chemistrydaily.com/chemistry/Ruvuma
  2. http://www.economicexpert.com/a/Ruvuma.htm
  3. http://fact-archive.com/encyclopedia/Ruvuma
  4. http://www.music.us/education/R/Ruvuma.htm

Sina uhakika sana kuhusu taarifa hizi ambayo ipo kwenye tovuti karibia tatu kwa kuwa nimeshindwa kupata kwa kina uthibitsiho. Na kwa mtazamo wangu, hata katika maeneo husika tofauti na ilivyokuwa zaman, hakuna kumbukumbu zozote za kujua takwimu halisi za wasomi au nasaba ya vizazi (family tree).

Na kwa kuwa taarifa kama hizi za kihistoria zinawekwa kwenye kumbukumbu za mtandao (zinazosomwa kote duniani) kwa makusudi maalumu ambavyo kimsingi ni vizuri zikapata uthibitisho wa kina ikiwemo vigezo.

Je, historia yetu inapotea kutokana na kukua kwa teknologia?...Kwa mtazamo wangu kungekuwa na jitihada za makusudi kwa maeneo husika kufuatilia kwa kina na kutunza kumbukumbu muhimu ili hata dhana ya kuwepo kwa makumbusho yetu iwe na mantiki.
 
its very true Ngoswe,thats my tribe wengi wao wanajiita wangoni just because wanyasa ni wachache pande za kule,but kuna viongozi wengi tu walitokea huko,pia hawa jamaa wanasifa ya usafi sana hasa ukiwaona kwenye ngo'oma ya mganda wakiwa wamevaa kaptula nyeupe na sharti nyeupe na soksi,ALWAYS SMART MPAKA UP STEAZ
 
Your heading has to be changed to.."Most educated tribe in RUVUMA region...! of which i see is NO WONDER!...right?
 
dude,
ki-blurei kimezidi hapo...!umeniacha
SIRUDII TENA MDOGO WANGU... NADHANI NIMEANDIKA NIKIWA KWENYE TAHAYARI....

ni basi tu nasikitika kuona bado kunajaribu kuibua ishu za ukabila hiki, ukabila kile... kuna siku itakuja hapa kabila lenye kengele kubwa kuliko wenzao... sijui tutasema nini!!
 
very irritating indeed.... Tribalism!!! An indication of a desperate community lifting some shoulders

Naona wengi wenu mmekuwa na hisia zaa "ukabila" zaidi kuliko ambacho nilitaka nimaanisahe hapa.Labda kama tunatofautiana hisia na uelewa, kuataja, kusifia kabila fulani sidahni kama ni ukabila!.

Binafsi sitetei ukabila na pia kutokuwa mkabila haimanjisni sina kabila na kuwa taifa haina maana dhana ya kuwa wa kabila fulani inafutika vinginevyo tusingeongea lugha za makabila wala kujitambulisha asili zetu za kikoo, kitamaduni, mila na desturi za kule tutokako.

Ipo historia mzuri kabisa kuhusu "makabila ya kitanzania na mengine ya Afrika kwenye vitabu na kumbukumbu za kale kama vile kiatbu cha "Zamani Mpaka Siku hizi" . Katika maandhish hayo, unasoma kusifiwa au kukashfiwa kwa makabila fulani kutaoka na aina za utamaduni na maisha waliyoishi enzi hizo. Hata hivyo maandishi hayo, haya maanishi ukabila bali kuelezea hali halisi ya kabila husika. Tukisema kwa mfano wahaya wanapenda sana kuongea lugha ya kwao, hii haimannisha wahaya ni wakabila kwani wasipofanya hivyo, hawawezi kuitwa tena wahaya, kwani wanaitwa wahaya kutokana na hilo kabila.

Kwa mfano tukiseme kabila la Wahehe, Wanyamwezi na Wangoni ndiyo yenye msimamo mkali zaidi katika makabila yote Tanganyika kwa kurejea vita dhidi ya kutawaliwa na Mjerumani, haimaanishi kutaja makabila hayao ni ukabila, hii ni hali halisi kwa mujibu wa historia ya Makabila husika na ukweli huu hauwezi kufutikwa millele hata Taizania ikiwa nchi yenye kabila moja!.

Turudi kwenye mada na kuelewa mantiki, sina dhamira ya ukabila hapa bali ni kuangalia kama upo uwezekano wa kila kabila kutunza kumbukmbu zake katika kizazi hiki kama ilivyokuwa zamani na wote tumezikuta hizo histioria na ndizo zatufanya leo tujiite "sisi ni wakabila fulani" na tuliwa pamoja kama hap kwenye JF twasema sisi ni wataifa fulani (utaifa na ukabila ni sawa) . Makabila ni tofauti na ukabila, Makabila ndi yanajenga "Taifa"na badaae "Mataifa".
 
its very true Ngoswe,thats my tribe wengi wao wanajiita wangoni just because wanyasa ni wachache pande za kule,but kuna viongozi wengi tu walitokea huko,pia hawa jamaa wanasifa ya usafi sana hasa ukiwaona kwenye ngo'oma ya mganda wakiwa wamevaa kaptula nyeupe na sharti nyeupe na soksi,ALWAYS SMART MPAKA UP STEAZ

BWANJI PEAL, YOU MEAN THIS



IMG_8388.JPG




IMG_8543.JPG



Wanafunzi wa shule ya msingi ya Matarawe iliyoko katika mji wa Songea wakicheza ngoma ya mganda kumkaribisha Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete wakati akikagua kazi mbalimbali za wajasiriamali wa mjini Songea katika siku ya pili ya ziara yake mkoani Ruvum
http://mawasilianoikulu.blogspot.com/2009_11_01_archive.html
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=otjzqEEDZPw[/ame]

OR

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=KyKVCF08O3E[/ame]
 
Nilikuwa na tafuta taarifa fulani kuhusu Mkoa wa Ruvuma kupitia mtandao nikakutana na tovuti zaidi ya tatu zinaelezea kabila la watu wasomi zaidi hili:


Sina uhakika sana kuhusu taarifa hizi ambayo ipo kwenye tovuti karibia tatu kwa kuwa nimeshindwa kupata kwa kina uthibitsiho. Na kwa mtazamo wangu, hata katika maeneo husika tofauti na ilivyokuwa zaman, hakuna kumbukumbu zozote za kujua takwimu halisi za wasomi au nasaba ya vizazi (family tree).

Na kwa kuwa taarifa kama hizi za kihistoria zinawekwa kwenye kumbukumbu za mtandao (zinazosomwa kote duniani) kwa makusudi maalumu ambavyo kimsingi ni vizuri zikapata uthibitisho wa kina ikiwemo vigezo.

Je, historia yetu inapotea kutokana na kukua kwa teknologia?...Kwa mtazamo wangu kungekuwa na jitihada za makusudi kwa maeneo husika kufuatilia kwa kina na kutunza kumbukumbu muhimu ili hata dhana ya kuwepo kwa makumbusho yetu iwe na mantiki.

Bwana Ngoswe sielewi unataka kuachive nini ktk hii thread.

Kwanza unasema huna uhakika na hizi tovuti zako, hivyo huezi sema uko objective.

Labda ni rahisi kujua kwamba hii sentensi imekopiwa kutoka sehemu moja tu na wengine wakaichukua nzimanzima huhitaji kuwa theoretical Physicists (kama mimi ambaye si Mnyasa hata hivo he he he..) kujua kwamba kulikuwa na chanzo kimoja tu na wengine wakaichukua hiyo sentensi bila kui-edit.

Ruvuma is a region in Tanzania. Ruvuma has a lot of tribes. The most educated is the Wanyasa from Mbamba Bay along Lake Nyasa, especially from Linda Village.
..and it doesn't take an astrophysicist kujua kwamba original author wa hio garbage anatokea kijiji cha Linda huko Mbamba Bay bin Bomba Mbili ..

Anyways, my point is to free urself from prejudices ni kwamba maarifa hayapo entitlted kwa kikundi fulani tu cha watu, maarifa ni kwa wote kwa sababu binadamu wote ni sawa(refer imani ya wanaTANU) tunatofautiana tu vinasaba.Sio upstairs I mean inter-kabilakally.

Ukianza kuassociate maarifa na ukabila utafeli and you will never be objective enough, maana siku hizi watu wameoana(kuzaana to be precise) toka makabila chungu mzima, mfano my stepbrothers & sisters wana jumla ya makabila 5 kibindoni na watoto wao wako na makabila ova 7+, sasa mfano mmoja wa hao manephew wangu akiwa mwanasayansi wa NASA au engineer wa AIRBUS utaasema amechukuaga akili ya nani??

Save your time kwa mambo ya maana.
 
Abdulhalim you are so https://jamii.app/JFUserGuide'n educated but you got issues kweli vile. whats your problem money honestly kuanzia leo im on ya case
 
Nilikuwa na tafuta taarifa fulani kuhusu Mkoa wa Ruvuma kupitia mtandao
Sina uhakika sana kuhusu taarifa hizi .
Ngoshwe, kwa kuwa ulikuwa unatafuta taarifa fulani kuhusu mkoa wa Ruvuma, headline yako ingesomeka "The Most Educated Tribe in Ruvuma", kitendo cha kuiacha bila kutaja Ruvuma, kunamaanisha Tanzania in general.

Nikirudi kwenye hizo kuhusu Ruvuma, ni kweli most educated ni Wanyasa simply because wamesoma Malawi. Ni kweli they are smart upstairs, na wako very organized and trustworthy, wakati wa ukoloni, ndio waiokomba kazi zote za ukarani humu nchini na kuishia kulowea.

Ukigoogle, the most educated tribe in Tanzania, matokeo ni haya:-
<LI class=g>tribes in Tanzania - the Chaggas

- [ Tafsiri ukurasa huu ] 26 Nov 2008 ... Indeed, the Chagga are the one tribe you're almost guaranteed to meet in even the most obscure corners of Tanzania, working as traders, ...
www.tanzania-adventure.com/tribe-chagga.htm - Zilizo kwenye kache - [ame="http://www.google.co.tz/search?hl=sw&q=related:www.tanzania-adventure.com/tribe-chagga.htm+most+educated+tribe+in+Tanzania&sa=X&ei=Swh-S4KTEcuVtge7-tWxDw&ved=0CAkQHzAA"]Zinazofanana:[/ame]
<LI class=g>
Tanzania Travel Blogs - TravelPod


<LI class=g> - [ Tafsiri ukurasa huu ] He also said that the Chagga are the "most educated" of the 100+ tribes in Tanzania and that they're smart business people. The Mount Kilimanjaro remained ...
www.travelpod.com/blogs/.../Tanzania.html - Zilizo kwenye kache
<LI class=g>This is a fact, wakifuatiwa na Wahaya, Wanyakyusa na Wasukuma, wakifuatiwa na Iringa, etc. Tikija kwa walosoma sana, Wahaya ndio wanaongoza kwa idadi ya ma profesa na Ma Ph.D holders.
Makabila hayo yameweza kusoma sana kutokana na mikoa yao kuwa na mazao ya biashara, Kahawa kwa Moshi, Bokoba na Mbeya, Pamba Mwanza, na Chai Iringa.

Kuwepo kwa mazao hayo ya biashara kulipelekea makabila hayo kuwa na uwezo wa kulipia ada ya mkoloni, mikoa ambayo haikubahatika kuwa na mazao ya biashara, shule za Misheni ndio mkombozi wao.

Hata hivyo, makabila yenye wasomi wengi, haimaanishi ndio wenye akili sana, kuna vichwa vigi tuu maeneo ambayo hawakuwa na mazao ya biashara.

Angalizo, kuna baadhi ya maeneo, ni wazito kidogo kwenye kupokea elimu na maeneo mengine ni wepesi zaidi, baada ya uhuru, tuliendelea na system ya elimu ya mkoloni kwa kufanya mtihani mmoja Tanzania nzima, Cambridge. Tukajikuta wanaopasi kuingia sekondari ni makabila fulani fulani tuu, hivyo Nyerere aliliona hili na kubadili mfumo kwa kila mkoa kuwa na passd rate yake kuingia sekondari ili Watanzania wote wapate fursa sawa.

Mpaka kesho, cut off point ya Kanda ya Kaskazini ni juu ikifuatiwa na Kanda ya Ziwa, the lowest ni Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, ikifuatiwa na Kanda ya Kati.

Haukuna ubaya kuuzungumzia ukabila ili yale mazuri ya makabila yetu tuyatumie positively na yale mabaya tuyaepuke.

Kuna makabila wanapenda sana maendeleo na kuna wapenda ngoma, kuna makabila wanaongoza kwa kupenda na mlolongo wa vimada, kuna makabila hawajui kusema hapana, kuna makabila ni wakatili, wako wachoyo, wako waosema sana, yako makabila ya wachapa kazi, kuna makabila yana wezi sana, wako wanawake wa makabila fulani huongoza kwa kupenda pesa, wengine kupenda game, wengine kufanya biashara, wengine wana wivu sana, etc, etc, kuyazungumza haya in a contructive way sio ukabila.
 
Your heading has to be changed to.."Most educated tribe in RUVUMA region...! of which i see is NO WONDER!...right?
Bravo. Sijui Ngoshwe kakurupuka? Alikuwa anatafuta mkoa wa Ruvuma na wala sio Kanda au Taifa. Nshomile sana je, yuko Nyasa? Hicho kijiji kina watu wangapi wanakotoka wasomi wengi zaidi mkoani Ruvuma? Try to be realistic, hata ukisema Kabila lililo na wasomi zaidi Tanzania ukiniambia ni wachaga nitakubali kwa records kwamba Kilimanjaro inazo shule nyingi sana za msingi na sekondari, karibu kila kijiji. Lakini utafiti huo kama ni utafiti kweli, unayo tija gani tukifahamu? Tunashindanisha makabila kielimu? Kila kabila lina identity yake lakini hatupendelei kuendekeza hayo bali umoja wa kitaifa. Tungekubali kuishi kama Rwanda na Burundi na Kenya isingekuwa salama mtu kufanya vitu vyake vya kimaendeleo nje ya kijiji chake. Huoni Mara wanaoendekeza vita za koo, maendeleo yao yakoje ukilinganisha na penginepo pasipokuwapo hayo?
 
Back
Top Bottom