The Monitoring Thread - Prime Minister & Ministers!

M

MegaPyne

Guest
On our ongoing "Monitoring Thread" Series, (We have the JK Version) this is Prime Minister Mizengo Pinda and his/her ministers monitoring thread. We are going to try and track down all they do and give you updates. We 'll try to update it regularly


Here we start...


0150 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Ahmed Shaker (kulia), Kiongozi wa Maonyesho katika banda la Kampuni ya Arab Authority for Agricultural Investment and Development, (AAAID) kutoka Dubai baada ya kufungua Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara, barabra ya Kilwa jijini Dar es salaam Julai 1, 2008. Kushoto ni Thani Zayid Alghelani pia wa AAAID. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

0151 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama moja ya bidhaa katika banda la Kampuni ya Arab Authority for Agricultural Investment and Development (AAAID) kutoka Dubai baada ya kufungua Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara, barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam Julai 1, 2008. Kulia ni Kiongozi wa Maonyesho katika banda hilo, Ahmed Shaker na kuhoto ni Msaidizi wake, Thani Zayid Alghelani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

9915 Meya wa Manispaa ya Kigoma/ Ujiji, Nashon Bindyanguze wa CCM (kulia) akikumbatiana na meya aliyemealiza muda wake, Kitita Magonjwa wa CHADEMA baada ya makabidhiano ya umeya wa manispaa hiyo yaliyoongozwa na Waziri Mkuu , Mizengo Pinda kwenye viwanja vya Manispaa ya Kigoma/Ujiji Juni 30,2008. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

9931 Meya wa Manispaa ya Kigoma /Ujiji Nashon Bindyanguze akiwasilimi wananchi baada ya kukabidhiwa umeya wa manispaa hiyo na meya aliyemaliza muda wake, Kitita Magonjwa wa CHADEMA katika makabidhiano ya umeya yaliyoongozwa na Waziri Mkuu MizengoPinda kwenye viwanja vya Manispaa hiyo mjini Kigoma Juni 30, 2008. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 

Attachments

  • IMG_9931.JPG
    IMG_9931.JPG
    448.5 KB · Views: 77
  • IMG_0151.JPG
    IMG_0151.JPG
    454.3 KB · Views: 71
  • IMG_9915.JPG
    IMG_9915.JPG
    348.9 KB · Views: 69
  • IMG_0150.JPG
    IMG_0150.JPG
    359.2 KB · Views: 61
RAIS KUFUOR ATAKA NCHI ACP ZIJALI VIJANA


RAIS WA GHANA, John Kufuor amezitaka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika, Caribbean na Pacific (ACP) zitafute mtazamo mpya kwenye masuala ya maendeleo na usalama ili vijana wa nchi hizi waweze kuwa makini na wajiamini.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Alhamisi Oktoba 2, 2008) wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa Wakuu wa Nchi za jumuiya hiyo unaofanyika Accra, Ghana.

Rais Kufuor ambaye ameshika uenyekiti wa jumuiya hiyo kuanzia leo, amesema wajumbe wa mkutano wa sita wa ACP wanapaswa kuangalia ni kwa jinsi gani wanaweza kuafikiana juu ya kuwepo kwa mifumo ya biashara ya kimataifa yenye usawa ambayo itasadia kukuza uchumi wa nchi maskini.

“Ili kuhakikisha vijana ambao ni taifa la kesho wanalelewa na kuingia kwenye mifumo ya utandawazi kwa umakini na kujiamini, nchi wanachama wa mkutano huu hazina budi kuazimia kuboresha sekta muhimu za kijamii hasa elimu, huduma za afya na mawasiliano ambazo zinaathiri moja kwa moja wananchi na maisha yao ya kila siku,” alisema.

Amesema inasikitisha kwamba majukumu yote haya yameachiwa kwa Serikali za nchi husika ili zijitegemee kuhakikisha watu wake wanapata maendeleo na wanaishi kwa usalama kwa sababu misaada inayotolewa ni finyu na haisaidii kuunga mkono juhudi za kujenga uchumi na maendeleo ya wakazi wa nchi husika.

“Misaada inayotolewa hivi sasa inafanywa kama sadaka badala ya kuwa chachu ya kukuza uchumi na ndiyo maana imekuwa haitoshelezi mahitaji, haitolewi kwa wakati inapohitajika na hairatibiwi vizuri ili izibe mapengo ya kiuchumi yanayozikabili nchi zetu …. Misaada tunayopewa haisaidii kupunguza matatizo yetu ya umaskini, ukosefu wa ajira na kiwango kikubwa cha maradhi na ujinga,” alisema.

Amewataka wanachama wa nchi hizo waangalie kwa undani masuala ya mazingira, mabadiliko ya hali ya hewa, uhamiaji, kupanda kwa bei za vyakula na bei za mafuta pamoja na Makubaliano ya Ushirikiano wa Kiuchumi (EPA).

Mapema, Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Rais Omar El Bashir wa Sudan amesema kuongezeka kwa bei za vyakula katika nchi wanachama wa ACP kutaleta changamoto kwa nchi kushindwa kufikia malengo ya milenia kama ilivyoazimiwa kuwa yawe yametekelezwa ifikapo mwaka 2015.

Akigusia suala la Darfur, amesema taasisi za kimatifa zisitumiwe kama silaha ya kuendeleza ukoloni mamboleo.

Amesema nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, zinapaswa kujifunza kutokana na matukio mbalimbali yanayoendelea kulikumba eneo hilo kama vile, vimbunga, mafuriko na uharibifu wa mazingira unaosababisha jangwa na kuyachukulia kama changamoto za kutambua udhaifu wao katika karne ya 21.

Mkutano huo unaendelea leo mchana ambapo Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kutoa hotuba fupi.
 
WAZIRI MKUU AENDESHA HARAMBEE YA PAPO HAPO IRINGA


WAZIRI MKUU Mizengo Pinda leo (Jumatano, Oktoba 15, 2008) ameendesha harambee ya papo kwa papo na kukusanya sh. milioni 11.5 ili kusaidia ununuzi wa fimbo nyeupe kwa ajili ya walemavu wasioona zenye thamani ya sh. 20,000 kila moja.

Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Fimbo Nyeupe yaliyofanyika kitaifa mkoani Iringa alisema amelazimika kuchukua hatua hiyo ili kupunguza tatizo la ukosefu wa fimbo hizo linalowakabili walemavu hao.

Kati ya fedha hizo ambazo yeye mwenyewe alichangia sh. milioni 5, sh. milioni 3.525 ni fedha taslimu na sh. milioni 8.090 zilizobaki ni ahadi, zilitolewa na viongozi mbalimbali na watu waliofika kwenye Bustani ya manispaa kuhudhuria sherehe hizo.

Mapema akiwahutubia wananchi wa mji huo, Waziri Mkuu amewataka wajasiriamali wote wenye ulemavu wajiunge pamoja na kuanzisha SACCOS zao ili waweze kukopeshwa.

Alisema: “Niliwahi kuona kazi za mikono za wajasiriamali wenye ulemavu nchini ambazo zinatia moyo. Ninawapongeza wajasiriamali wote wenye ulemavu ambao wamejituma kufanya kazi licha ya hali zao za kimaumbile. Wengi wao wamekuwa na nia kubwa ya kujikomboa kutoka katika hali duni ya umaskini. Natoa wito kwamba wajasiriamali wote mjiunge pamoja na kuanzisha SACCOs zenu ili nanyi muweze kukopeshwa.”

Waziri Mkuu aliwataka wataalam wa ushirika wachukue jukumu la kuwasaidia watu wenye ulemavu wakiwemo wasioona katika kuanzisha Vyama vya Akiba na Kukopa (SACCOS) kwa sababu Serikali inalo jukumu la kuhakikisha watu wenye Ulemavu nao wanashiriki kikamilifu katika kujitafutia maisha bora kama walivyo wananchi wengine wasio na ulemavu.

Akizungumzia kuhusu Sera ya Taifa ya Maendeleo na Huduma kwa Watu wenye Ulemavu, Waziri Mkuu aliiagiza Tume ya Kudhibiti UKIMWI nchini (TACAIDS) ishirikiane na Halmashauri zote nchini kuviwezesha Vyama vya Watu wenye Ulemavu kutoa mafunzo dhidi ya UKIMWI kwa wanachama wao na kwa watu wenye Ulemavu kwa ujumla.

Pia alimtaka Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Prof. David Mwakyusa alifanyie kazi suala hilo na ampatie taarifa ya namna suala hili la kutoa Elimu ya UKIMWI kwa Watu Wenye Ulemavu linavyotekelezwa.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Prof. Mwakyusa alisema licha ya mapungufu ya kimaumbile yanayoambatana na ulemavu, watu wenye ulemavu wakiwamo wasioona ni rasilmali, nguvu kazi, na hazina ambayo haijatambulika na kutumiwa ipasavyo kwa ajili ya maendeleoa yao wenyewe nay a jamii.

Alisema upo umuhimu wa kutambua vipaji maalum vya watu wenye ulemavu na kuviwekea mikakati madhubuti ya kuviendeleza ili waweze kujitegemea na kuondokana na utegemezi au kuwa ombaomba, hali ambayo itawafanya wachangie katika maendeleo na uchumi wa Taifa.

Lengo la kuadhimisha siku hii ya Fimbo Nyeupe ni kuihamasisha Serikali, jamii na wadau mbalimbali kutambua uwezo wa wasioona na kuwajengea mazingira mazuri ya kuwahusisha katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya uchumi.

Waziri Mkuu ameondoka Iringa leo mchana kuelekea Morogoro kuhudhuria mkutano wa kilimo utakaohusisha mikoa mitano ya Ruvuma, Mbeya, Iringa, Rukwa na Morogoro ikiwa ni juhudi za Waziri Mkuu kufufua ‘The Big Four’ ambayo sasa anataka iwe ‘The Big Five’ kwa sababu mkoa wa Morogoro uliteuliwa uwe ghala kuu ya kitaifa.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WAZIRI MKUU AINGILIA KATI DENI LA MAJI OLD MOSHI

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Mohammed Babu akae na wasaidizi wake na kutafuta fedha za kulipia deni la maji la sh. milioni 12.53 ili wanafunzi wasiendelee kuteseka.

Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Oktoba 23, 2008) mara baada ya kufungua bweni katika shule ya Sekondari ya Old Moshi na kuzungumza na walimu, wafanyakazi na wanafunzi wa shule hiyo.

“Mkuu wa Mkoa kaa chini na viongozi wa Halmashauri na Manispaa, wakurugenzi na Meya tafuteni hizo pesa mlipe halafu leteni risiti TAMISEMI tupeleke wizarani… watazirudisha,” alisema. Deni hilo ni la kuanzia Agosti mwaka jana hadi sasa.

Alisema ameamua kufanya hivyo kwa sababu deni hilo lienda kwa njia za kawaida litachukua muda mrefu sana kulipwa huku wanafunzi wakiendelea kuteseka.

Alisema matatizo madogo kama hayo yanaweza kumalizwa na viongozi wenyewe lakini tatizo ni kwamba wameweka ukuta unaowafanya washindwe kuona na kumaliza kesho ndogondogo za wananchi.

“Nimekuwa TAMISEMI kwa muda mrefu lakini nilichogundua ni kwamba tumejenga ukuta usio na maana… ndiyo maana Rais Kikwete akaamua kurudisha shule zote chini ya Halmashauri ili kusogeza huduma na kuongeza usimamizi… huwezi kuendesha sekondari kutokea Dar es Salaam hadi huku,” alisema.

Alisema hali aliyoikuta Old Moshi imemkumbusha hali ya shule ya Sekondari ya Ufundi Ifunda ambako alikuta hali ya majengo inayosikitisha. Alisema uendelezaji wa shule za sekodari bado ni mtihani kwa Serikali na ikibidi Serikali itabidi ijipange upya jinsi ya kuhudumia shule zote kongwe.

Akiwa shuleni hapo alielezwa na Mkuu wa shule hiyo, Bw. Ignas Sanga kwamba wanakabiliwa na matatizo mengi yakiwemo madeni ya maji na umeme, madarasa kuvuja wakati wa mvua, vyoo kufungwa sababu ya kuharibika, madeni ya wazabuni wa chakula na kemikali za kujifunzia darasani, kukosa uzio na ukosefu a nyumba za walimu.

Vilevile Bw. Sanga alisema bweni ambalo Waziri Mkuu amelizindua linahitaji vitanda 30 vya deka na makabati ya wanafunzi ili lianze kutumika. Gharama ya vitanda hivyo ni sh. milioni 11 na pia wanahitaji sh. milioni mbili ili kukamilisha jengo la walemavu.

Aliahidi kufanya harambee ya kutafuta sh. milioni 13 keshokutwa (Jumamosi, Oktoba 25) wakati akifanya majumuisho ya ziara yake ili zipatikane fedha hizo na wanafunzi wamaliziwe shida ya malazi shuleni.

Akiwa shuleni hapo alibaini kuwa mgeni wa kwanza alisaini kitabu cha wageni Januari 3, 1927 wakati Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee Rashid Kawawa alifika shuleni hapo Septemba 8, 1965 na hayati Baba wa taifa, Mwalimu Julius Nyerere alifika shuleni hapo Julai 20, 1966.

Shule hiyo ambayo imehamishwa maeneo mara mbili, ilianzishwa mwaka 1922 na hivi sasa ina wanafunzi zaidi ya 800.

Kesho Waziri Mkuu atakwenda Wilaya ya Mwanga ambako atapokea taarifa ya wilaya kabla kuelekea kijiji cha Raa kufungua zahanati ya kijiji na kuhutubia mkutano wa hadhara. Mchana ataenda Kirya kukagua lambo la maji, kilimo cha umwagiliaji na ujenzi wa nyumba bora. Atahutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Kirya.

Ends


IMETOLEWA NA

OFISI YA WAZIRI MKUU
23/10/2008
 
Back
Top Bottom