The Miracle Tree

MAMA POROJO

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
4,974
785
MIONGONI mwa miti yenye faida kubwa kiuchumi na kimazingira, ni mti wa mlonge.

Mti wa mlonge, umekuwepo nchini miaka mingi ya nyuma na kutokana na maajabu yake katika kuhifadhi, kutunza mazingira na kutoa tiba ya maradhi mbalimbali, mti huo ambao kwa kilatini umepachikwa jina la Oleifera, sehemu mbalimbali unaitwa Miracle Tree.

Mti huo kulingana na tafiti mbalimbali, una uwezo mkubwa katika kuhifadhi mazingira.

Maua yake yasiyo na msimu katika kuchipua, huanguka na kuwa mbolea nzuri kwa ardhi kwa ajili ya mimea mingine.

Kulingana na tafiti hizo, mti huo ukipandwa na kutumika vizuri, unaweza kuiwezesha jamii kujipatia tiba za maradhi mbalimbali bila kulazimika kwenda hospitalini, hususan katika maeneo ambako hakuna huduma za afya jirani.

Kwa mujibu wa tafiti hizo, maua ya mlonge, magamba, mti wenyewe na majani yake, hutumika kama dawa za maradhi mbalimbali.

Mti huo unaota kirahisi kila sehemu na ni wajibu wa kila mmoja kuamua kuotesha nyumbani kwake kutokana na ukweli kuwa una faida nyingi kuliko watu wanavyofikiri.

Mti huo una uwezo wa kuhifadhi maji, unastawi hata eneo la ukame na mti huo ambao ni jamii ya mikunde, maua yake yakidondoka yana madini ya calcium, hivyo hustawisha udongo na kuongeza rutuba na hustawisha mazao mengine na kuzuia upepo na kama ikipandwa kwa wingi kuna uwezekano wa kuliepusha taifa na jangwa.

Mbegu zake ikikamuliwa hutoa mafuta mazuri sana kwa kupikia na kutengeneza sabuni. Mashudu yake hutumika kusafisha maji yenye tobe kuwa masafi kwa matumizi ya binadamu.

Tatizo lililopo ni walio wengi kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu mti huo hali ambayo inafanya washindwe kuutumia au hata kuupanda na badala yake kushughulika na aina nyingine ya miti ambayo huchangia ukame na kuifanya nchi kuwa jangwa.

Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo na Huduma za Afya kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (SHIDEPHA), anasema kuwa mti wa mlonge umekua mkombozi kwa watu wengi ambao wanaishi na virusi vya UKIMWI ila anashangaa kwanini elimu ya kutosha haijatolewa kwa watu ili waweze kuutumia pengine hata kuufanya kuwa mbadala kwa dawa za kurefusha maisha.

Jamii ikielimishwa vema kuhusu mlonge, itakuwa katika nafasi nzuri ya kunufaika kutibu hususan kipindi hiki ambacho dawa za viwandani zimeonekana kushindwa kukabiliana na maradhi mbalimbali.

Wakati umefika kwa jamii kuelimishana faida za mlonge na serikali kwa upande wake, inapaswa kutoa kipaumbele hata katika operesheni za upandaji miti kwa kupanda miti ya mlonge ambayo ina faida nyigi kiuchumi na kitabibu.

Kwa habari zaidi kuhusu mti wa ajabu fungua attachement.
 
Information is power,yet serikali na wananchi wake hatufanyi jitahada za dhati to empower our societies with this powerful and useful information on health issues
 
Nashukuru sana kwa information hii. Mimi lazima niupate huu mti niupande na niwe nakunywa kama chai kupambana na malaria.. au kuna ubaya mtu akinywa kila siku?? naomba msaada tafadhali
 
ahsante sana mkuu binafsi nakula dozi ya hii kitu aisee naikubali mnooooooo,na nawashauri wote tuitumie kuliko kutumia madawa ya hawa Freemasons pale Muhimbili.
 
Back
Top Bottom