The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

Mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus, 20, anaamini kwamba ana kazi ya ziada kupata fursa ya kushirikishwa katika kikosi cha Brazil cha kombe la dunia licha ya kulifungia taifa lake bao la lala salama katika mechi ya kirafiki dhidi ya Japan. (Goal)
 
MESSI AMKATAZA AGUERO KUJIUNGA NA REAL MADRID


Lionel Messi amemshauri Mwargentina mwenzake Sergio Aguero kutojiunga na Real Madrid mwaka ujao, kwa mujibu wa Diario Gol .
Rais wa Madrid Florentino Perez amemtaja straika wa Manchester City, Aguero kuwa mchezaji sahihi na anaamini ataweza kumshawishi kujiunga na Blancos ikiwa Pep atamsajili Alexis Sanchez.
Lakini kwa mujibu wa habari Lionel Messi amemtumia ujumbe Aguero kwa njia ya WhatsApp, na amemwambia rafiki yake kipenzi na Mwargentina mwenzake kuwa ni vema abaki Manchester kwa sababu Madrid inaelekea kuporomoka na City wanazidi kuwa tishio chini ya Guardiola kwa sasa.
Kaogopa kuumizwa kweny laliga
 
Manchester City na Juventus wanatamka mchezaji wa kati wa Liverpool Emre Can, 23, ambaye mkataba wake utakwisha msimu huu. (Daily Star)
 
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Manchester City Sergio Aguero usiku wa kuamkia leo amedondoka ghafla na kuzimia katika chumba cha kubadilishia nguo baada ya mchezo dhidi ya Nigeria mjini Krasnodar, Russia.
Aguero aliifungia timu yake mara mbili kabla ya mshambuliaji wa Arsenal na Nigeria Alex Iwobi kuandika la kwanza.
Aguero alipata fahamu baadae akiwa hospitali lakini madaktari wanasema asalie kwanza wodini ili hali itengemae zaidi.
Kelechi Ihenacho aliindikia Nigeria goli la pili kabla ya Ever Banega kuongeza jingine kwa Argentina.
Haijaelezwa nini kilichomsibu Aguero mpaka kuanguka na kupoteza fahamu na huenda taarifa zaidi zikatoka baadae.
 
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Manchester City Sergio Aguero usiku wa kuamkia leo amedondoka ghafla na kuzimia katika chumba cha kubadilishia nguo baada ya mchezo dhidi ya Nigeria mjini Krasnodar, Russia.
Aguero aliifungia timu yake mara mbili kabla ya mshambuliaji wa Arsenal na Nigeria Alex Iwobi kuandika la kwanza.
Aguero alipata fahamu baadae akiwa hospitali lakini madaktari wanasema asalie kwanza wodini ili hali itengemae zaidi.
Kelechi Ihenacho aliindikia Nigeria goli la pili kabla ya Ever Banega kuongeza jingine kwa Argentina.
Haijaelezwa nini kilichomsibu Aguero mpaka kuanguka na kupoteza fahamu na huenda taarifa zaidi zikatoka baadae.
Asante kwa taarifa.
 
Tetesi
MAN CITY YAMFUKUZIA GORETZKA


Manchester City ni klabu nyingine ambayo imeonyesha nia ya kumsajili kiungo wa Schalke Leon Goretzka, kwa mujibu wa Sunday Mirror .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani ameibuka kuwa lulu katika Bundesliga na Bayern Munich wamehusishwa na tetesi za kuifukuzia saini yake.
 
Tetesi
CITY YAMGEUKIA VAN AANHOLT


Jitihada za Manchester City kusaka beki mpya zimewaongoza kumgeukia beki wa Crystal Palace Patrick van Aanholt, kwa mujibu wa The Sun on Sunday .
Bosi wa City Pep Guardiola anataka kuleta mtu wa kuziba nafasi ya Benjamin Mendy ambaye anauguza majeraha katika dirisha la uhamisho Januari, na anaona Van Aanholt ni mchezaji wa bei rahisi anayeweza kumsajili.
Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea na Sunderland anaweza kupatikana kwa kiasi cha takribani paundi milioni 12.
 
Tetesi
REAL IPO TAYARI KUTOA £60M KWA AGUERO


Real Madrid wanaandaa dau la paundi miiloni £60m kumleta Sergio Aguero La Liga, kwa mujibu wa Don Balon .
City wapo tayari kumuuza mfungaji wao wa muda wote ikiwa watampata Alexis Sanchez kutoka Arsenal, na hiyo itafungua njia kwa Zinedine Zidane kumsajili straika huyo wa Argentina.
 
Refa wa zamani katika ligi ya Uingereza Mark Clattenburg anasema kuwa beki Vincent Kompany wa Manchester City alifaa kupewa kadi nyekundi kwa kumchezea visivyo mshambuliaji wa Leicester Jamie Vardy huku mshambuliaji wa Everton Oumar Niasse akiadhibiwa na shirikisho la soka nchini Uingereza FA kwa kudanganya baada ya kushinda penalti dhidi ya Crystal Palace . (Times - subscription required)
 
Klabu ya Manchester City huenda ikamnunua winga wa Leicester Riyad Mahrez baada ya kiungo wa kati wa Barcelona Lionel Messi kukataa raia huyo wa Algeria ajiunge na Barcelona (Don Balon - in Spanish)
 
City pia inataka kumsajili kiungo wa kati wa Schalke na Ujerumani Leon Goretzka ambaye kandarasi yake inakamilika mwishoni mwa msimu huu na amewavutia Arsenal, Liverpool na Chelsea (Daily Mirror)
 
Manchester City itashindana na Liverpool kumununua beki wa Southampton na Uholanzi Virgil van Dijk, 26, katika dirisha la uhamisho la Januari.{Daily Mirror}
 
Back
Top Bottom