Undava King
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 3,181
- 5,317
- Thread starter
- #21
Sijajua wewe waamini katika imani gani kuweza kujustify hilo? Ila kama ni mkristo unakubaliana nami kuwa Mungu wako ni huyu hapa;Mungu yupo
Yohana 1:1-14 "Hapo mwanzo kulikuwako NENO, naye NENO alikuwako kwa MUNGU, naye NENO alikuwa MUNGU."
1.Huyu Neno ni nani?
Nategemea utanijibu Yesu=Emanueli 'Mungu yu pamoja nasi'
2. Kwanini Yesu anakana kuwa Mungu kama kweli yeye ndiye Neno?
3. Kwanini Yesu anajihita mwana wa Mungu na siye pia akitujulisha ni miungu tukilipokea NENO?
4. Je, uoni kama kuna uwezekano kwamba NENO ni ujumbe wa MUNGU na Yesu pia ni mfuasi kama sisi ambaye ni benchmark kwetu kujifunza na kuiga mfano mwema kwake namna yakuenenda na NENO?
5. Mwisho kama NENO ni ujumbe wa MUNGU unaotakiwa tuuishi na uwepo ndani yetu kama Mwangaza na Uzima na UJUMBE huo ndiyo MUNGU.
Je, uzi huu unakupa picha gani kuhusiana na possibility juu ya kuwepo na kile nilichoandika?