The Lucifer effect "Watawala bora wanapogeuka kuwa Mashetani

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,099
Wanabodi "The Lucifer effect "ni dhana inyoelezea jinsi watu wema kabisa na wanyenyekevu, washika dini na viongozi wanapogeuka na kuwa na matendo ya kishetani.

Utafiti umefanywa kwa muda mrefu Sana kwenye jamii tofauti kuanzia kwenye kambi za magereza za kikatili nchini Iraq "kambi ya Abu Gharaib "mpaka kwenye Chuo cha Stanford University ( Hapa walikusanywa wanafunzi na kutengwa kimakundi, kundi la wafungwa yaani Prisoners na viongozi yaani Guards,

Utafiti pia ulifanywa nchini Rwanda pia kwa wafungwa wa mauaji Ya kimbari na waliulizwa "Inakuwaje waliweza kuwaua majirani zao na marafiki na watoto wao walioishi nao pamoja miaka mingi? Hawa wanyarwanda walikula, kucheza na kufuga pamoja lakini waligeukana nini sababu "The Lucifer effect "

Wana Jf nitajadili kwa ufupi sana sana hii dhana halisi ya "The Lucifer effect "yaani watu wema mfano mkeo, mtoto wako ghafla wanageuka Mashetani na kutaka kukuangamiza Baba wakati muda wote mmeishi, kula na kucheka pamoja, Nini sababu? au Nini kinawafanya wanajeshi wa nchi jirani wanaoishi Kama ndugu ghafla kwa akili zao wanaamua kuanza kupigana na kuuwana nini sababu?

Mosi, The power of authority au Nguvu Ya kimamlaka, Hawa viongozi tunaowachagua na kuwapa Nguvu kikatiba ni hatari Sana kwa kauli zao, Wengi huchochea mambo kwa maslahi binafsi au kwa kutaka sifa, Wao hujificha nyuma na kuamuru watu wa chini wema na wapole kutekekeza amri zao, Mamlaka hizi huwezi kuziona moja kwa moja bali watekelezaji ndio hubebeshwa mzigo

Nchini Rwanda baadhi Ya wafungwa wa mauaji Ya Mwaka 1994 walihojiwa Kama wanajutia makosa walijibu hapana, Wanasema wao ujasiri waliutoa toka kwenye kauli za viongozi wao waliowaaminisha kuwa jamii Fulani haitakiwi kuwepo kwenye ardhi Ya Rwanda, Hivyo walijikusanya uwanjani kila siku wakiwa na mapanga na silaha wakigawana majukumu ya kuanza kusaka binadamu au majirani zao Kama msako wa Panya nyumba kwa nyumba na kuwateketeza

Pili, Jamii inyojiona imetengwa au kuonewa, Hii ni jamii ambayo bila kuigeuza na kuiheshimu ni hatari zaidi sana sana, Ni jamii inyojiona imedharaulika sana na watawala, Ni jamii tulivu na nyenyekevu inayonyimwa fursa za maendeleo na kujieleza,

Wakati vita ikipamba moto nchini Iraq na Afaghanstan Marekani ilipeleka wanajeshi wake wadogo kabisa kiumri mstari wa mbele vitani akina dada wenye umri wa miaka 20+ .Hili kundi la wanajeshi wa kike lilijihisi kutengwa na kudharauliwa sana, kilichofuata waliamua kugeuza wafungwa wa kivita Sehemu ya kumaliza hasira zao kwa kutoa mateso ya kisaikolojia, Wafungwa waliamriwa kuvua nguo zote na kubaki uchi Kisha wenzao kuwapigisha punyeto na wao wakicheka pembeni, Makamanda wa kike waliwaamrisha wafungwa wa kiume kuwalamba papuchi wakiwa wafungwa wanapiga push-up huku Makamanda wamewawekea papuchi zao kwa mbele usoni, Vitendo hivi walivirekodi na kuzua taharuki Marekani, Jamii ilihoji inawezekana vipi watoto wadogo kufanya ukatili huu?

Tatu, Kila binadamu ni mtu katili kulingana na mazingira hivyo hatupaswi kuwacheka wenzetu wanaofanya matendo ya kikatili, Kwani siku tukiwekwa kwenye mazingira tofauti, Tofauti na tunayoishi au kuyazoea binadamu humpasa kubadilika, Hivyo basi fikiria siku ukiishi mazingira tofauti kabisa na unayoyazoea hapa namaanisha unaishi mazingira ambayo kukuta miili Ya watu waliouwawa barabarani ni kawaida, Watu kupigwa risasi mbele Ya uma ni kawaida sana, Au wanafamilia kuchinjwa na kupotezwa ni kawaida, Hali hizi za kimazingira zisipodhibitiwa binadamu hugeuka shetani

Tano, Hisia za kutokufahamika au kujificha nyuma ya wengine hupelekea watu wema kuwa Mashetani, Watu hufanya mambo wakidhani hawafahamiki au hakuna anayewafuatilia na kuwagundua, Utafiti unaonyesha maeneo ambayo watu wanahisi watajulikana watu wema huendelea kuwa wema zaidi ukilinganisha na maeneo ambayo watu wanahisi hakuna anayekuona, Mfano ukiliacha gari lako Manzese Dar es Salaam nje bila kufunga milango unaweza usikute kitu ndani ya gari, Lakini ukiliacha maeneo yenye camera mfano baadhi ya maeneo Ya Posts Dar es salaam watu wataliacha wakihisi kuonekana

The Lucifer effect ni practical approach iliyothibitishwa, Lengo la kuleta uzi huu ni kukumbushana kuwa tunapaswa kusamehe changamoto lakini Sio kuzisahau, Kutosahau mazingira na changamoto zake kunaifanya jamii kutorudia makosa

Mwisho, unaweza jifunza zaidi "How good people may turn evils "Haya yanayotokea hayatakupa shida bali yatakujenga kusonga mbele
 
Hiyo ni dhana tu ya muandishi...ni story kama ya kusadikika.
Unaweza kumshangaa Mbowe anawezaje kuamrisha maandamano ya kwenda kufanya vurugu manispaa mida ya saa moja kasoro usiku huku akijua wazi hairuhusiwi?
 
Hiyo ni dhana tu ya muandishi...ni story kama ya kusadikika.
Unaweza kumshangaa Mbowe anawezaje kuamrisha maandamano ya kwenda kufanya vurugu manispaa mida ya saa moja kasoro usiku huku akijua wazi hairuhusiwi?
Real !!!!

Inaonekana umeguswa sana Sana nilitegemea hilo

Huo ni Utafiti uliofanywa mwanzoni mwa miaka ya 2000 baada ya uvamizi wa Marekani nchini Iraq ukatili ulioendeshwa na mateso yaliyotokea,

Nafahamu wewe hupendi kusoma wala kujifunza, Mara nyingine jifunze kukaa kimya, Mada ikikuwasha njoo na hoja

Jingalao, Nipinge kwa hoja Sio vioja, Leta hoja zako kupinga Kama umeelimika
 
Real !!!!

Inaonekana umeguswa sana Sana nilitegemea hilo

Huo ni Utafiti uliofanywa mwanzoni mwa miaka ya 2000 baada ya uvamizi wa Marekani nchini Iraq ukatili ulioendeshwa na mateso yaliyotokea,

Nafahamu wewe hupendi kusoma wala kujifunza, Mara nyingine jifunze kukaa kimya, Mada ikikuwasha njoo na hoja

Jingalao, Nipinge kwa hoja Sio vioja, Leta hoja zako kupinga Kama umeelimika
Huwezi kuaminisha watu haswa wasomi dhana flani kwa kutumia utafiti mmoja.
Nipe idadi ya waliohojiwa nipe profile ya mtafiti na affiliation yake
 
Asante kwa hoja nzuri. Ni kweli, huku mtaani utakuta mtu anatumia madaraka yake kuchimba mkwara, utasikia "unambishia DC, Mimi ni mteule wa Rais nk. Mmoja aliwahi Sema "km wewe unatosha Njoo Kaa hapa na hutumia badala ya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Reference Mkuu.
Cover page kasome attached
Screenshot_20190314-062526.jpeg
 
Asante Sana kwa hii mada, nami niliwahi kuuliza kuhusu hili ila sikujua jina ni The Lucifer's Effect.
Nani hatari zaidi kati ya malaika aliyegeuka shetani, Au shetani aliyegeuka malaika?! - JamiiForums
P
Pascal tafuta kitabu Hicho Soma ni kizuri sana kitakubadilisha mtazamo kabisa, Ni real life ya maisha ya watu, Ni practical experience

Kina page zaidi ya 500,Lakini kila page itakufanya upate kitu kipya

Sio hadithi ni mambo yalivyo na uhalisia, unapozidi kusoma utapata picha halisi za binadamu
 
Mwandishi ni very much infamous kwa sababu ya tafiti zake zisizofuata methodologies za kisayansi...
Kwa style hiyo wewe ni maskini, Huna maendeleo wala huwezi kuendelea

Kaa chini Soma na Jifunze dhana zima Ya "The Lucifer effect "Halafu ndio unaandaa hoja za kujibu

Hapa kwenye uzi hatuongelei mtu au personal identity, kujadili mtu ni umaskini wa fikra, Tunajadili mawazo au Ideas

Real men always discuss on Ideas

Weak people or Power people discuss on personality

Jingalao Jifunze kutulia Soma mada, unakurupuka Sana kujibu, Fikiri kabla ya kuandika hatujadili watu kwenye uzi huu

Wewe unaelewa nini kuhusu "kwanini watu wema hugeuka Mashetani au wabaya "
 
Kwa style hiyo wewe ni maskini, Huna maendeleo wala huwezi kuendelea

Kaa chini Soma na Jifunze dhana zima Ya "The Lucifer effect "Halafu ndio unaandaa hoja za kujibu

Hapa kwenye uzi hatuongelei mtu au personal identity, kujadili mtu ni umaskini wa fikra, Tunajadili mawazo au Ideas

Real men always discuss on Ideas

Weak people or Power people discuss on personality

Jingalao Jifunze kutulia Soma mada, unakurupuka Sana kujibu, Fikiri kabla ya kuandika hatujadili watu kwenye uzi huu

Wewe unaelewa nini kuhusu "kwanini watu wema hugeuka Mashetani au wabaya "
Kuna Gazeti moja liliwai kumuoji kiongozi mmoja aliekuwa kinara kwenye mauaji ya Sierra Leone miaka ya tisini,
Na kwa maelezo yake mwenyewe alikili kuwa hakuzariwa kuwa muuaji ila mazingira yamemfanya kuwa alivyo ina maana kuwa kama mazingira yangekuwa tofauti yeye angekuwa mtu mwingine kabisa, ilo ni moja lakini mara ngapi vikosi vya waasi huwachukua watoto wadogo ambao ni malaika kabisa na kuwapandikiza chuki na roho ya kikatiri mwisho wanaishia kuwa watu hatari sana kuwai kutokea kwenye hii dunia.

Back soon
 
Back
Top Bottom