The Lesson Africa can learn from China!

Apr 27, 2006
26,588
10,375
Wanabodi niliipitia hii article nikaiona to be interesting:

NO ONE IS LAUGHINH AT CHINA ANYMORE,
BY: FEMI AKOMOLAFE

(1). It is now official, China has overtaken the UK to become the 4th largest economy in the world, behind the US, JAPAN, and GERMANY. Given the fact that just 20 years ago China was a country that was lampooned as a "sleeping giant", this is nothing short of an astounding miracle, if you do not believe this go to www.made-in-China.com.

(2). Since both China and most of Africa were in the same economic badlands in the 70s and 1980s, China rapid economic transformation holds special lessons for those of us in Africa. Whilst the Chinese opted for an indigenous solution to their economic backwardness, African governments, against the advice of eminent economists such as professor Adedeji, chose to follow the prescriptions of the World bank and the IMF!

These Western-dominated organizations prescribed the vile Structural Adjustment Programmes (SAPs) which later metamorphosed into the Enhanced Structural Adjustment (ESAP) which, in turn, metamorphosed into the insulting Highly Indebted Poor Country (HIPC) programmes.

The results, which could not be more contrasting, are there for all to see, whereas African economies which devoutly followed the IMF/World Bank's prescriptions have been devastated, While China's economy managed by Chinese themselves, is surging ahead at an unprecedented, breathtaking pace.

(3). Africa was dealt a double-whammy:
1. The economic prescriptions of the IMF and World Bank comprehensively ruined the African economies, and
2. Africans got blamed for the continuing economic non-performance!

The overpaid Western consultants dumped Africa on a laughed all the way to their banks, and the Africans have to pick up the pieces of their crumbled infrastructure, destroyed education and health services, and ill-fed citizens. Sadder still, the Africans have to look on as the Western media continue to lampoon the continent, as though their "experts" have nothing to do with the pictures they are airing of us!

There are five lessons to be learned by Africans from China economic success;

(1). It is possible, people with confidence, determination and vision can achieve!

(2). National economic development always comes through the effort and determination of the nationals!

(3). Rapid economic transformation is possible within two decades!

(4). There is no alternative to industrialization!

(5). There should be more intra-African trade and commerce!
 
Mzee Es,

niliyasema haya na mengine mengi tu awali watu waliniona mchawi tu. Sikupenda maendeleo hasa pale Marekani inapoabudiwa.... Ajabu kubwa kuliko yote ni kwamba wakati wazungu wachumi private wanapopingana na serikali zao kuhusu globalization kwa faida ya Africa, viongozi wote wa Africa wanazidi kukaribisha na kupongeza globalization.

Tumeingia Ubepari bila kuwa na fahamu akilini ni kitu gani kinachokuja na Ubepari. Wananchi na viongozi wote hawana elimu yake zaidi ya imani tu kama ilivyo imani ya dini.. Na kwa bahati mbaya hata haya tuliyoyapata ni mageni kwetu, hakuna aliyefahamu kinachokuja - hatukutegemea kupata kitu zaidi ya tulichokuwa nacho, hatukujiandaa kupokea kitu kwa hiyo basi haya tuliyo nayo ni maendeleo tosha kwa maskini mlalahoi. Wakati wenzetu wanaweka mikataba ya kiuchumi baina ya nchi sisi ndio kwanza tunalazimishwa kupokea misaada kwa kuweka rehani maliasili zetu. Kisha tunatafsiri globalization kuwa uwekezaji toka nchi, ubinafsishaji toka nje na hata wataalam toka nje ndio maana kamili ya globalization.
 
Mkandara,
Can we say Nyerere was a visionary? Wakati wengine woote wanaangalia Ulaya/Marekani, alikuwa wa kwanza kuangalia China.
 
Jasusi,
Nyerere alikuwa visionary...... No doubt, na hii ndiyo ina -separate kati yake na viongozi wengine. Tatizo kubwa alilokuwa nalo Nyerere navyosikia mimi ni Ubishi kama wa mzee Mkandara hapa. Nyerere alikuwa akiamini Ujamaa kiasi ambacho aliufanya kama dini lakini hakufahamu kwamba dini ni imani ambayo sio lazima ikubalike kwa kila mtu..

Nyerere aliu-study Ubepari akafahamu mazuri yake na mabaya yake (all sides of the coin). Kisha akaanza kutafuta dawa ya kupambana na Ubepari na kwa wakati ule Ujamaa peke yake ndio ulisimama kutetea mnyonge.

Kusema kweli sio Nyerere peke yake, kuna akina Abdulrahan Babu na wasomi wengi wa visiwani ambao walikuwa tayari wameisha pikwa na Uzalendo..

Tatizo kubwa alilokutana nalo Nyerere ni hawa wasomi wa bara ambao walikwenda Ulaya na kupenda waliyoyaona huko kisha wakaanza kuota ndoto za kubadilisha maisha yao wenyewe ndani ya Tanzania ili wao kuwa kama wazungu watawala..

Wasomi hawa ndio waliotaka madaraka baada ya uhuru wakimbilia majumba ya uzunguni na kuendesha serikali za nchi vibaya kuliko hata Mkoloni, hawakuwa na vision kabisa zaidi ya kuendeleza yale ya Mkoloni chini ya Utawala wa mweusi. Hesabu ya viongozi kama hawa Afrika ilizidi hesabu ya watu kama Nyerere ambao walijawa na uzalendo mbali na kuwa na vision ya hata mwaka mmoja mbele. Kati ya mataifa 42 ya wakati huo miaka ya sitini labda nchi sita tu ndizo zilikuwa zimeukubali Ujamaa ama niseme Uzalendo. Hapo dhahiri dalili ya kushindwa kwa Ujamaa Afrika ilikuwa kubwa sana.

La pili, Ukiangalia China wamefanikiwa ktk transition ya kutoka Ujamaa kuingia Ubepari. mapinduzi waliyafanya wao ni kuondoa viongozi wazee ambao walichukulia muhali Ujamaa kujitajirisha wao, wakawaweka vijana wanamapinduzi (wajamaa wa kileo) ambao pia wameusoma Ubepari na madhara yake. Wakatazama njia za kujiunga na adui ambaye ana nguvu kuwashinda kwa sauti na support. Kabla ya mapindizi ya kiuchumi China nadhani ulisikia jinsi Wachina walivyokuwa wakikamatwa kila siku nchi za magharibi kwa wizi wa technologia. Serikali ya China ilianzisha mafia za wanafunzi wake kuvamia nchi za magharibi kutafuta elimu.... walipoteza mabillioni ya fedha kuwasomesha watoto wao nje kutafuta elimu kisha wakawapa nafasi vijana hao kushika mashikirika makubwa ya nchi. Tofauti na na Castro wa Cuba ambaye yeye alijaribu kuwapeleka majambazi wote wabaya nchi za magharibi kuharibu tamaduni na uchumi wa nchi hizo. Kwa castro adui ni adui tu hana msalie! Mchina alicheka na wazungu na kujifanya anaonewa kishenzi nchini mwao na serikali yao ilizidisha kichwa ngumu kwa western world.

Nadhani, kwa mtazamo wangu tuwapongeze wa china kwa kuwa na subira na maendeleo. Kisha wameweza kuutumia Ujamaa wao ktk mazingira ya Ubepari na transition imekwenda kwa mikataba ambayo Marekani walifikiri wao watatoka Washindi kutokana na ile population ya China. Kwa hiyo wakati Ulaya waligoma kabisa kuingiza mali toka China kwa sababu ya standard, Marekani waliingia mkenge wakakubali kuuziana mali. Kwa kila kitu kilichotoka Marekani -Imports), Wachina waliweza kuzalisha mara kumi zaidi (fake) na kusambaza kwao vijijini na nchi maskini za kiafrika. Na kila Kilichotoka China kwenda Marekani kili-affect mali zote za aina hiyo ndani ya Marekani na ile iliyoagizwa toka Ulaya. Mara Canada na Uingereza nao wakaishiwa soko kwa hiyo nao wakajiunga na biashara za China kwa sababu ya cheap labour na soko.

Kwa matazamo wa kibiashara dunia ilikuw na maskini wengi kuliko hata middle class na hata hao middle class maisha yao yalikuwa ktk kulipa nyumba, magari na hawana akiba zaidi ya kutumia kwa vitu vya thamani kubwa. Kwa hiyo hapa Mchina akawa mshindi kwa biashara zote za retails ktk mataifa yote makubwa na madogo. Kikubwa zaidi China hawakubinafsisha mali ambazo walifahamu ndizo ngao yao kwa nchi za magharibi. Serikali ilitoa shares kwa wananchi kidogo kidogo na mamlaka mikoani yalipewa sauti na nafasi kubwa ktk kujiendeleza kiuchumi.

Hali Tanzania sisi tumeuza mashirika yote na badala ya shares za mashirika makubwa kuwekwa ktk soko letu la Dar-es-Slaam Stock exchange tumewaachia wazungu haohao wakishirikiana na wahindi kutafuta wawekeshaji na kuchukua shares za wananchi. Mali ambayo Nyerere aliiweka kama mirathi ya Watanzania baada ya kujifunga mikanda miaka ishirini na mitano ya Ujamaa. Leo hii mwananchi hana sauti kabisa kwenye miradi zaidi ya sigara, pombe na mingine michache. And we are opt to sale the all country!...

Kama ulivyo msemo wa baadhi viongozi wataalam kila wanapojadili swala la Uwekeshaji -Tunaiuza nchi... wakifikiri neno hili lini maana nzuri sana kwa taifa letu kiuchumi hali wamesahau kabisa kwa nini tuligombea Uhuru wetu 1960.
 
Mkandara,
Kwa kweli inasikitisha kuzungumzia viongozi wetu wa leo. Si Tanzania peke yake, lakini ukiangalia Afrika kote leo hii, mimi nilidhani wajukuu za akina Mkrumah, Sekou Toure, Nyerere, wangetoa uongozi ambao ungeendeleza vision ya mababa/babu zao lakini kumbe ni reactionary watupu. Unawezaje kuuza NBC, madini na kuona fahari eti tunapata asilimia 3? Is that something to be proud of? Na hawa wamesoma na wakati mmoja walikuwa karibu na Nyerere kabisa. Judas Iscariots all of them. Yaani Africa tulibahatika kupata kizazi cha akina Nyerere, Mandela, Ben Bella, Nasser, wote wapigania uhuru kumbe waliofuata ni mashabiki tu wa neo-colonialism?
Nasikia safu ya leo ya viongozi wa China wote wana shahada za engineering, je hii ni kweli?
 
Mzee Bob na Jasusi,

Mmetoa maneno mengi muhimu hapo juu,

(1). Nyerere's Visionary?
Katika dunia ya leo kinachotakiwa ni results, au ushindi, sasa Mwalimu aliwaangalia Wa-china ambao sasa ni washindi, maana yeke ni kwamba Mwalimu alikuwa na good visionary kwa sababu toka enzi zile aliweza kupima na kuona mbali kuwa hawa jamaa wana ideas ambazo zikitekelezwa kikamilifu zinaweza kuleta mafanikio kwa wananchi na taifa bila ya kutegemea the West.

Sasa hapa what can debated kuhusu kwetu bongo ninadhani ni watekelezaji, na mazingira yetu ya kisiasa na kisheria. Maana huko Uchina tunajua hakuna mchezo, kiongozi akiwa mwizi adhabu yake ni kupigwa raisasi hadharani au jela maisha, hata awe nani! Halafu Wachina hawa-tolerate incompetence, wakikujua tu huna kazi hata uwe mwenyekiti wa chama! Halafu they have no compromise na issue zao muhimu za kitaifa hata ije US wao hawayumbi, ile kamati yao kuu ya chama haina mchezo bro! Na kama mzee Jasusi ulivyosema wengi wa viongozi wao wa juu ni ma-engineers na wenye elimu ya kweli kutoka kwenye vyuo vinavyotambulika. Ukitaka kuwaelewa hawa jaribu kutafuta notes za vikao vya kamati kuu yao ndio utaelewa jinsi jaamaa walivyo na upeo wa kuona mbali na kusimamia maamuzi yao!

(2). Mzee Jasusi hapo uliposema kuwa huku bongo ni kina Yuda, hakuna la kuongeza, halafu kuwaita reactionary ni kuwapa cheo cha bure hawa hawna lolote ni wababaishaji hawa na wezi wakubwa. Hawa wamesoma na kusomeshwa na Mwalimu, Ben ni mwanafunzi wa Mwalimu na amepitia vyuo vyote Mwalimu alivyosoma, sasa leo baada ya kustaafu ndio anakubali kuwa hakutilia mkazo Kilimo! Akiwa kwenye power ameambiwa mara kibao kuwa Kilimo hakuna kitu kina Keenja wanakula hela tu buree yeye ni ubabe tu! Leo JK anasema ana baraka za Mwalimu, na kutonyesha biblia ambayo anadai alipewa na Mwalimu na wananchi wasioelewa masikini wa Mungu wanakubali tu, Mwalimu hakuwahi kusafiri na watu 50, Mwalimu hakuwa na makundi, na hakuwa matafuta umaarufu tu bila sababu, ni matendo yake ndiyo yaliyomletea sifa, hakubeba wajinga tuuu na wapambe ambao kazi yao ni kumsifia tu! Unajua ilikuwa aibu kumsikia Waziri Mkuu wetu kule NY, anavyomisfia his co-president yaani mpaka unasikia kutapika, Mwalimu alikuwa na unyonge wake lakini sio kiasi hiki cha kuuza nchi kwa ajili ya sifa!

Pamoja na mawzao mengi unrealistic ya Mwalimu, lakini aliiacha nchi yetu ikiwa na viwanda na mashirika, leo yakiuzwa kwa watu binafsi yanatoa faida sio kwamba hawa watu binafsi wanaya-renovate au kuleta miracles kwani kiwanda cha Sigara na kile cha Bia havikuletewa kitu chochote kipya zaidi tu ya kubadili watu basi! Hela iliyouziwa NBC na Kilimanjaro mapaka leo hawajasema ukweli ni ngapi, maana ni aibu kutamka hadharani!
 
Jasusi,
Yes, nakubaliana na wewe kabisa uliposema Judas Iscariots!...mtu huyu mwanzo alikuwa msitari wa mbele ile mbaya utadhani kaahidiwa ufunguo yeye. Lakini basi tuangalie kimoja kizito zaidi, kuondoka kwake ndiko kulikoboresha imani ya watu na kuwapa nguvu zaidi. Tanzania na nchi za Kiafrika hawa akina Judas ni among us hadi leo, wanakula na sisi na hata baada ya kufahamu mabaya na usaliti wao huko nyuma bado wanakula nasi meza moja. Tamaduni mbovu ambayo nchi kama China haiwezi kabisa kuvumiliwa wala kupewa nafasi.

Sidhani kama ni kweli kuwa viongozi wote wa China wana shahada ya egineering. Kumbuka kwamba China ktk mabadiliko yake ya kiuchumi walikuwa bado wanakitumia chama kimoja tawala - cha Ujamaa, chama cha Mao Tse Tung kuweka mikakati yote ya kiuchumi wakifuata kanuni za Ujamaa (kama tulivyo sisi na CCM). Isipokuwa nachofahamu mimi ni kwamba jamaa hawa badala ya kuunda vyama vya upinzani waliunda bodi za kiuchumi kutoka kwa wataalam wao, wanafunzi wao na maoni ya wananchi kwa kila strategy iliyohusu uchumi na Ustawi wa jamii. Makomangano yaliendeshwa humo badala ya vyama na wote wakiwa na lengo moja. Mafanikio yao yote yametokea nje kabisa ya vitabu vya kiuchumi toka nchi za magharibi. Wataalam wote wa nchi za magharibi kimahesabu walijuwa - China is doomed to fail kutokana na kuwa na chama kimoja cha kijamaa na pia baadhi ya wazee walikuwepo bado wameshika nafasi kubwa za uongozi.

Matokeo ya maendeleo ya China ni Uzalendo wao, hekima na Busara za watu kama kawawa hazikupuuzwa na wasomi. Hakuna Mchina anayeamini mzungu kuwa ni bora kuliko Mchina hata kama hakusoma. Wachina hawaamini kwamba elimu toka nchi za magharibi ndiyo nguzo ya maendeleo ama mafanikio kimaisha ila elimu ya darasa na ufundi (techonology)inaharakisha mafanikio hayo kwa ufanisi.

Bongo hatuna kabisa Uzalendo ndugu yangu na msomi ndiye Mungu wa mafanikio hali tunao matajiri wenye maisha mazuri hali hawana elimu ya darasa isipokuwa vision na elimu ya kuendesha shughuli yao. Nyuma ya utajiri wao ndiko wamesimama wenye elimu ya darasa. Bongo tunataka kiongozi msomi hata kama hana vision, busara wala hekima ya uongozi ili tupate kitu gani sijui!. Tanzania hata hiyo vision inaletwa na mzungu kupitia kwa akina Juda....Kwa hiyo vision muhimu sana kwa kiongozi.

Nakumbuka China kitu cha kwanza kilikuwa kukuza kilimo na mashamba yote yalipewa wananchi toka mikono ya serikali. Wakulima China walizidi population ya ajira zote combined kama Bongo vile, na iliposemwa serikali itawasaidia wananchi kupata zana za kilimo na pia kuwaambia wananchi zao gani linatakiwa toka sehemu fulani, kisha wakajenga viwanda sehemu hizo kuhakikisha mazao yanafika ktk finished product hukohuko vijijini!...

Looh nchi za magharibi walicheka sana, kwa sababu nchi za magharibi wakulima ni asilimia ndogo sana na nchi nzima viwanda vipo mijini sio mashambani.

Well it worked for Chinese kwa sababu viwanda hivyo hivyo vilivyojengwa mashambani ndivyo leo hii vinazalisha mali zote za Marekani na Ulaya. Viwanda hivyo vingejengwa mijini ambako maisha ni ghali na hakuna cheap labour leo hii China ingekuwa ni hadithi nyingine. Wachina waliyaona haya mapema kabla ya mzungu.. vijijini wananchi wake hawahitaji mshahara mikubwa. Chakula rahisi wanalima wenyewe, nyumba zao za kuezeka matumizi ya umeme sio makubwa wala mtu kuwa na gari sio hoja, baiskeli zinatosha...Na kubwa kuliko yote watu hawana haja ya kwenda mijini kutafuta ajira.

Now tell me, who can come to invest in Tanzania ambako mshahara wa chini ni Tsh 60,000 - USD 50 kwa mwezi (tena hazitoshi bado) hali China kuna watu wenye uwezo huo huo kwa chini ya Tsh 30,000 - dollar moja kwa siku?. Kisha basi zana na vifaa vingi vinapatikana nchini humo huna haja ya kuagiza mashine expensive toka Ulaya.

Kwa hiyo mshikaji mkenge tumeisha vikwa na akina Judas na bahati mbaya wapo wanaoamini kabisa kwamba Tanzania tunaweza kwenda mbele hali kila kitu kinachojengwa Tanzania leo hii kimejengwa nchi nyingine za kiafrika miaka ishirini iliyopita. Tazama Nigeria, Kenya, Ghana, Ivory coast na kadhalika vitu hivi vimejengwa kwao toka miaka hiyo na hakuna walichokwisha fanikisha. Toka hadi zote za nchi za magharibi zianze 1970s jamani hata nchi moja basi tuseme inawezekana?.

Sababu kubwa ni kama ulivyosema... Afrika hatuna tamaduni nzuri ya mirathi ama kurithishwa! Warithi wote wa mali za wale waliokufa huwa kati ya mojawapo, aidha hawafahamu biashara nzima kwa sababu hawakuwahi kuhusishwa na biashara nzima ama warithi wenyewe ndio wamekuja jipatia nafasi ya kujitajirisha hali hawapo ktk mirathi....

Umeona wapi Mjomba (Mwinyi na Mkapa) anakuja kudai urithi mbele ya watoto wa marehemu (Warioba na JM) na wamepewa hali wajomba wenyewe wana familia zao, jua kali walikuwa wakiyumba na maisha!...man, ONLY IN AFRICA!.

Jamani tujifunze kuandika WILL na tuwafundishe watoto wetu kazi zetu, vision zetu na hata nani marafiki na adui wetu. Huu ndio utamaduni wa nchi nyinginezo na katika kufanya hivyo utaweza kufahamu nani anaweza kuendeleza mirathi yako sio maneno ya mtu mezani wakati wa kula..
 
Wazee,

Tokea uingie msemo wa “Globalization”, imekuwa ni vigumu kuongea siasa ya Ujamaa hadharani unless uwe na kichwa mithiri ya kile cha “Mwendawazimu” kama alivyosema Nyerere mwenyewe. Labda hii siasa ya Ujamaa tuiweke pembeni, hivi kuna dosari gani katika siasa ya kujitegemea? Hii sera ya kujitegemea imechukuliwa na sera gani katika nchi yetu? Kuanzia ngazi ya mtu binafsi mpaka ngazi ya Taifa, ukikataa kujitegemea unataka nini?
 
Mzee Kyoma,

Ninaomba kuuliza hawa Wachina wantumia siasa gani, ya Ujamaa au Kujitegemea? Na hawa kina Chavez na Morales nao wanatumia siasa gani? Maana hapa ninaona kuwa huenda ujamaa una tafsiri tofauti nyingi, kwani nia na madhumuni ya hizi siasa za Uchina, Venezuela, na Bolivia inaonekana ni ile ile ya Mwalimu na bongo, na Mwalimu si ailkuwa anaiga Uchina au?
 
Kyoma,
Unajua unaweza kuuliza wasomi mia moja Tanzania kuhusu swala hili na kila mmoja akaja na jawabu lake. Na sababu kubwa ni kwamba kila kitu tumeiga badala ya kuelewa elimu yenyewe tunayofundishwa kama vile hesabu...

KUJITEGEMEA hata mabepari walikuwa au wanaendelea kuwa na malengo hayo hayo. UJAMAA ni mfumo wenye maana kubwa sana zaidi ya jina lenyewe hata baadhi ya sera za kibepari zipo kijamaa. Tatizo kubwa hapa ni jinsi ya kufikia mafanikio ya kujitegemea ama Ujamaa wenyewe, yote inategemea na mtazamo wa mhusika.

Kuna msemo mmoja watu tunaweza bishana hadi kesho.

Nani muhimu zaidi ktk mafanikio ya kiuchumi - TAJIRI au MWAJIRIWA...

1. Kuna fungu linalosema Tajiri:- Muhimu ni tajiri KURIDHIKA na mfumo wa biashara ili kumwezesha kuendesha atakachowekasha kiurahisi, laa sivyo (asipo -invest), wafanyakazi watakuwa hawana ajira, kama kazi haitafanyika -basi uzalishaji ni zero.

2. Fungu la Pili wanasema wafanyakazi:- Bila wafanyakazi KURIDHIKA na mfumo mzima wa ajira, huyo tajiri hawezi kuzalisha kitu peke yake pamoja na kuwa na utajiri wake kwa hiyo wafanyakazi ni muhimu zaidi.

Hadi hapa half time, bao mshikaji ni bila bila. Sijui kama mfano huu umeeleweka.

Ukitazama kiundani utaona kwamba tajiri kuridhika ina maana moja tu faida kubwa. Na wafanyakazi kuridhika ni mapato zaidi... kwahiyo hapa ibilisi mkubwa ni FEDHA.

Na mfano kama huu ndio ulitumika sana ktk kutenganisha Ujamaa na Ubepari...I mean inachanganya akili za watu kuchagua hasa kwa watu maskini kwani hilo fungu la kwanza haliwezi kutoka kwetu. Ukichagua la kwanza ndio umekubali kutawaliwa kiuchumi hivyo kujitegemea hakuwezi kutokeao na ukichagua la pili, mshikaji huna mtaji - kujitegemea ni ndoto ya mchana!

Mzee Es, tatizo la Ubepari leo hii sio ukoloni wa utawala mathalan malkia....sasa hivi mkoloni ni mtu yeyote mwenye nguvu ya fedha! Big Corparates ndio wanaoendesha uchumi wa nchi sio tena koloni. wakati ule tulipokuwa tukitawaliwa mapato yote yanayotoka nchi maskini yalikuwa mali ya watawala yaani Malkia, serikali za Marekani, France, Ureno n.k lakini leo hii watawala ni mafia - wafanyabiashara wakubwa ambao wamezishika serikali kuliko hata malkia. mwenyewe unaona sasa hivi CCM sio chama tena tawala ila kuna kitu kinaitwa Mtandao. Bob Mtandao ndio unatawala kila nchi, dunia nzima. Akina Chavez, China, Venezuela na wengineo ni wapinzani wa hiyo mitandao (big corps) kama unavyofanya wewe na utawala wa JK.

Bahati nzuri vita yako ni baridi na wanaiona haina madhara makubwa kwao lakini mshikaji JK kawekwa kati kama akina Bush na wengineo lazima wafuate wanayoagizwa laa sivyo Ikulu hawawezi kukaa hata usiku mmoja.
 
Mzee ES

Hakuna ubishi kuwa China wanatumia siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Kulikuwepo na dhana potofu miongoni mwa wapinga ujamaa kuwa binadamu ana asili ya ubinafsi hivyo, hawezi kuisimamia mali ya Umma kwa ufanisi. Wachina wameweza kuendesha mashirika yao ya Umma kwa nidhamu na ufanisi wa hali ya juu bila ufujaji wa fedha kama uliyoyaua mashirika ya nchi yetu.

Wachina walifunga milango kwanza na kuimalisha soko lao la ndani. Walihakikisha watu wao wanapata elimu ili waweze kuyaendesha mashirika yao kitaalamu. Waliyavalisha nepi na kuyapangusa kinyesi kilichotokana na ufisadi wa wale walioendekeza tabia ya ubinafsi. Mwisho, walijenga utamaduni wa kutokuwatania watu waliofuja fedha za Umma.

Nyerere aliwahi kusema pale Kilimanjaro Hotel kuwa the rule is to protect the weak kwa kusudio la kumfanya awe strong ili aweze kushindana. Hivi ndivyo Wachina walivyofanya na matunda yake unayaona sasa. Baada ya kuona kuwa wako imara, wakafungua milango kwa ajili ya mashindano na makampuni makubwa kutoka pande zote za dunia. Wamarekani walikuwa wa kwanza kunusa pua zao nchini China. Wamekuta Makampuni mengi yanamilikiwa na Serikali (Umma), lakini yako “tough”.

Wamarekani ndio vinara wa kushinikiza mfumo huu wa soko huria wakiamini kuwa makampuni yao yako imara. Mambo yanaanza kuwatokea puani. Angalia mfano wa WAL-MART ambao ni mfumo wa maduka makubwa nchini Marekani unaokua kwa kasi. Kila sehemu wanapojenga maduka yao, yale yaliyokuwepo jirani yanafilisika na kufungwa. Hakuna mfanyabiashara wa maduka nchini Marekani anayependa WAL-MART ijengwe karibu na duka lake.

WAL-MART wanauza bidhaa zinazotengenezwa China na kwa bei rahisi. Kuna mijadala ya hali ya juu kuhusu uzalendo wa mmiliki wa WAL-MART. Wamarekani wamefikia mahala na kuamini kuwa wanahitaji kufunga mipaka na kutoruhusu bidhaa kutoka nje mpaka makampuni yao yatakapo pata akili timamu. Hawa ndio wanazishinikiza nchi masikini kama yetu ili vijikampuni vyetu vishindane na makampuni yao makubwa. Nyerere aliwahi kuuliza kuwa “can NBC open branch in New York?”

Huu ni mfano tosha wa kunifanya niamini kuwa ile dhana ya kwamba shirika la Umma haliwezi kuendeshwa kwa faida ni potofu. Wachina wameweza kufanya hivyo na wanayasimamia bila utani. Mashirika yetu yaliendeshwa kisiasa zaidi kuliko kitaalamu. Viongozi walifuja fedha kwa kiasi kikubwa bila kudhibitiwa. Tulichotakiwa kufanya sio kuanza upya na mfumo mwingine tofauti. Tungeiga mfano wa Wachina badala ya huu tulionao usiowanufaisha wananchi.

Dhana ya kwamba binadamu ana asili ya ubinafsi na hawezi kusimamia shirika la Umma kwa ufanisi imedhalilishwa na matendo ya Wachina. Inakuwa je binadamu huyo huyo asiyeweza kusimamia shirika la Umma aweze kukusanya kodi kutoka katika shirika la Kibepari kwa manufaa ya Umma? Ubepari unafunika tabia ya ubinafsi? Jibu lake tunajionea wenyewe kinachoendelea sasa hivi nchini kwetu.

Ni kweli kuwa mashirika yetu mengi yalikuwa yanaendeshwa kwa hasara. Tulichokifanya ni kuyakimbia matatizo. tumeluka mkojo na kuanguka kwenye kinyesi. Hivi TANESCO ya sasa ni bora kuliko ya zamani? Tunabinafsisha hata maji? Tumejaliwa maziwa makubwa duniani. Kwa nini Serikali isikope fedha na kuhakikisha inasambaza maji kwa raia wote wa mijini na vijijini alafu ikaweka mfumo bora wa kukusanya mapato? Maji sio ulevi, ni mahitaji muhimu kwa binadamu hivyo hakuna asiyeweza kuishi bila kuyanunua. Hata biashara ya Maji inatushinda? Umeme je?

Nchi yetu ingetafuta soko la ndani kwanza. Kopa fedha alafu jenga barabara za kuunganisha mikoa yote ili kuimalisha soko la ndani. Hakuna mazao kuoza tena Mbeya wakati Dodoma wanakufa na njaa.

Tumebahatika kuzungukwa na nchi nyingi zinazopigana kila kukicha. Miundo mbinu ya hizo nchi imebomolewa kwa kiasi kikubwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. Kwa nini tusiwauzie maji Wanyarwanda, Warundi, na Wazaire? Kinyume chake, sisi ndio tunao nunua bidhaa kutoka kwao na hatuna cha kuwauzia. Mfano Wazaire wameusambaratisha utamaduni wetu kwa kutuuzia “ekibinda nkoye”. Nashangaa Dar es Salaam kuna tatizo la mgao wa Umeme. Kule Bukoba Umeme haukatiki hata siku moja. Nchi yetu inanunua Umeme wa Bukoba kutoka Uganda.

Kuna ukweli pia kuwa Serikali inabidi ijiondoe kwenye mambo ya biashara ili iweze kusimamia mambo ya msingi kama ukusanyaji wa kodi, na huduma kwa wananchi. Lakini lazima tukubali kuwa mifumo yote miwili ikisimamiwa kwa uadilifu mkubwa ina manufaa kwa nchi husika.

Tofauti kubwa kati ya Ujamaa na Ubepari ni kwamba katika Ujamaa, shirika la Umma kama ilivyokuwa TBL linaendeshwa kwa asilimia mia moja na wananchi (Umma). Likipata faida kwa mfano $ 100.00 linalipa kodi Serikalini kutokana na viwango vilivyowekwa labda tuseme $ 20.00. Kiasi kinachobaki yaani $ 80.00 kinakuwa cha wote (Umma). Likipata hasara, basi inakuwa ni ya wote (Umma).

Katika Ubepari, Shirika linamilikiwa na mtu binafsi au kikundi cha watu. Linapopata faida kwa mfano $ 100.00 linalipa kodi Serikalini kutokana na viwango vilivyowekwa labda tuseme $ 20.00. Kiasi kinachobaki yaani $ 80.00 kinamilikiwa na mtu binafsi au kikundi cha watu. Likipata hasara, inakuwa ni ya mtu binafsi au kikundi cha watu.

Katika mifumo yote miwili, yaani Ujamaa na Ubepari, Serikali inapata kodi ya $ 20.00. Ndiyo maana mataifa yaliyoendelea hayana mzaa katika ukusanyaji kodi. Mfano; Kiuendeshaji, shirika la kukusanya mapato la Marekani (IRS) linafanana na lililokuwa shirika la Kijasusi la Urusi (KGB). Usipolipa kodi Marekani utajuta kuzaliwa.

Hata hivyo, katika Ujamaa pamoja na kupata kodi ya $ 20.00, pia ile $ 80.00 ni ya Umma. Inaweza ikatolewa $40.00 kupelekwa kwenye sekta muhimu kama Elimu na $ 40.00 ikabaki kukuza mtaji wa hilo shirika. Ndiyo maana enzi zile tulikuwa tunasoma bila kukopeshwa, tunalipiwa nauli, au hatukulipa ada kubwa shuleni. Pia kwa wale waliobahatika, tulikuwa tunapata msosi wa nguvu pamoja na matunda katika shule zote za kutwa au kulala zilizomilikiwa na Serikali.

Kuanza upya kuna madhala yake. Mfumo tulioanza nao wa Kibepari, Serikali inategemea kodi ya dola $20.00 tu. Kama Serikali haikusanyi kodi, basi hakuna kiasi cha kufidia gharama katika sekta nyingine muhimu. Inabidi tukakope fedha au tuwe ombaomba. Tumeyagawa Mashirika yote ya Umma kwa “wawekezaji”. Kutokana na sheria ya uwekezaji Act No. 26 of 1997, Mwekezaji anatakiwa kurudisha gharama zake za uwekezaji kwanza kabla ya kuanza kulipa kodi. Sheria imetoa kipindi cha miaka mitano kufanikisha zoezi hili.

Tulikuwa na mashirika yaliyokuwa yakiendeshwa kwa hasara na mengine kwa faida. Ni makosa makubwa kumkabidhi Mwekezaji shirika kama TBL na kumwambia asilipe kodi kwa miaka mitano. Kutokana na Mnyambulisho wangu ambao sio wa kitaalamu, ina maana Serikali haipati kitu chochote cha maana kutoka katika shirika lililokuwa linaendeshwa kwa faida.

Kutokana na udhaifu katika sheria ya uwekezaji, kumekuwepo na wasiwasi kuwa baada ya miaka mitano, Mashirika ya kimafia yanauzwa kwenye Makaratasi ingawa wamiliki wanabaki kuwa walewale. Jina linabadilishwa na shirika halilipi kodi kwa miaka mingine mitano. Kuna mjadala wa kwa nini kila baada ya miaka mitano baadhi ya mashirika nchini kwetu yanabadilisha jina? Mfano; Hotel ilianza kuitwa Sheraton, miaka mitano ikabadilishwa na kuitwa Royal Palm, na baada ya miaka mitano ikaitwa Moven Pick. Bila shaka kuna jambo!

Wenyewe wanasema kuwa Milango ikiwa wazi haingizi hewa safi tu bali hata Mainzi. Tumefungua milango bila kuangalia tunawafungulia akina nani. Mashirika yaliyokuwa ya Umma yanafilisiwa, madini yetu yote yanapolwa, sisi tunakwenda kukopa nje. Mchezo huu wa miaka mitano mitano ukiendelea, hakuna kitakachobaki. Ni kweli Mzee Mkandara, hata Nyerere aliwahi kusema kuwa Ubepari una sifa ya Unyama. Kinachoupa Ubepari sura ya Utu ni huduma za kijamaa zinazoingizwa ndani ya mfumo wa kibepari na watu wanaotetea Utu wa Mtu. Hawa waheshimiwa wanataka “Maxim profit” hata kama ni kumdhalilisha Mtu.
 
Wazee vyote msemavyo ni kweli kweli tupu! Hakuna cha nyongeza!

Kuna kitabu hichi nimekiona: The Silent Takeover : Global Capitalism and the Death of Democracy by Noorena Hertz.

Nimesoma summary yake tu wiki mbili zilizopita na nika amua kukinunua, bado sijakianza ila inaonyesha kitanifumbua macho zaidi.

Capitalism in its extreme sense kama wamaerkani wanavyo practice ni tishio la democracia. Sababu mojawapo kubwa ikiwa kuachia corporates kuendesha uchumi wa nchi ambapo wenye navyo wanzidi kuwa navyo na ambao hawana huzidi kupungukiwa!
Hivyo basi hawa wachache wenye fedha hufanya maamuzi yao si kwa kujali maslahi ya umma, bali kujali maslahi ya ma millioni yao, hii confilct of interest ndio inaleta mgogoro na tunaona ma "JUDAS ESCARIOT" wakiongezeka!
Kila siku husali (kwa mungu yeyote anayeniskia) kuwa aniwezeshe kufikia cheo cha kuweza kuongoza umma kwa manufaa ya umma wa watanzania lakini cha muhimu zaidi ni aniepushe na jini la tamaa na kujilimbikizia mali ambalo linakamata kile mtu afikapo ngazi za juu!

Dual citizenship itawaongeza hawa ma "Judas Escariot" kwasababu believe me, uamuzi wao si kwa manufaa ya wananchi bali kwao wenyewe.

Capitalism is not an ideal governance ideology but the quickest way to make a dollar.
Mahatma Gandhi aliulizwa what is his opinion on western civilisation/capitalism.
He said "My opinion on Western Civilisation is that it is a good IDEA."

(and he stopped their.)
 
Tanzania: Dar China Trade Reaches Climax

East African Business Week (Kampala)

June 12, 2006
Posted to the web June 12, 2006

Jacob Bondia
Dar Es Salaam

Bilateral trade between China and Tanzania has increased by almost 70% climaxing US$47million last year.

According to Mr Zhou Jun, the secretary of Bilateral Trade at the Chinese Embassy in Dar es Salaam, imports by China from Tanzania went up by 150.1% valued at $17million while exports from China to Tanzania increased by 40.6% to $3.0 million.
Mr Zhou told this paper last week that the increase is attributed to the special preferential tariff (SPT) agreement-involving 190 tariff items-to the most undeveloped countries in Africa.

"Tanzania uses its quarter well under the agreement. There is still a room for more export to China in the coming days," he said.

Last year, the main importations from Tanzania were cotton, gold minerals, and sisal among other commodities.

Mr Zhou said under the special tariff agreement-tariff six-China has imported from Tanzania various products worth $12.13 million which promoted bilateral trade.


Products under tariff six include sesame seeds, coca beans, wet goat skins, sea shells, waste plastic and seaweeds, among others.(this is good)

"It is believed that with further understanding of the agreements, more preponderant products originated in Tanzania will be exported to China in the coming days," Mr Zhou said.

In recently years, there have been frequent business relations between the two countries. In 2002 and 2003, China Council for the Promotion of International Trade (CCPIT) participated in the Dar es Salaam International Trade Fair. This year's fair set to start next month will be presented by 15 Chinese companies.

Hesabu ni ndogo bado, 17 million on export and 3 million import, lakini inatia moyo. Inabidi tufikie tripple figures in the mid hundreds of millions tukiendelea kuhakikisha tofauti kubwa kati ya thamani ya tunavyowauzia na thamani ya tunvyonunua! (Seems simple until u see the decisions these leaders make, we can't leave anything to chance with these goons.)
 
Fikiraduni,
Good to see you again man. Unasema tusiongelee China lakini mfano wake lazima uangaliwe. Unakumbuka a few years ago, China iliwekwa kwenye kundi moja la "developing countries" kama akina sisi. Lakini leo wenzetu they are bigger than the Asian tigers. I am sure Mjapani leo anatetemeka katika suruali yake ukimtajia China. But how did they get there? Kama alivyoeleza Bob Mkandara, they invested in the rural areas. They built their industries there, they invested in kilimo, education, and today they produce cheaply than if they had built their industries in the cities.Wamekaribisha wawekezaji kama vile VW, GM, Ford etc. lakini wakati huo huo wamo mbioni kutengeneza motakaa zao wenyewe. Mwaka kesho nasikia katika soko la Marekani Mchina anaingiza motakaa yake. Na tofauti na sisi hawakuwaachia wageni wachukue kila kitu. Kwa hiyo kuna mengi tunayoweza kujifunza kutoka kwa hawa rafiki zetu ambao Mwalimu aliwatambua hata kabla ya wao kuanza kutambaa. :)
 
Fikraduni,

Mimi nadhani Azimio la Arusha halikufa kwa sababu ya kutokueleweka. Lilipata umaarufu lililonao kwa sababu ya kutangazwa. Viongozi wetu waliamua kulizika sio kwa sababu ya kutokulielewa, bali hawakupenda lilichosimamia. Kumbuka ndani ya Azimio la Arusha ilikuwemo “Miiko ya Uongozi” ambayo haifanani na matendo ya viongozi wa sasa. Azimio la Arusha lilipinduliwa na Azimio la Zanzibar. Ninajiuliza swali kwamba, Azimio la Arusha na lile la Zanzibar lipi lilitangazwa au kujadiliwa sana? Hivi watu walipata nafasi ya kiliunga mkono au kulipinga? Lakini lipi linashamiri sana na kukumbatiwa na viongozi waliomwengi? Hata hivyo, ni lipi lililenga kulinda maslahi ya wananchi?

Nakubaliana na wewe kuwa Kiswahili kilifanikiwa kwa sababu ulizozitaja. Kumbuka kwenye Kiswahili hakuna ulaji. Kama kukua kwa Kiswahili kungekuwa na mahusiano ya moja kwa moja na kubana bana watu kuhusu suala la mlo, kingekwisha zikwa zamani. Hawa viongozi tulionao siwaamini kabisa. Tajiri akiwaambia kuwa siwapi fedha mpaka Kiingereza iwe ndio lugha ya Taifa, watafuta mitaala yote mashuleni. (Joke). Hata hivyo, Kiswahili kulikuwa kupitia juhudi za makusudi zilizofanywa na Viongozi pamoja na wananchi. Ngoma, Nyimbo, Maigizo, Ngonjera, Majigambo, Vitabu vya hadithi na simulizi za kale, Bendi za muziki, mashuleni, etc. Fikraduni, umekwisha fika Tanzania na ukasikiliza nyimbo za kizazi kipya na ukajaribu kuweka maono ya mwelekeo wa Kiswahili baada ya miaka 40 kuanzia sasa?

Nyamgluu

Hizo takwimu zinavutia sana kuzisoma. Hata hivyo, zimetolewa kwa ujumla sana kiasi kwamba haieleweki kati ya hizo bidhaa zinazonunuliwa na China, Tanzania kama nchi inapata kiasi gani? Au ni watanzania wangapi wanamiliki migodi ya maana ya Dhahabu? Hii migodi si ilibinafsishwa na hawa waheshimiwa wanaishia kulipa asilimia 3 ya mapato yao kwa sasa. Hata tukiuza dhahabu China yenye thamani ya $17 Million, tunaweza kusema nchi yetu inanufaika na huu uuzaji? Mimi nadhani Makaburu, Wamarekani, na Wakanada ambao wanamiliki hii migodi ndio wanapaswa hasa kufurahia hizi takwimu. Hivi kuna wakulima wa kawaida wanaomiliki mashamba ya Mkonge?

Hata hivyo, naona kuna mazao na mbegu za kila aina. Labda hii inaweza ikawanufaisha wananchi wa kawaida.
 
Mzee FD,

Heshima yako mkuu, katika society yoyote ile lazima kuwa na viongozi au kiongozi, sio kila wakati ni lazima kiongozi awahusishe wananchi katika maamuzi muhimu kwa ajili ya their future, Mimi sio kabisa fan wa JKN, lakini kwenye hili la Wachina ni lazima kumpa heshima yake kuwa alikuwa na vision ambayo ni moja kati ya important skill kiongozi anapaswa kuwa nayo,

kuwashirikisha wananchi alijitahidi, tena afadhali yeye wabishi aliwaweka kizuizini Mao aliwaua wote waliopinga, baada ya Mao kufa kuna waliojaribu kugeuza muelekeo wa China, guess what? Wote walifungwa au kuuliwa na wengine walipigwa marufuku kushiriki siasa tena! Lakini angalia kwetu, hata kabla Mwalimu hajafariki tayari wakaua Azimio La Arusha, wakapitisha IPTL, wakabinafsisha kila kitu, sasa Mwalimu hayupo niambie wamefanya mangapi maovu?

Mwalimu aliwashirikisha wananchi na viongozi, tatizo ni wananchi wasio kuwa na mwamko wa kisiasa, elimu ndogo ya kuelewa faida na hasara ya maamuzi makubwa au ya kitaifa kisiasa, na viongozi waongo na wanafiki tena nitakutajia kwa majina viongozi waliokuwa karibu na Mwalimu ambao walipaswa kufa kabla ya kukubali kuona mambo ya Mwalimu yanaharibiwa,

Kingunge, Nsa Kaisi, Warioba, Butiku, Salimin, Natepe, Mwakanjuki, Makame, Nassoro Moyo, Lusinde, Sozigwa, Mnauye, Anna Abdallah, Kawawa, Jumbe, Salim, Msekwa, Musuguri, Mongella, Tandau, Mwakawago, Makweta, Siovelwa, Sozigwa, Ndejembi, Sarakikya, Mbita, Munanka, Bomani, Kahama, Mwangoka, Kisumo, Mama Swai, Mungai

hao juu ndio viongozi waliokuwa karibu na Mwalimu, na mpaka leo hawa bado wana influence kali katika siasa za bongo kwani hata JK mwenyewe asingeenda kokote katika uchaguzi bila ya kukubaliwa na 75% ya hawa wazee, hawa ndio waliopaswa kuweka mguu chini na kuwakatalia hawa kina BM maamuzi yao machafu. BM hayumo kwenye hilo kundi juu kwani he was never close to Mwalimu kabla ya uchaguzi wa 1995, BM siku zote alikuwa karibu na Butiku lakini sio Mwalimu kwa sababu elewa kwamba kabla ya kuwa rais BM hakuwahi kuchaguliwa hata NEC, kila alipogombea alikuwa akishindwa, kule Uchina kuna viongozi kama hao juu waliobaki katika chama hawayumbi hata siku moja katika kusimamia misimamo ya maendeleo ya nchi yao iliyowekwa china na Mao na mzee DeoPing!

Mzee FD Mwalimu alifanya ya kutosha, somebody had to take it to another level, badala ya kuvunja misingi yake bila kuwa na cha ku-replace, China ni mfano mkubwa wa kuigwa na sisi kwani kama walivyosema waliotangulia, ni kwamba at one point sisi na wao tulikuwa tunawekwa meza moja nao na wakubwa wa West!
 
Mzee ES,
Ni kweli Butiku alikuwa na jukumu kubwa kumshawishi amkubali/amwunge mkono Mkapa in 1995. Lakini baada ya hapo Mkapa alipata marafiki wapya wakamshawishi akeep away from these people from Musoma. You know what? Tangu Mkapa alipoingia Ikulu he has never had a one on one with Butiku? Kila mara Butiku akipiga simu walikuwa wanampa chenga. Hata ule wakati Mkapa alipovimba miguu Butiku wanted to visit but he never got an appointment. That is the kind of person Mkapa was. Kitu kilichinisikitisha zaidi, marehemu Mzee Bomani told me what Mwalimu told him about NBC. You know, by 1997 Mwalimu was going around the country talking to the wananchi about keeping NBC in Tanzanian hands. Mkapa did not like that. Alimfuata Butiama akamwambia Mwalimu naomba uache kuzungumzia NBC. Trust me and see what I will do. So Mwalimu goes back to Butiama and keeps quiet. Guess what Mkapa did? Aliwakabidhi makaburu benki ya wananchi wa Tanzania na mpaka leo tuna kilio kisicho na mwisho wake. Sasa kama huyu si Yuda ni nani? And see how much the Kaburus have made by selling NBC to Barclays. Afadhali hata sisi wenyewe tungekubaliana na Barclays in the first place we would have gotten a better deal!
 
Mkandara na Kyoma,

Mpo sahihi katika somo la siasa, ila nadhani lilikosewa namna ya kulifundisha. Ngoja nitoe hadithi, Katika somo la Political Economy(A level nilisoma Economics), Tulikuwa tunasoma Socialist analysis of capitalism, Mfano wanapozungumzia ku calculate Rate of exploitation, wanadai kama unalipwa Tzs 1,000 per hour na kazi yako ni kuweka kreti za bia kwenye conveyor belt inayoenda speed X, then kukawa na change of technology, same conveyor belt ikawa inaenda kasi mara mbili 2X na wewe ukaendelea kulipwa 1,000Tzs per hour basi Rate ya exploitation is 100%!!!!! Hiyo ndiyo ilikuwa fikra ya Ujamaa tuliokuwa tunaufundisha, tulilelewa kuuchukia Ubepari kama wa palestina wanavyochukia WaIsraeli. Ilitakiwa ifundishwe kuwa hapo Labour productivity imeongezeka mara 2.To me that was wrong approach, fundisha ubepari unafanyaje kazi, fundisha ujamaa unafanyaje kazi, elezea uzuri wa ujamaa. Convice people dont put ideology in their heads!, hilo linakuwa tatizo pale wanapoenda nje ya nchi na kujifunza mambo mengine!

Turudi sasa kuhusu China, Kwanza so far tumekubaliana kuwa ELIMU is a prerequisite, Elimu kwa wataalamu ambao wakimaliza ujue utafanya nao nini, tatizo elimu ilikuwa ikitolewa watu wanaishia nje, hatukuwa na mipango.

Pili Capital, tutapataje capital?, we can reduce Govt expenditures by restructuring Govt depts, tunaweza kuondoa mlolongo wa vyeo, Katibu tawala mkoa na mkuu wa mkoa = duplication. Mkuu wa wilaya, meya, mkurugenzi wa wilaya - mmoja aondoke. tupunguze wizara etc etc Nadhani wataalamu wataleta mbinu tu.

Tatu, kuwe na mikakati ya kuzungusha pesa humuhumu, Ukichukua sera za CUF na chadema unatekeleza hili bila taabu. Muheza kuna machungwa, tutumie TASAF au kama inaweza kuundwa chombo cha kuunganisha wananchi mwenye mtaji wa millioni au laki tano, ukipata kama 100, basi unawafungulia ka kiwanda kidogo cha kusindika matunda (kuna mtu alishatoa wazo hili hapo juu), wanakuwa wamiliki na wanafanya kazi hapo, unawasaidia wataalamu wa juu tu!

Nne, Wahandisi, hawa ni kiini cha kunyanyua uchumi, kama unataka kubadili kabisa mwelekeo wa uchumi basi inabidi uwatayarishe hawa na uwe na Labs za kutosha, yaani inatakiwa heavy investments on these guys. Pale Udsm kuna Bicco, sijui bado wapo?, hawa ndio watatengeneza mashine zote tutakazotumia kuwa wezeshea wananchi, How do they do that? peleka hata nje miaka mitatu wakaibe technologia, waibadili kidogo iendane na hali halisi.

Kyoma umeongelea Takeoff, Yes BWM alitakeoff bila kujua ndege inaelekea wapi, ila mradi aondoke uwanja wa Mwalimu JKN, unajua akatua wapi? akatua kwa akina Escobar (yule gwiji wa madawa ya kulevya aliyekamatwa), Huko Boyz to men wamechukua nchi wanaelekea Marekani! Jamani turudi Tanzania, Nilimsikia rais wetu anataka kufufa Ranch zilizokufa, good one.

Naomba tukae chini kila mmoja atoe TUFANYE NINI KUELEKEA WALIPO WACHINA SASA HIVI. Once done mmoja anaweza kutoa summary, Mzee Es na wengineo wanaweza kuwakilisha kwa JK

FD
 
fikiraduni said:
Naomba tukae chini kila mmoja atoe TUFANYE NINI KUELEKEA WALIPO WACHINA SASA HIVI. Once done mmoja anaweza kutoa summary, Mzee Es na wengineo wanaweza kuwakilisha kwa JK

FD

Above is what is The most ambitious suggestion on a Tanzanian chat forum!
 
Mzee Jasusi,

Aahaa aksante, huwa nipo nipo, ukiona nakaa kimya ujue wamekuja watu na wana represent vilivyo, Thank you Kyoma kujitokeza hadharani na kutoa michango.

BTW tunachangia mada nyingi tu sehemu mbalimbali tena almost kila siku!

Nipo

Nyamgluu, sawasawa mzee!

FD
 
Back
Top Bottom