The late Justinian Rweyemamu, Tanzania's foremost economist

I truly agree with you. This man was a genius. Tatizo, uongozi wa nchi kipindi kile walim'frustrate, hawakutaka ushauri wake na ikabidi aende zake UN. Also, do note that this man had his first international publication at the age of 22, wakati akiwa undergraduate kule US. He is the youngest Tanzanian to hold the title of 'Professor', being one at 27 (mwaka 1969).
Ukitaka kusoma zaidi jinsi gani alivyokuwa makini ktk umri wake mdogo, chini ni mchango wake ktk jarida moja maarufu kuhusu masuala ya maendeleo Africa, 1971 (hapa akiwa akiwa na umri wa miaka 28). I don't know if the paper is publicly available.

http://www.jstor.org/sici?sici=0022-278X(197110)9:3<453:TCOPIT>2.0.CO;2-Y&cookieSet=1

Mtati
 
Nina kitabu chake cha 'Underdevelopment and Industrialization in Tanzania: A Study of Perverse Capitalist Industrial Development' kilichochapishwa na Oxford University Press mwaka 1973. Pia nina mkusanyiko wa makala zake zote muhimu katika kitabu cha 'Third World Options: Power, Security and the Hope for Another Development' kilichochapishwa na Tanzania Publishing House (TPH) mwaka 1992. Tatizo ni kuwa siwezi kukuuzia maana hata mimi navihitaji ili vinisaidie kupata economic formula ya kuinusuru Tanzania kutoka katika lindi la Mkukuta. Ila nakushauri uende TPH pale mtaa wa Samora ukakiulizei hicho cha kwanza na pia uende ofisi za Oxford, bahati mbaya nimesahau siku hizi wamezihamishia wapi, zamani zilikuwa karibu na maktaba kuu.

Ni kweli huyu jamaa alikuwa kichwa sana hasa katika development economics ila sidhani ni haki kumuita Tanzania's foremost economist bila kumpambanisha na kina Lipumba, Wangwe, Ndullu, Semboja n.k. Kwani umetumia vigezo gani kumpa hiyo title? Alafu ukumbuke alibwaga manyanga ya uchumi wa bongo, uzalendo ukamshinda akamwacha Nyerere kwenye mataa na kwenda kutumika huko ughaibuni!Mpaka leo kuna hisia kwamba aliishia kuwa mamluki wa kitaaluma huko katika mashirika makubwa ya kifedha ya dunia kama vile IMF na WB yaliyotunyonya sana enzi zile za SAPs!
 
asante Companero kwa maelekezo. Kitabu chake 'Third World Options' ninacho tayari. Tanzania ndio tumejaliwa kupata heavyweight scholars in development Economics. No doubt Wangwe, Semboja etc are equally respected. Kumuita Rweyemamu 'TZs foremost scholar' ninamaanisha msomi wetu wa kwanza aliyekuwa na 'impact' kimataifa ktk nyanja za Uchumi. Pamoja na hayo wote uliowataja hapo juu ni wanafunzi wake Prof. Rweyemamu, ingawa walikuwa wanapishana kiumri kidogo tu. Yawezekana ya kwamba kulikuwa na wasomi wachache enzi hizo, lakini his stature in the field was renowned globally (soma Preface ya Third World Options) kwa kipindi kidogo alichokuwa active. Yasemekana, alimkimbia Nyerere kwasababu mwalimu hakutaka ushauri, na akaenda kujishughulisha na UN, na sio IMF wala WB.

Ninatafuta hasa paper yake “The formulation of an industrial strategy for Tanzania”, iliyochapishwa kwenye jarida 'Africa Development' Nº 1, vol. VI, Dakar: Codesria, january-april (1981).

Rweyemamu alikuwa bingwa,professor at 27? Impact yake ingekuwa kubwa kama asingekufa bado mdogo,angekuwepo mpaka sasa im sure tungekuwa na nobel prize winner. Huyu jamaa hakuwa tu mwanauchumi, alikuwa mathematician, philosopher kabla hajafikisha 40. nimgependa kujua hostoria zaidi ya maisha yake kama kuna mtu anaijua.
 
Habari za Prof Rweyemamu nilizisikia wakati nilipokuwepo pale Mlimani nikisoma Economics. Ni kwamba wakati akiwa seminari kule Bukoba miaka ya 1950s mapadri waalimu waligundua kipaji chake masomoni. Akiwa ktk mwaka wake wa mwisho wa sekondari wakamsaidia kupata Scholarship kwenda Fordham University, NY. Mwenye umri wa miaka 19, akaelekea Marekani akiacha nyumbani mbiu ya Uhuru zikilia. Pale Fordham alisoma BA ya Economics na Mathematics, na akawakimbiza kisawasawa wanafunzi wenzake. Niliambiwa ya kuwa marehemu akiwa chuoni alikuwa mweka hazina katika Klabu ya Uchumi ya hicho chuo chake. Alipomaliza degree ya kwanza, alijiunga chuo kikuu cha Harvard na kusomea PhD ya Uchumi. It is here where he published his great thesis on Tanzania's perverse industrial strategy. Miaka ya Sabini alirudi bongo na kuwa Dean pale Mlimani. Nyerere alipogundua umahiri wa bwana huyu mdogo, akampatia ukatibu wizara ya mipango na uchumi, na nafasi ya kuwa mshauri mkuu wa rais. Muelekeo wa Uchumi wa Tanzania ukaanza kumomonyoka, kutokana na sababu chungu mzima, Rweyemamu akaondoka nchini na kwenda Kufanya kazi Geneva, na baadaye New York ktk UN. Hadi alipofariki akiwa na umri wa miaka 40, alikuwa ameandika zaidi ya vitabu/paper 50.
Nadhani itabidi niwe official biographer..
Lakini ni kweli, wasomi wetu inabidi tuwaenzi. Chachage, Sokoine, Babu, Shivji etc pia, inabidi watu waandike life story za hawa watu. Ningeshauri watu wa mlimani waanzishe Chachage Prize, or JF Rweyemamu Prize for researchers/students on order to honour them.
 
nice biography katoma.. ndugu yako nini?
sasa hivi tu nimetoka google his 1964 paper. Yaani, akiwa na umri wa miaka 22, he published a paper "Development Planning in the United Republic of
Tanzania," in the United Nations (ECA) Economic Bulletin for Africa. (Vol. XII.
No.1
si mchezo. official biography yake inahitajika kuwapa vijana motisha.
 
Habari za Prof Rweyemamu nilizisikia wakati nilipokuwepo pale Mlimani nikisoma Economics. Ni kwamba wakati akiwa seminari kule Bukoba miaka ya 1950s mapadri waalimu waligundua kipaji chake masomoni. Akiwa ktk mwaka wake wa mwisho wa sekondari wakamsaidia kupata Scholarship kwenda Fordham University, NY. Mwenye umri wa miaka 19, akaelekea Marekani akiacha nyumbani mbiu ya Uhuru zikilia. Pale Fordham alisoma BA ya Economics na Mathematics, na akawakimbiza kisawasawa wanafunzi wenzake. Niliambiwa ya kuwa marehemu akiwa chuoni alikuwa mweka hazina katika Klabu ya Uchumi ya hicho chuo chake. Alipomaliza degree ya kwanza, alijiunga chuo kikuu cha Harvard na kusomea PhD ya Uchumi. It is here where he published his great thesis on Tanzania's perverse industrial strategy. Miaka ya Sabini alirudi bongo na kuwa Dean pale Mlimani. Nyerere alipogundua umahiri wa bwana huyu mdogo, akampatia ukatibu wizara ya mipango na uchumi, na nafasi ya kuwa mshauri mkuu wa rais. Muelekeo wa Uchumi wa Tanzania ukaanza kumomonyoka, kutokana na sababu chungu mzima, Rweyemamu akaondoka nchini na kwenda Kufanya kazi Geneva, na baadaye New York ktk UN. Hadi alipofariki akiwa na umri wa miaka 40, alikuwa ameandika zaidi ya vitabu/paper 50.
Nadhani itabidi niwe official biographer..
Lakini ni kweli, wasomi wetu inabidi tuwaenzi. Chachage, Sokoine, Babu, Shivji etc pia, inabidi watu waandike life story za hawa watu. Ningeshauri watu wa mlimani waanzishe Chachage Prize, or JF Rweyemamu Prize for researchers/students on order to honour them.

Ahsante sana Katoma kwa biography hiyo ambayo ni ya kiundani zaidi,wanasema the best are already dead, hizo information umezipataje?Au una undugu?Basi itakuwa vizuri ukiendeleza ule ukurasa wake kwenye wikipedia tukapata habari zaidi hasa kwa jinsi alivyo excel huko Amerika.
 
Wakina Rweyemamu ndio waliokuwa nshomile wenyewe originalQ!

Oh baba waitu, nshomile mpaka form four but no course!
 
Back
Top Bottom