epigenetics
JF-Expert Member
- May 25, 2008
- 269
- 79
Ningependa kuuliza kama kuna mtu anamfahamu Profesa Justinian Rweyemamu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature currently requires accessing the site using the built-in Safari browser.
asante Companero kwa maelekezo. Kitabu chake 'Third World Options' ninacho tayari. Tanzania ndio tumejaliwa kupata heavyweight scholars in development Economics. No doubt Wangwe, Semboja etc are equally respected. Kumuita Rweyemamu 'TZs foremost scholar' ninamaanisha msomi wetu wa kwanza aliyekuwa na 'impact' kimataifa ktk nyanja za Uchumi. Pamoja na hayo wote uliowataja hapo juu ni wanafunzi wake Prof. Rweyemamu, ingawa walikuwa wanapishana kiumri kidogo tu. Yawezekana ya kwamba kulikuwa na wasomi wachache enzi hizo, lakini his stature in the field was renowned globally (soma Preface ya Third World Options) kwa kipindi kidogo alichokuwa active. Yasemekana, alimkimbia Nyerere kwasababu mwalimu hakutaka ushauri, na akaenda kujishughulisha na UN, na sio IMF wala WB.
Ninatafuta hasa paper yake The formulation of an industrial strategy for Tanzania, iliyochapishwa kwenye jarida 'Africa Development' Nº 1, vol. VI, Dakar: Codesria, january-april (1981).
Habari za Prof Rweyemamu nilizisikia wakati nilipokuwepo pale Mlimani nikisoma Economics. Ni kwamba wakati akiwa seminari kule Bukoba miaka ya 1950s mapadri waalimu waligundua kipaji chake masomoni. Akiwa ktk mwaka wake wa mwisho wa sekondari wakamsaidia kupata Scholarship kwenda Fordham University, NY. Mwenye umri wa miaka 19, akaelekea Marekani akiacha nyumbani mbiu ya Uhuru zikilia. Pale Fordham alisoma BA ya Economics na Mathematics, na akawakimbiza kisawasawa wanafunzi wenzake. Niliambiwa ya kuwa marehemu akiwa chuoni alikuwa mweka hazina katika Klabu ya Uchumi ya hicho chuo chake. Alipomaliza degree ya kwanza, alijiunga chuo kikuu cha Harvard na kusomea PhD ya Uchumi. It is here where he published his great thesis on Tanzania's perverse industrial strategy. Miaka ya Sabini alirudi bongo na kuwa Dean pale Mlimani. Nyerere alipogundua umahiri wa bwana huyu mdogo, akampatia ukatibu wizara ya mipango na uchumi, na nafasi ya kuwa mshauri mkuu wa rais. Muelekeo wa Uchumi wa Tanzania ukaanza kumomonyoka, kutokana na sababu chungu mzima, Rweyemamu akaondoka nchini na kwenda Kufanya kazi Geneva, na baadaye New York ktk UN. Hadi alipofariki akiwa na umri wa miaka 40, alikuwa ameandika zaidi ya vitabu/paper 50.
Nadhani itabidi niwe official biographer..
Lakini ni kweli, wasomi wetu inabidi tuwaenzi. Chachage, Sokoine, Babu, Shivji etc pia, inabidi watu waandike life story za hawa watu. Ningeshauri watu wa mlimani waanzishe Chachage Prize, or JF Rweyemamu Prize for researchers/students on order to honour them.