JERUSALEM 2006
JF-Expert Member
- Apr 23, 2012
- 526
- 583
Haujambo Mwana Jamvi, Heri na hongera sana kwa sikukuu ya Eid-Al-fitr. Kwa niaba yangu binafsi nakutakia sherehe njema, ikawe heri na amani kwa upande wako. Eid Mubarak!!!!
Mwaka 2006 viliibuka vita kati ya Israel na Lebanon. Lebanon ( Hezborah) ilivurumisha maelfu ya makombora katika anga ya Israel.
Mwaka uliofuata Israel iliutangazia Ulimwengu kwamba chombo chake cha kujilinda "RAFAEL ADVANCED DEFENCE SYSTEM" kwa kushirikiana na Taasisi ya Technologia ya anga ya Israel (Israel Aerospace Industries) ziko mbioni kuvumbua na kutengeneza technologia mpya na ya uhakika ya kukabiliana na uvamizi wa anga kwa kutumia makombora ya masafa mafupi na kati, helcopter na zana nyinginezo za kivita.
Mwaka 2011, Israel ilikamilisha uvumbuzi wake na kutambulisha mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora ya masafa mafupi uitwao "The Iron Dome".
The Irone Dome ni mfumo wa kisasa wa kujilinda kutokea ardhini kwenda angani dhidi ya makombora ya masafa mafupi mpaka kilometer 70. Mfumo huu unatumia msaada wa radar na makombora ya Tamir Interceptors ambayo yanafuatilia na ku-neutalize makombora kutoka upande wa adui katika anga linalo-lindwa. Mfumo huu unazuia Makombora, silaha za kivita za C-RAM, ndege, helecopter na ndege zisizo na rubani.
Ufanisi wa mfumo huu unakadiriwa kuwa ailimia 90, na ina uwezo wa kuzua makombora kutoka pande tofauti tofauti kwa wakati mmoja. Kwa lugha nyepesi ni kuwa, Israel inaweza kuzuia Makombora kutoka Lebanon, Misri, Jordan, Syria na Hamas(Palestina) kwa wakati mmoja.
Gharama ya Kombora moja ni mpaka dola elfu 40 za kimarekani ( Sawa na TZS 92,000,000) na betri ya system moja ni sawa na billion 115 za kitanzania.
Ndani ya juma hili, kumekuwa na mvutano mkubwa sana kati ya Israel na Palestina(Hamas). Huku kila upande ukitupa lawama kwa mwenzake kuwa chanzo cha ugomvi huu. Hamas mpaka sasa wamerusha zaidi ya makombora 1000 na kati ya hayo ni moja tu ndiyo limeweza kufika ardhini. Bila shaka hayo mengine yamekuwa neutralized na mfumo thabiti wa "The Iron Dome".
Kama taifa, Israel wamewekeza sana kwenye technologia ya ulinzi wa kisasa. Na wanafanya biashara kubwa sana na mataifa makubwa ikiwemo Marekani na Uingereza hasa kwenye Technologia ya Ulinzi. Kwa sasa hakuna nchi duniani yenye uwezo na uvumbuzi mzuri kama taifa hili dogo mashariki ya kati.
Wamejipambanunua katika taaluma hii, na hakika wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Kwa sasa hakuna nchi ya Kiarabu yoyote inayotaka vita na hawa jamaa. Palestina anashambuliwa na kuuliwa kama kuku huku majirani zao wametoa macho. Nadhani hawapendi kiwakute kilichotokea 1967 (A six day War) ambapo Israel iliwachapa waarabu ndani ya siku sita tu na kunyakua sehemu kubwa ya ardhi yao.
Kama taifa TEULE la Tanzania. Tunajifunza nini kutoka kwa hawa wenzetu wa Israel? Kuna lolote tunaloweza kujivunia nalo zaidi ya umbea na ushambenga kwenye mitandao ya kijamii ya wazungu na wachina? Je, tuko tayari kuendelea kuletewa kila kitu bila kufanya mapinduzi ya kitaaluma na kiviwanda? Hakika tunalo la kujifunza na kuchukua hatua kutoka kwa hawa wenzetu.