"The Iron Dome" Kama Taifa tunajifunza nini kwenye Teknolojia hii ya Israel?

JERUSALEM 2006

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
467
500
Haujambo Mwana Jamvi, Heri na hongera sana kwa sikukuu ya Eid-Al-fitr. Kwa niaba yangu binafsi nakutakia sherehe njema, ikawe heri na amani kwa upande wako. Eid Mubarak!!!!

Mwaka 2006 viliibuka vita kati ya Israel na Lebanon. Lebanon ( Hezborah) ilivurumisha maelfu ya makombora katika anga ya Israel.

Mwaka uliofuata Israel iliutangazia Ulimwengu kwamba chombo chake cha kujilinda "RAFAEL ADVANCED DEFENCE SYSTEM" kwa kushirikiana na Taasisi ya Technologia ya anga ya Israel (Israel Aerospace Industries) ziko mbioni kuvumbua na kutengeneza technologia mpya na ya uhakika ya kukabiliana na uvamizi wa anga kwa kutumia makombora ya masafa mafupi na kati, helcopter na zana nyinginezo za kivita.

Mwaka 2011, Israel ilikamilisha uvumbuzi wake na kutambulisha mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora ya masafa mafupi uitwao "The Iron Dome".

The Irone Dome ni mfumo wa kisasa wa kujilinda kutokea ardhini kwenda angani dhidi ya makombora ya masafa mafupi mpaka kilometer 70. Mfumo huu unatumia msaada wa radar na makombora ya Tamir Interceptors ambayo yanafuatilia na ku-neutalize makombora kutoka upande wa adui katika anga linalo-lindwa. Mfumo huu unazuia Makombora, silaha za kivita za C-RAM, ndege, helecopter na ndege zisizo na rubani.

Ufanisi wa mfumo huu unakadiriwa kuwa ailimia 90, na ina uwezo wa kuzua makombora kutoka pande tofauti tofauti kwa wakati mmoja. Kwa lugha nyepesi ni kuwa, Israel inaweza kuzuia Makombora kutoka Lebanon, Misri, Jordan, Syria na Hamas(Palestina) kwa wakati mmoja.

Gharama ya Kombora moja ni mpaka dola elfu 40 za kimarekani ( Sawa na TZS 92,000,000) na betri ya system moja ni sawa na billion 115 za kitanzania.

Ndani ya juma hili, kumekuwa na mvutano mkubwa sana kati ya Israel na Palestina(Hamas). Huku kila upande ukitupa lawama kwa mwenzake kuwa chanzo cha ugomvi huu. Hamas mpaka sasa wamerusha zaidi ya makombora 1000 na kati ya hayo ni moja tu ndiyo limeweza kufika ardhini. Bila shaka hayo mengine yamekuwa neutralized na mfumo thabiti wa "The Iron Dome".

Kama taifa, Israel wamewekeza sana kwenye technologia ya ulinzi wa kisasa. Na wanafanya biashara kubwa sana na mataifa makubwa ikiwemo Marekani na Uingereza hasa kwenye Technologia ya Ulinzi. Kwa sasa hakuna nchi duniani yenye uwezo na uvumbuzi mzuri kama taifa hili dogo mashariki ya kati.

Wamejipambanunua katika taaluma hii, na hakika wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Kwa sasa hakuna nchi ya Kiarabu yoyote inayotaka vita na hawa jamaa. Palestina anashambuliwa na kuuliwa kama kuku huku majirani zao wametoa macho. Nadhani hawapendi kiwakute kilichotokea 1967 (A six day War) ambapo Israel iliwachapa waarabu ndani ya siku sita tu na kunyakua sehemu kubwa ya ardhi yao.

Kama taifa TEULE la Tanzania. Tunajifunza nini kutoka kwa hawa wenzetu wa Israel? Kuna lolote tunaloweza kujivunia nalo zaidi ya umbea na ushambenga kwenye mitandao ya kijamii ya wazungu na wachina? Je, tuko tayari kuendelea kuletewa kila kitu bila kufanya mapinduzi ya kitaaluma na kiviwanda? Hakika tunalo la kujifunza na kuchukua hatua kutoka kwa hawa wenzetu.
 
TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
4,661
2,000
Hili neno nitakubariki Mungu amelitimiza hata nyakati za sasa kwa taifa la Israel. Jambo lakitisha. Zaid hata nobel prize ndio taifa linaongoza kwa kuwa nazo nyingi. Huyo waziri mkuu wao una ana ambiwa is among world genius.
 
Burke

Member
May 12, 2021
27
125
Ni kweli nasi tunahitaji mabadiliko na maendeleo katika kila nyanja kama wanadamu wengine, nafikiri huenda mifumo yetu mbalimbali hususani ya kielimu inahitaji kuboreshwa zaidi.
Kingine ni kuinuana pale mtu anapofanya kitu chake basi ni kukifanyia namna kipate fursa zaidi kisonge mbele na sio kukatisha tamaa kwa sababu za chuki,wivu na roho mbaya.
 
Copts

Member
Apr 25, 2017
33
95
Kiteknolojia ya kujilinda wapo vizuri, ila kinachoenda kutokea palestina hamas watajuta
 
Glenn

JF-Expert Member
May 22, 2018
10,921
2,000
Hili neno nitakubariki Mungu amelitimiza hata nyakati za sasa kwa taifa la Israel. Jambo lakitisha. Zaid hata nobel prize ndio taifa linaongoza kwa kuwa nazo nyingi. Huyo waziri mkuu wao una ana ambiwa is among world genius.
Ben akitoa speech utampenda bure, jamaa yuko vizuri mno
 
tathmini

JF-Expert Member
Feb 10, 2011
270
250
Hili neno nitakubariki Mungu amelitimiza hata nyakati za sasa kwa taifa la Israel. Jambo lakitisha. Zaid hata nobel prize ndio taifa linaongoza kwa kuwa nazo nyingi. Huyo waziri mkuu wao una ana ambiwa is among world genius.
Unachosema hapa ni cha kubuni tu. Hakina ukweli
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
7,570
2,000
Hao wanao jiita Waizrael, ni wahuni fulani tu wanaolindwa na Mabeberu wa Marekani na Uingereza. Hakuna chochote cha kujifunza kutoka kwao. Na hawana sifa ya kuitwa Taifa la Mungu! Maana hakuna Taifa la Shetani! Wote tunao amini uwepo wa Mungu, tunaamni Mataifa yote ni ya Mungu.

Bahati mbaya tu hao Waarab wamesalitiana wenyewe kwa wenyewe. Wange uimarisha ule umoja wao wa Arab League na kujipanga vilivyo, naamini mpaka muda huu hao Wahuni wangekuwa wamesha waachia maeneo yao kwa lazima.
 
pureView Zeiss

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
5,121

Kusalitiana Kwa waarabu ni mbinu/akili iliyotumiwa na wenye akili zaidi(wazungu) ili kuendelea kuitawala dunia....hata Leo hii ukatae au ukubali bado waisrael wataendelea kuwa juu ya waarabu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom