THE HONEY MOON at Kibiti is OVER, Uhalifu Haulipi - Lucky Philip Dube

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
11,324
17,829
Mhenga Lucky Philip Dube alishawahi kuimba "Crime Does Not Pay" yaani uhalifu haulipi. Kwa dhati ya moyo wangu naamini fungate(honey moon) la mauwaji Kibiti limeisha. Wale wenye kushabikia mauwaji ya binadamu wenzao sasa watakosa furaha yao.

Najua (nahisi kwa kutabiri tabia za serial Killers) kama wauwaji wote hawajafa na wanaweza kujaribu kuuwa tena mara moja ili kujaribu kuhamasishana kwamba wao wameshindikana yaani invisible lakini wakifanikiwa kuuwa mara mbili (maeneo ya Kibiti, Rufiji, na Mkuranga) hadi kufikia 15/08/2017 naomba mni-tag nitakuwa na jambo la kujifunza zaidi kwamba watu wetu wa ulinzi na usalama si chochote mbele ya hao wahenga wa Kibiti. MWISHO WA UBAYA NI AIBU.

NB:
Hizi ni hisia tu kwa hivyo neno langu sio unabii au rocket science inaweza kuwa muziki wa Kibiti bado sana. Hisia hizi zinatokana na kuwaamini baadhi ya watu wa serikali wanaohusika na kukomesha hili sekeseke mfano Kamanda Sirro na wengine unsung heroes waliokuwepo uwanja wa mapambano na washiriki toka idara/taasisi mbalimbali za serikali na washirika toka taasisi zisizo za serikali yetu.

UPDATE:
Huzuni kubwa, Wauwaji wameendelea kujibu ujumbe kwamba bado wapo.
News Alert: - Mauaji Kibiti: Mtu mmoja auawa kwa risasi ya kichwa
 
Wadau wana JF hasa wafuatiliaji wa sakata Kibiti naomba mlete tathimini hapa. Je Kibiti ni shwari? Je nilikuwa sahihi kuhusu hisia zangu kuhusu kudhibitiwa uhalifu wa Kibiti kama nilivyo elezea ktk thread hii?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom