The Highs & Lows katika burudani na 'ubuyu' 2016

Nifah

JF-Expert Member
Feb 12, 2014
31,313
64,364
The highest & the lowest za kiburudani na ubuyu kibongobongo kwa mwaka mzima wa 2016.

Kwa kuwa tumefikia mwisho wa mwaka 2016 mimi kama mdau na shabiki mkubwa wa burudani na masuala yetu yale ya ubuyu nimefanya tathmini ya matukio yaliyotikisa kwa mwaka huu unaoelekea ukingoni.

Yafuatayo ni matukio yaliyotikisa zaidi... Huenda unajua ila mimi nitakujuza zaidi.
Au kama hujui basi ni wakati wako wa kuyajua...twende nami;

THE LOWS
Haya ni matukio yaliyotikisa zaidi mwaka huu negatively

5."KUPUMULIWA"
Sakata hili japo limetokea mwishoni kabisa mwa mwaka huu ila lilishika chati na kutikisa tasnia nzima ya burudani na 'ubuyu'.
Kama mnakumbuka vyema sekeseke lilianzia kwa Omary Nyembo-Ommy Dimpoz alipoweka hashtags za kununua views YouTube ambalo lilitafsiriwa kama 'dongo' kwa kijana wetu wa kutokea Tandale Diamond Platinumz.

Kama ilivyo ada ya mswahili havumilii dongo ndivyo ilivyokuwa kwa Diamond aliyeamua kujibu mapigo kwa dongo la 'kupumuliwa' kwa Ommy Dimpoz.

Sakata hili lilishika kasi pale Wasanii hao walipoitwa kwa nyakati tofauti ktk kipindi za XXL cha Clouds FM na kila mmoja alijieleza kwa utashi wake.

Mwisho wake Ommy Dimpoz alionekana mwenye busara zaidi kwa jinsi alivyoweza kulihandle sakata lile tofauti na Diamond aliyepanic na kujiharibia taswira yake mbele ya jamii.

4.TEAM WCB (DIAMOND) VS TEAM KIBA

Niseme kwamba kama mdau katika mojawapo ya team hizi,hizi team zina faida kwa pande zote yaani ule upande wa Diamond na upande wa Ali Kiba.

Timu hizi zinafanya waongelewe kila siku na muziki wao kuwafikia kirahisi mashabiki wao.

Pia zimeongeza ushindani ambao ni chachu ya maendeleo kwa wahusika wakuu (Diamond & Kiba)
Mfano mzuri ni kila mmoja amejitahidi kutoa nyimbo pamoja na videos nzuri.
Lengo kuu likiwa ni kuufikisha muziki wetu kimataifa na 'kutokuziangusha timu zao'

Lakini ukweli mchungu ni kwamba kwa maslahi mapana ya muziki wetu timu hizi zinadumaza kiwanda za muziki nchini.

Hasara kubwa ni kwamba wasanii wengi hawasikiki kama inavyopaswa na badala yake 'attention' yote imeelekezwa kwa Diamond na Ali Kiba.

Mfano mzuri tumchukulie msanii Darassa ambaye amejitahidi kutoa nyimbo nzuri lakini ilikuww vigumu kwake 'kutoboa' hadi alipokuja kufanikiwa hivi majuzi na single yake matata ya Muziki aliyomshirikisha Ben Paul.
Na hii ni kwa sababu alifanya 'timing' ya kuachia single yake hiyo...endapo angeiachia wakati ambao Diamond na Ali Kiba wameachia single zao huenda yangekuwa yaleyale ya miaka iliyopita.

Sio Darassa pekee,wapo wasanii wengine waliotoa single nzuri lakini wameshindwa kabisa kusikika.
Wakiwemo Ibranation-Nilipize,Timbulo ft Barakah Da Prince-Usisahau,Bright-Nitunzie,Barger,Selfie,movie remix (Belle9,G Nacko,Izo,Maua Sama,Linah n.k)

Hasara nyingine kubwa ya team hizi ni pale msanii mmojawapo kati ya Diamond au Ali Kiba anappchaguliwa kuwania tuzo za nje.
Hakuna team iliyo na utayari wa kumpigia kura msanii wa team pinzani.
Mifano ipo ya jinsi gani team hizo zilivyotugharimu ktk tuzo za kimataifa.

3.DIAMOND NA MICHEPUKO

Hili liizuka katikati ya mwaka na kuzua kizaazaa mitaani na kwenye mitandao ya kijamii.
Kwanza ilianza na Diamond kuchepuka na Lyn video vixen wa kwenye video ya Rayvany Kwetu.
Na liliongezewa uzito na mama pamoja na dada yake Diamond kwa kuonekana kusapoti hilo suala.

Baadae zikaja tuhuma za Wema Sepetu kulala madale.
Kabla tuhuma hizo hazijapoa likaja sakata la mwanamitindo Hamisa Mobetto kutoka na Diamond.
Hii lilikuwa zito zaidi kwani duru za ubuyu zilidai Hamisa kubeba ujauzito uliosemekana kuwa wa Diamond, picha ambazo zilionesha kulala hotel 1 Afrika Kusini n.k

2.MIMBA YA WEMA SEPETU

Hili ni moja kati ya matukio yaliyotikisa kwa kiasi kikubwa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Fununu zilianzia kwa rais wa Shirika La Wambea Duniani (SHILAWADU) Soudy Brown kwa picha aliyopost Instagram ikimuonesha Wema Sepetu akiwa ktk maumivu makali ikisindikizwa na caption yake maarufu 'inasemekana lakini'

Japo wahusika (Wema & Idris) walijitahidi kukaa kimya lakini baadae walikiri kupoteza mapacha wao.

Hadi leo kila mtu ana jinsi alivyotafrisi tukio lile,haieleweki ni kick au tukio halisi.

Binti huyu ameshindwa kuielewa potential yake na jinsi gani aitumie kujiingizia kipato.

Kutokujielewa huku kumepelekea kila afanyalo 'kubuma'.
Moja kati ya matukio makubwa aliyowahi kuyafanya na yakapata suppprt kubwa ni filamu aliyodai kuiandaa ya Mrs. Superstar.
Movie hii katika uzinduzi wake alimualika muigizaji mkubwa na mwanamama mjasiriamali Mnigeria Omotola Jalade.
Endapo Wema angeitoa filamu ile kwa wakati ule basi ingevunja rekodi ya mauzo.
Lakini hadi leo hakuna anayejua ni nini kilichomsibu hadi kushindwa kuiweka movie hiyo the most wanted sokoni.

Baada ya hapo alijitahidi kuja na mambo kadha wa kadha ikiwemo reality show yake iliyokuwa ikirushwa kupitia kituo cha runinga cha EATV chini ya kampuni yake ya Endless Fame,Lipstic za Kiss,Vigoma n.k

Lakini kama ilivyo ada ya wa mbili havai moja ndivyo ilivyokuwa kwa mwanadada huyu.
Biashara/movie zimemshinda badala yake ameendelea kuwa Wema yule tunayemjua wa siku zote.

1.MANGE KIMAMBI vs EVERYONE

Nadhani hakuna mwaka ambao socialite Mange Kimani amepata attention kubwa kama mwaka huu.
Alianza kwa kugombana na mashoga/marafiki zake.
Likafuatia sakata la January Makamba na kumtapeli muwekezaji wa kizungu kwa kushirikiana na dada yake, sakata lake la talaka,Makonda na sasa amehamishia majeshi kwa serikali ya JMT na viongozi wake kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu.
Itoshe tu kusema kuwa kwa kuzingatia nguvu ya mitandao ya kijamii iliyopo sasa nchini,Mange ni moja kati ya majina yanayotrend sana kwa sasa hivi (positively & negatively)
She is very smary thou...ukweli na usemwe tu.
Mnyonge mnyongeni....

THE HIGHS

Haya ni matukio yaliyotikisa positively

5.NAAMKA TENA TOUR

Hii ilijumuisha matamasha ya Naamka tena Mlimani City na Tours za mikoani.

Hii ilidhihirisha influence kubwa aliyonayo mwanamama wa shoka Judith Wambura - Jay Dee.
Sio rahisi kwa msanii/mwanamuziki kufanya vizuri huku akiwa na mgogoro na Clouds Media group lakini kwa mwanamama huyu hali ilikuwa tofauti.

Japo wamezimaliza tofauti zao lakini ukweli ni kwamba Jide aliwatoa Knok Out Clouds Media Group chini ya Ruge Mutahaba.

4.TUZO ZA KIMATAIFA

Ni dhahiri kwamba sasa Bongofleva imepiga hatua kubwa kimataifa.
Na hili linadhihirishwa kwa tuzo walizopata kushiriki/kushinda wasanii wetu.

Tuliingiza wasanii wengi kwenye tuzo za MTV MAMA tofauti na mwaka jana ambao alishiriki Diamond pekee.
Mwaka huu tulikuwa na Navy Kenzo,Ali Kiba,Vanessa Mdee,Rayvany naYamoto Band.

Pia tuzo nyingine tulizopata kung'ara ni Afrima kwa kuchukua tuzo tulizowakilishwa na Diamond,Harmonize,Ay na DJ Ommy.

3.MBWANA SAMATTA

Huyu anaingia ktk list kwa mafanikio makubwa aliyoyapata mwaka huu.
Kwanza alianza mwaka kwa kuchukua tuzo ya mchezaji bora Afrika.

Baada ya hapo akapata shavu kwenda kuchezea timu ya ligi kuu ya Ubeligji.
Pia ametutoa kimasomaso kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Europa League.

2ALI KIBA NA MKATABA WA SONY

Ali Kiba ameandika historia kwa kuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania na wa pili Afrika kwa kusaini mkataba wa kiduania (Global Deal) na kampuni ya Sony moja kati ya kampuni kubwa zaidi ya muziki Duniani.

Matunda ya mkataba wake huu yameanza kuonekana kwani Ali Kiba hivi sasa yuko daraja la juu akiwa kama moja ya wasanii wakubwa zaidi Afrika.

1.FROM TANDALE TO THE WORLD TOUR

Diamond Platinumz katikati ya mwezi Machi na April amefanya tour kubwa ya kihistoria katika nchi 12 barani Ulaya.

Kinachofurahisha zaidi ni kwamba Diamond alifanikiwa kujaza kumbi katika karibia ya kila nchi aliyotembelea na ticket zilikuwa sold out kiasi kuna baadhi ya mashabiki walilalamika kwa kukosa tiketi.

Nimeweka tukio hili kama ndilo tukio kubwa zaidi kutokea katika mwaka huu kwani sio tukio lenye manufaa kwa Diamond pekee,bali kwa nchi (kuitangaza) pamoja na kuupaisha muziki wetu kimataifa.

Hili ni tukio la mfano na linapaswa kupigwa pamoja na kupewa pongezi.

HITIMISHO

Huu ulikuwa mwaka mzuri kwa tasnia ya burudani hasa muziki wetu umepaa na kukuwa maradufu ukilinganisha na tasnia ya filamu ambayo imezidi kudumaa.
Ni dhahiri pengo la Marehemu Steven Kanumba limeshindwa kuzibika.

SHUKRAAN
 
Wow uchambuzi makini kabisa.. Linapokujaga suala la sekta ya 'ubuyu' na industry ya mziki, my girl your the best

Shukrani kwa uchambuzi huu! Nimependa the way ulovyoweka maslahi pembeni ukaandika uzi kwa weledi.. Kula tano

Thank you for the credit, nimefurahi kuona umezingatia baadhi ya maoni niliyokupa!

Nilimiss nyuzi zako malkia wa ubuyu

#TeBold's#
 
Kinachofurahisha bongo tunazidi kung'ara kwenye sekta ya burudani hasa kwenye muziki.

Wanaija wafunge mkanda wakaze na kamba mwaka ujao tunawapita
Mimi Ninachokiona Muziki Uliokuwa Sio Wa Tanzania Bali Ni Muziki Wa Diamond

- Hata Muvi Tuliwahi Kusema, Filamu Zetu Zimekuwa Kumbe Movie Zilizokuwa Zimekuwa Ni Movie Za Kanumba, Leo Kanumba Hayupo Kila Mtu Anajua Kinachotokea

- Hata Leo Diamond Aseme Anaacha Kuimba, Muziki Unakosa Hamasa Kama Muvi
 
Ni dhahiri pengo la Marehemu Steven Kanumba nimeshindwa kuzibika.

SHUKRAAN

Napenda kuutambua mchango wako The bold katika maandalizi ya makala hii.
Hivyo makala hii imeletwa kwenu kwa hisani ya #TheBold's#
Wenu katika ubuyu,
Nifah.
Nimeipenda hii imepangika vyema kabisa(sina shaka udaku specially kashaikopi hii),ushauri wangu kwako kwa vile una kipaji cha kuandika basi jitahidi uanzishe blog/kijarida/kijitabu kinacho ongelea mambo mbalimbali ya celebrity wa bongo haki ya mungu utapiga pesa aisee Nifah
 
Mabloga uchwara lazima wakopi hii wakaweke kwao..

Hahahahah Nifah akianzisha blogu itabidi shigongo afunge ofisi.. Kwenyw hiyo sekta Nifah sio mtu wa mchezo mchezo..
 
Kinachofurahisha bongo tunazidi kung'ara kwenye sekta ya burudani hasa kwenye muziki.

Wanaija wafunge mkanda wakaze na kamba mwaka ujao tunawapita
Mwaka huu kiukweli tumekuwa vizuri sana kimuziki kuliko sekta yoyote ya kiburudani.
Sio mpira sio maigizo...
Juzikati nilikuwa na Mnigeria mmoja nilishangaa anayo miziki ya wasanii wetu katika simu yake na anawajua vizuri tu.
Nilifurahi sana.

Ili kuwafikia Wanaija na kuwapita sio kazi rahisi,umeona team nilivyo zilivyotugharimu hivyo tunatakiwa tulichukulie suala la team in a serious way.
Timu zibakie Kwa ushindani wa ndani tu,katika masuala ya kimataifa hatuna budi kuwa wamoja.
Na inawezekana tukiamua Kwa nia ya dhati kabisa.
[HASHTAG]#TaifaKwanza[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom