Story: The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)

The Hidden Truth ( Ukweli Uliofichika)
MTUNZI : Akida Siri Rambao
Contact : 0658328596
Email: akidasiri@gmail.com

Sehemu 1 (D) : Msasani, Kinondoni -Dar es Saalam

Ilipoishia....
Ghorofani Winifrida wazo la kujiua bado lilikuwa limeutawala mwili, akili na nafsi “qataa” huo ndio mlio pekee uliosikika
masikioni akatulia sekunde kadhaa kusikilizia maumivu ya risasi itakayopenya katika kichwa na kuvuruga ubongo....

Endeleaa....
cha kushangaza hapakuonekana kutoka kwa risasi alistaajabishwa inawezekanaje bastola isiwe na risasi aliiangusha bastola chini kwa kuwa haikuwa na msaada
kwake. Wini alibaki kasimama huku akiwaza na kuwazua njia nyingine maana alidhamiria haswa kuutoa uhai wake mara akagutuka katoka mbio na kufungua mlango akashuka ngazi moja kwa moja hadi jikoni sura imemvimba kwa kulia kwa
uchungu “Heee muone wifi kachukia…” Eva alimshtua dada ake kumuonesha kwa kidole “Khaa! hahahaa sasa tusiseme
ukweli aende zake uko” Ester aliongea kwa sauti na kuendelea kurusha roho, Winifrida muda wote akibumburusha droo akifunga na kufungua Fatuma alibaki kaduwaa tu asijue la kufanya mara Wini akatabasamu akautoa mkono katika droo moja ukiwa na kisu kikubwa, “Haa dada Wini” Fatuma aliacha mwiko katika sufuria na kumrukia Winifrida kumzuia kabla hajakisimika kisu tumboni “Niache Fatuma nasema niache”
Wini alipaza sauti iliyochanganyika na hasira “Nasema niache hunielewi” sauti ya Wini ilisikika tena “Jam… jamani dada
anajiua”. Upande wa sebuleni, “Dada unasikia huko Fatumaanahitaji msaada” Eva alimtumbulia macho dada yake akiwa
na macho ya wasiwasi “We usifanye mchezo na kifo anatuchezea tu achana nae” Ester alijibu na kujikalisha
kwenye sofa huku akiongeza sauti ya kwenye redio huku akiutikisa mwili wake mnene kufatisha miondoko, kelele za
pukurushani ziliendelea jikoni huku Fatuma akihitaji msaada, Fatuma hakumpa nafasi hata kidogo aliendelea kuminyana ili
kukitoa kisu mikononi mwa Wini, kwa bahati mbaya Fatuma akashika makali na Winifrida akiwa na mpini ile kujaribu
kuvuta loo! Kisu kikapita katika kiganja cha fatuma na kula nyama damu ikaanza kumwagika Fatuma kwa maumivu
akiwa kashikilia mkono wake asiamini macho yake damuyakimvuja akabaki kupiga mayowe ya maumivu. Winifrida
akabaki kaduwaa macho yamemtoka akaanza kuyumba akayumba mwisho akadondoka mzima mzima “puuh” “Jamani dadaaaaa” Fatuma akapiga ukelele mkali akisogelea mwili wa
Winifrida, “Kuna nini …Mungu wangu…mafuta ya taa yako wapi” Ester aliongea huku kamshika bega Fatuma macho
yamemtoka, Fatuma alimuonesha tu kwa kidole hakuweza kutokana na uchungu aliokuwa nao, licha ya kuwa alikatwa na kisu na kupatiwa maumivu makali lakini alibaki kuwaza usalama wa mwajiri wake pale chini ambae alionekana kupoteza fahamu, Ester na Eva walishirikiana kwa pamoja kumpa huduma ya kwanza Fatuma na kisha wakamgeukia
Wini aliyekuwa amepoteza fahamu kumjulia hali yake kwa kumpepea na kumkanda na kitambaa cha maji ya vuguvugu mpaka alipo pata fahamu.
Baada ya fahamu kumrudia, Wini alijiswaga swaga mpaka ukutani na kukaa kitako sakafuni akawatazama mawifi zake waliokuwa wamesimama na Fatuma wakimtazama yeye, akawaangalia kwa hasira kwa muda kisha ghafla akanyanyuka na kutoka kwa kasi kuelekea ghorofani kama kishada, na kuwaacha alama za mishangao nyuma yake.
“Wewe sikiliza akirudi bosi wako ole wako unyanyue mdomo wako umenielewa?” Ester aliongea akimtazama Fatuma kwa
jicho la ole wako akimaanisha.

Fatuma alikuwa kajiinamia tu
dhahiri macho yakionesha kutoridhishwa na hali ilivyo akionekana akitamani kufanya kitu kama angepata fulsa.
Winfrida alifanikiwa kuingia chumbani akaufunga mlango.Nje ya nyumba, Jumaa akiwa kajibanza kwenye ukuta kwa
tahadhari simu sikioni akisikiliza upande wa pili, “Ndio madam Moo nimeelewa na nimejaribu kumpigia sana lakini
hapokei…ndio hakuna walinzi zaidi yangu hapa nahofia usalama maana hawaonekani kuwa ni watu wazuri kabisa” Jumaa akajipinda na kuchungulia sebuleni kisha akajirudisha alipokuwa “Sawa sitawaruhusu waondoke” Juma aliongea na kuchungulia tena “…najua, nipe muda ndio kwanza nina siku moja hapa…haina shida haitakuwa rahisi nakuhakikishiamadam nitafanya kwa moyo mmoja mpaka nikamilishe”
Jumaa aliiongea kisha akajichekesha simu bado ikiwa sikioni “Aaah acha tu ilikuwa bahati tu kama ingeshindikana
ningekuwa hata daktari wa familia nisingekubali kirahisi kukosa kazi hapa…naelewa naelelewa nitajitahdi kucontrol
hasira zangu.” Jumaa alitabasamu huku akikuna pua yake“…sawa ngoja niendeleee kumtafuta sawa nitaripoti kwako kila siku” Jumaa akakata simu.

Chelsea Hotel, Mtaa wa uhuru Ilala -Dar es Salaam.
Gari aina ya Subaru Impreza nyekundu iliingia kwa maringo na kusimama katika sehemu ya maegesho, dakika moja tu
ilipita kisha Richard akatoka ndani ya gari na kusimama kwa sekunde na kuitoa miwani yake myeusi toka katika mfuko wa
shati na kuivaa kisha akanyanyua kichwa kutazama urefu wa jengo lililojengwa kwa aina yake na kuelekea eneo la mapokezi. “Ooh mheshimiwa karibu sana…mbona upo mwenyewe nasio kawaida yako” Richard akapokea mkono wa salamu na karibisho katika ukumbi wa mikutano “Ahsante waziri kwanza bila shaka taarifa ya kuchelewa kufika uliipata mapema” aliongea Richard huku bado akiwa kaushikilia mkono wa Waziri “Ndio niliipata” alijibu Waziri na kutabasamu “Basi vizuri…Pili, nafikiri kila kitu nilishakisema kwenye vyombo vya habari kuwa nahitaji kuwa huru na kuwamtu wa kawaida kama zamani sitaki kuongeza maadui na nilionao napenda waache kunichukia na wanione kuwa mimi
si mbaya wao hivyo tu” aliongea Richard kwa kujiamini, waziri akamtazama Richard kwa sekunde kadhaa kisha akaongea “Ni kweli ulisemalo watu kama sisi tunaojihusisha na mambo ya siasa tuna maadui wengi na huwezi mjua yupi ni
yupi unaweza shangaa kisu cha tumbo au bastola ya kichwa bila kutegemea na ukashindwa jua ni nani anaye husika” kisha akatabasamu “Skia waziri kiukweli siasa imenigawa mimi na watu wangu wa karibu hasa mke wangu na hata watu
waliokuwa wananifahamu kama ujuavyo roho yangu ya kutoa lakini imekuwa nikifanya inaonekana naifanyia chama tawala ikanipelekea kuweka migawanyo ya imani juu yangu sijapenda japo wewe hujui yaliyojiri lakini amini hivyo
tafadhari” alimaliza kuongea mheshimiwa Richard na kumuacha mdomo wazi waziri huyo wa elimu bwana Mwijaku Mwasenga “Nimekuelewa vizuri kijana naomba tuanze kikao chetu tafadhari”. Majadiliano yakaanza, nusu saa ikaenda lisaa likapotea “Nashukuru sana Mheshimiwa kwa mara ya kwanza nimeona uwezo wako ambao nilikuwa tu nausikia toka midomoni mwa watu waliowahi kushiriki nawe mambo
kadhaa ya kimaendeleo wakidai una kila sifa nzuri ya kuvutia, hebu niache nikuombe kitu kijana wangu kama hutojali” aliongea Waziri huyo kwa kunong’ona, “Sema tu mzee wangu
kama nitalimudu nitafanya kama sitalimudu itakuwa bahati mbaya kwako” aliongea Richard huku akiachia tabasamu
jembamba akiuvuta mguu wake na kukunja nne. “Unaonaje kama utakuwa mtu Fulani uliyeteuliwa ukasimamia taasisi Fulani nchini ninauwezo wa kumshawishi Mheshimiwa Rais,
kwa sababu nakuona una kila kitu muhimu katika maisha haya una mali za kutosha, elimu, akili, maarifa, busara, unapendwa na watu, una huruma, una moyo wa kutoa,
muungwana…” aliongea Waziri huku Richard akionekana kubadilika akajikuta akikosa raha “Mzee wangu nasikitika kukuona kuwa hujanielewa inatosha sitakuwa tayari” aliongea kwa sauti ya kunyongea sana kisha akasimama
nakuaga huyo akashika njia. ‘Nina kila kitu lakini sina mtoto’ alijisemea nafsini huku akipiga hatua fupi fupi ‘Aisee waziri
kama umetumwa kunichunguza basi huna cha kukipata’ akaingiza mkono mmoja katika mfuko wa suruali na kutoa
simu yake ndogo “Ujumbe…missed call shenzi nimezikosa” alijisemea huku akisogeza mguu wake kwa hatua moja fupimara akasimama sura ikakunjamana ikiambatana na mshangao “Haiwezekani” Haraka haraka akaingia kwenye lift
na kushuka, dakika mbili tu zilimtosha kuwa chini ya ghorofa akakazana kuifata gari yake huku watu kadhaa wakimtazama namna alivyokuwa kawaida bila makuu. “Halow natoka hapa
usalama wangu upo sawa? vizuri naelekea nyumbani kuna tatizo naomba baadhi yenu mumfatilie Waziri Mwijaku kwa
karibu zaidi” aliongea huku akikikandamiza kitu sikioni.

Haraka alizungusha funguo akavuta mafuta na kubadili gia mkuku mkuku akatoka eneo hilo. “Haloow mheshimiwa raisnimejaribu kumshawishi kadri nilivyoweza lakini inaonekana bwana huyu amenuia kabisa na kwa taarifa nilizozipata amefukuza walinzi wote nyumbani kwake na kuwapunguza
baadhi ya wafanyakazi wa ndani… “ndio mheshimiwa lakini anaonekana mara zote ni mtu anaejiamini lakini ni kama ana
wasiwasi kama sio hofu” aliongea waziri Mwijaku huku akichukua glasi ya maji mezani “Yaah hata mimi naamini hilo
kuna mtu atakuwa ameamua kufanya kazi naye kwa siri si bure…ngoja nitatuma vijana wangu wamfatilie taratibu
mheshimiwa huenda tukajua sababu iliyomvunja nguvu” waziri Mwijaku akatoa simu sikioni na kushusha pumzi nzito
huku akiwatazama vijana wake.
Msasani, Kinondoni-Dar es Salaam
“Brhiiiiiiik” matairi ya gari yalisuguliwa katika rami kwa breki kali karibu kabisa na geti. Geti likafunguliwa kuipisha gari
kuingia, “Inamaana wapo hapa muda mrefu” aliongea akimuacha Juma kwa nyuma na kuelekea mlangoni, “Mbona
mnakuja bila taarifa” maneno yalimtoka mheshimiwa huku akihema na kurudishia mlango kwa kuubamiza akawatazama
dada zake ambao waliishia kuinamisha vichwa vyao. Sura ya Richard ikaendelea kujawa na hofu zaidi, akaamua kutoka
eneo alilokuwepo na kuzikabili ngazi kupandisha ghorofani kiasi cha kuwafanya dada zake kusimama huku
wakitazamana.

Miguu ikaanza kuwa mizito nguvu zikiendelea kumuisha “Ooh nimechelewa kukuokoa mke wangu tafadhari
kuwa salama” alijikuta akijiongelea mwenyewe huku machozi yakimtoka akiendelea kupanda.Hamadi alipofungua mlango tu mwili ulianza kumzizima
hakuamini macho yake hakuamini alichokiona akayafumba macho yake na kuyafumbua loo! alipoona si utani uchungu ulimzidi kutawala moyo wake mdomo ukaanza kutetemeka
machozi nayo yakaanza kumtiririka kama maji mlimani “Mmmmh mmmmh…. mke wanguuuuuu” kwikwi haswa ilikaa
koooni maneno hayakumalizwa kinywani mwake. Mwili wa Winifrida sakafuni haukujigeuza wala kutikisika tangu
ulipotulia, Richard alianza kupiga hatua za taratibu mfano wa mtoto anae anza kujifunza kutembea akijihimu huku akipepesuka mpaka karibu yake. Kilichommaliza zaidi nguvu na kumfanya ashuke taratibu sakafuni ni pale macho yake yalipokutana na bastora iliyokaa karibu na mwili wa mkewe. Richard alikuwa kama zuzu aliangazaangaza kukitazama chumba ambacho kilikuwa vululu vitu vimetapakaa pahala
pote pa chumba alijisogeza na kuegemea kitanda alipo tazama mkono wake wa kuume akaona kifuko kidogo cha dawa
alikitazama na kukitambua alijiinamia kisha akanyanyua kichwa na kuizungusha shingo pahala pengine na mwishowe
macho yakaishia katika kitanda ambapo napo hapakuwa Patupu alikiona kikaratasi chenye maandishi juu ya godoro.
Richard bado na muonekano wa kama zuzu kamasi zikimtokapuani alijitahidi kusimama akapiga hatua moja ya pili akiruka damu damu ambazo zilikuwa zina vuja toka kichwani mwa Winifrida, alisogea na kukaa katika kona ya kitanda. Richardakakichukua kipande cha karatasi na kuanza kukisoma. “Mke wangu… mke wangu jamani” aliyaongea maneno hayo baada ya kusoma ujumbe alioukuta. Kijana wa watu akajikalisha sakafuni taratibu akamtazama mkewe kwa jicho la huzuni kumbukumbu mbalimbali zikamtembelea na kumuumiza sana
moyo wake loo alijiona mkiwa kweli kweli hasa tabasamu zuri la mkewe lilimmaliza nguvu, aliwaza mengi sana na
kukumbuka kauli mbalimbali za mkewe kipindi kile walipo toka Hospitali.

Mawazo yalipofika tamati alijipangusa machozi akajiburuza hadi karibu na bastora akaikagua kisha akajisimamisha kiuchovu na kulisogelea kabati la nguo
alinyanyua mkono wake na kupapasa mpaka alipopata alichokitaka akaacha, mkononi alikuwa kashikilia risasi moja
akajisogeza hadi kwenye mwili wa mkewe akajikalisha na kutulia akaiweka risasi katika chemba na kuipachika kichwani
tayari kwa kufyatua. Richard wala hakuwa na wazo lingine zaidi ya kujiua hakuwaza kumtikisa mkewe hakuwaza
kumpeleka hospitali hakuwaza kubahatisha kuokoa maisha ya
mkewe kwa sababu aliamini asilimia mia kuwa mkewe ni marehemu hivyo hakuwa na mpango tofauti zaidi ya kujiua.
Baada ya kuweka vizuri akafumba macho huku mkono mmoja ukiwa begani mwa mkewe, “Mke wangu ngoja tu nikufate
maana nikibaki nitakuwa nimevunja ahadi yangu” alipo kuwa anaendeleaa kulia kwa uchungu na kujiongelesha mwenyewe
mwili wa Wini ukaanza kutikisika, Richard wa watu alibaki akitazama kwa mshangao akiwa na hali ya furaha akatulia
kumuangalia mkewe vizuri, Wini akajigeuza tena hukukujinyoosha huku akiyafumbua macho yake. Richard akamvamia mkewe na kuanza kumtingisha na kumuita kwa
jina huku akimgusa mapigo ya moyo “…Ooh asante Mungu mke wangu hujafa?!!” Richard akaitupa bastola ukutani na
kumnyanyua mkewe kumkalisha kitako huku akiwa anahema hovyo hovyo akimuita mfululizo “Mke wangu …mke
wangu…jamani mke wangu… ooh jamani mke wangu”. Richard alimkumbatia kwa furaha mkewe, Wini yeye alibaki
kumtazama tu usoni mumewe bado akiwa na wenge la kuponyoka na kifo alionekana kama mtu asiyejielewa alibaki
kumtazama tu usoni. “Mke wangu sina thibitisho la kunipendainatosha usifanye hivi tena tafadhari, najua mwenyezi Mungu amenipendelea sana kunirudishia furaha yangu naahidi kuto rudia kosa mke wangu sito kuacha ata nzi akukere sitakaa mbali nawe tena” Richard alimkumbatia zaidi mkewe na
kumpiga mabusu mfululizo ya kichwa huku Wini akionekana kutulia akaiweka risasi katika chemba na kuipachika kichwani
tayari kwa kufyatua. Richard wala hakuwa na wazo lingine zaidi ya kujiua hakuwaza kumtikisa mkewe hakuwaza kumpeleka hospitali hakuwaza kubahatisha kuokoa maisha yamkewe kwa sababu aliamini asilimia mia kuwa mkewe ni marehemu hivyo hakuwa na mpango tofauti zaidi ya kujiua.

Baada ya kuweka vizuri akafumba macho huku mkono mmoja ukiwa begani mwa mkewe, “Mke wangu ngoja tu nikufate
maana nikibaki nitakuwa nimevunja ahadi yangu” alipo kuwa anaendeleaa kulia kwa uchungu na kujiongelesha mwenyewe
mwili wa Wini ukaanza kutikisika, Richard wa watu alibaki akitazama kwa mshangao akiwa na hali ya furaha akatulia
kumuangalia mkewe vizuri, Wini akajigeuza tena hukukujinyoosha huku akiyafumbua macho yake. Richard akamvamia mkewe na kuanza kumtingisha na kumuita kwa
jina huku akimgusa mapigo ya moyo “…Ooh asante Mungu mke wangu hujafa?!!” Richard akaitupa bastola ukutani na
kumnyanyua mkewe kumkalisha kitako huku akiwa anahema hovyo hovyo akimuita mfululizo “Mke wangu …mke
wangu…jamani mke wangu… ooh jamani mke wangu”. Richard alimkumbatia kwa furaha mkewe, Wini yeye alibaki
kumtazama tu usoni mumewe bado akiwa na wenge la kuponyoka na kifo alionekana kama mtu asiyejielewa alibaki kumtazama tu usoni. “Mke wangu sina thibitisho la kunipendainatosha usifanye hivi tena tafadhari, najua mwenyezi Mungu
amenipendelea sana kunirudishia furaha yangu naahidi kuto rudia kosa mke wangu sito kuacha ata nzi akukere sitakaa
mbali nawe tena” Richard alimkumbatia zaidi mkewe na kumpiga mabusu mfululizo ya kichwa huku Wini akionekana kwenye sofa maana alipigwa la kushtukiza alitulia kajishika shavu akiugulia maumivu makali. “Mpumbavu wewe usiongee
upuuzi mbele yangu shwaini” alifoka Richard huku akimuangalia Eva kwa jicho lenye hasira sana. “Sikiliza Richard najua unaongea kwa kujiamini sana kwa kuwa tupo kwako, lakini tambua kuwa sisi ndugu zako tunakupenda sana halafu kingine kaa ukijua kuwa unapoteza muda bure na huyo mwanamke” Ester aliingilia kuongea kwa utulivu sana na sio kwa kupayuka kila mtu pale sebureni aliweza kusikia vizuri hapakuhitajika kurudiwa, yalikuwa ni maneno mazito kwa
kijana Rich yalitibua tibua chungu ya moyo akashindwa kujizuia alijikuta anapayuka kwa nguvu “Nasema ondokeni
nyumbani kwangu sasa hivi” “Hatuondoki lolote fanya mpaka utuelewe” Ester nae aliongea kwa jazba tena kwa kujiamini,
Richard aliona anapotezewa muda aliamua kuchukua simu mfukoni mwa suruali yake na kutafuta namba na kupiga, dada zake walibaki wakimtazama tu. “Hallow…yes afande maunaomba mje nyumbani kwangu kuna uvamizi hapa… okay sawa” Richard alitoka eneo hilo na kusogea pahala ambapo meza ya chakula ilikuwepo na ndipo mkewe alikuwa
amejituliza akishuhudia malumbano yanayo sababishwa na yeye. ‘Roho inaniuma sana matatizo yangu leo yana
wapelekea ndugu kugombana’ Winifrida alijisemea nafsini.

Richard alisogea na akaanza kupakuwa chakula na kumnawisha mkewe na kuanza kula huku akimlisha na mkewe kwa tabu tabu. Ndugu wakabaki wakitazama tu kwa mishangao.
Chakula hakikuisha kwenye sahani nje kulisikika honi kali, Juma akiwa hana hili wala lile alitazama katika ukuta kupitia kifaa maalumu “Hee magwanda tena” aliongea na kuchapuka kutoka mbio “Jamani polisi wamekuja…” kauli hiyo ndo ya kwanza kumtoka baada ya kufungua mlango na kuingia ndani huku akihema bila mpangilio macho yakimtoka na kushangaa shangaa “Waruhusu waingie tu” aliongea Richard akiwa hana
wasiwasi kabisa, dada zake walibaki wakitazamana kwa mshangao. Jumaa huyo akatoka, punde Juma na maaskari
watatu wakawa wapo ndani ya nyumba ya Richard “Karibuni sana maafisa nawaomba mnitolee hao watu kwa sababu wanatishia usalama wa familia yangu na muwaambie wasije
wakakanyaga tena hapa ni hilo tu wala msiwapelekerumande” Richard aliongea huku akionesha kidole kwa dada
zake “Jamani Richard wewe wakutuitia polisi leo ama kweli dunia hadaa walimwengu shujaa, wewe niliyekuachia ziwa wewe ukanyonya unanitoa kwako kwa kutumia polisi?” Ester aliongea kwa uchungu mkubwa huku machozi yakimlenga, dada huyu yeye hakuamini kama kweli ndugu yake atafikia
hatua hiyo sasa ndipo alipo amini kuwa basi nia yake imefeli, aligeuza sura akamtazama wifi yake kwa jicho la hasira sana akarudisha uso kwa ndugu yake Eva, “Mdogo wangu naona umejionea amechagua penzi na ndugu kawaacha basi kuanzia sasa sisi sio ndugu zake” Eva alitingisha kichwa huku jicho la chuki likiwa kwa wifi yake, polisi hawakuacha ngonjera ziendelee waliwasogelea na kuwaamuru watoke na wao wakatii. “Tafadhari naomba muhakikishe habari hizi haziwafikii waandishi wa habari kwa gharama zozote…mnajua wazi watu wananiwinda kuchafua sifa yangu…vizuri” Richard alimaliza kuongea akakata simu huku akirudishia pazia alilokuwa amelipenyua.“Mke wangu pole, hakuna atakae kuja kututenganisha zaidi ya
Mungu na wala sio watu, sipo tayari kukukosa kabisa” aliongea Mheshimiwa huku akimvutia mkewe kifuani hii
baada ya kukaa sofani. “Haa Fatuma …” Wini akatahamaki na kujinasua kifuani akanyanyuka na kumfata Fatuma ambaye
alionekana kujiegemeza ukutani akitabasamu huku ameushika mkono wake uliojeruhiwa akamkumbatia “Pole
jamani pole mdogo wangu” aliongea Winifrida huku akimshika bega Fatuma na kumvutia kifuani “Hamna dada
usiwe na hofu kikubwa wewe ni mzima ndio jambo la kushukuru” Fatuma aliongea huku kichwa kikiwa begani mwa
Wini, Richard alikuwa hajaelewa kitu hivyo alibaki kuwatazama tu kwa furaha. Wini alijinasua katika kifua cha Fatuma na kumuangalia mumewe, “Mume wangu Fatuma alikuwa ananizuia nisijiumize pindi nilipokuwa nampokonya kisu nikamjeruhi katika kiganja chake inaniuma sana” Richard ndipo akazibuka masikio nakushangaa akanyanyuka kujionea
“Asante sana Fatuma kwa moyo wako haya jiandae basi nikupeleke hospitali ukatazamwe majeraha” “Sawa kaka
ngoja nimuwekee chakula Jumaa aje kula bado hajakula nilisahau kumuita” “Ooh hapana nitafanya na uende Hospitali
mpendwa” alidakia Winifrida.Tatizo la mtoto katika nyumba ya mheshimiwa Richardlilianza kuzoeleka, lakini haikuwa rahisi katika moyo wa Winifrida liliendelea kuishi na kuitafuna subira na imani yake
iliyobakia ndani ya moyo wake. Winifrida aliendelea kucheka, kufurahi, kula na kuendelea na shughuli zake za kila siku
lakini yote yalikuwa ni maigizo. Usiku mmoja, Winifrida akiwa kajilaza macho juu, alijigeuza na kumuangalia mumewe aliyekuwa mbali kwa usingizi akamtazama jinsi alivyo “Wewe ni Handsome sana mume wangu ukilala hata ukiamka” alijiongelea Winifrida na kutabasamu akaanza kumshika shika mashavu mumewe na lips, alifanya hivyo mpaka Richard alipofumbua macho na
kumtazama “Vipi mke wangu mbona hulali” aliongea bwana Richard kwa sauti ya kichovu chovu, Winifrida alichukua
muda wa takribani dakika tatu akimuangalia tu ndipo alipoamua kusema “Mume wangu najua hupendi kuniona
naongelea tatizo hili ila mimi nimepata njia” “Umepata njia” Richard usingizi ulimpaa macho yakamtoka na akajinyanyua kukaa kitako, “Njia gani mke wangu” Wini nae alifata kwa kunyanyuka na kukaa kitako, “Sio njia nzuri sana…ni kuwa mume wangu, mi naomba utafute mwanamke mwingine uzae nae mi uniache…” kabla haja malizia, Richard alishtushwa sana, hali yake ilianza kubadilika moyo ulimbana pumzi
zikaanza kutoka kwa tabu, akaanza kutweta akikohoa hovyo huku mkono ukiwa katika koo lake kama mtu aliyebanwa kwa loba kooni. Wini alishtuka na kuogopa sana akaanza kumpiga
piga mgongoni kumtuliza lakini wapi akachukua nguo na kuanza kumpepea huku akilalamika “Mume wangu unanini…
jamani mume wanguu” mwisho hali ikaanza kupungua huku Richard macho yakiwa mekundu yamemtoka na machozi
yakimteremka, Wini alimsogeza na kumkumbatia “Basi mume wangu sitataka kukuacha tena sitarudia nakupenda mume wangu, sitasema tena nilichokisema basi tujaribu kumuhasili
mtoto” Richard akiwa kakiweka kichwa kwenye mapaja ya mkewe alisikia lakini uwezo wa kujibu hakuwa nao kwa taabani aliyokuwa nayo, ama kweli mapenzi ni uchawi wa ajabu.

Siku nazo zikaanza kusonga zikienda mbio mbio kama zinakimbizwa, watu mbali mbali wakaanza kumshauri Winifrida kuhusu kuingia katika masuala ya waganga wa jadi kujaribu bahati yake maana wengi hubahatika waliongea kwa
majivuno. Maneno mengi aliambiwa yeye aliishia kuwajibukuwa atafikiria, upande wa mumewe nae mambo yalikuwa
sawa tu na kwa mkewe marafiki na jamaa wengine walimshauri kuhusu kutafuta waganga nae aliwajibu atafikiria.
Kadri siku zilivyokwenda na wao walianza kulewa na maneno ya watu imani ikawatoka na kuanza kuamini mambo ya
waganga wa jadi na sio Mungu tena kama awali. Hatua ya kwanza ilikuwa ni kuwatembelea hao waganga waliokuwa
wanasifika tena bila kukata tamaa, walichanjwa chale wakalishwa madawa ya kila namna wakapewa masharti ya
namna tofauti kulala chini, kuoga na nguo, kwenda kutupa vitu makaburini na mambo mengine ya ajabu kibao kama kawaida ya waganga wengi walivyo. Marafiki na jamaa zao baada ya kuona hakuna mfanikio wala mabadiliko yoyote ndipo wakayaweka wazi midomoni kuwa Winifrida atakuwa
ni tasa kabisa hakuna la ziada. Kama ilivyo marafiki si wakufanana wapo wazuri na wabaya, kati yao kuna waliojikuta wakimkosea sana Richard kwa kuthubutu
kumshawishi amsaliti mkewe na kuzaa nje ya nyumba yake kisiri ili tu awe na mbegu ambayo itakuja kurithi mali zake, jambo hilo lilipelekea kutofautiana baina yake na hao marafiki na hata kuvunja mahusiano kabisa. Richard alikuwa mkali sana hakuwa tayari. Richard na Winifrida walikaa wakachambua wakawaza mioyo yao nayo ilianza kubadilika taratibu na kuanza kusalimu amri kukubali hali halisi kuwa mtoto ni zawadi na hupewa yoyote endapo mwenyezi Mungu akipenda na sio kuwa inatoka kwa binadamu wenzao,
walitubu kwa tabia mbaya walioyoifanya kwa kumkosea mola wao na kuanza maisha mapya.“Ni balaa zito! Tumemuona Bwana Fanuel Mkwasi akiwa makaburini dhahiri ni mtu mwenye uchungu na familia yake aliyoipoteza, alimvamia Mzee
Ishengoma akihitaji ukweli kuhusu familia yake lakini aliukosa na kuishia kumuua huku akibaki na kiapo cha sehemu ya ukweli uliobaki. MheshimiwaRichard nae alifanikiwa kushinda kesi dhidi ya washindani wake bila kutegemea huku akipewa taarifa na wakili wake kuhusu kufojiwa kwa ushahidi na kuhitajika kukutana na mheshimiwa raisi haraka, lakini hatujajua walikutana au hawakukutana na kama walikutana waliongea nini! Miaka mitano ikapita, Winifrida mke wa Richard anaonekana kuwa na kitu kinachomnyima raha kwa miaka mingi hadi kufikia kukumbuka namna ndoa yao ilivyofungwa bila kubainisha, na mwisho wa siku alimshawishi mumewe kuishi maisha ya kawaida na kuyatupilia mbali maisha ya Siasa, je! kwanini? Waliwapunguza walinzi na wafanyakazi na kumuajiri mlinzi mmoja ambaye hatukujua alimtolea wapi, lakini alionekana mheshimiwa Richard kuwa na
walinzi wa siri wakimlinda kila aendapo bila mkewe kujua. Mgongoni mwa
mheshimiwa Richard anaonekana akifatiliwa na watu wa Raisi kwa siri kupitia waziri Mwijaku aliyetumwa kumshawishi bila mafanikio pamoja na Kijana aliyemuamini na kumuajili kuwa mlinzi wa nyumba yao naye kuoneakana
kuwa na kazi ya ziada tofauti na ulinzi. Huzuni ya kukosa mtoto ilimtawala
Richard na mkewe na kuamua kufanya matibabu wanaligundua tatizo na
kuamua kuishi nalo lakini changamoto nyingi zakuingiliwa na ndugu, jamaa
na marafiki hazikukoma kuwaandama. Je! Kijana Jumaa anampango gani na
familia ya Richard na aliwezaje kuishi humo? Je! wanandoa hao wataweza
kuvumiliana kwa hali hiyo ya kukosa mtoto na kudumisha mapenzi yao? Je!
Fanuel Mkwasi atawezakufanikisha ataweza upata ukweli anao utafuta?”

Itaendeleaaaa....

Mijadara inaruhusiwa
IMG_20210320_131445_046.jpg
 
BAADA ya kumaliza Msimu wa 1 sasa tunaingia Msimu wa Pili
 
The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)
MTUNZI : Akida Siri Rambao
Contact: 0658328596
Email: akidasiri@gmail.com

SEHEMU 2 (A) : FURAHA NA MAJONZI

Dodoso:
“Richard anabahatika mtoto wa kiume mrithi wa utajiri wake nakumshangaza kila mtu kama miujiza vile lakini Samuel na Peter wanaonekana kujawa na wivu na kuamsha hisia za chuki walizozifukia Kusiko julikana, mtu aliye jiita Tall anapokelewa na Madam Moo nakuziomba tarifa za Samuel, Peter na Richard. Upande mwingine Winifri da anaamua kitu ambacho anaamini kitamsaidia yeye kuimarisha ndoa yake dhidi ya Sabrina mke wa Samuel kwa kumuingiza mumewe mtegoni na kuzituma picha za mumewe akiwa na Sabrina kwenda kwa Samuel huku akizisindikiza na maneno ya shombo na kejeli bila kujua alikuwa anaupalilia moto kuni. Samuel anachukia na kuzua maafa makubwa nani wakulaumiwa?”

Tuendeleeee....

“Karibuni sana karibuni” sauti ya mwanamke iliyoathiriwa na
lafudhi ya kihindi ilisikika kipindi wakina Richard wakifungua
mlango kwa kubisha hodi, “Asante sana daktari” “Ooh mheshimiwa habari za siku nyingi kijana wangu” mama huyo
kwa tabasamu pana alinyanyuka kwenye kiti na kuunyoosha
mkono wake wa salamu kwa Richard. “Safi tu mama Shikamoo”“Shikamoo” Winifrida nae alisalimu “Marhaba….haya karibuni sana jamani kuweni huru kueleza
hali zenu” wote wakakaa “Asante mama leo nimeona niwatembelee bwana…Mke wangu anashida hebu elezea
unavyo jisikia” aliongea Richard na kumshika bega mkewe
Winifrida akamtazama mumewe kisha akatabasamu “Ni kweli… sasa hivi nina miezi mitatu kasoro sijaona siku zangu,
naumwa sana kichwaa, mwili unachokaa, nina kuwa na hasira sana bila sababu najiskiaa kukaa peke yangu tu, halafu
kichefuchefu kinanisumbuaa mpaka inafikia hatua natapika sana pia vyakula vingi nilivyokuwa nakula na kuvipenda sasa
hivi siwezi kuvila.” Daktari alimtazama kwa makini Winifrida akatabasamu na kutingisha kichwa na kuanza kuandika
andika katika fomu ambayo waliingia “Okay pole sana mwanangu vipi kuhusiana na moyo kwenda mbio siku hizi…?”
aliuliza daktari “Yaah hilo nalo ninalo” Winifrida alidakia kwa wasiwasi daktari aliendelea kuandika andika alipo maliza
akaisogeza fomu “Sasa naomba muelekee upande wa Maabara chumba namba saba akafanye vipimo kisha mtakuja tena
kwaajili ya majibu”. Baada ya dakika 45
Tayari mke na mume walikuwa mlangoni mwa daktari na makaratasi mkononi wakibisha hodi tena “Karibuni wanangu”
ilisikika sauti tokea ndani “Asante” waliitikia kwa pamoja na kuingia wakakaa, daktari akaichukua karatasi ya majibu
iliyowekwa mezani sekunde chache za nyuma akaanzakutabasamu “Hongera Mr. Richard” Richard na mkewe wakatazamana na kurudisha macho kwa daktari bila kusema neno “Bi winifrida umeonekana huna maradhi yoyote
yanayokusumbua bali umebarikiwa kuwa na Ujauzito wa miezi miwili” aliongea daktari akiachia tabasamu “Heeee”
Winifrida alihamaki na kutoa macho “Ujauzito au sijasikia?!!”Richard aliuliza daktari aligeuza shingo kumtazama Richard ambae nae alikuwa na mshangao, “Ndio anaujauzito bibie hivyo mnapaswa kuanza kutembelea kliniki ili upate
miongozo kuhusu ya afya ya mama na mtoto”. Winifrida akaanza kushika tumbo lake huku akilitazama kwa furaha
akaendelea kulipapasa huku machozi yakimtoka wakati huo Richard kaganda tu akiwa ameduwaa kama mtu asiyeelewa
kinacho endelea “Asante sana Mungu wangu, Ooh nakupenda sana mwanangu” Wini aliongea kwa sauti Richard akaanza
kutoa tabasamu “Mtoto tumepata mtoto?” aliongea Richard akijisogeza zaidi kwa mkewe. “Ndio mheshimiwa mkeo ni
mjamzito” alisisitiza daktari huku akiendelea kutabasamu.Mungu hamtupi mja wake, baadhi ya watu kwa nafasi zao
walijisemea maneno hayo baada ya habari kutokuwa ya siri tena na kusambaa katika vyombo vya habari watu wakabaki
kushika midomo wengine wakijesemea “Ama kweli mtu akiwa nacho huongezewa”. Walio muombea dua walishukuru kwa habari hizo zilizofurahisha wengi. Maisha yale waliosota kwa miaka mingi kwa kukosa mtoto, walinusurika kutoa maisha
yao waliishi kwa masimango mahusiano ya ndugu na jamaa pamoja na marafiki yalififia kisa Mtoto looh! Ama kweli baada
ya dhiki faraja.

Msasani, Kinondoni -Dar es Salaam
Katikati ya usiku mmoja, Winfrida alianza kuyahisi maumivu makali tofauti na yale yanayokuja na kuondoka kama
alivyozoea, aliendelea kugugumia kwa kuamini yataacha na atafika asubuhi kama inavyokuwa lakini wapi uchungu ulizidi. Kilio cha taratibu mara kikaongezeka na sasa hakuweza
kuhimili wala kujizuia mdomo ulion’gata mto ukaachiwa wazikuruhusu mayowe kutoka kadri uchungu ulivyokuwa ukizidi
mkono mmoja ukishika chini ya kibofu mmoja kashika sehemu ya kiuno mara unaenda kushika kichwa na kurudi
kiunoni akigaagaa miguu ikirushwarushwa na kujikunjamfano wa korosho. Kelele zilimpelekea mumewe kukatiza
usingizi na kumuangalia mkewe aliyekuwa taabani kwa maumivu yaliyomzidia na kumfanya kupigapiga kitanda
akilalamika “Kiunooo chaangu…. jamani kiuno, mume wanguuu uwiiii nakufaaaa…”. Harakaharaka Richard alinyanyuka na kutoka chumbani haikupita muda alirudi na Jumaa kwa pamoja wakasaidiana kushuka naye ghorofani na kumpakia kwenye gari, safari ni Hospitali ya jirani na makazi yao.

Msasani Peninsula Hospital, Kinondoni-Dar es Salam.
“Haraka haraka nesi fungua mlango tafadhari” ilikuwa ni sauti ya daktari bwana Mark Wambura aliyekuwa mstari wa mbele kuhamasisha kunususru uhai wa mama na mtoto wakimuacha
Richard akiwa njia panda kwa wasiwasi tele mkewe akiwa katika kitanda cha matairi akigugumia maumivu makali
akirusharusha mikono kwa uchungu. Punde mwanamke mmoja nesi alionekana kufungua mlango alimopelekwa Wini
na kumsogelea “Vipi anaendeleaje mke wangu” Richard aliuliza kwa wasi wasi akimsogelea mwana mama yule
mwenye sare nyeupe, “Mheshimiwa mgonjwa wako amepatwa na uchungu wa uzazi hivyo yupo katika matayarisho ya kujifungua kama hutojali uje kesho asubuhi, lakini ni vema tukiendelea kumuombea” alimaliza na kuondoka. Richard bila hiyana alijiinamia kisha akanyanyua uso wake juu kwa wasiwasi akijishauri.Sauti ya mlio wa simu uliendelea kulia ukalia ukalia tena na
mwishowe Richard akafumbua jicho na kupapasa pajani akiwa twii kwa usingizi uliomchukua “ Heeh! ni asubuhi!?”
alijisemea na kuisaka simu inayoita, alijikalisha sawasawa na kuipeleka simu machoni mara akaikunja sura “…Waziri
Mkwasi shiti” akapokea “…Ndio kiongozi… bado nipo Tanzania…hapana mkuu ” mara akaitoa simu sikioni na kuitazama Safari hii usingizi wote ulionekana kukata
“…hapana sikukosei heshima kiongozi wangu kwa sasa nashughulika na mambo ya familia nionee huruma walau
kiduchu” safari hii aliongea kwa wasiwasi sana huku simu ikiwa bado sikioni mwake akiwa amesawajika uso kwa huzuni. “…hapana kiongozi nilikwambia sijaipata flash badonitafatilia…Swai asikuumize kichwa Mkuu…hallow hallow aaaah shit amekata…basi bwana” kwa tahadhari aligeuka kutazama pande zote kama mtu mwenye wasiwasi wa kuogopa kushtukiwa huku akionekana kuwa na hasira za ndani kwa ndani.
Kulikuwa kumeshaanza kupambazuka watu wachache walionekana wakienda na kurudi, wengi wakiwa wanapita na
kumshangaa maana wazi walimjua ni mheshimiwa Richard ndiye aliyejiegemeza katika ukuta kwenye benchi. “Habari za
asubuhi mheshimiwa…” Dr Mark Wambura alimsalimu bwana Richard “Aah salaama tu Dr Wambura vipi maendeleo” haraka
alisimama tayari kupokea taarifa mpya “Habari ni nzuri tu mheshimiwa pole kwa kulala hapo usiku kucha lakini sijisikii
vizuri kwa kweli wewe si wa kulala katika mabenchi mzee” aliongea Wambura na kusawajika uso huku akionesha uso wa
aibu akitazama huku na kule Richard alimwangalia tu kisha akaongea, “…yaah..yaahah najua asante kwa kujali vipi mke wangu” Dr. Wambura akatoa tabasamu na kumpa mkono Richard “Hongera mheshimiwa kwa kupata mtoto mzuri wa Kiume mwenye afya” “…unasema kweli Dr. hebu nimuone
mara moja”, “Bila shaka tuongozane tumemuweka chumba spesho mama na mtoto siunajua tena hahahaha” alijichekesha daktari Wambura akiongoza njia huku bwana Richard akiwa
ni mwenye hamasiko kwa taarifa alizozisikia.

Watu waliomfahamu waliduwaa kwa muonekano wake maana alikuwa na kibukta, makubazi miguuni na fulana yake ya mazoezi jambo ambalo halikuwa rahisi kuonekana kwa watu maarufu kama yeye na wala hakujali aliona kawaida tu
“…Karibu mheshimiwa unaweza kuingia tafadhari”. Wambura aliongea huku akiufungua mlango Richard hakuvunga kwa furaha iliyo kifani akaingia alichokiona machoni mwake kilikuwa ni kitu chenye kuvutia sana alisogea na kukaa
pembeni ya mkewe huku macho yakiwa kwa mtoto ambae wakati huo alikuwa amelala, alirudisha macho kwa mkewe
“Hongera sana mke wangu” “Hongera na wewe mume wangu” ilivutia sana kuwaona wapendanao hao wakiwa na nyuso za furaha sana, walikumbatiana kila mmoja sasa akilia kwa furaha sana. Wala haikuhitaji matangazo tayari wale
wanahabari wanayoijua kazi yao walishazirusha habari juu ya familia hio kupata mtoto wa kiume. Kwa namna gani ilikuwaje wanajua wenyewe.

BAADA YA WIKI
Msasani, Kinondoni-Dar es Salaam
“Habari zenu mabibi na mabwana” Richard akiwa na kipaza sauti aliongea huku uso ukiwa na tabasamu la haja, watu
wakaitika na kuacha pilikapilika zilizokuwa zikiwashughulisha wakati huo wakamtazama “…jioni ya leo napenda kumpongeza mke wangu kipenzi Winfrida ni mwanamke wa nguvu, amevumilia mengi sana katika maisha yake ikiwemo matusi, masimango na majina yanayo kera lakini alivuta subra siku zote akiendelea na kazi yake ya Uwalimu na kuliendesha shirika lake la Mwanamke simama kwa juhudi zote na leo hii amejaaliwa kuwa mama, hivyo
naomba tusherehekee kwa pamoja furaha iwe kubwa kadri tutakavyoweza tafadhari tumpongeze mama na kumkaribisha
mtoto Pius” akimaliza kuongea na wageni kwa pamoja wakapiga makofi na kuendelea kufurahia baadhi yao
wakianza kutikisika kwa kufata midundo ya bendi ya Msondo Ngoma iliyoanza tena kutumbuiza “Hivi unasema kweli
Sabrina hakusumbui tena?” bwana mmoja mrefu aliongea kwa kumnong’oneza mwenzake ambaye alikuwa mfupi na
mnene “…acha tu siri ya mtungi ajuaye kata sitaki kuyakumbuka ya nyumbani ninapofunga mlango maana yanaumiza na hapa nimtazamapo Richard natamani nigeuke mbwa mwitu nikamkwarue nimuachanishe kichwa na kiwiliwili” aliongea bwana huyo mfupi, mweupe mnene hasira ikidhihirika machoni mwake mkononi akiwa na glasi ya mvinyo “Samuel nakuelewa na namuona anavyofurahiamaisha yake” aliongea bwana yule mrefu huku akimtazama Richard kwa jicho la chuki “…wala asikushughulishe dawa yake ipo jikoni tulia nita kwambia cha kufanya soon” bwana yule mfupi na mnene aliongea kwa sauti ya kunong’onamacho yakiwa bado kwa Richard. Wakatoka pamoja na
kusogea upande ambao familia ilikuwa imekaa ikipata chakula huku watu mbalimbali wakisogea kuwapa hongera.
“Hongera sana bwana mkubwa kwa mafanikio naona una bahati sana hela zimekutembelea, umaarufu na sasa umepatamrithi” bwana yule mrefu aliongea mkono wa salamu akiuelekeza kwa mheshimiwa Richard ambaye alionekana kushtuka mbele za watu “...aah asante Peter nimefurahi mno naomba endeleeni kufurahia pia” Richard akatoka kwa haraka na kuelekea upande waliokuwepo baadhi ya wabunge na
mawaziri waliotembelea nyumbani hapo, Samuel alibaki kumuangalia kwa jicho la dharau sana huku mwenzake akimpigapiga bega “Naona anatukwepa sana pesa ina jeuri”, Samuel aliongea
“Tuondoke zetu hapa tusijejikuta
tumewekwa kwenye magazeti waandishi wa habari hawakosekani hapa tujihadhari” Peter aliongea huku akionesha macho ya wasiwasi.

BAADA YA MWAKA NA MIEZI
Kaunda Road, Arusha Mjini.

Mlango wa kushoto wa gari kubwa Lori ulifunguliwa “Bwana we usiye na jina amka safari yako imefika ukutani” kwa
mkono wake aliendelea kumtikisa mtu aliyekuwa twii kwa usingizi wa kufa. “Abwe!” alisema tena huku akimshangaa
abiria wake kwa namna anavyojinyoosha mwili kwa uchovu mkubwa huku akipiga miayo mfululizo macho yakiwa
mekundu kwa haja ya usingizi uchovu ukiwa umemzidi. “Weee niite Tall inatosha” aliongea na kufumbua macho
“Kumbe kumeshakucha” aliongea tena huku akipepesa macho akiangaza huku na huko “…na hili baridi mwezi huu wa sita
litatuua” aliongea tena huyo akatoka kwenye kiti na kushuka kwenye gari kwa kuruka. Alikuwa mrefu, mrefu kweli kweli
maana si kwa urefu aliokuwa nao lakini hakuchosha maana alijaaliwa mwili wa kiume haswa licha ya baridi lakini misuri
ilionekana na sehemu ya shati lake chakavu lililopoteza vifungo vya juu liliacha sehemu kubwa ya kifua kilichojaa kwa nje “Subhana llah doooh! Ingekuwa si kuokoa mali yangu na wale shusha shusha walaiih nisingekupa lifti haaa! Wewe ni mtu au jitu” aliongea bwana dereva kwa lafudhi yake ya Kipemba kisha akaongea tena “Weee mtu jitu?! kama mla
mawesalaleee”alitahamaki mikono ikiwa kiunoni akimtazama “Malipo ya wema ni wema bwana mkubwa tutaonana Mungu akipenda shuka lako lipo hapo juu” Huyo
akashika njia na kuondoka bila kugeuka “Weee Toluuuu Ngoja nikuongezee hela nyingine ya mahitaji kijana walau ukanunue fulana, suruali na makubazi maana hayo uliyo nayo kama yamepigwa bomu heheheee” aliongea dereva wa Lori na kujichekea akiutumbukiza mkono wa kuume kwenye mfuko wa nyuma wa suruali yake huku akitazama chini akiendelea kuyacheka maneno yake taratibu, akautoa mkoba mdogo wa
ngozi na kuuchanua katikati na kuanza kuzitenganisha noti za elfu kumi kumi akihesabu kisha akanyanyua uso huku kiganja kimoja kikiwa na noti na kingine kikiwa na mkoba “Amaa!
Weye TOLUUU Kenda wapi tena!” mdomo akauacha wazi mwaaa! kwa mshangao akatoka alipo na kutazama huku na
kule na kusogea akimtafuta katika baadhi ya mikusanyiko ya watu mchana huo aliambulia patupu “Dunia inastaajabisha
sana” alijisemea huku akirudi sehemu ya gari lilipokuwa. “Sijui hata amepotelea wapi haya na iwe ya kheri safari yake
huko aendako” alijiongelea akaingia na kuliwasha gari tayari kwa safari.
Bwana yule alijitambulisha kwa jina la Tall aliendelea kutembea akikata mtaa mmoja baada ya mwingine macho yakiwa na tahadhari kubwa kama mtu asiyetaka kuonwa au kujulikana nyendo zake, wakati anakatiza katika moja ya maduka makubwa alisimama na kuwatazama watu waliokusanyika wakijisomea magazeti ya asubuhi hiyo baada
ya kujishauri akasogelea na kujumuika na moja ya watu aliowakuta. Mara ghafla moyo ukampasuka mapigo yakabadilika na kuanza kudunda mfululizo kwa mshtuko baada ya kuitambua picha iliyomuonesha kijana mtanashati
huku maneno ya herufi kubwa yenye habari kumuhusu yenye mkolezo mweusi kuhamasisha umuhimu wa habari yake
katika moja ya magazeti yaliyopangwa kwa ustadi kwenye kibanda cha mbao. Hasira hazikujificha usoni mwake macho
yalimtoka akiikazia picha ambayo waziwazi alimtambua muhusika “Tafadhari nipatie gazeti hili” aliongea akimaanisha kwa kuonesha kwa kidole macho yakiwa kwa muuzaji
akapatiwa akatoa noti ya shilingi mia tano akalikunja na kutimka zake huku akionekana yu tofauti na alivyokuwa
awali. Ilimchukua takribani masaa mawili akipita mtaa mmojana kufata mwingine akiwa bado mwenye hamasa ya kuwahi
akipiga hatua ndefu.

Kipanga Street, Arusha Mjini.
Tall akiwa ni mwenye wasiwasi na tahadhari alisogea na kusimama chini ya mti kando ya barabara akitazama upande
wa pili uliokusanya nyumba za kifahari, macho yake yakagota kwenye nyumba ya ghorofa moja “Sasa huu ndio muda mzuri” alijiongelea baada ya kutazama upande wa mashariki jua linapozama. Nusu saa ikapotea na kukaribisha giza kunyemela na mwisho likatawala eneo lote. Bado kwa umakini mkubwa
aliendelea kuitazama nyumba ileile lakini hapakuonekana mtu kuingia wala kutoka mwishowe akajitoa akiwa na
tahadhari kubwa na kuvuka barabara hadi katika ukuta wa nyumba ile, alizunguka upande wa ukuta kisha akatazama
huku na kule akarudi nyuma hatua tano kisha kwa kasi aliruka na kugota miguu ukutani kisha akajikusanya kwa
umahiri na kujirusha kama ngedere akirukia matawi mwituni na tayari mikono ikakutana na mwisho wa urefu wa ukuta
“Shabbash” aliongea kwa sauti ya taratibu bila kulaza damu akauvuta mwili kwa juu kwa kutumia mikono yake na mara
akarukia upande wa pili wa nyumba. Akatua ardhini kwa kuweka mikono chini miguu yote kaikunja kama mtu aliye
tayari kuanza mbio za mashindano hii ni baada ya kutoka juu ya uzio wa ukuta. Alitulia akisikiliza kitu alipo ridhika
akajinyanyua taratibu kwa tahadhari na hatua za taratibu za kunyemelea zikaanza huku akitazama kila kona kuhakikisha
usalama wake “Inamaana hakuna mtu hapa…” alijisemea.

Bado kwa tahadhari aliendelea kuikagua nyumba kadri alivyoweza na akili yake ilivyomuagiza “Sasa naweza kuingia”
alijisemea akasogea hadi katika lango la uhifadhi wa magari akanyanyua upenyo aliouhitaji na kuingia kwa ndani. Akapapasa ukuta na kukutana na kitufe cha saketi akatabasamu kisha akakibonyeza bahati haikuwa yake
hakuna taa iliyowaka “Dah hakuna umeme” alijiongelea tenana sasa akianza kupapasa akitembea kwa tahadhari machosasa yakaanza kuzoea kiza kilichopo “Ooh afadhari” alikuwa
ameshikilia kitasa akakinyonga na mlango ukafunguka lakini hata hatua moja hakupiga kitu kizito kikatua kichwani mwake akaanguka na kupoteza fahamu.

Baada ya masaa kupitaTall Alikuwa kajiinamia muda mwingi mkononi glasi ikiwa nusu ya kinywaji kilichomiminwa saa zima lililopita kichwani bandeji lilokunywa damu iliyotoka sehemu ndogo ya jeraha
lililomkuta “…Unajua ungeweza kufa kwanini hukunipigia hata simu jamani unafikiri lile chuma yaani ungekufa wewe”
aliongea mwanamke wa makamo akiuegemeza ukutani akionekana kutokufurahishwa “Lady Moo hakuna haja ya kunilaumu sikutaka kukusumbua unajua ulisha niambia usiku hautakuwepo kikubwa ulinihakikishia bado unaishi hapa basihalafu kingine ajali ajali tu.” aliongea Tolu huku akiendelea kujiinamia tu “Pole sana, nilijikuta naacha kabisa kazi yetu na
kuendelea na biashara zangu japo nilikuwa nikichunguzwa sana nilitekwa nikapigwa na watu wasiojulikana lakini
hawakuambulia chochote toka kwangu” Lady Moo aliongea kwa huzuni kubwa akaendelea “Nakuonea huruma kwa hiyo
familia yako yote imeuawa hukuwahi niambia ulikuwa katika maficho gani huko… pumzika badae kidogo ngoja nijiandae nitoke kila kitu kipo hapa uwe huru tutaongea jioni nikirudi”
lady Moo akanyanyuka kwenye kiti na kutoka. Muda wote Tolu macho yalikuwa yameganda kwenye picha kubwa katika
ukurasa wa mbele. “Wakati huacha mabadiliko bwana Richard bado sijachelewa nitakutafuta mpaka nikupate.”

Sahil Hospital, Masaki Kinondoni - Dar es Salam.
“Waoo vizuri sana mtoto anaendelea vizuri sasa inatia moyo maana nilikuwa na wasiwasi sana mwezi huu” Richard
aliongea huku akitazama kadi la Kliniki “Hata mimi nimefurahi mume wangu ahueni sasa ameanza kula vizuri,
haaa! mtoto wa mwaka mmoja na nusu kuwa na kilo kumi tu pekee sio sawa walau leo ana kumi na moja na nusu
nimefurahi” aliongea Winifrida huku akimpatia mtoto mumewe “Ni kweli kabisa cha msingi kama tulivyo ambiwa na
nesi tusijisikie vibaya sana hali kama hizi zinawatokea watoto wengi sana wa umri huu isitoshe kutokuwa na uzoefu
kunachangia” Richard alijichekesha kisha akamkonyeza mkewe na kumfanya atabasamu, safari ya miguu katika
korido ikaanza “Kilichonishangaza zaidi ambacho sikuwahi kukijua ni kuwa mtoto anapokataa kula haimaanishi hataki
kula bali anahitaji utulivu na kwenda nae taratibu kwa kumbembeleza kama atakavyo yani huyu mwanao mara
kakimbia huyo unamfata na kijiko mara kakimwaga, mara anakula, ukimpa tena hataki saa moja na nusu zima linaisha
kwa ajili ya kula matonge matano tu yaani mmh unaweza pata hasira kwakweli” wote wakacheka “Kweli kabisa bora
umejionea mwenyewe ungeambiwa na Fatuma ungekataa, nakwambia hawa wadada wa majumbani wana pata shida
sana mpaka unamkuta mwanao ana afya ni jambo la kushukuru, ni kazi ambayo kiukweli wewe kama mwanamke kwenye lile shirika lenu muipigie debe wafanyakazi wote wa ndani wapate mshahara unaofaa na hata ikiwezekana wawe na kampuni maalumu itakayosimamia haki zao kwa ujumla” aliongea Richard na kuendelea na mazungumzo mengine .

Winifrida akafungua mlango wa gari na mumewe akaingia, mara mlio wa simu kwenye mkoba wa Winifrida ukasikika
akiwa ameketi tayari kwa kuwasha gari “Mume wangu simu yako hii…halafu ni namba mpya sijui ni waandishi wa habari
maana nao” alielekeza kumpatia “ Haya Nipatie mtoto na naomba uongee taratibu au kaongelee nje ya gari usije
muamsha” Richard alipokea simu na kumpatia mtoto kisha akatoka nje ya gari na kuipokea kabla ya kukata “…yes
Hallow…” mara uso ulimbadilika na wasiwasi ukamuingia kwa tahadhari aligeuka na kumtizama mkewe ambaye
alikuwa bize akimuweka sawa mtoto Pius aliyekuwa hajiwezi kwa usingizi. “…unasemaje umeingia uchizi kwani?
inawezekana vipi…lakini mbona unanifanyia hivi lakini nimekukosea nini we mwanamke…nikupatie kiasi gani
uachane na mimi ” aliongea kwa sauti ya chini yenye kuhimiza huku akipiga hatua kusogea kando zaidi na lilipo gari
“…haitawezekana unanitafutia matatizo katika familia yangu…” sasa alionekana kuchukia macho yamemtoka
akiendelea kusikiliza “Nitajaribu na itakuwa mwanzo na mwisho leo…naona
unanitumia kwa maslahi yako
tulishayamaliza haya…” akagutuka na kuitazama simu yake “Shit inamaana ameamua kukata simu itakuwaje sasa”
alijiongelea huku akiitazama simu yake kusadiki maneno yake kisha akageuka kimachale kumtazama mke wake kwenye gari akaingiza simu mfukoni na kurejea ndani ya gari “…Vipi mume unaonekana hauko sawa kulikoni” Winifrida aliongea
huku akimkazia macho mume wake akaongea tena “…sikumbuki mara ya mwisho kuiona hali hiyo ilikuwa lini?!”
aliongea tena Winifrida “…endesha tu gari mke wangu tutaongea nyumbani wala sio wanahabari kama ulivyodhania”
Richard aliongea “Ni nani huyo?” aliongea Winifrida kwa hasira kidogo macho akiwa kayakaza kumtazama “Tafadhari
hivi sasa mimi sio mnyonge kama zamani na sio dhaifu tena sitaacha kuitambua hatua yako hata moja hivi sasa” aliongea
Wini kwa sauti kavu “Ooh nitakwambia ni stori ndefu mke wangu” aliongea tena huku akimchukua mtoto Pius na
kumpakata na kumuacha Winifrida akiwa mdomo wazi“Jamani mume wangu unanificha nini unadhani sitakuja
kujua?” huoni aibuuu” aliongea Winifrida kwa mshangao unaoendelea Richard alibaki tu katulia akijiinamia Winifrida
alikunja midomo yake kwa ndani kwa sekunde kadhaa “Najithibitishia kuwa hujawahi nisaliti tangu umenioa na
itakuwa hivyo milele si ndio mume wangu” aliongea Winifrida kwa sauti yenye uchungu ndani yake, akaendelea “Mume ni bora uniambie ukweli kwa sababu nikiujua kwa jitihada zangu itakugharimu nakwambia” Winifrida aliongea tena kwa
sauti kavu akimkazia mumewe macho “Mume nimeshakushuhudia mara kadhaa ukitoka kitandani na kuondoka nyumbani, wakati mwingine ukiniwekea hata
madawa ya usingizi, wakati mwingine unasafiri na kwenda ughaibuni sababu ikiwa ni biashara usidhani kwamba
nilikuwa sijui” aliongea kwa uchungu tena huku sauti ikiwa kavu na macho kayakaza “Unajua nini ni kwa sababu sikuwa
na cha kujitetea ndomana nilichukulia kama shida zangu na nilikupenda wewe tu nikavumilia lakini sio sasa siwezi kubali
uendeleze kunifanyia usiri” Richard alionekana kushtuka ‘Amepatwa na nini mara hii amegundua nini, siwezi kubali
ajue kila kitu’ alijiongelea nafsini macho yakiwa na wasiwasiwa waziwazi mkononi akiwa bado kamshikilia mtoto Pius akaongea “Unaongelea kuhusu nini mke wangu sikuelewi, shida nini kwani” aliongea Richard huku akimtazama mkewe Winifrida akatabasamu “Wivu tu mume wangu ndio unanisumbua si unajua tuna mtoto sasa sipo tayari
kukupoteza unajua, samahani kama kuna kitu nimeongea hakijakupendeza” Winifrida alimaliza na akawasha gari na
kuanza kulitoa taratibu katika eneo hilo la maegesho huku Richard akiwa na mshangao gari hiyo ikaondoka. ‘Lazima
niweke mambo sawa kabla hajafikia kujua yale yote ya kweli kunihusu’ alijiongelea Richard ‘Lakini mimi sio mjinga’
Winifrida alijisemea na yeye nafsini huku akimuangalia kwa macho ya wizi mume wake tayari akiwa barabarani. “Mke
wangu ni hivi nisikie, kama ni kuhusu simu ni kweli sikutaka kukwambia saizi nilitaka kumaliza mwenyewe maana ni
kichefuchefu ni Sabrina anataka tuonane leo hii bila kukosa” aliongea Richard safari hii akiwa ni mwenye kujiamini “Ooh
kumbe, sasa mume wangu si unajua kuwa yeye ni mke wa mtu? Na uliniambia mwenyewe kuwa sasa amehamishiwa
makazi Dubai na mumewe pia ulinihakikishia kuwa hujawahi
fanya lolote na yeye zaidi ya urafiki tu na wala hamkuwahi kuwa wapenzi sio?” aliongea Winifrida “Sahihi mke wangu”
alijibu Richard “Ni hivi naomba unikutanishe nataka kuongea na yeye ana kwa ana” alionge Winifrida na kumfanya Richard atoe macho “…mke wangu sikia naomba unipe nafasi ya mwisho hii nikutane na yeye mwenyewe ikitokea au ukisikia chochote sitakuzuia kukutana na yeye muda wowote ule nakuomba tafadhari” aliongea Richard akidhihirisha ombi lake kwa uso wa kumshuka ‘Ushaingia kwenye mtego wangu
mume’ alijisemea Winifrida
kwenye nafsiyake“Unanihakikishia hilo?..sawa fanya hivyo ukaonane naye leo…kingine naamini mimi ndiye mwanamke pekee uliyewahi
kufurahia penzi langu na wala hutakuja nisaliti” aliongea Winifrida huku akitabasamu “Hilo wala sio la kuliuliza mke wangu, asante kwa hilo”.

Itaendeleaaaa......

IMG_20210319_214332_452.jpg
 
View attachment 1753474
Vipi iendelee???
 
The. Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)
MTUNZI : Akida Siri Rambao
Contact: 0658328596
Email : akidasiri@gmail.com

Ilipoishiaa.....
“Unanihakikishia hilo?..sawa fanya hivyo ukaonane naye leo…kingine naamini mimi ndiye mwanamke pekee uliyewahi
kufurahia penzi langu na wala hutakuja nisaliti” aliongea Winifrida huku akitabasamu “Hilo wala sio la kuliuliza mke wangu, asante kwa hilo”.

Tuendeleeee...

Sehemu 2 (B)
Kipanga Street, Arusha Mjini.
“Haya baba mahitaji uliyoyataka haya hapa” Lady Mooakaweka box la simu mezani pamoja na laini akimtazama tolu
machoni kisha akaongea tena “Tayari laini imefanywa kuwa maalumu kama ulivyoniagiza bosi na pia kama tulivyoongea gari mpya uitakayo ipo nje inakusubiri, kuhusu mavazi na
mengineyo nakusikiliza bila kusahau taarifa za Richard, Peterna Samuel zote utazipata kabla ya kuchwa kwa jua la leo
asilimia 96 ipo tayari” Lady Moo alimaliza akakenua kuliachilia tabasamu zito lililofanya mwanya wake mkubwa
wa juu kuonekana na kufanya sura yake ilete mvuto zaidiikisaidiwa na macho yake makubwa ya duara na pua yake ya
mchongoko ikisaidiwa na shepu yake namba nane, ilikuwa sekunde kadhaa mpaka Tall kubwenza baada ya kuridhika
kumkodolea macho “Hakika umrembo sana Lady” aliongea bwana Toluu akiendelea kumtazama zaidi “Hebu kwenda hukooo,” aliongea Lady Moo kwa kudeka “Hebu naomba unieleze Kiongozi inakuwaje wewe uhusike kwenye biashara haramu samahani lakini nimeomba tu” aliongea madam Moo “Unajua nini Moo kama ndugu yangu asingekufa huenda
ningehisi ni yeye hatukuwahi kukaa pamoja na kumaliza tofauti zetu maana alikuwa ni mtoto wa nje tuliotofautiana mwezi tu baba alimkataa ili kuilinda ndoa yake nililijua baada ya kuwa mtu mzima na akaugawa urithi wote kwangu huku
akidai hana mtoto tofauti na mimi” aliongea kwa masikitiko “Ooh pole sana basi itakuwa ni mambo ya edition waliedit
kukuchafulia sifa yako ni lazima utafute ushahidi wa hili, haya pumzika wacha niwahi” Madam Moo akajinyanyua kwenye kiti na kuondoka , toluu akamsindikiza mpaka alipofunga
mlango wa kutokea “Haya bwana” alijisemea na kutazama vitu alivyoletewa akiwa mezani. Akatoa simu ya smartphone mpya na kuipachika laini, akawasha. Akanyakua kalamu
iliyokuwa juu ya diary mpya ukurasa wa kwanza akanyanyuka akiwa kakishikilia kijitabu hicho chakumbukumbu na kusogea nacho hadi katika dirisha lililokuwa karibu akapenyua pazia na kuchungulia akatabasamu
akasimama na kuanza hatua fupifupi huku akipiga mluzi huku akielekea upande uliokuwa na chumba kidogo akafungua na kuingia kisha akabonyeza sehemu ya ukuta nayo ikaingia ndani akaingiza mkono na kufungua kitasa kwa ndani na
ndipo mlango upande wa pembeni ukafunguka na kuonekana
vibonyezeo vya namba naye akabonyeza vile ajuavyo na mlango ukafunguka na akaingia “ asante sana Lady” alijisemea
na kutabasamu.

Baada ya wiki.
Sinza Park, Kinondoni Dar es Salaam.
Mlango ulio nakshiwa maandishi ya VIP ulifunguka na Bwana mmoja mrefu aliyeficha sura yake kwa kapelo aliyovalia
kichwani aliingia moja kwa moja na kukaa katika moja ya sofa kubwa ya kisasa katika eneo hilo lililokuwa na mwanga
mwekundu hafifu sana huku sauti ya mziki isiyokera ikiendelea kuburudisha masikio yake. Mhudumu wa kikealiyevalia nguo fupi na inayobana mpaka kiasi cha kuchora umbile lake na kudhihiri machoni mwa watazamaji alifika pahala hapo akitokea eneo la juu lililo na kaunta na kuinama karibu kabisa na bwana yule akimuongelesha kisha akatabasamu na kuondoka kwa maringo, punde alirudi akiwaameshikilia sahani iliyo na chupa mbili za wine na glass akafungua moja na kumiminia kwenye glasi na kuondoka.
“Ooh umefika muda mrefu” Samuel aliongea na kutabasamu
hukuakiwa kasimama katikati ya mlango
mwiingine baada ya kuufungua, macho makali ya bwana yule yenye kumaanisha onyo yalikutana na Samuel na kumfanya
ameze mate kwa wasiwasi Samuel akaingia ndani akiuacha mlango wazi bwana yule akanyanyuka bila kusema kitu
kumfata na mlango ukafungwa. Ilichukua takribani saa moja mlango ukafunguliwa na bwana yule akatoka na kuondoka
zake. “Unajua huyu jamaa sijamuelewa na kwanini katulenga sisi ametujua hatuna hela tunafilisika kwa hiyo ataweza
kutushawishi au kuna cha ziada nisichokijua” Peter aliongea,
Samuel kwa macho ya utata yenye kuficha kitu alitazama pembeni na kulivuta tabasamu la kinafki “Hakuna kaka wala hakuna haja ya kufika huko mi namuamini, tusubiri na tuone…kwani uongo Richard anakipi cha maana alichotufanyia?” Samuel aliongea huku akiirudisha glasi
mezani akachukua sigara akaiwasha akaipeleka mdomoni na kuishikilia na midomo yake mipana kipindi chote Peter
alikuwa akimtazama tu, ‘Ungejua yaliyo moyoni mwangu ndugu yangu nafikiri usingeniuliza maswali mengi
yanayoumiza, haswa huyo mke wake namchukia zaidi’ alijiongelea ndani ya nafsi yake “Oya…Ni hivi kuna haja ya
kumueleza Johnson pia” aliongea tena Samuel mkono ukizungusha zungusha glasi yenye kinywaji cha scotch whisky
iliyobaki kiduchu, kikapita kimya.

Samuel akaanza kushusha
tabasamu la kivivu, tabasamu ambalo liliendelea kumpa wakati mgumu Peter kulielewa. “Sasa fanya kumpigia simu
tuonane nae sasa hivi usiku huu huu tena hapa hapa” aliongelea Samuel kama jemedari mkuu huku akiendelea
kuizungusha glasi yake kama awali. Peter kwa upande wake bila hoja yoyote alivuta simu yake ya kiganjani aina ya
samsung galaxy M30 iliyokuwa mezani muda wote na kupiga “…habari yako mchungaji…naomba uje Sinza Park hapa kuna dharura….ni muhimu sana” Peter akamtupia macho ya wizi Samuel ambaye alikuwa bize akivuta sigara yake na kutoa
moshi kwa njia ya pua “Hebu nipatie hiyo simu usiikate…”aliongea Samuel, Peter akampatia “Hallow Samuel naongea
nataka uje hapa mara moja bila kukosa…” kisha akakata simu.

Samuel akaangua kicheko “…. ehhh haitakiwi kumbeleza
hatumuombi ni amri tu”. Peter akatabasamu tabasamu la
maswali huku akimtazama kwa makini Samuel aliyekuwa anaonekana kuwa na furaha hasa naye akatabasamu nitafanya chochote ili kuhakikisha unapata furaha rafiki yangu hiyo ni ahadi, nakuona huna furaha kabisa kwa namna
Richard alivyo hivi sasa’ alijisemea nafsini na kuchukua glasiyake ya pombe na kunywa huku akikunja sura na kumeza
fundo.

Baada ya dakika chache, Mchungaji kwa mbali alionekana akiingia huku simu ikiwa masikioni akitazama huku na kule
kisha akatoa masikioni na kuelekea upande walio kuwepo kina Samuel “Habari zenu…mambo gani ya kuitana usiku
kama huu tena sehemu kama hii jamani ustaarabu gani huuhamjui hadhi yangu?!” Johnson aliongea mikono kiunoni huku
akiwatazama wenzake kwa zamu, “Baba kaa kwanza usitusimamie kama wakili aliyechanganyikiwa na kesi inayomshinda” Samuel aliongea kikakamavu huku mdomo ukitoa harufu ya bia. Mchungaji Johnson akauma meno yake
kwa hasira kisha akavuta kiti na kukaa sura yake ikiwa na maswali mengi yanayohitaji majibu, “Sikiliza ndugu yetu
najua unatujua sana sisi kuliko Richard si ndio, sisi ndio tulikukutanisha na Richard miaka ile” Samuel kwa sauti
iliyoingiwa na ulevi aliongea huku akisigina sigara katika chombo maalum cha sigara na kumtazama Johnson ambae
alikuwa anamshangaa tu, “Samuel unavuta sigara siku hizi” “Hatuja kuita kwa ajili ya kuja kuhubiri kama ufanyavyo kwa
kondoo zako, tulia na usikilize” Samuel aliongea huku macho yakimtoka kiasi cha kumuogopesha Johnson akabaki
kuwatazama tu kwa zamu, Samuel akaendelea “Unajiskiaje unapomuona Richard akitangazwa katika vyombo vya habari kila uchwao na yule mkewe anavyoendesha miradi mikubwa
ya kina mama na hata wanapofungua mawe mbalimbali ya hospitali, shule na maofisi kwa heshima waliyonayo?”.
Mchungaji Johnson alionekana kuelewa kitu alitazama meza kwa muda kisha akanyanyua uso, “Jamani ni mtu na maisha yake na jitihada zake lakini kwa nini msimuache” “Nini…” Samuel alifura akaigonga glasi mezani kwa hasira na kumsogelea karibu mchungaji Johnson ambae kwa muda huo wasiwasi ulianza kumuandama, “Upo upande wetu au upande wa Richard?” aliongea huku akiwa amemuinamia macho kayatumbua “Mimi…ni…nyinyi nyote ni jamaa zangu wa
karibu Samuel”, aliongea kwa kubabaika, Samuel alimuangalia Peter kisha akarudisha uso kwa Johnson akasogeza mdomo hadi kwenye sikio la Johnson na kumnong’oneza “Sikiliza ndugu mchungaji, Richard ameshapata mrithi tena wa kiume hatutavumilia tena vituko vyake tushirikiane tuzitoe roho zao
wote”. “Yesu wangu!! Unasemaje wewe…” aliongea Johnson akasimama kwa ghadhabu macho yamemtoka. Tukio hilo
lilimfanya Samuel kumkandamiza begani akae kwa lazima.

Tukio hilo liliwafanya hata watu wa mbali kushtuka lakini wakapuuza na kuendelea na habari zao. “Hapana hilo sitaweza kuvumilia mmeanza kutawaliwa na mapepo nyinyi watu roho mchafu yumo ndani yenu”. Aliongea mchungaji uso
akiutupia pembeni kwa hasiraSamuel
na Peter wakatazamana kwa muda kisha Samuel akajikoholesha“Johnson unaweza kwenda nyumbani ila kafikirie vizuri”.

Samuel aliongea huku akimkazia macho Peter kwa ishara fulani. Johnson akanyanyuka kwenye kiti haraka haraka
akionekana dhahiri ndio fulsa pekee aliyokuwa akiitamani itokee pahala hapo na kuanza kuongoza njia kuelekea nje.
“Tumfate haraka” Samuel aliongea na kunyanyuka Peter naye akanyanyuka. ‘Yaani Leo marafiki wamefikia hatua ya kutaka kuuwana!’ alijisemea katika nafsi yake mchungaji Johnson kisha akasonya “chaguo ninalo” alijisemea huku akiharakisha kutembea.

Mchungaji akasogea hadi katika gari yake mitsubishi Pajeroiliyokuwa imepaki mbali kidogo na lodge aliyotoka kando ya
barabara. Akafungua mlango na kuingia ghafla bini vuu mlango wa pili ukafunguliwa na Samuel akaingia kupitia
mlango wa kushoto mwa dereva bila kuchelewa na Peter nae alifata kwa kupitia mlango wa nyuma. “Ndugu sikia hatukuwa tayari lakini sasa hatuna jinsi” Johnson akiwa hana hili wala
lile akimtolea macho Samuel ambaye alianza kuvaa gloves za mikono. Bastora ndogo ikatolewa katika ubavu wa Samuel
“Mbona siwaelewi” mchungaji Johnson aliongea kwa wasiwasi na kutoa macho tu akimuangalia Samuel akiweka kiwambo
katika bastora. “Nimewaambia siwezi kufanya mauaji yoyote jamani” mchungaji aliongea akiendelea kutetemeka mara
mshtuko ukamvaa bastora yenye kiwambo tayari ikielekea pajini mwa uso wake ikishikiliwa na Samuel mara moja risasi
ikapenya katika paji la uso kabla hajapata hisia za maumivu hayo nyingine ikapita katika kifua karibu zaidi na pahala pa
chemba ya moyo. Sasa mchungaji Johnson akapata kuamini kuwa jamaa zake hao wamedhamiria kufanya mauaji kutokana na hali iliyomfika, alijitahidi kushindana na roho yake maana damu zilianza kumvuja na mwili kumuishia nguvu akigugumia maumivu huku mkono wa kuume akiwa kashika sehemu ya kifua upande wa jeraha mdomo akiuchezeshachezesha kutaka kusema neno akitweta akishindana na roho ambayo ilianza kuuaga mwili, masikini Johnson roho yake iliacha mwili akabaki kaachama mdomo wazi jicho limemtoka. Sasa Samuel na Peter baada ya kuhakikisha roho imeshamtoka Mchungaji Johnson Peter akatokea upande wa nyuma ya gari akaanza kumvua koti ambalo bwana Johnson alikuwa amelivaa na kumfunika kana kwamba ni mtu aliyejipumzikia zake.

Sinza Park, Kinondoni- Dar es Salaam
“…Kwa kweli muuaji au wauaji wanaonekana ni watu wenye
uzoefu na elimu kubwa sana ya uhalifu, na kwa muonekano wa tukio zima ni wazi kabisa kuwa marehemu alikuwa na kisa
na watu fulani enzi za uhai wake kwa sababu leo mchana baada ya kikosi kufika eneo la tukio alikutwa na simu yake,
gari lilikutwa na kiasi cha pesa cha shilingi Laki mbili na elfu kumi hivyo kama wangekuwa ni majambazi nafikiri
tusingekuta mali hizo zikiwa kwenye gari, kikosi cha polisi cha upelelezi kitachukua kazi yake na kuwafikisha katika
sheria wahusika tunaahidi hivyo, asante”, “Alikuwa afande Mwaipopo kutoka katika kituo cha polisi Sinza…lakini pia
mwana habari wetu alipata fulsa ya kukutana na mheshimiwaRichard na yake ya kusema” aliongea Mtangazaji wa tvc , “Hebu ongeza sauti tumsikie huyo marehemu mtarajiwa” Samuel aliongea akiwa kashikilia glasi ya mvinyo kajitanua macho yamelegea kwa ulevi mabega yakiminywaminywa na
wasichana wawili warembo waliovalia nusu uchi msichana mmoja wao akachukua rimoti na kuongeza “…ninachoweza kusema kwa sasa ni kuwa wahusika watapatikana tu tena
mapema naamini hilo, lakini watu wote walioguswa na kifo hicho nawapa pole, tuwe na subra katika kipindi hiki kigumu na zaidi ya yote tujumuike kwa ukaribu na familia ya marehemu ili tuwafariji katika kipindi hiki asante” Richard alimaliza. “Hebu zima hiyo TV” Samuel aliongea kwa hasira ikazimwa mara moja “Mmmh bro…” Peter aliguna, “Mbona jamaa ameongea kwa kujiamini sana hivi hivi yeye ni nani
hasa, mbona kama kuna kitu sikijui mzee?” Peter aliuliza, Samuel alimuangalia huku akihema kwa hofu pombe ikiwa
imemtoka akibwenza bwenza akameza mate “Ndugu yangu hebu acha kuwa na wasiwasi visa vyao tusiviingilie tayari
tuna bahati tuitumie hakuna haja ya kuwaza waza hapa” Samuel akanyanyua glasi yake ya mvinyo akameza fundo
huku akibwenza bwenza kwa hofu, akaongea “Jambo la msingi
inatupasa tuanze mambo haraka sana, tusubiri na tuone namna atakavyo tuwinda” alimaliza Samuel na kusimama
“…sitakusindikiza mzee” Peter kiuchovuchovu alinyanyuka
“Sawa lakini wasiwasi ndio akili mzee” Peter akatoka chumbani humo na kumuacha Samuel peke yake ‘Siwezi
amini ulichonifanyia mke wangu lakini ninalo chaguo la kufanya’ Samuel aliongea nafsini kisha akaingiza mkono
mfukoni mwa suruali na kutoa simu yake kubwa ya smartphone, akatulia kutazama picha za mwanamke na mwanaume zilizokuwa katika simu yake taratibu katika mazingira tofauti chozi likaanza kumtoka na kuendelea
kumtoka “Mke wangu kwanini unanifanya nifanye ambayo sikutaka kuyafanya kwenye maisha yangu” akatulia kisha
akahamia katika jumbe ya maneno iliyoandikwa chini ya picha alizotumiwa na kuanza kusoma taratibu “Wewe
mwanamke wewe mtalipa na mumeo haya, sio kwa kunitukana kiasi hiki” aliongea sura ikiwa imemvimba kwa
hasira.

Siku mbili baada ya mazishi.
Kimara, Kinondoni - Dar es Salaam.
“Shemeji nakuambia ukweli alipigiwa simu usiku ule baada ya kupigiwa simu ilionesha wazi ni taarifa mbaya
iliyochanganyika na vitisho shemu” mheshimiwa Richard kwa makini aliendelea kumsikiliza huku akiuma midomo yake. “Shem, kwani alikuwa na tabia ya kutoka usiku kabla ya hapo” kwa uchungu mke wa mchungaji aligeuza shingo kumtazama shemeji yake “Shemeji Rich haijawahi tokea hata siku moja” Richard macho yakiwa usoni mwa shemeji yake akaongea “…nimeelewa kitu, je vipi polisi uliwambia hivi hivi ulivyoniambia walipokuhoji?” kwa uso uliosawajika mama mchungaji akatingisha kichwa akimtazama Richard machoni.
“…vipi kuhusu simu yake iko wapi?” kwa masikitiko mama wa watu akatingisha kichwaa “…simu aliondoka nayo na hata
nilipo ipigaa iliita mwisho haikupatikana mpaka leo…” alijikuta akiangua kilio cha chini chini lakini ghafla akagutuka
na kunyanyua uso wake huku akijifuta uso wake “…shemeji nimekumbuka kitu, nakumbuka… alipokuwa anatoka
nilimsikia akilitaja jina la Samuel lakini sikulipatiliza”. Taarifa ilionekana ni ya kushtusha kidogo Richard akaduwaa akaongea “...okay hii nayo uliwaambia polisi” “…hapana shemeji” “Vizuri sana shem”. Mama mchungaji kwa mshangao
akamtazama Richard huku akiiweka vizuri kanga yake iliyokuwa imefunika sehemu ya kichwa. “…usinielewe vibaya usiwaambie mpaka nitakapo kuambia waambie sasa acha nichunguze ukweli lakini usiache kunipigia simu kila utakapokumbuka kitu” “Sawa shemeji” bwana Richard alimpa mkono na kuondoka eneo hilo. ‘Lazima niujue ukweli, lazima niifanye mimi mwenyewe hii kazi’ Richard alijisemea nafsini.‘Lakini Samuel anamuingizaje Johnson kwenye matatizo
yangu, kuna haja ya kuwasiliana na mkuu’ alijiongelea nafsini huku akitoa simu mfukoni “Habari…ndio mkuu nina uhakika
na Samuel pamoja na Peter wanahusika na hili nimeshafanya chunguzi za awali” aliongea kwa sauti ya chini akitazama
huku na kule jioni hiyo nje ya geti la nyumba ya Marehemu Johnson akiwa amevalia fulana ya kahawia, suruali ya jinsi nyeusi na raba nyeupe huku miwani myeusi ikiwa machoni.
“Nina uhakika na hilo nawaona wanachuki nami, Johnson ni mtu pekee wa karibu aliyekuwa…kiongozi nielewe niko radhi
kuifanya hii kazi kwanza Cd nimekuahidi nikiipata nitakupa nimekumbuka nilibadilishiwa begi siku ile” aliongea kwa ukali kidogo “Skia kiongozi kwanza tambua Cd yenyewe ni mali ya taifa na sio wewe usinikere…hata kama…kumbuka
nimekabidhiwa kwako toka kwa rais haimaanishi kila kitu niripoti kwako hiyo sio nidhamu ya kazi yangu kuna mambo
na mambo na tena sidhani kama unaujua undani wangu” aliongea akiwa na ghadhabu kubwa “Potelea pote” akakata
simu kisha akasimama kwa muda akitafakari ‘Huyu bwana vipi mbona simuelewi kuna kipi cha ziada kwenye ile Cd kuna tukio ambalo sikulitilia maanani kweli, lazima niwe makini nifanye mambo chapuchapu kabla sijageukiwa’ alijiongelea katika nafsi yake kisha huyo akakata kushoto huku akiwa na
tahadhari asijulikane.

Sinza Park, Kinondoni - Dar es Salam.
Hazikuwa kelele bali burudisho la mioyo ya wanywaji na walevi waliokusanyika katika viwanja hivyo huku watoto wakike wakiwa na mavazi ya nusu uchi wa kila rangi, kimo na shepu wakipita huku wengine wakienda kule wakijirahisishakwa wanaume. Licha ya kuwa walishikwa shikwa sehemu zao
za mwili hawakujali waliacha huku wakijichekesha tu. Bwana mmoja mwenye asili ya kihindi akiwa maeneo ya nje ya uzio aliendelea kuwatazama akajitingishia kichwa kwa masikitiko mara akapita jamaa akiwa chwii akikokotwa na warembo wawili ambao wazi hawakuonekana kuwa na mapenzi na
bwana huyo mana si kwa kumsachi na kutoa hela wakizitia kwenye pochi zao bila kujali.
Akaachana nao akarudisha macho kwenye meza za watu wengi kupitia matobo ya uzio huku mara chache akitazama
saa mkononi, akiwa ametulia nje gari moja aina ya Mitsubish Montero GLX (4×4) ikaingia na kupaki eneo la maegesho
akasogea ukutani na kuchungulia kupitia matobo yaliyowekwa kama fasheni katika ukuta huo. Bwana huyo mwenye asili ya kihindi alionekana kuikodolea sana namba za gari huku akionekana kujiwazia kitu kwa haraka cha ajabu alitoa simu yake na kuziandika kisha akarudisha macho
kulikodolea, haikuchukua muda Mwanaume mrefu akiwa na jaketi jeusi lenye kofia wazi akionekana ni mtu asiye taka kujulikana kwa namna alivyojiweka, akaikunja sura yake na kutoka mafichoni kuingia ndani.

Akiwa na hatua chache tu tangu kuingia aliachama mdomobaada ya kumuona akipeana mikono na Samuel na kuingia
naye ndani. Kwa makini bwana huyo mwenye asili ya kihindialiwaza kidogo na kutafuta sehemu na kukaa eneo la nje ya
baa hiyo ambapo kulikusanya watu waliokuwa wakiendelea kustahereka na mziki uliokuwa ukipigwa live wakati huo wa saa tano usiku. Mara simu yake ilinguruma akapapasa kuitoa ulikuwa ni ujumbe wa maneno “Nimekuona tayari…mambo yako poa sasa nimefanya kama ulivyonielekeza na picha nitakutumia, ila usiingie nitakuja tuonane” aliachia tabasamu na kuirudishia simu yake mfukoni. Dakika tano tu alionekana
binti mmoja aliyevalia sare akitembea kwa madaha moja kwa moja hadi katika meza aliyokuwemo bwana yule akaweka
glasi moja pamoja na chupa ya bia aina ya Tusker leaguealiinama kidogo “Habari bwana Raja” na kuweka kikaratasi
kilichokunjwa bila mfumo mzuri juu ya meza na kuiweka glasi ikifatiwa na chupa ya Tusker na kuifungua kisha akaondoka
mara moja.

Bwana Raja hakupoteza muda akakifungua kikaratasi na
kutoa memory card na kuipachika katika simu yake mara moja na kuendelea kutazama kitu fulani ndani yake. Kisha
alitoka alipo kuwa akitazama picha na kuandika ujumbe wa maneno kwenye namba ile aliyotuma ujumbe “…asante
tazama katika akaunti yako tayari pesa imeingia. Haraka akanyanyuka na kuondoka bila kuifungua ile bia. Kwa kasi ya ajabu akaliondoa gari lake lililokuwa limeegeshwa mbali na Baa hiyo akiacha misururu ya magari mengine kwa spidi
kubwa mkuku mkuku hadi sehemu ambayo haikuwa na misongamano ya magari wala shamla shamla za watuakaegesha gari pembeni ya mti mkubwa. Haraka akakichukua kikopo cha mafuta pembeni ya siti akajipaka usoni na
mikononi baada ya muda akaanza kuvuta kiganja kimoja na ngozi iliinza kutoka na kuwa mfano wa gloves akafanya kwa
mkono mwingine na kubaki na mikono ya rangi nyeusi kishaakajipaka usoni na sehemu za shingo akijishika chini ya
shingo na mara alitoa ngozi ya plastic na kuiweka katika siti ya pembeni looh! Kumbe alikuwa ni mheshimiwa Richard
Edward katika muonekano wake halisi na sio tena yule Raja muhindi akatabasamu “Komando Swai” alijisemea mwenyewe
na kutingisha kichwa na kufungua sehemu ya picha katika simu yake baada ya kuzipangilia vizuri picha zilizomuonesha
Komando Swai akiwa na wauza unga zingine akikagua silahakali akiwa na waarabu kadhaa na wasomali akabonyeza kitufecha send, “Shenzi weeee” akatoka eneo la picha na kupiga simu “…Hallow Swai pokea zawadi yako hiyo niliwahi
kukuonya hukusikia sasa ushahidi wa biashara yako ya madawa ya kulevya itakuwa hadharani juu ya mashtaka yako
ya Uasi na ugaidi dhidi ya Taifa lako, halafu bila huruma ukanigusa pabaya kutoa uhai wa Johnson, waziwazi nauona
ushirika wako na kina Samuel kwa kweli sitawaacha salama…” aliongea mfululizo kwa hasira huku simu bado
ikiwa sikioni “…unasemaje weweeee…”
Ghafla akashtuka huku macho yakamtoka akitazama katika kioo cha pembeni kwa shauku “sio wewe kivipi wakati
nimekuona mwenyewe kwa macho yangu…usinidanganye Swai najua mchezo unao taka kunichezea” sasa akihema kwa
fujo na hofu nyingi “…CD iko wapi?...niwashe GPS tracker ya
kazi gani siwezi liamini hilo…flash sitakupa kirahisi hivyo mzee…Familia yanguuuuu?...usinifanye mjinga nikikupata nitakunyonyaubongo Swai”wazi alionekana kuchanganyikiwa simu ikakatwa “Hallow haloww Swaiiii “ akawasha gari yake na kuondoka mkuku mkuku “Mungu wangu iokoe familia yangu” alijiongelea huku akivuta mafuta
na kubadili gia.

Nini kitatokeaaaa

Itaendeleaaaa....

Mijadara inakaribishwa

IMG_20210320_131445_046.jpg
 
The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)
MTUNZI : Akida Siri Rambao
Contact: 0658328596
Email: akidasiri@gmail.com

SEHEMU 3 (A na B): MSIBA MZITO

Dondoo:
“Familia masikini ya mvuvi maarufu mzee Habibu kutoka Bagamoyo inamuokota
mtoto kando ya fukwe za bahari ya Hindi, wakati huo huo kunapatikana taarifa za
kupotea kwa mtoto wa kitajri huku donge nono likitangazwa na raisi wa nchi kwa
mwenye ushahidi wowote au dodoso za mauaji ya Familia ya Mh. Richard Edward
Kobero na kupotea kwa mtoto. Je! Wataamua nini? Na ni na yapi yaliyomsibu mtoto huyo na familia yake?”

Tuendeleeee...
Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Mzee Habibu alikuwa sebureni akijifunga vizuri msuli wake,
“Mume wangu hebu leo swalia nyumbani nataka tuliongeleeswala la huyo mgeni maana unanikwepa tu hapa, isije ikawa
umeniletea jini humu ndani”.

Mzee Habibu akamuangalia
mkewe ambae alikuwa anapakua ugali na kuweka katika sinia ya bati akajisogeza katika jamvi kinyonge na kukaa
“Alhamdulillah”, alichukua rimoti na kubadili chaneli na kuweka tvc bila kutia neno lolote. Kipindi Mzee Habibu akiwa
amekaa katika jamvi akitazama runinga alikodoa macho katika habari iliyokuwa inaendelea.
“Ni taarifa iliyowashtua
watu wengi sana kwa kweli, kifo hichi cha mheshimiwaRichard
Edwardkila aliyesikia alishtuka wahusika
wamemuua kikatili sana yeye na familia yake, lakini kama jeshi la polisi hatutalikalia kimya jambo hili” Kamanda wapolisi wa mkoa wa Dar es salaam akiwa ndani ya vazi lake lakiaskari aliongea huku maiki nyingi za vituo tofauti vya habarizikimzunguka nje ya hospitali ya Muhimbili,
“…mpaka sasa ni miili mingapi mliyoipata katika eneo la tukio?” mwanahabari mmoja wa kike wa kituo cha tvc alimtwanga swali kamanda.
“Iliyopatikana na kutambulika ni mheshimiwa Richard, mkewe Bi Winifrida, Fatumaa ambaye alikuwa ni kijakazi
pamoja na mkono uliokosa mwili, mtoto Pius na Jumahawajatambulika walipo na haijulikani wapo hai au wamekufa
na hakuna taarifa yoyote iliyopatikana mpaka sasa hivi kuwahusu…hivyo taarifa kamili itatolewa wakati ukifika
samahani”.

Baada ya kuyaongea hayo akapanda gari yake akiwa chini ya ulinzi mkali na kutimka bila kuongea zaidi. Mzee Habibu na mkewe wakiwa na mshangao zikapita
sekunde kadhaa pakiwa kimya mara Mzee Habibu akaweka rimonti chini akanyanyuka mkuku mkuku akielekea katika moja ya vyumba mkewe akiwa nyuma yake. Mzee Habibu akasogea hadi katika kitanda na kumtazama mtoto aliyekuwa kitandani akiwa na usingizi mzito kwa makini huku mkewe
akiwa nyuma yake akimtazama tu. “Alilia mchana huyo mwisho wa siku akaamua kulala na hataki mtu amguse kabisa
anaita baba tu yeye”.

Mzee Habibu machozi yakaanza
kumlengalenga “…mke wangu huyu mtoto ukimuangalia anafanana na nani?” Bi Aida alitoka katika kiambaza cha mlango na kusogea karibu kumtazama mtoto, alimuangalia kwa makini “Mmh mume wangu sura inakuja inatoka inaangia
na kutoka lakini sijui ni nani?”. Mzee Habibu alimuangalia mkewe kwa huzuni, “Nisubiri mara moja” mzee Habibu
akatoka ndani ya chumba hicho na kumuacha mkewe akiwa kabung’aa akiumiza kichwa kuwaza huyo aliye fanana na huyo mtoto, punde tu aliingia Mzee Habibu na picha mkononi akampatia mkewe
“Haya tazama halafu uniambie” Bi Aida
aliitazama picha na kumtazama mtoto hakutosheka akasogea zaidi, “Haiwezekani mume wangu…” Bi Aida alitoa macho akamtazama mumewe mara mbilimbili “Subhanallah…mume
wangu anafanana sana na marehemu mheshimiwa Rich… haa mbona….haa huyu ni mtoto wa marehemu Richard huyu ni
Pius aliyepotea?!!” Mzee Habibu alimuwahi mkewe akamziba mdomo.

Picha ilimuonesha Mzee Habibu na Richard wakiwa mbele ya boti pembezoni mwa fukwe huku wamepeana mikono kwa furaha baadhi ya watu pembeni wakishangilia.
“Jamani kijana huyu juzijuzi tu hapa ametutembelea kijijini kwetu…na akagawa boti leo hii ni marehemu!!!”. Mzee Habibu
alijikuta nguvu zikimuishia taratibu akakaa sakafuni. Mkewe akiwa kajiziba mdomo na kanga yake aliyojisitiri kichwani
machozi yalianza kummiminika hovyo kwa uchungu.
“Ndiomaana nikawa nashangaa mbona nasitasita kusema juu ya mtoto huyu kwa wenzangu, hata kuthubutu kusema kuwa
nimeokota mtoto, kumbe bwana ni mtoto wa…” alishindwa kumalizia kwa uchungu akajiziba mdomo. “Mke wangu
nakuomba kwa mapenzi yako na huruma yako huyu mtoto tumlee sisi wenyewe na tuiweke siri hii nzito na tutamuita
Salimu”.
Mkewe alibaki kutingisha kichwa kuonesha kukubali “Yarabi wewe ndiye unaejua kesho yetu, tunakuomba umjalie
mtoto huyu amani ya maisha katika makuzi yake, umjalie awe
na tabia njema na mtu mwema, umfanye awe na amani na familia hii na atuchukulie kama wazazi wake, tunajua una
makusudi ya kuyafanya haya yote mpaka kumleta mtoto huyu katika mikono yetu na sisi tunaahidi kumlea kama mwanetu,
tunakuomba utuepushe na shari ya mtoto huyu na ile uliyomuumbia, na utujalie kheri za mtoto huyu na kheri ulizomuumbia, umuepushe na hasadi za walimwengu, majini na mashetani awe na amani katika maisha yake na umjalie akili na rizki”. “Amiiiin”.

Baada ya mzee Habibu kuomba dua
hiyo wote yeye na mkewe waliitika kwa pamoja na kushusha mikono yao taratibu. “Muamshe tujaribu kumbembeleza ale
walau kidogo”. Mzee Habibu alimwambia mkewe huku akijinyanyua pahala alipo kaa. Bahati ni bahati tu hasa mwenyezi mungu akikuchagua, Pius aliamka japo alionekana kusumbuasumbua akilia akiita mama na baba, maneno matamu ya kubembeleza aliyokuwa akiambiwa na wazee hao yalidanganya mawazo yake na kujikuta akila kishidashida japo akili bado ilikuwa inapingana na mazingira, kwa hofu ya wazee hao juu ya kulala kwa tabu waliamua kumchanganyia dawa ya usingizi kwenye maji na kumnywesha hii ni baada ya mzee Habibu kutoka kwenda madukani kutafuta.

Licha ya hayo yote kufanyika swali lililokuwa likimuumiza kichwa ni
kuhusu Pius kuonekana katika fukwe za bahari asubuhi ya siku hiyo, Dar es salaam na Bagamoyo sio safari ya miguu hata
kama ingekuwa lakini si kwa mtoto yule kwa maana lazima kuna mkono wa mtu au watu hapo ambao wanahusika
kumfikisha hapo je ni akina nani? Na kama siku wakija kusema kuwa walimleta wao hapo itakuwaje? Alikuwa kila wakati akiwaza akaiona taa nyekundu ya hatari kichwani lakini haikumfanya
kuthubutu kumshirikisha mkewe
kutokana na roho nyingi za wanawake kuwa na woga hivyo alimezea na kusubiri litakalo kuja mbeleni. Mzee Habibu
akakikuna kichwa chake akiwa katika dimbwi la mawazo macho yakimtazama Pius mkewe tayari akiwa amechukuliwa
na usingizi siku nyingi upande wa pili Pius naye akiwa hajiwezi kwa uchovu, ‘Eeh mwenyezi Mungu sina la kusema zaidi ya kuwa nilikuwa na Karimu kule ufukweni laa sivyo huyu mtoto ataangamia kabisa na atakuja nilaumu kuwa nilichangia kuharibika kwa maisha yake eeh Mungu nisamehe kwa uongo huu’. Alijisemea nafsini mzee huyo.

MASAA 24 YALIYOPITA.
Msasani, Kinondoni -Dar es Salaam
Mlango wa gari ulifunguliwa Richard akatoka kwenye gari na kusimama kwa muda akitazama huku na kule kwa macho ya mashaka “No nooo Richard kuwa na nguvu” alijiongelea kwa
sauti ya chini huku akipiga hatua fupi fupi za kuvizia mkononi akiwa ameshikilia funguo za gari. “Daadiii” Mtoto Pius aliita
akiwa sebuleni tabasamu likiwa limesheheni akimtazama
baba yake “Yess my son” alijibu Richard na kuubana Mlango kisha akalegeza tai shingoni akavua na kuliweka koti lake
kwenye sofa macho yakiwa kwa Jumaa “Pius sasa unaweza kwenda kulala utaongea na Dadi kesho sawa” “Okay mom” mtoto Pius alijibu na kushuka toka kwenye kiti, “Usisahau kusali my son” alidakia Richard huku akimsindikiza kwa
macho mwanawe Pius aliyekuwa ameshikwa mkono na Fatuma wakielekea upande wa vyumba “Okay Dad Good
Night” “Good Night” Richard akatabasamu na kuyapelekamacho kwenye runinga akimtazama mkewe kimachale
machale kisha akachukua simu yake na kupiga namba fulaninakusikiliza ‘Haipatikani’ alijiwazia akapiga na nyingine na nyingine ‘Zote hazipatikani ooh my God Swai ananitega aumbona sielewi mbona mke wangu yupo kawaida’ alijiwazia
tena. “Naomba niwaache nikaweke mazingira sawa nje”aliongea Jumaa huku akiutoa mto aliokuwa ameuegemea
“Unaweza kwenda tu”. Richard alimtazama Jumaa kwa machoya mashaka kisha akachukua simu yake na kuwasha data
kisha huyo hadi katika sreensaver akafungua applicationiliyoandikwa kwa jina la Mzalendo akaweka password na
kuifungua na kuanza kuandika ‘Ukweli ulionyuma ya mgongo ni sawa na kiza mbele ya macho hata kwa kupapasa huwezi ujua mpaka iwashwe taa, nikipona basi nitauwasha mshumaa
nikishindwa nitaushika utambi’ “Kuna nini mbona unanitazama namna hiyo? kila kitu kiko sawa mke wangu” aliongea Richard na kuutuma ujumbe aliouandika. Winifrida
alitoka na kumsogelea mumewe kwenye sofa akiwa na glasiya juisi mkononi na kumpatia “Mke wangu kuna mzigo
wowote uliofika hapa jioni hii” aliongea “Yaaah sijatazama ni bahasha lakini ina kitu ndani cha mfano wa Cd hivi”
mheshimiwa akashtuka macho yakamtoka “Vipi kulikoni”Winifrida alihoji “Kuna kitu kingine zaidi ya hicho” aliuliza
Richard na kumuacha mkewe akimshangaa
“Mke wangu kuna kitu hakipo sawa tunatakiwa tuondoke na familia sasa hivinenda kawachukue” Richard alisimama kwa msisitizo

“Unasemaje? Wewe sikuelewi unajua nakuona kama umeanza yale mambo yako” Wini kwa Shauku na mshangao aliongea “...walinzi yani hakuna mlinzi hata mmoja anayepatikana”
Richard alijiongelea “…mume wangu una nini leo walinzi gani hao unaowaongelea” aliongea Winifrida “Mke wangu
tuondoke nitakueleza kila kitu kwa sasa tuondoke tafadhari tunachelewa” aliongea Richard akishika mkono wa mkewe
kusisitiza mara Winifrida alishtuka na kugeuka nyuma akitazama dirishani
“Nini?” mheshimiwaRichard akatahamaki kumuona mkewe akiwa ametoa macho
akionekana kutulia kusikiliza kitu “We hujasikia kishindo kizito?” Richard akatoa bastora yake ndogo nyuma ya kiuno
“Mume wangu kuna nini” Richard kwa umakini akamsogeza mkewe kando huku akinyata kwa tahadhari kusogelea dirisha
kuchungulia. Mara mlango ulisukumwa kwa nguvu kufumba na kufumbua njemba zikaingia ndani zikiwa zimejifunika sura
kwa vinyago wakiwa wamevalia mavazi meusi tii na bunduki mikononi macho ya Richard na mkewe kwa mshangao yalitua
kwa njemba hizo “Kimya kimyaa mkithubutu kupiga kelele au
kujisogeza risasi za kichwa zitawakabiri” mmoja wao aliyekuwa mfupi kuliko wote aliongea na kuwasogelea huku
bastora akiwa kawaelekezea, watu hao walikuwa wamebeba siraha nzito dhahiri walionekana kujipanga.

“Tupa silaha yako chini kabla hatujalianzisha sebene” aliongea kiongozi huyo Richard akauma meno na kutupa chini bunduki yake “Vizuri
sana mheshimiwa mzembe Fanya haraka utupe pesa na wengine jigaweni vyumbani mlete watu wote hapa” alitoa
agizo wawili wakatawanyika akamfata Richard “Jamani tunaweza kuongea ni nani aliye watuma nitawapa kila
mnachotaka lakini msiumize familia yangu nani kawaagiza” “Hahahaha hebu acha kutufanya wajinga twende ukatupe
pesa” aliongea kiongozi huyo huku kamuelekezea silaha yake
mmoja akitishia kumuua Winifrida kwa kumkaba na kumuwekea bastora kichwani na kupelekea Winifrida
kuangua kilio cha chini chini “Mume wangu mbona sielewi hawa ni akina nani mbona sijui chochote” Winifrida alilalamika kwa machungu, Richard akameza fundo la mate akiwa na macho ya uoga ‘Nimesalitiwa Mungu wangu nisaidie’ alijiongelea nafsini huku mikono ikiwa juu kama mateka kisha akaongea “…jamani mbona kama mmekosea nyumba ya
kuivamia mnauhakika na mnachokifanya lakini” ‘Ni nani amethubutu kunifanyia uhuni huu au Swai… mshenzi? Na
walinzi wangu wanahusikaje na Swai ooh nimezungukwa’ aliwaza na kubaki njia panda kichwa kikimfikirisha “Hatuna
muda wa kusubiri” aliongea mmoja wao na kulikusanya shati la Richard shingoni kiasi cha kumkaba koo “Ongoza njia na
ukileta ujanja tu itabaki historia kwa ulimwengu” Richardakiwa anashughulika kuwaza akaanza kupanda ngazi
kuelekea ghorofani.

Akafungua mlango na kuingia huku mtutu
wa bunduki ukiwa nyuma ya shingo yake alifungua droo ya kitanda na kutoa bahasha iliyojaa, “Hizi hapa ndugu yangu
naomba utuache sasa muende” ‘Hakika Swai umeniweza leo, ole wako nitoke salama sitakuacha mzima’ alijiwazia akiwa kapiga goti “Ziko ngapi” bwana yule mwenye sauti nzito alinguruma “Hizo ni milioni ishirini kamili” “Acha ujinga
ongeza nyingine wewe” Jamaa akaiseti vizuri bastora kwa ajili ya kufyatua kiasi cha kumfanya mheshimiwa Richard azidiwe na wasiwasi ‘Mungu wangu nifanye nini nipe akili’ alijiongelea
nafsini na mara akasema, “Nyingine ziko huku ndugu…”

Richard akainama chini ya kitanda “Wee angalia usilete ujanja” “Hapana pesa zingine niliziweka huku” Richard
alianza kupapasa chini na kukutana na sime, alishukuru kimoyomoyo ‘Asante Mungu’ alijisemea kimoyomoyo, alijitoa
taratibu huku mkono mmoja akiwa ameshikilia vizuri sime huku akipiga mahesabu ya kumkabili adui yake alijihesabia mara tatu akanyanyuka kwa kasi na kulengesha sime katika
mkono uliokuwa umeshikilia vizuri bunduki na kuhakikisha kipande cha mkono na silaha ukelelee wa maumivu ulisikika
bwana yule akiwa haamini damu nyingi zikiwa zinamvujafumba na kufumbua tayari alishawekwa chini ya ulinzi
lilikuwa ni shambulizi la sekunde tu kwa maumivu.

Familia ilikuwa chini kwa ulinzi mkali hawakuamini macho yao baada
ya kuona kiongozi wao akiwa chini ya ulinzi huku akilia kama mtoto, “Wekeni silaha zenu chini haraka” njemba kwa mshangao wakiwa wanatazamana hawakuwaamini macho yao “Jamani msisikilize fanyeni kazi yenu iliyowaleta” Njemba
iliongea kwa ukakamavu huku ikiwa imeshika sehemu ya mkono iliyokatika damu zikimvuja “Hamtakii” “Mheshimiwa
Richard alipaza sauti” mmoja akatupa na wengine wakafata, Richard aliendelea kumkabili huku akiisogelea familia yake na kuwaamrisha njemba zikae pahala pa pamoja, huku akisogea nae kwa kuupa mgongo mlango wa nje.

Juma akiwa nje ya nyumba alionekana kasimama huku mkononi akiwa kashikilia bastora ndogo akichungulia katika
dirisha akiwa kaikunja sura huyo akatoka na kuufata mlango mkubwa. Ghafla bin vuu zilisikika sauti za maumivu
zilizomfanya kila mtu kushtuka na kubaki na butwa zilikuwa ni risasi zikiingia mfululizo mgongoni mwa Richard kimya
kimya na kuulegeza mwili kwa mshtuko mkubwa “Haaa weweee” Winifrida aliongea kwa machungu na mshangao
ukamvaa asiamini macho yake. Mlangoni Alionekana Jumaamkononi akiwa kashikilia bunduki ndogo aina ya Walther PPSM2 9MM toka ujerumani na kusimama kishujaa akiwatazama
njemba zilizobakia. Richard aliyapokea maumivu makali yaliyomlevya akabaki akiyumba yumba Kwa kuishiwa damu
zikianza kumtoka mdomoni akaanguka kama mzigo wa viazi na kubaki kama mnyama aliyechinjwa na kuachwa akitweta tu.

Pius, Winifrida na Fatuma wote walishuhudia tukio hilo wakabaki kutoa macho na ukelele ukaanza kila mmoja
akiomboleza kivyake hakuna aliye amini alichokiona toka kwa Jumaa. “Mnatakiwa mkiagizwa kazi mnapaswa kufanya kwa
uhakika mnakuwa kama mambwa koko” aliongea Jumaa na kuondoka eneo hilo akipandisha ghorofani huku Njemba zote
zikimshangaa kwa kuonesha kutokuelewa kinachoendelea “Jumaa umefanya nini lakini umemuua mume wangu”
aliongea kwa uchungu Winifrida huku akitambaa kama mtoto akisogelea mwili wa mumewe. “Malizeni kazi na muhakikishe hakuna anaye weza kutoka mzima” Jumaa aliongea akiwa
anatokea ghorofani mkononi ameshikilia bahasha ya kaki akaiweka bastora nyuma ya kiuno na kuondoka zake. Mkuu
wa kikosi kwa hasira aliokota bastora moja ambayo nayo ilifungwa kuzuia sauti akamuelekezea Winifrida kwa mkono
wake mzima uliosalia na kufyatua risasi zilizomkabiri moja kwa moja Winifrida kifuani mwake ni sauti za maumivu tu
zilizosikika wakati huo huku akitweta na kuanza kusota akiita kwa tabu jina la mumewe huku akijivuta kusogelea mwili wa mumewe uliolala sakafuni ukivuja damu tu.

Pius akiwa na utoto wake lakini haikumtosha kuamini kuwa ni jambo la
mchezo lile analolishuhudia matukio hayo yote yalimfanyaawe na uoga mkubwa uliomfanya alie kimya kimya
akitetemeka huku akiwa amekumbatiwa na Fatuma ambaye nae alikuwa anagugumia kwa uchungu na hofu akiwatazama mabosi zake wakiwa sakafuni damu zikiwavuja. Njemba
ikamsogelea Fatuma na kumnyakua Pius kama kifaranga akinyakuliwa na mwewe akamrusha kwenyesofa akamuelekezea bastora Fatuma ambaye muda huo alikuwa anajivuta kwa nyuma akitamani kuinusuru nafsi yake lakini
haikusaidia chochote maana alikutana na ukuta mgongoni ikawa ndio kikomo cha utetezi wake hakupata fulsa hata ya
kumtazama Pius na kumuaga alishtukia vitu vikipenya kifuani kwa mfululilizo mpaka roho ikaaga mwili, kwa kweli
walikuwa si watu wa mchezo mchezo na kama ni kusomea roho mbaya basi walikuwa wamefuzu.

Macho yakamgeukia mtoto Pius na bastora ikimuelekea “Hapana hatupaswi
kumfanyia hivi mtoto mdogo kama huyu sisi pia tuna watoto kumbuka” Mizozo ikaanza na mabishano mwisho mmoja
akasema“Hapana mkuu haina haja ya kumuua…je kuna anayejua yule jamaa ni nani au alitumwa kuja kutusimamia
kwa siri na hakuwa na haja ya pesa kingine aliondoka na bahasha tu inaonekana inathamani kuliko hata hizi pesa je!
vipi kama na sisi tupo mtegoni?” bwana huyo baada ya kuongea akachepuka na kutoka nje kuwahi lakini alikuwa na
bahati alimuona Jumaa akiwa nje akipanda gari ya kifaharinakuondoka, haraka akarudi ndani “Jamani yule ameondoka na gari sasa hivi inaonekana imemfata tena itakuwa ni gari ya
mtu mkubwa fulani hivi…tunapoteza muda mi naona tumchukue huyu mtoto hatujui atakuwa nani baadae tusiyakatili maisha yake” aliongea bwana huyo na wenzake
wakatikisa vichwa. Taratibu za kumdhibiti Pius kwa kumzimisha na kumfunga funga na kumtia katika foronya ya shuka zikafanyika chapu chapu wote wakatoka na mmoja pekee akalitoa dumu lililo na maandishi makubwa ya Petrol na kuingia nalo ndani akimwagia kuzunguka nyumba kishabaada ya zoezi hilo njiti ya kiberiti ilitupwa ukutani na moto ukashika nakusambaa kwa kasi ya ajabu wanaume hao wakaingia kwenye gari na kuondoka kwa kasi wakiiacha nyumba ikiteketea. Hapakuwa na siri ya tukio hilo moshi
mzito uliosambaa eneo hilo nakuingia katika nyumba za jirani ndio uliamshaamsha kelele za moto huku baadhi wakijitahidi kadri walivyoweza kumwaga maji kupitia mipira ya mabomba yao lakini zoezi halikufua dafu moto ulikuwa mkubwa na
kusababisha milipuko kadhaa iliyoshtusha sana huenda ilikuwa ni mitungi ya gesi iliyohifadhiwa.

Magari ya zima moto takribani mawili yakawasili na kuendelea na zoezi la
kuzima moto. Waandishi wa habari hawakupitwa na tukio nao wakafika na kuchukua habari na picha muhimu huku polisi wakiwepo nao kuhakikisha usalama wa mali na watu. Midomo ya watu wengi ilikuwa wazi sana hapakuwepo na
sababu hasa iliyojulikana juu ya chanzo cha moto huo pia haikujulikana kama kuna watu wangapi humo ndani na
wangapi watakuwa hai na wangapi watapitiwa na kifo usiku huo, polisi walibanwa na waandishi wa habari kutoa maelezo kidogo lakini hawakuwa tayari kujibu chochote na kuwafanya waandishi na baadhi ya raia wa kawaida kubaki wakisubiri zoezi la uokoaji likamilike.

Ufukweni mwa Bahari ya hindi, Bagamoyo - Mkoa wa Pwani.
Usiku ulikomaa na kuwa mnene kweli kweli hapakuwa na hata nyota ya kubahatisha giza totoro too na kwa namna mikoko ilivyo shonana utisho ulizidi haswa, vishindo vya miguu kwa mbali vilianza kusikikika na sasa kusikika vizuri.
Wanaume wawili ambao hawakuonekana vizuri sura zao kutokana na kiza walionekana kubeba mzigo wakiinama na
kunyanyuka kukwepa matawi ya mikoko “Hapa panatosha bwana” mmoja aliongea na kusimama kabisa wakaliachia zigo
lao na mmoja akaanza kulifungua “Haina haja kwani ndugu yako huyo unamjali saana” “Hata kama Mogisha huyu ni
mtoto kama watoto wengine” “Nakusubiri hapo mbele nisije badili mawazo nikakinyongelea mbali mimi” Huyo akapiga hatua kutoka eneo hilo.

Bwana yule haraka akaanza kuzifungua kamba za mikono na miguu haraka akanyanyukaakahisi kitu cha mfanano wa kisu akakishika “Kisu hiki ni kisu
cha Mogisha imekuwaje?” alijisemea kwa sauti ya chini kisha
haraka akaharakisha kumfata mwenzake.

Baada ya masaa kadhaa.
Mtoto Pius akaanza kukohoa mfululizo, huku akitetemeka na kupelelekea meno kugongana akiwa na kifulana na kibukta tu, akaanza kufumbua macho kuyatazama mazingira ambayo bado alikuwa hajayaelewa alikuwa mgeni nayo. Kando ya bahari katika mikoko iliyo achanaachana Mtoto Pius akasimama na kutazama kulia na kushoto huku akiwa na uso wa kutaka kulia na hofu ikimuandama mtoto huyo wa miaka saba tu akiwa kakusanya mikono yake kwa baridi iliyokuwa inamshambulia, aliangaza angaza huku akijaribu kufata njia
ambayo hakuelewa inampeleka wapi akapita na kukatiza vichaka vya mikoko kama bahati alitokeza sehemu ambayo
ilikuwa ni ya wazi na kwa bahati nyingine aliona watu kwa mbali moyo wake ukamsihi awakimbilie basi Mungu nae
akampa nguvu za mwili akaanza mbio huku akiita kwa sauti yake ya kitoto kutaka msaada. Kwa mbali walionekana watu
wawili mmoja akihangaika kuifunga boti ufukweni na mwingine akiburuta mzigo mara akasimama na kugeuza
shingo huku na kule akitazama kitu “Mbona ni sauti ya mtoto
au jini” alijisemea mara sauti ilikuja tena na kupotea. Pindi alipogeuka na kutazama upande wa kulia alikiona kitu kwa
mbali kikianguka kitu kilichomshangaza “Zuberi hivi kile kitu kilichoanguka kule umekiona” aligeuka kumtazama Zuberi
ambae sasa alikuwa amekwishamaliza kufunga boti sasa alikuwa anakusanya samaki wadogo na kuwaweka katika
ndoo ndani ya boti. “Hapana Mzee Habibu ila kuna kasauti sijakaelewa kama ya kike hivi, lakini nimepuuza siunajua
maajabu ya bahari” aliongea bwana Zuberi na kuendelea na shughuli yake, Mzee Habibu nafsi ilimsukuma kwendakushuhudia kile alichokiona akaacha shughuli yake na kutoka mbio kuelekea upande ule alioanguka kijana Pius. Mzee
Habibu alistaajabu ya Firauni maana yale aliyoyaona ni ya musa, alimuona kijana mdogo sana wa kiume nguo ikiwa
imetapakaa damu kamelala mchangani hakajiwezi alitazama kulia na kushoto asijue la kufanya mwisho alipandwa na
ujasiri na kumsogelea alimtazama mapigo ya moyo na kuona yanaenda sawa, aliamua kumvua shati akamfuta damu
zilizokuwa zimeganda katia sehemu za mwili wake na akavua shati lake akamfunga vizuri na kumbeba mgongoni akaanza mbio, Zuberi kwa mbali alimuona Mzee Habibu akitimua mbio na kumfanya ashangae “Mzee Vipiiiiii?” alipiga ukelelee,
“Tazama samaki najaaaaaa” Mzee Habibu alijibu huku akiendelea mbio bila kusimama njiani, Zuberi alisikitika kisha
akacheka “Yani Mzee huyu na mwanawe, leo tena Kalimu amemfata baba yake baharini huyu mzee huyu, kweli mtoto
wa nyoka ni nyoka” aliendelea na kazi yake taratibu.

Mzee Habibu akakatiza mitaa watu wakimuangalia na kumcheka wengine wakamuita kwa jina lake na wengine wakimrushia matusi, “Yani huyu mzee hasikii leo tena kaenda baharini na
mtoto wake” watu walinong’onezana, mzee Habibu wala hakujali yeye akaendeleaa na safari mpaka nyumbani kwake
kikomo kikawa ni katika kitanda katika chumba kidogo uwani mwa nyumba yake aliangazaangaza katika vyumba vingine
huku akiita lakini hapakuwa na mtu yeyote zaidi ya wao tu.

Mzee Habibu akawaza na kuwazua cha kufanya akaamua aondoke baada ya kuhakikisha usalama wa Pius nyumbani
hapo. Njia ilikuwa ni ile aliyopita mwanzoni wazee wenzie walionekana kumnyooshea vidole na kumtazama kwa macho ya hasira, Mzee Habibu akaishia kuwatazama na kukubali ayasikiayo “Mwaongea kwa kuwa hamjui yaliyonikuta” aliishia kujisemea mwenyewe baada ya kutoka katika kundi la watu lililokusanyika.

Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Watu wengi walibaki kujiinamia wakisonona mikono ikiwa mashavuni wakifikiri wengi wao machozi yakiwa tayari mashavuni yakitirika kwa uchungu. Baadhi yao hawakuwa wakiamini kinachoendelea hawakuamini mkusanyiko wa maelfu ya watu wazee, vijana na watoto waliojikusanya uwanjani hapo wakizidi kuingia na kuingia shauku zikiwa
mioyoni mwao kutaka kuaga mwili wa marehemu Richard pamoja na familia yake. Uwanja ulikuwa kimyaa wenye iman
zao walifumba macho wakiomba waliosalia wakabaki kushangaa shangaa mara mwili wa marehemu Richard,
mkewe na binti Fatumaa katika magari tofauti ikaanza kuingia na watu wote wakasimama kwa ajili ya kutoa heshima hapo sasa vilio vikaanza toka kona zote za uwanja sasa waliokuwa wanaona wapo ndotoni wakatoa macho kumbe haikuwa
ndoto ni kweli wapendwa wao hao wamewatoka kimwili. Kwa heshima kuu gari ya polisi ikiwa mbele kuongoza na nyuma ikiwa nyingine ikisindikiza mwendo wa taratibu twende huku picha ya kila marehemu ikiwa juu ya gari. Bendi maalumu ya kiaskari iliendelea kupiga wimbo wa heshima wakiomboleza,
magari yalizunguka mzunguko mmoja kisha yakasimama pahala maalum. Watu kimya, askofu Bwana Emanuel Elibariki
akiwa na watawa wake walionekana wakisogelea katika membari ya kipaza sauti na kuanza sala mara moja. Baada ya lisaa limoja tayari ibada ilikuwa imetimia na sasa Peterakajisogeza mkononi akiwa na kitambaa cha machozi fulana
yenye picha ya marehemu Richard ikiwa mwilini na yeye kwa nafasi yake akasoma historia ya marehemu Richard na familia
yake.

Historia iliyoamsha hisia za maumivu kwa kila mmoja waliokuwa wanajua wakabaki kujua na wasiojua wakajua
kilichokuwa. “…mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemuwote mahali pema peponi … amiiin” Bwana Peter alimaliza na
kujifuta machozi kisha akatoka katika membari. Baada ya kutoka alienda Waziri mkuu bwana Abubakari Ali Mwinshee
na kusoma risala maalumu akiwakilisha serikali kuu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Magari ya kuzika yalikuwa tayari nje ya uwanja yakisubiri watu kwaajili ya safari, magari toka makampuni tofauti nchini yanayosafirisha watu mikoani yalikuwa yamepangana tayari
kwa safari, na wenye yao binafsi walianza safari ya taratibu huko mikoani. Serikali nayo ilitoa magari yake ya mwendo
kasi kwaajili yakufanikisha kwa namna moja au nyingine ili mazishi yakamilike. Mwili wa Richard ukipelekwa Morogoro,
mkewe na Bi Fatuma miili yao ikipelekwa mkoani Tanga. “Masikini umati huu unakumbusha mambo makubwa kama
siku ile ya ndoa na harusi watu wengi walijitokeza wakafurahi na hata siku yake ya mazishi siwezi kutofautisha” mwana
mama mmoja wa makamo alisikika akiongea kwa machungusana huku akitembea mwendo wa kulazimishwa huku akiwa ameshikiliwa na nduguze kwa namna alivyoguswa na msiba
huo.

BAADA YA MAZISHI
IKULU -DAR ES SALAAM
Wanahabari mbalimbali walioneka kutulia masikio yamesimama macho mbele na kamera zao zikirekodi video
“…nasikitika baada ya kuamini kuwa kijana wangu mpendwa wangu mheshimiwa Richard Edward Kobero ni marehemu
tena amekufa kifo kibaya sana kifo kisichoendana na hadhi yake amekufa kama mwizi amekufa kama mtu asiyetambulika amekufa kama…, sijui nisemeje…Niliposikia umauti wake
niliishiwa nguvu nilijikuta nikiwa ndani hoi hofu ikiingia na kuunyong’onyesha mwili kwa taarifa nzito” Macho yakiwa mekundu aliongea mheshimiwa Emanuel Godfrey Meza Raiswa jamuhuri muungano wa Tanzania, akajifuta uso kwa
kutumia leso yake na kuendelea kuongea

“…Nikweli ametutoka na tumelipata pengo kubwa sijui nani atakayeliziba, mtu kama Richard alikuwa ni mtu wa kujitoa
sana katika mambo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na hata kiimani kiujumla hakuna asiyelijua hilo. Mambo aliyoyafanya
ni mengi siwezi yasema mana muda hautatosha amechangia
miradi mbalimbali ya kijamii amechochea hisia za vijana kujiajiri wenyewe na kutotegemea ajira toka mashirika
mbalimbali” Mheshimiwa Meza akatoa miwani yake machoni na kujifuta chozi kisha akaendelea “Napenda kuwasisitiza
ndugu zangu wananchi tuwape ushirikiano wa dhati sanajeshi la polisi na pia natumaini miongoni mwetu wapo
wanaojua ukweli juu ya tukio hili basi msisite kuweka mambo hayo bayana na mtu atakayehakikisha kuwa na ushahidi
wowote juu ya tukio hili baya mimi Rais wenu nitampatia kiasi cha Milioni mia moja na usalama wa yeye na familia yake
popote pale duniani. Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika.”

Alimaliza Mheshimiwa Rais na kunyanyuka kwenye kiti na kuwaacha waandishi wa habari wakinong’onezana wengine wakibaki wametoa macho. Mheshimiwa Rais katika matembezi ya kurudi sehemu ya mapumziko akiwaamezungukwa na walinzi alipatiwa simu toka kwa mlinzi
mmoja kati yao “…nani tena?” mara akakunja sura “Unanipa hongera mapema yote hii” aliongea akiwa kasimama akaitoa simu masikioni akaitazama simu na kuanza kuandika haraka haraka ujumbe wa maneno “Nataka tukutane mapema kesho unieleze vizuri habari zako nataka unishawishi kwa vithibitisho la sivyo utajutia” akautuma haraka na kufuta
sehemu ya kumbukumbu akiwa bado kashikilia simu ujumbe mwingine ukaingia akaufungua “Sawa kila kitu kipo ni wewe
tu na muda wako” Mheshimiwa rais akauvuta mdomo wake na kufuta ujumbe huo kisha akatazama kushoto na kulia. Mara simu ikaita ikiwa mkononi, “Fanuel Mkwasi alitaja jina hilo na kupokea, “…ndio kijana wangu…hapana sijakataa ombi lako lakini inatupasa tumchunguze kwa makini Swai kabla ya kumtangaza kama gaidi” mara simu ikakatika “Haaa…sasa kila mtu akitaka lake nimkubalie itakuwa nchi au shamba la bibi fyuuu” alisonya na kumpatia simu moja ya walinzi wake ‘Bado nahitaji kumchunguza mimi mwenyewe bado siwezi kukubali
kirahisi kuendeshwa’ alijiongelea katika nafsi yake kisha huyo akaongoza safari.

Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Mzee Habibu aliwaza na kuwazua usiku huo akitafakari juu ya makuzi ya Pius kwa kuanza siku hiyo na zijazo itakuwaje,
alilia na mola ampe mawazo mazuri tena ampe moyo wa subira kijana Pius walau asiwe na kumbukumbu juu ya maafa
mazito yaliyomkuta, aliamua kuwasiliana na mwanae mkubwa ambae alimuoza miezi kumi iliyopita kwa bahati
mbaya mumewe alifariki baada ya mwezi mmoja tu katika ndoa na kumuacha mjane akisimamia mali za mumewe. Mzee
Habibu alimueleza kila kitu na kumuomba ampelekee Pius ambae kwa sasa ni Salim aishi nae walau miezi kadhaa na
yeye arudi na Karimu ambaye alienda likizo kwa dada yake. Mzee Habibu alifanikiwa mwanawe Shakira alikubali kwamoyo mmoja basi Mzee alimpeleka Salim kwa mwanawe.

Sinza Park, Kinondoni-Dar es Salaam.
“Sasa ndugu itakuwaje ikibainika kuwa tunahusika na kifo cha Richard? na aliyekuwa anawasiliana na Anita kwa siri ni nani? Tuwe macho mzee”, Peter aliongea na kumtazama Samuelkwa macho ya wasiwasi “Ni kweli inatia mashaka lakini
tusiwe na moyo dhaifu kiasi hicho” aliongea Samuel na kukunja nne kwa dharau “Kaka sikia hatukupanga mauaji ya aina ile zingatia hilo, target ilikuwa ni Richard tu lakini imekuwa tofauti unajua” aliongea tena Peter, Samuel uso wa
hasira ukamkaa “Unaonaje ukibadilisha maada mzee mana sikuelewi, kwani wewe una undugu nao, uzuri Anita tumeshamuua na Richard hayupo la msingi hapa nikumfatilia
kibaraka muhindi mpaka tumpate” Samuel aliongea na kunyanyuka kuchukua chupa ya wine na kujimiminia kwenye
glasi. Wakati huo Peter akimtazama rafiki yake kwa mshangao.

Tumemaliza Msimu wa kwanza wa simulizi yetu ya Hidden Truth

Tuendeleeee kufatilia
 
Story nzuri sana...

Ngoja tuone msimu wa pili mtoto akikua itakuaje...
 
BMtunzi : AKIDA S. RAMBAO
Contact : 0658328596, Email : akidasiri@gmail.com)

MSIMU WA PILI

SEHEMU YA 4 A : NADHIRI YA MOYO

Dondoo:
Kijana Salimu anagundua kuwa mauji ya familia yake hazikuwa ndoto bali ni ukweli, anawagundua wahusika wa mauji ya familia yake akiwamatembezini na kujiwekea Nadhiri ya moyo ya kuutafuta ukweli na kulipa kwa wahusika ambao amewahisi. Pembezoni mwa mji nchini Uganda Komandoo Ochola anatembelewa na Waziri Fanuel Emanuel Mkwasi kwa mara nyingine akishawishiwa kurudi kazini na kuunda kikundi maalumu cha kijasusi huku akikumbushwa mauji ya Mh. Richard na Joka huku akiahidiwa ulinzi na usalama wake anakumbuka alipokuwa Israel alichungulia kaburi na kunusurika kifo kwa kupigwa risasi na Komandoo Swai kisha kuokolewa na jeshi la India hasira zinampanda maradufu. Je! Nini atakachokiamua

Bagamoyo, Mkoa wa Pwani

‘Sijui nikushukuru kwa kiasi gani mola wangu, umenifanya nijivunie sana kuwa na kijana huyu wa kipekee sana, amekuwa familia yangu lakini sasa sina…’ Mzee Habibu aliwaza na kugeuza shingo kuwatazama vijana wawili mashababi wakiwa katika mazungumzo ya furaha chini ya mti wa muembe. ‘Najua kwangu ulikuja na rizki yako kijana wangu leo umeyabadilisha maisha yangu kwa kweli’ “Mzee Habibu” alisikia akashtushuka na kuwahi kushika kifua chake na akageuka kumtazama mkewe Bi Aida “Ahh mke wangu utaniua kwa presha” aliongea kwa kulalama “Jamani mbona sijakuita kwa ukali kwani wawaza nini…watoto wanakusubiria wewe au unataka kuyavusha?!” aliongea Bi aida, Mzee Habibu akauvuta mzuzu wake kidevuni akaivua kofia yake na kuacha kichwa kikiwa cheupe na kuikunja kisha akairudisha kichwani “Najua, waite hapa…”.

Baada ya muito vijana wakakaa kibarazani wakiwa hawana hili wala lile “Kwa hakika wanangu mnaonekana kama ndugu wa tumbo moja” Salimu alimtazama Karimu naye Karimu alifanya wakiwa na sura za mishangazo kidogo zilizochanganyika na maswali, hawakung’amua kitu “…mmenifanya niwe maarufu zaidi wanangu kwa juhudi zenu za masomo hata tabia njema kila mzazi angetamani kuwa na watoto kama nyinyi, najivunia sana” Mzee Habibu akakokhoa kidogo na kuendelea “Salimu mwanangu leo kuna kitu nataka kukwambia maana sasa we si mtoto tena”, Mzee Habibu alipeleka macho kwa mkewe kana kwamba kuna lolote la kusemwa lakini palikuwa kimya akaamua kuyarudisha macho kwa vijana wake. Mzee Habibu alijifuta uso wake kwa mikono yake akionekana ni mtu anae tafuta pakuanzia kuongea, palipita kimya macho ya Mzee Habibu yakiwa katika Jamvi mguu mmoja kaukunja. “Salimu mwanangu…sisi sio wazazi wako wa kukuzaa bali ni walezi wako tu” moyo wa Salimu ulifanya paa hata Karimu naye alishtuka macho yakamtoka alitazamana na Salimu, “Jina lako halisi wewe ni Pius Richard Edward Kobelo na sio Salimu Habibu Mwinyi” sio Salimu pekee hata Karimu ali hamaki na kubaki wametumbua macho Mzee Habibu akaendelea wala hakuwa wapatiliza “…hilo jina tulikupatia sisi, familia yako ilivamiwa ikauwawa na kuteketezwa kwa moto miaka mingi iliyo pita, wewe uliponyeka hivyo nilikuokota ufukweni na tukakulea mpaka sasa” Mzee Habibu akameza mate kwa shida na kufumba macho dhahiri alionekana alikuwa kajilazimisha kuongea akafumbua macho na kuyaaacha na mawingu ya machozi kuwafanya watu wote nao kutokwa na machozi, huzuni ikatawala Salimu akiwa na maamivu mazito ya moyo alibaki kaduwaa mdomo wazi machozi yakimtoka huku akitetemeka.

Akaendelea “…kuna kitu kinacho nishangaza mpaka sasa kutoka jijini mpaka Bagamoyo nikipande kirefu imekuwaje kwa umri ule nikukute pale ufukweni sielewi ilikuwaje” alipo maliza akauma midomo yake kwa nguvu kisha akendelea na habari zingine Mzee Habibu aliongea kila kitu na juhudi zote za kutafutwa kwa kijana Pius na sababu za kutomuweka wazi. Salimu kijana Pius aliangua kilio kikubwa kiasi cha kuwafanya watu wote wamgeukie na kumbembeleza. Salimu kilichomliza si kingine bali ni zile kumbukumbu na njozi alizokuwa anaziota kipindi cha mwanzo na hata kuwaeleza walezi wake nao kumzubaisha na kumwambia asizizingatie kumbe zilikuwa qq1q1pqp0ppp1kweli tupu. “Nakumbuka kila kitu, mauaji ohh wazazi wangu kwanini muwe nyinyi kwanini mfe vile?” Salimu aliongea kwa uchungu mzito na kumfanya Karimu kumsogelea na kumshika bega huku nay eye akitokwa na machozi. Basi huzuni ikatawala na ikawa ni kubembelezana tu. Afuheni ilipofikika Mzee Habibu alijinyanyua jamvini na kuingia hazikupita dakika nyingi akatoka na mfuko mkubwa...

Itaendelea....
IMG-20211211-WA0046.jpg
 
The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)

Mtunzi : Akida Siri Rambao
Contact : 0658328596
Email : akidasiri@gmail.com

MSIMU WA PILI

SEHEMU 4 B : NADHIRI YA MOYO

Tuendeleeee...

....na mfuko mweusi wa Rambo ambao ulionekana kuwa na magazeti mengi yaliyofubaa akayaweka katika jamvi “Ukikaa na kutulia nakuomba pitia pitia haya magazeti ili ujue yaliyo jili kipindi hicho”, Mzee Habibu akarudi sehemu yake aliyokaa mwanzo “Kingine sasa hivi una hiyari kuendelea na Uislamu au kurudi katika dini ya wazazi wako” Salimu alitingisha kichwa kuonesha kukubali kisha akasogeza mfuko wa Rambo na kutoa gazeti moja moja na kusoma vichwa vya habari vilivyo kolezwa na wino mweusi. “Serikali yatoa donge nono kwa atakae mpata Pius” , “Familia ya Pedeshee Richard yateketea kwa moto” “Mtoto wa Richard kutokomea kusiko julikana” alisoma na kusoma vichwa vya habari vingi sana na kumfanya apatwe na hasira sana na mengine yalimfanya kushindwa kumalizia kwa uchungu “Lazima niutafute ukweli kwanini waiue familia yangu” Salimu alijikuta akiongea kwa uchungu na kuangua kilio. Muonekano wake na baba yake ulikuwa sawia kabisa walifanana mno nakumfanya kuhisi kuwa sio yeye bali ni baba yake aliye katika mwili wake.

Picha kazaa ziliwaonesha Samuel na Pater na vichwa vya habari vikionesha namna walivyoguswa, “Hao walikuwa ni marafiki wa baba yako lakini waliishia kuwa maadui” Salimu alimuangalia Mzee Habib. “…haijajulikana, lakini baba yako aliishia kuachana na Siasa akitokea chama tawala wakati huo Samuel akiwa chama pinzani lakini ilikuwa ajabu pale anapotembelea katika majimbo kwa mambo binafsi aliishia kupata mapokezi kana kwamba yeye ni mfalme hivi, ilikuwa nzuri lakini naamini kwa wasio mpenda walichukia” aliongea Mzee habibu huku Salimu akibaki kumtazama tu. “Kuna kitu cha ziada nitakuja kukwambia siku moja ila kwa sasa mwanangu fanya ufanyavyo usije ukautoa utambulisho wako kokote kule na kwa mtu yeyote” aliongea Mzee Habibu.

Karimu muda wote alikuwa kimya akitafakari alijawa na huruma sana, “Kaka nitakusaidia bega kwa bega hatua kwa hatua zote mpaka tone la mwisho”, Salimu aligeuka na kumkumbatia “Ni sawa wewe ni ndugu yangu” aliongea Salimu huku kichwa kikiwa juu ya bega la Karimu. “Vijana wangu teyari mmefanya mambo mengi makubwa sana yakuwa fanya mfikie malengo yenu kama hili la kuongoza kitaifa mpaka kutangazwa kitaifa na kusoma bure katika masomo yenu ya Advance na chuo kikuu hapa nchini teyari inamaanisha mafanikio Allah subhanahu wataala yupo pamoja nanyi” Mzee Habibu fumba macho kwa muda akiwa kasimama. “Chamsingi tu mnapokwenda mzingatie yale mliyokuwa ukiyazingatia mkiwa hapa nyumbani tutawakumbuka sana na nyumba itakuwa pweke mno” Mzee Habibu aligeuka kichovu na kuingia ndani kwa mwendo wa sitaki nataka.

Itaendelea....
IMG-20211211-WA0046.jpg
 
The Hidden Truth (Ukweli uliofichika)

Nani Anahusika?!!?

Mtunzi: Akida Siri Rambao
Contact : 0658328596
Email: akidasiri@gmail.com

MSIMU WA PILI

SEHEMU 4 C : NADHIRI YA MOYO

Ilipoishia...

...Mzee Habibu aligeuka kichovu na kuingia ndani kwa mwendo wa sitaki nataka.

******
Changamoto hazikukosekana katika maisha ya mazingira mapya ya masomo, tabia nyingi mpya waliweza kukutana nazo wakiwa Kibaha High school ikiwemo unyanyasaji na wizi uliokithiri katika Hosteli zote. Ushirikiano wa pamoja ulihamasisha hisia mpya ya mapinduzi ya tabia mpya shuleni hapo japo ilikuwa ni kwa shida kutokana na uwoga wa wanafunzi wengi.
******
Katikati ya jiji Dar es Salam
Ndani ya likizo ya kwanza ya mihula, Ijumaa moja Salimu na Karimu walikuwa ndani ya jiji tayari. Macho yalikuwa kodoo wakishangaa hili na lile, wanawake wa mji hu waliwastaajabisha zaidi maana walizoea kuona wanawake wakiwa wamevaa suruali na vifua vikiwa wazi wakienda na kurudi, wao waliwaita watembea uchi lakini jijini humo waliyaona zaidi ya hayo maana walikuwa kama hawana nguo kabisa. Wanawake wengi wajiji walimezwa na tamaduni za kimagharibi kuusiana na mavazi, wachache wao wa kuhesabu utawaona na magauni marefu lakini kichwani sasa hawakuwa salama na mila za kimagharibi. Wengi wao walivaa mawigi na kushonea nywele ndefu za bandia wakienda wakijibinua binua wakitembea kwa maringo. Wapo pia waliokuatana nao wakiminyana kwenye dalala na matembezi yakawaida wakiwa kama watu walio ungua na maji yamoto au mafuta maana walikuwa na mabaka kwenye ngozi kwa kutumia vipodozi visivyo salama sijui taasisi za kusimiamia vitu hivi walikuwa wapi. Wanawake wanaosemwa wako uchi hawakuwa uchi ule wa mwana anapo toka tumboni mwa mamaye walivaa nguo fupi zaidi ya neno lenyewe fupi kiasi cha kuacha habari zao za siri zikionekana wazi hazikuhitaji nguvu nyingi kuona.
Wakiwa jijini nyakati hizo za mchana wakipita pita hapa na pale katika majengo ya kifahari ghafra binvuu Salimu alibonyea na kujificha katika maua kitu kilicho mpasua roho Karimu bila kupenda na yeye akazama. “Vipi mzee mbona umenishtua” kwa macho ya wasiwasi Karimu alimuuliza ndugu yake huku moyo ukimuenda matiti. Salimu alitulia tu huku akiwa kaikunja sura akionekana kufikirisha ubongo wake kukumbuka kitu, alinyanyua shingo kwa kuibia kutazama vizuri upande wa pili wa barabara kuhakikisha alichokiona, “Haaaa, tuondoke hapa hapafai”.

Kunani???!! Salimu ameona nini?

Itaendelea
AKIDA%20S.%20RAMBAO%20%3D%20THE%20HIDDEN%20TRUTH%20(UKWELI%20ULIOFICHIKA)%20(2).jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom