The HELL RUN! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The HELL RUN!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lole Gwakisa, Mar 23, 2011.

 1. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  [​IMG]

  Si watu wengi wanajua ugumu wa utumiaji wa barabara hii ya Mbeya-Dar es salaam.
  Katika miaka baada ya uhuru wakti wa kusafirisha bidhaa kwenda Zambia hasa baada ya mgogoro wa kisiasa kati ya Afrika na Rhodesia wakati huo, kamba ya uhai kwa nchi ya Zambia ilikuwa hii baarabara ya DSM hadi Lusaka- Zambia.
  Wakati huo ikihulikana kama "The Hell Run".
  Hadi leo hii barabara hii inabidi kila anyeitumia aiheshimu sana sana kwani inaendelea kutafuna watu wengi mno.
  Kwa masikitiko makubwa natoa rambi rambi kwa familia za wale wote waliopoteza maisha katika ajali ya hivi karibuni kwa wanamuziki wa 5 Star.
  Kosa la wazi linalojionyesha ni uzembe wa dereva wa coaster iliyowabeba marehemu na wanamuziki wengine.
  Nasikitika sana kwa vifo vilivyotokea , na pengine kutokana na uzembe wa dereva na kutojua matumizi mazuri ya barabara hii.

  Ni wiki moja tu nimesafiri toka Mbeya hado Dsm kwa hii barabara na nina weza kutoa dondoo kadhaa kwa wana JF juu ya hii njia:
  • Ni barabara pekee ambayo mwenye gari zuri na imara unaweza endesha hadi 200km/hr, nimeshuhudia mabasi yakienda hadi 160km/hr
  • Ni barabara vilevile yenye sehemu ambazo dereva huthubutu kwenda zaidi ya 20km/hr
  • Hii ni barabara yenye malori ya mizigo mizito mengi sana, na magari haya ndio wafalme wa barabara, ignore them at your own risk.Usilipite lori BILA kupata kibali chake na akikuruhusu unapiga kihoni kifupi cha kushukuru!
  • Barabara hii inabeba mizigo kwenda Zambia ,Malawi Congo,Burundi, Rwanda na hata Zimbabwe hivyo basi magari madogo au mini buses, pick up nk ni akina bwana mdogo katika njia hii.
  • Unashauriwa sana kuyaogopa mabasi ya abiria kwa vile hawa vile vile wanakwenda kwa mwendo ambao unakaribia kichaa!
  • Safari yako unashauriwa uianze mapema sana(saa 11 hadi saa 12) kama utasafiri kwa siku moja kutoka Mbeya(Kyela,Tunduma) hadi Dar es salaam, mwendo huu ni karibu 900km ambazo si rahisi kuona ukubwa wa Tatizo hadi umeendesha kwa kilometa 300-400 na ukaanza kusikia usingizi!!
  • Usithubutu kunywa pombe usiku wa kuanzia safari au uwapo safarini, ukinywa utajisikia vizuri na kusinzia hatimaye kuangusha gari!!
  • Endesha kwa mwendo wa kawaida , hata kasi inapobidi, lakini uangalifu ni muhimu sana sana ukizingatia magari mengi yaliyomo barabarani.
  Kwa kuzingatia dondoo hizo nimeshangaa kuwa ajali ya coaster ilitokea kukiwa na giza , kitu kinacho ashiria gari lilikuwa likisafiri usiku, kitu cha hatari sana kwa mgeni wa barabara hii.
  Kwa kawaida ukiondoka mapema sehemu za Mbeya unaingia Dar kabla jua halijazama, hivyo kuweza kuona yote yanayojiri baerabarani.
  Narudia pole na rambirambi zangu kwa ndugu za wale waliopoteza maisha.
  Mungu awarehemu, Amen
   
 2. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,272
  Likes Received: 558
  Trophy Points: 280
  Uko sahihi isipokuwa magari yaendayo Rwanda na Burundi yanapinda kulia morogoro na kufuata barabara iendayo Mwanza.
   
 3. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Inasikitisha sana kwa kweli....

  Unapoendesha safari ndefu kwenda mikoani unashawishika sana kwenda speed kubwa mpaka unajisahau...ki ukweli barabara zetu sio za kwenda speed kali sana kwa kujiamini kiasi hicho...
   
 4. M

  Mzalendoo Member

  #4
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Shukuran mtoa mada,watumiaji wa barabara tuwe makini.
   
Loading...