The guide: Ukishaamua kuwa na 'nyumba ndogo' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The guide: Ukishaamua kuwa na 'nyumba ndogo'

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by The Boss, Oct 14, 2011.

 1. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Kama ambavyo tunaelimishwa kila siku madhara ya kuvuta sigara, na bado mpaka madaktari wanavuta, na tunaelimishwa kila siku kuhusu pombe, lakini watu wanajikuta wamefika bar, bila hata ya kujijua, hata kama asubuhi waliapa pombe basi.

  Basi na hili la nyumba ndogo, kuna watu ni 'almost impossible' kuwaambia wasiwe na nyumba ndogo.

  Sasa iliyobaki kama watu wazima sio vibaya kufundishana 'how to do it the right way.

  zifuatazo ni kanuni ukizifuata hutapata matatizo makubwa na pengine uka enjoy life kupita maelezo.

  1. Nyumba ndogo lazima iwe na heshima kwa mkeo na wewe mwenyewe, akileta dharau au kujifanya ana mrusha roho wife, unapiga chini fasta, hii ndio kanuni ya kwanza na muhimu na ndio muongozo wa mpango mzima. Kama hutaki mkeo ajue, basi iwe hivyo, na sio vinginevyo, marufuku mashindano kati ya wife na nyumba ndogo, bora zaidi wasijuane wala kukutana kwenye shughuli zao.

  2. Nyumba ndogo isisababishe kwa njia yeyote ile kupungua kwa huduma nyumbani au kwa wife, ikiwezekana huduma ziongezeke home, ili 'wasihisi' chochote...hii ni ngumu kwa baadhi ya watu ukishindwa kipato basi jitahidi, chakula cha usiku but ukiweza vyote bora zaidi.

  3. Usimponde au kuzungumza siri za mkeo kwa nyumba ndogo au kumuonesha yeye ni bora zaidi hata kama 'amekukoleza kupita maelezo' hii itazuia kumpa hisia kuwa unataka kumuacha mkeo na yeye achukue nafasi, hata kama ni hivyo, usioneshe hivyo, iwe siri yako mpaka utakapoamua hivyo.

  4. Usimtambulishe waziwazi au kuongozana nae kwenye sherehe za kiofisi au za familia, hasa kwa watu wanaomfahamu vizuri mkeo unless wewe na mkeo mpo kwenye process ya talaka officially...akijitia kimbelembele kujitambulisha muonye au mpige chini fasta.

  5. Usianze 'kuinvest' mali kwa nyumba ndogo wakati hata future ya watoto bado ya kubabaisha, ukiona nyumba ndogo
  ni gold digger unapiga chini fasta.

  6. Nyumba ndogo usiipe majukumu ya mke kwa njia yeyote hile, kazi ya nyumba ndogo ni kuku burudisha na kustarehe na wewe, majukumu kwa mkeo, ukifanya kosa hili, si ajabu ukajikuta na nyumba ndogo ya pili nyingine.

  7. Nyumba ndogo lazima iwe kifaa cha uhakika, ikiwezekana imzidi wife ili mkeo akigundua awe mpole, ukichukua mwanamke mbovu, wife atakudharau na asiwe 'kicheche maarufu, utaumbuka.

  8. Kwa wanaopenda kuhonga, ukihonga gari nyumba ndogo, hakikisha wife analo tayari ikibidi yawepo zaidi ya moja home, sio wife anahangaika na daladala, nyumba ndogo umeinunulia vitz, utadharaulika kupita kiasi na wote wawili na jamii ikigundua.

  9. Usitafute sifa kwa ndugu wa nyumba ndogo, tafuta sifa kwa ndugu wa mkeo ili hata zogo likitokea watakutetea.

  10. Nyumba ndo sio wife, usilete wivu kupita kiasi, ukiona uaminifu hakuna, piga chini kimya kimya sio kuanzisha ugomvi mpaka siri zinavuja.

  Wengine mtaongezea.
   
 2. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Du!Nashukuru sana kwani hapa tayari nimepata mteja wa kumpa ushauri na naenda kumpa data sasa hivi ili aweke mambo yake sawa kabla hajaharibikiwa,asante sana Boss!
   
 3. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #3
  Oct 14, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  OMG!! Boss usiniambie ushakuwa recruited kwenye Chama..... Please say NO!... Dah!... lol
   
 4. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Mkuu, ushauri wa maana sana, ngoja nikaufanyie practice nione mafanikio yake.
   
 5. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Mkuu nakupa big five,umepigilia nondo sawasawa,binadamu haishi kwa mkate tu bana!
  Additional note: Mwambie kimada mwisho wa kukupigia simu sa mbili usiku.Once upo na bi mkubwa no mawasiliano,si ya simu,si ya sms,asubiri mpaka muonane kesho yake.Akileta za kuleta mbwage.
   
 6. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Acha hizo Asha,chama kipi?
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  the boss, plz weka na rules za small house ya kiume manake nataka kujiunga na chama on a serious note. na zikitangazwa afasi za uongozi unistue,plz (naomba usimuambie ashadii eeh,ni mdau)
   
 8. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  wifi,we cant fight them,lets nt only join them bt lead them. kama small house zinaleta amani nyumbani, ngoja na sie tudumishe amani. who wants stress? (kuna jirani yangu hapa namuona potential flani, nitakukutanisha nae. the boss kasema muhimu sweetie wako asijue..)
   
 9. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  we King'asti wee,ndoa zina rules zake,there are rules for men and rules for women,acha kuvuka mipaka usije ukaishia kuweka mikono kichwani.
   
 10. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Daaah!


  Kazi ipo!..lol
   
 11. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #11
  Oct 14, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  B' naona Boss atakua ameelewa.... Sijui kwanza kakimbilia wapi!!! lol
   
 12. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Haki sawa aisee! Hakuna mipaka wala mistari hapa!
   
 13. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  Nyumba ndogo inatikiwa isizae,ikiwezekana unakula deal na doctor amchome sindano ya kuzuia mimba ili awe available muda wowote
   
 14. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  kawahi kupeleka mapochopocho small haus,si unajua leo public holiday,bila shaka nyumbani kaaga anaenda shamba chanika kumbe yuko kwa bi mdogo.Mwache astarehe bana.
   
 15. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  subiri ukibambwa ndo utajua kwa nini punda alinyimwa pembe akapewa mlio!
   
 16. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #16
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  na mwisho kabisa.....never ever sleep kwa nyumba ndogo. hakikisha kila siku ya mungu unaenda lala nyumbani na wife!!!!
   
 17. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #17
  Oct 14, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Hilo nalo neno Wifi King... i like the leading them part... maana tukiwa join moja kwa moja jamii haitachelewa kutugeuzia kibao kua hatufai!.... Sasa King wote wawili hatukak stress lets do the needful; Swali- huyo jirani pontential it is OK.... Sasa mbona sina mzuka wa kuenda huko maana yote napata.... Niende sababu naiga na kukomoa AMA niende sababu kuna mapungufu?? (For there is no mapungufu kwa Sweetie..) naomba ushauri tafadhali....
   
 18. neggirl

  neggirl JF-Expert Member

  #18
  Oct 14, 2011
  Joined: Jul 30, 2009
  Messages: 4,830
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Mmh The Boss wewe!
   
 19. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #19
  Oct 14, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  absolutely right Mkuu!
   
 20. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #20
  Oct 14, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Na wewe subiri ukibambwa ndo utajua kama dc wa igunga alivuliwa hijab au mtandio...'hakunaga' siri kwenye hii dunia Bishanga!
   
Loading...