The Golden Words of Hitler

NGULI

JF-Expert Member
Mar 31, 2008
4,803
637
Golden Words of Hitler:

When you are in light, everything will follow you. But when you enter dark, even your own shadow will not follow you. That is life.

God made relatives, Thank God we can choose our friends, Money glitters, beauty sparkles, and intelligence shines.

Keep a very firm grasp on reality, so you can strangle it at any time. Life is like a box of chocolates, you never know what you're getting. People may not always believe what you say, but they will believe what you do.

I've always wanted to be somebody, but I should have been more specific.

You can't have everything - where would you put it? Laugh and the world ignore you. Crying doesn't help either.

God is not moved or impressed with our worship until our hearts are moved and impressed by Him. Life is like a mirror, if you frown at it, it frowns back; if you smile, it returns the greeting.

Never trust a person who isn't having at least one crisis. Goodness is the only investment that never fails. The only thing lazy people do fast is get tired.

Never deprive someone of hope; it may be all they have.

Silence is the only thing that can't be misquoted!

If we don't control our money, it will control us.

Life Insurance: A contract that keeps you poor all your life so that you can die rich..Some drink at the fountain of knowledge. Others just gargle.

Everyone has a photographic memory. Some don't have film. If you r living on the edge, make sure you're wearing your seat belt.

A classic is something that everybody wants to have read and nobody wants to read.

Minds, like parachutes, only function when they are open.The shortest distance between two points is under construction.

Learn from other people's mistakes, life isn't long enough to make them all yourself.

On the road, never argue with a vehicle heavier than yours.

One thing you can give and still keep is your word. Life is funny if you don't think about it. Life is like a grammar lesson. You find the past perfect and the present tense.

There are two kinds of lawyers, those who know the law and those who know the judge. More doors are opened with 'please' than with keys.
 
Kuna mkondo wa mawazo kwamba ingawa Adolf Hitler alisababisha maafa makubwa kwa kuanzisha vita kwa sisi waAfrica hiyo ilikuwa kama baraka kwa sababu baada ya vita nchi za wakoloni zilielemewa kiasi cha kwamba ilikuwa rahisi kwa waAfrica kupigania uhuru. Je hii imekaaje?
 
Binafsi sidhani, Wakoloni walikuwa na mahesabu yao maksusi, lilikuwa siyo lengo lao kukaa na mfumo huo huo siku zote, wanasema unamwibia Yohana umlipe Petro. Hitler au bila Hitler, ukoloni una matabaka, unaanza na mitulinga ukishitukiwa wanakumalizia kwa kutawala kwa hila za kiakili. Baada ya vita vya kwanza Marcus Garvey na chama chake cha UNIA walikampeni makoloni yaliyokuwa chini ya Wajerumani wapewe UNIA-hawakufanikiwa.
 
Wakoloni walikuwa na mahesabu yao maksusi, lilikuwa siyo lengo lao kukaa na mfumo huo huo siku zote
Hapa sijakuelewa, ni "mahesabu" gani ya wakoloni unayoongelea?

...unaanza na mitulinga ukishitukiwa wanakumalizia kwa kutawala kwa hila za kiakili
And this is what is currently happening, slowly but surely, in Africa: Recolonization

Baada ya vita vya kwanza Marcus Garvey na chama chake cha UNIA walikampeni makoloni yaliyokuwa chini ya Wajerumani wapewe UNIA-hawakufanikiwa.
Have you really studied the history of the anti-colonial struggles in Africa? Granted, Marcus Mosiah Garvey did not succeed but then his was a campaign mainly based on the Pan-African philosophy of repatriation. No wonder UNIA stands for Universal Negro Improvement Association. FYI, I am a great believer of Garvey's teachings.

By the way, are you aware that Marcus Garvey through his publication "The Black Man" recommended that his readers peruse Mein Kampf while at the same time expressing his hope that one day the Black race would produce its own Hitler? I quote "Hitler has a lesson to teach and he is teaching it well

As I said in my earlier post though, I am not supportive of Adolf Hitler. I am just interested in discussing about history from an objective standpoint.
 
NI kweli, hitler alisaidia sana kumaliza ukoloni afrika.baada ya vita kuu ya pili nchi za ulaya zilikuwa zimefilisika zisingeweza kuendelea na ukoloni.
 
Mzee2000 hii ni kweli. Tatizo ninaloliona hapa ni kwamba Europeans wanataka tukubaliane nao kila walisemalo kuhusu Hitler wakati wao wenyewe (kwa mfano waingereza) wanamtukuza sana Winston Churchill, ambaye ni mkoloni nambari wani. Sawa, wayahudi walifanyiziwa mbaya na Hitler lakini je sisi waafrika hatusikii maumivu?

I remember reading stories about how African soldiers in King's African Rifles (KAR) who fought side by side with the Allied forces in the trenches in places like Madagascar and Burma. Upon being asked by the european troops why were they fighting they answered that they (African soldiers) were defending the Empire. These europeans soldiers told them that they were wasting their time, because it was the same Empire that was colonizing them; that they would be better off fighting for their own freedom. This was one of the wake-up calls. That's why most of the these returning soldiers (as well as intellectuals, who were in Europe at the time) formed the bulk of those who stood up against the colonizers after WWII.

The post-war period in Africa was characterised by a general feeling that if Europeans rallied against Hitler, because they did not want to be ruled, how come they want to rule Africans? The gathering of pace of the Mau Mau movement in Kenya is just one of the examples (Mzungu Aende Ulaya, Mwafrika Apate Uhuru).

Ukiangalia sana bila Hitler kuharibu mpaka leo labda waAfrica tungekuwa bado tumezidiwa nguvu. Akina Kinjeketile walijaribu lakini walizidiwa kete kwa sababu Mjerumani aliwazidi nguvu wakati ule.
 
Kuna mkondo wa mawazo kwamba ingawa Adolf Hitler alisababisha maafa makubwa kwa kuanzisha vita kwa sisi waAfrica hiyo ilikuwa kama baraka kwa sababu baada ya vita nchi za wakoloni zilielemewa kiasi cha kwamba ilikuwa rahisi kwa waAfrica kupigania uhuru. Je hii imekaaje?

Tulivyosoma history tulikaririshwa sana madhara ya ukoloni kuwa ndio chanzo cha sisi kuwa nyuma. Nadhani mwanafunzi angeandika paragrap mbili au tatu za kuongelea uongozi mbovu kama sababu ya sisi kutondelea angekosa maksi.

Tukirudi kwenye mada huwezi kusema ilikuwa baraka kwa sisi waafrika kupigania uhuru kwa sababu hakuna tulichokipata zaidi. Labda useme ilikuw a rahisi kupigana UTAWALA na sio Uhuru. Mpaka leo hii Watanzania na waafrika wengi hatuko Huru.

Pili hata historia Wakoloni waligundua wana njia efecctive na efficient ya kuendeleza Ukoloni bila wao kuendelea kukaa Dar.( UKOLONI MAMBO LEO)

Kifupi hakuna baraka yeyote unless japo tungekuwa tumepiga hatua kidogo kama singapore, Malysia.
 
Hitler alikuwa racist, kama angefanikiwa pengine Africa nzima ingekuwa labor camp.

Ukielewa historia ya aggression ya Hitler na rafiki zake kama kina Mussolini (aliyepigana na Selassie huko Ethiopia) na Hirohito (aliye kolonisha sehemu ya China) huwezi kusema bila ya Hitler Africa ingekuwa bado chini ya ukoloni.

Naona watu hawaelewi unyama wa Hitler bado.
 
Naona watu hawaelewi unyama wa Hitler bado.

Wakati mwingine inasaidia kusoma mada kabla ya kukurupuka kujibu. Mkuu nisome vizuri kwanza kabla ya kuanza kupotosha mambo. Nimeishasema na kurudia kwamba simsapoti Hitler!

Nakumbuka nilipokuwa darasa la sita praimari (hii ilikuwa 1969, miaka miwili baada ya kutangazwa Azimio la Arusha) kwenye mtihani kulikuwa na swali kama hivi:

Kabaila ni.....? Kwa pupa nilijibu msukuma (manaake nilifikiri naulizwa kabila ni....?). Nilichapwa fimbo na mwalimu na sintosahau mpaka leo, alikua anaitwa Mwalimu Muruke! Tangu siku hizo huwaga nasoma kwa makini na kutafakari kabla sijajibu. Ni ushauri wa bure.
 
Hivi waafrika haya madhila tuliyopata ni kwa sababu ya udhaifu wa kimawazo au kitu gani? Iweje siye ndio tuliokumbwa na misukosuko mingi ukilinganisha na watu wengine kiasi kwamba hadi hii leo sisi wenyewe hatuwezi kujitawala?
 
Rungu, kwa heshima na taadhima ningependa kuhitilafiana kidogo na wewe kuhusu suala hili ka ukombozi na African Nationalism. Nadhani tutakuwa tunakosea sana endapo tutakubaliana hiyo hoja kwamba, kama isingekuwa Hutler's dictatorship, basi bara la Africa bado tungekuwa au tungechelewa kupata uhuru, kwani tukikubaliana na dhana hiyo, basi zile monvement za African Nationalism championed na wakina William Dubois, Marcus Gurvey na Edward Wilmot Blyden, kabla ya wakina Nkurumah hazitakuwa na maana kabisa.
Ila nakubaliana na wewe kwamba vita vya II vya dunia viliupa msukumo wa hali ya juu ukombozi wa Africa kuliko ilivyotegemewa. Kama alivyosema Prof. Robert I. Rotberg kwenye makala yake itwayo, "The Rise of African Nationalism, The case of East and Central Africa," kwamba:

"Those elements of change unleashed by the war and by the subsequent estrangement of two of the victors did indeed accelerate the emergence of popular movements in Africa South of the Sahara. More rapidly than even the aspirants themselves could have hoped."

Mwisho kabisa, nadhani hatutautendea haki ukombozi wa bara la Africa endapo tutaangalia mambo yaliyotokea mwanzoni mwa karne ya ishirini, na kusahau zile jitihada zilizoanzia kwenye abolotion of slavery na slave trade mpaka kwenye racism, colonialism, and neo-colonialism.
 
Hitler alikuwa racist, kama angefanikiwa pengine Africa nzima ingekuwa labor camp.

Ukielewa historia ya aggression ya Hitler na rafiki zake kama kina Mussolini (aliyepigana na Selassie huko Ethiopia) na Hirohito (aliye kolonisha sehemu ya China) huwezi kusema bila ya Hitler Africa ingekuwa bado chini ya ukoloni.

Naona watu hawaelewi unyama wa Hitler bado.

Hitler alikuwa mnyama sana na wajerumani wenyewe hawataki hata kumsikia manake kawachafulia historia dunia nzima. Cha kushukuru ni kwamba alishindwa vita zote mbili na kupelekea ujerumani kugawanywa kwa mataifa manne. Kama ageshinda vita nadhani wafrika tungeuwawa wote kama wayahudi halafu Africa ageuze mashamba au holiday camps. Kwa hitler binadamu ni mzungu mwenye mwonekano wa Arier peke yake, kama huna muonekano wa ki arier wewe kwake ni trash. Japo yeye mwenyewe hakuwa Arier... lol
 
m_kishuri nakubaliana na mawazo yako na nadhani hapa
...vita vya II vya dunia viliupa msukumo wa hali ya juu ukombozi wa Africa kuliko ilivyotegemewa.
ndio naona umeielewa vyema mada ilivyoanza. Sababu ya kuleta mada hii ni baada ya kujiuliza je sisi waAfrica ni lazima kila mara tukubaliane na Eurocentric view of history?
 
Afadhali Watanganyika tungetawaliwa muda mrefu zaidi maendeleo yangekuwa mazuri zaidi. Wajerumani walikuwa na mpango mkubwa wa muda mrefu wa kuendeleza Tanganyika. Tazama reli ya kati toka waijenge zaidi ya karne iliyopita sisi tunaodai kuwa hawakufanya lolote, mbona tumeshindwa hata kuiendeleza? hata hiyo ya TAZARA waliyojenga wachina nayo imetushinda. Migodi ya Buhemba na mingineyo mizengwe kibao. Bora arudi huyu mjerumani atutawale ili maendeleo yawepo. Hivi hivi Tanganyika itakuwa inarudi RIVASI kwenye maendeleo. Nawasilisha
 
Afadhali Watanganyika tungetawaliwa muda mrefu zaidi maendeleo yangekuwa mazuri zaidi. Wajerumani walikuwa na mpango mkubwa wa muda mrefu wa kuendeleza Tanganyika. Tazama reli ya kati toka waijenge zaidi ya karne iliyopita sisi tunaodai kuwa hawakufanya lolote, mbona tumeshindwa hata kuiendeleza? hata hiyo ya TAZARA waliyojenga wachina nayo imetushinda. Migodi ya Buhemba na mingineyo mizengwe kibao. Bora arudi huyu mjerumani atutawale ili maendeleo yawepo. Hivi hivi Tanganyika itakuwa inarudi RIVASI kwenye maendeleo. Nawasilisha

Temea mate chini.

Wajeremani walikuwa na malengo yao..kuendeleza nchi hilo halikuwa ktk TOR zao..it is incidental tu kwamba walijenga reli na maboma etc , lengo lao kuu haswa ilikuwa kusafirisha malighafi na kui-exploit nchi. Pia sio sahihi kusema 'walitujengea', it is more walijenga mababu zetu through forced labour tena kwa bakora.
 
Binafsi sidhani, Wakoloni walikuwa na mahesabu yao maksusi, lilikuwa siyo lengo lao kukaa na mfumo huo huo siku zote, wanasema unamwibia Yohana umlipe Petro. Hitler au bila Hitler, ukoloni una matabaka, unaanza na mitulinga ukishitukiwa wanakumalizia kwa kutawala kwa hila za kiakili. Baada ya vita vya kwanza Marcus Garvey na chama chake cha UNIA walikampeni makoloni yaliyokuwa chini ya Wajerumani wapewe UNIA-hawakufanikiwa.


Ndityo Africa inatawaliwa kwa akili na wajanja wa Ukaya. Kuna thread nyingine. Wanajua mwanadamu ni mnyama na kuna limit ya kumtesa mnyama. Hata mbwa ambaye ni rafiki yako sana ukimtesa kupita kiasi lazima atabadirika na kukuuma
 
Hivi waafrika haya madhila tuliyopata ni kwa sababu ya udhaifu wa kimawazo au kitu gani? Iweje siye ndio tuliokumbwa na misukosuko mingi ukilinganisha na watu wengine kiasi kwamba hadi hii leo sisi wenyewe hatuwezi kujitawala?
Naomba u-substantiate hapo kwenye red mkuu
 
Asante sana Rungu kwa mjadala huu, nashukuru pia kwa kutuelezea zaidi kuhusu UNIA na Garvey, siyo kila 'issue' aliyo ijadili Garvey ina nafasi kwenye kizazi chetu, ni karibu na maajabu makubwa kwamba Tanzania Garvey hajulikana kabisa! Kuna nchi Mein Kampf ya Hiter imepigwa marufuku hivi Tanzania kitabu hiki kinaruhusiwa? Watu wengi walimchukia na wanamchukia Hitler kwa sababu mbalimbali, lakini kuliwa na watu wachache kama Churchill aliyemchukuia Hitler na hapohapo alimheshimu na kuupenda upendo wa Hitler kwa Ujeremani. Ya Garvey naamini alitaka watu Waafrika wajifahamu na pia wajue hila, ujanja, mbinu, harakati na pilikapilika za kisiasa na kijamii-tumpende tusimpende Hitler alikuwa anawafahamu watu wake na hali zao.
Na zaidi ya yote Garvey kama sikosei alilaaniwa sana USA kwa kutumia magwaride na mbwanga za kijeshi, na aliwajibu watuhumu wake waangalie Hitler na NAZI walivyofanikiwa(kuwa na wanachama wengi)kwa kuiga mbwembwe za UNIA-KIMAGWARIDE NA KIUNIFOMU .
Kwangu mimi, kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka kwa Garvey, hebu nionyeshe kiongozi mpigania UHURU mwafrika ambaye hakusukumwa na changamoto za Hayati Garvey!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom