SoC01 The game of Pray, Motivators: Jini mla watu katika ujasiriamali wa kiafrika

Stories of Change - 2021 Competition

Ginner

JF-Expert Member
May 8, 2011
1,459
1,832
Kwa kipindi cha hivi karibuni, tatizo la ajira limepelekea mlengo wa ujasiriamali kuwa ndio habari ya mjini. Tumesikia maneno ya hamasa kwa vijana kuingia kwenye shughuli za kijasiriamali toka kwa watu mbali mbali ikiwemo wanasiasa, watumishi wa serikalini pamoja na taasisi zisizo za kiserikali. Katika kufanikisha hili, kumeibuka makundi makuu mawili. Wahamasishaji na wahamasikaji.

Kundi la wahamasikaji wa nyimbo hizi huwa ni wastaafu, vijana wahitimu wa vyuoni, pamoja na kina mama. Pia kuna kundi la pili la wahamasishaji, hawa kwa kiasi kikubwa wamegueka wanaharakati wa ujasiriamali. Hawafanyi shughuli za uzalishaji, ila wako vizuri kwenye media kuandika makala na kutuma picha kwenye mitandao ya kijamii wakiwa kwenye majukwaa, wakifanya uwasilishaji wa hoja kwenye vikao vta kisekta na mikutano ya wadau wa ujasiriamali. Hawa kwenye andiko langu tuwatambue pia kama "The cannibals- Jini mla watu" .

Mada hii itachambua kwa ujumla dhana na ujasiriamali wa kiafrika na nitaelezea namna "Cannibals" wanavyotumika kuwatafuna (kuwala vichwa) "wahamasikaji".

Awali ya yote, tujiulize ujasiriamali ni nini hasa, ? Je neno ujasiriamali ni sawa na neno la kiingereza la entrepreneurship kimaana? mbona nikigoogle picha za wajasiramali sioni majibu yanayofanana na nikigoogle neno entrepreneurs? Kwanini naona picha za wachuuzi, na washiriki wa maonesho ya juakali katika majibu ya picha google inayonipa? Mjasiriamali ni nani? Je ni yule anaeuza shanga za kimasai pale kariakoo? au ni mkulima wa nanasi pale kiwangwa? au ni vikundi vya kinamama wanaosindika pilipili na achali?

Kimsingi ujasiriamali katika dhana ya kiafrika umekuwa na maana tofauti kabisa na dhima halisia tasnia hii. Mjasiriamali wa kiafrica amekuwa ni mtu duni, mwenye uhitaji wa msaada baada ya yeye kuwa msaada wa kutatua changamoto zinazoikumba jamii yake. Ni mtu tegemezi anaetakiwa kuletewa fursa na miradi. Ni mtu asiekuwa na mipango na hili limepelekea wao kugeuzwa kuwa fursa na wachache (cannibals).

Hili linathibitishwa kwa uwepo wa taasisi nyingi zisizo za kiserikali kutunga miradi yenye dhima ya "(kusaidia....kuwezesha, kuhamasisha.....nk) vijana, wakulima au wajasiriamali. Tumeona wachache wanatumia ombwe hili kuwageuza fursa wahamasikaji hawa walio desperate na kujipatia fedha nyingi na kuwaacha kwenye hasara kubwa..

Mfano rejea mchakato wa kutugeuza mamilionea kupitia forex na q-net, tuko wapi sasa? wangapi tulihamasishwa na miradi ya sungura. tuko wapi sasa? wangapi tuliingia kwenye ufugaji wa samaki, tuko wapi sasa, wangapi waliweka kambi kwenye kilimo cha vitunguu Iringa tuko wapi sasa? wangapi tuliamasishwa kulima tikiti, tuko wapi sasa.? Tumeliwa kichwa.

Lakini je? wako wapi waliotuhamasisha tuingie huko? wao walifanya nini? utagundua waliofanya uhamasishaji huu wao walikuwa si wakulima, bali ni wasambazaji wa pembejeo na kutufanya sisi kama soko lao. Alieamasishwa kufuga kuku, aliamasishwa na mzalishhaji wa vifaranga. Alieamasika Kufuga samaki aliamasishwa na muuzaji wa vifaranga vya samaki.
Alietuhamasisha tufuge sungura, ndie alie tuuzia mbegu, alietujengea mabanda, na ndie alie tuuzia chakula, alietupa fursa ya forex ndie aliekuwa dalali wa malipo na mafunzo hapa nchini. mnyororo unaendelea...

Leo nitatoa mbinu chache zitumikazo wa wanaharakati wa ujasiriamali (Cannibals) kuwala vichwa wahamasikaji. Nawaita desperate pia kwa vile huingia katika hizi fursa bila kufanya tafiti za kutosha na kujiridhisha na kunasa katika mtego wa jini mla watu.

1. Creation imaginary demand.
Hii ni mbinu ya kutengeneza soko lisilo na uhalisia kupitia mitandao ya kijamii na kuacha ujumbe uende "viral". mfano, mkulima mmoja alifanikiwa kuja na mbegu ya kipekee kidogo ya sungura. Akaanza kufanya uzalishaji wa mbegu hii shambani kwake. Kupitia mitandao ya kijamii,aliandika anahitahi sungura 30000 kila wiki, kwani anasoko kubwa ndani na nje ya nchi kwa bei ya 8000 kwa kilo. mbegu elekezi ilikuwa na uwezo wa kufikia mpaka kilo 3. ujumbe wake ulienda viral kutokana na uhitaji aliouonesha na bei inayohamasisha.

watu wakaanza kutafuta sungura wa mbegu ile wakaikosa, ila wakaambiwa shamba fulani wanayo. shamba likawa linauza wale sungura wa mbegu kwa sh 70,000 kwa kila mmoja, na kuweka sharti ya kiwango cha chini ni kuwa na sungura waaa mbegu 6, mafundi wa shamba wawajengee wateja wao mabanda elekezi pamoja na wateja kulisha chakula kinachozaalishwa na shamba pekee kwani ndicho chenye ubora unaoendana na soko. Shamba lilitoa mkataba wa soko la uhakika wa sungura wote watakao zaliwa toka kwa wateja wao.

Watu wakahamasika, ma elfu wakaingia kwenye mradi wa sungura,soko la ssungura wa mbegu likawa halishikiki. Shamba ilichokuwa ikifanya ni wao kununua watoto wote sungura wote wa wateja wa mwanzo wenye uzani wa kilo 2 kwa 16,000 na kuwauza kwa wateja wapya kwa shilingi 70,000 kwa kuwaita ni sungura wa mbegu na kumuuzia chakula na kumjengea banda. Kilichokuja kutokea wote tunakikumbuka, walipoanza kusokena wateja wapya, shamba lilikosa mahali pakuwapeleka sungura wa wateja wao. walifunga shamba na kuingia mitini. lile soko lla sungura ndani na nje ya nchi kumbe halikuwepo, japo wafugaji ndio walikuwa soko bila kujijua. A dead man fell into the trap. Wahamasikaji wengi walianguka kwenye hili na hawataki kusikia habari za sungura tena.

2. Ujasiriamali kama sehemu ya uganga za jadi?
Ni ngumu sana kutofautisha biidhaa za wajasiriamali wetu na tiba asilia. Nimejaribu kupitia tag line za bidhaa za wenzetu mitandaoni. Tag line za wenzetu wa cocacola wanakuwambia tii kiu yako, onya msisimko, etc. bidhaa za wajasiriamali wa kiafrika ni lazma utasikia, kama ni msindikaji wa majani ya mchaichai, atakwambia inasaidia vidonda vyaa tumbo, kama ni mzalishaji wa mafuta, atakwambia inaondoa chunusi na madoa, kama ni unga wa lishe `watakwambbia unapunguza uwezekano wa magonjwa ya sukari. Kila bidhaa ya mjasiriamali tuizalishayo ni dawa. Sipingani na hoja ya swala la lishe kuwa ni muhimu kwa jamii yetu, ila ni vyema kuwa na mipaka kwani ili bidhaa ithibitike kuwa na tiba inabidi ipitishwa na mamlaka husika.

Kichaka hiki cha kutag bidhaa na dawa, imewaingiza hasara watu wengi sana kwa kujiingiza kwenye uzalishaji wa bidhaa hizi na mwisho wa siku wameeanguka kwa hasara kubwa. Nadhani tunakumbuka vyema swala la mayai ya kware kama tiba ya sukari, pressha na HIV, tunakumbuka kiwango gani tumekunywa na kuzalisha mafuta ya ubuyu...ilikuja kuaje sasa baada ya mamlaka kutangaza vinginevyo.?

3. Kutumia mwanya wa wananchi kutofanya tafiti..
Tunachangamoto ya wengi wetu kutofanya tafiti binafsi kabla ya kufanya uwekezaji. na mara chache inapotokea kufanya utafiti, wengi huangukia kuomba taarifa kutoka kwa wanaharakati wa ujasiriamali ambao lengo lao wao ni kukufanya mteja. wengi wetu tunaangukia kwa wadau ambao wanashamba darasa la papai, watakuhamasisha ulime papai ili wao wakuuzie miche. watatumia kila lugha kukuonesha papai inalipa. watakupa bei ya mauzo isio na uhalisia sokoni etc mwisho wa siku watakupotosha...ni vyema tuangalie upya namna ya kufanya tafiti ya soko na kubaini changamoto za uzalishaji toka kwenye mazingira halisi na si kwa muhamasishaji.

Kuna haja ya kubadilika, ujasiriamali wa kiafrika haunatofauti na ile dhana ya Charles Darwin Ya "survival of the fittest". You are the maker our your own destiny....ujasiriamali ni kama pori lenye wanyama wengi wakali na wewe ni swala.Inabidi umakini kuweza kusurvive. Na kwa wale walioanguka katika mitego hii, bado nafasi ipo ya kufanya vyema. in entrepreneurship, failure is inevitable, but its importnat to note....when you fail, make sure you fail quicky and cheaply....aluta continua....
 
Very true.....binafsi bila kufanya ka utafiti, huwa cna iman wala utayar wa kufanya maamuzi ya kuanza kinachohamasishwa
 
Well said..umakini unahitajika.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kweli tupu
 
Tatizo kubwa pia linatokana na watu kutaka mafanikio ya haraka. Wanapoona tu mtu mmoja amefanikiwa kupitia fursa flani bas wanakurupuka na wao kwa kutaka mafanikio kama yale. Mafanikio yanahitaji uwekeze kwenye muda na utafiti wa kina sio kukurupuka. So you are 100% correct.
 
Nawashukuru sana JF kwa hii platform napata madini ya kutosha kuwa mtu mpya kila nikitembelea ndani ya Jamii Forum.
 
Nakubar mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom