The Future of Freelance is BRIGHT and demand is increasing globally. Many talented professionals and businesses turn to this mode of work

$500 kwa mwezi huwezi tengeneza?

Haelewi sana huyo.

Binafsi baadhi ya miezi natengeneza hadi kufika $1,000.

Lazima uwe wa viwango vya juu ili uwe unapata gigs nyingi.

Kingine....kufanya kazi kama freelancer haimaanishi unategemea kazi katika hizi platform kama UpWork, Fiverr au Freelancer.com pekee.

Kuna mbinu nyingi zakufanya kazi kama freelancer.

Ukiwa na uelewa wa juu juu utataabika sana na kuona kila kitu kibaya.

Cheers
 
$500 kwa mwezi huwezi tengeneza?
Sio rahisi mkuu. Labda iwe ni kazi yako fulltime. Ili uweze kuingiza kiasi hicho cha pesa labda ufanye kazi 8 hours a day. Na kazi zile zinazohitaji skills kubwa. Watu wanaongelea urahisi sana kuhusu hizi freelancing lakini sio rahisi kihivyo.
 
Mbona maelezo yako hayajitoshelezi. Kwa nini usiweke wazi kazi zipi wewe unafanya ili kutengeneza hiyo $1000. Navyojua kuna bonus kama utatuma link na kushawishi watu kujiunga na hizo freelancing jobs. Ki ufupi kazi zake ni ngumu.

Na haina tofauti sana na networking market, yaani aliyeanza mapema na kushawishi wengine anakuwa na gawio zuri. Pia inafikia kipindi yule aliyeanza anakuwa kama mkaguzi wa kazi za wengine hii kidogo ina kipato.

Tuweke bayana mkuu. Sio kutueleza juu juu tu kama motivational speeker.
 
Mbona maelezo yako hayajitoshelezi. Kwa nini usiweke wazi kazi zipi wewe unafanya ili kutengeneza hiyo $1000. Navyojua kuna bonus kama utatuma link na kushawishi watu kujiunga na hizo freelancing jobs. Ki ufupi kazi zake ni ngumu. Na haina tofauti sana na networking market, yaani aliyeanza mapema na kushawishi wengine anakuwa na gawio zuri. Pia inafikia kipindi yule aliyeanza anakuwa kama mkaguzi wa kazi za wengine hii kidogo ina kipato.

Tuweke bayana mkuu. Sio kutueleza juu juu tu kama motivational speeker.

Mkuu ukiona wewe mbinu zako hazifanyi kazi usidhani wote wapo kama wewe.

Kama wewe huna personality nzuri + uwezo wa kushawishi utapata tabu sana kupata kazi kwenye platform hizi za freelance.

Mimi kazi zangu ni zakuwango cha juu na clients wanasema hivyo kwenye reviews.

Mimi nilisajili account UpWork nimefanya kazi miezi michache nikapata status ya UPWORK RISING TALENT badge.

Pia nimewahi kupata Top Rated badge.

Unafahamu umuhimu wa hizi badge?

Sasa wewe ukiandika proposal yako na na mimi nikaandika yakwangu + nina badge ya Top Rated lazima nitakushinda tu.

Inaonyesha huelewi jinsi hizi platforms zinavyofanya kazi.

Nikuulize umewahi kuudhuria hata webinar moja ya UpWork au platform yoyote unayotumia?

Je, wewe unatumia platform yoyote ya kulipia kupata kazi kama freelancer?

Unataka kufahamu ninapata vipi hizi $500+

1 • Ninafanya kazi kama Swahili copywriter kwenye kampuni ipo hapo Dar es Salaam na nilipata hii kazi baada ya kumuonyesha general manager wa hii start up kazi zangu za nilizofanya UpWork. Nikapiga Aptitude test nikapata hii kazi $300 - $450 kila mwezi.

2 • Ninafanya kazi for a very very long time kama Swahili Over the Phone interpreter na hii ni kazi ya kudumu na nilipata UpWork. Sipati sana $100 - $200 kwa mwezi. This is a very demanding job.

3 • Nafundisha kiswahili. Na unafahamu nimepata wapi hawa watu? UpWork. Kiasi gani kwa mwezi $300

Hizi ni kazi za KUDUMU si za kubahatisha. Ukijumlisha na gigs za muda mfupi napata zaidi ya hapo.

Sorry mkuu I’m not telling you this to brag.

Ni pesa ndogo tu hizo.

Mimi nafanya kazi nyingi hapa Arusha.

Nimeishi na white people nafahmau namna yaku win trust yao.

Ndiyo maana nimekwambia kama huna good personality utapata tabu sana kupata kazi kwenye hizi freelance platforms

Cheers
 
Mbona maelezo yako hayajitoshelezi. Kwa nini usiweke wazi kazi zipi wewe unafanya ili kutengeneza hiyo $1000. Navyojua kuna bonus kama utatuma link na kushawishi watu kujiunga na hizo freelancing jobs. Ki ufupi kazi zake ni ngumu. Na haina tofauti sana na networking market, yaani aliyeanza mapema na kushawishi wengine anakuwa na gawio zuri. Pia inafikia kipindi yule aliyeanza anakuwa kama mkaguzi wa kazi za wengine hii kidogo ina kipato.

Tuweke bayana mkuu. Sio kutueleza juu juu tu kama motivational speeker.

Uelewa wako kwenye haya mambo upo chini sana mkuu. I am sorry.

Hata huelewi jinsi referral program zinavyofanya kazi.

Ushauri wangu.

Usikate tamaa.

Unahitaji kujinoa zaidi.

Ili ufanikiwe sehemu yoyote ile lazima uwe mweledi.
 
Wabongo wengi ni waongo sina uhakika na ripoti zako mkuu
 
Wabongo wengi ni waongo sina uhakika na ripoti zako mkuu

Mkuu Internet ni gold mine.

Kuna opportunity nyingi kama unafahamu unachofanya.

Jifunze na si kuishia kusema “wabongo ni waongo”

Je, itakuwa rahisi?

Nop, utashindwa mara nyingi zaidi ya utakavyofanikiwa. Kumbuka hilo.

Lakini mwisho wa siku kutengeneza hizi $500 - $1,000 utafahamu ni kawaida tu.

Ona hapa...hii ni source nyingine tofauti na freelance work.

Hiyo pesa inaingia wakati wewe unasema “wabongo ni waongo”

Mimi ni mtu very very busy kusaka mapesa. Siachi hata shilingi kumi mezani.

IMG_3182.jpg
 
Wabongo wengi ni waongo sina uhakika na ripoti zako mkuu

Wewe bado ni “boy”

Ukiwa unaongea na kaka zako uwe na HESHIMA na HEKIMA

Ungekuwa karibu ningekupatia kibao cha uso halafu ningekupatia $40 upate hata pesa ya holidays maana najua umefulia.

Shenzi kabisa
 
Sio rahisi mkuu. Labda iwe ni kazi yako fulltime. Ili uweze kuingiza kiasi hicho cha pesa labda ufanye kazi 8 hours a day. Na kazi zile zinazohitaji skills kubwa. Watu wanaongelea urahisi sana kuhusu hizi freelancing lakini sio rahisi kihivyo.
Mtu akilipwa dola 20 kwa siku kwa mwezi ana dola 600,inawezekana mkuu watu wanapiga zaidi ya hiyo
 
Sio rahisi mkuu. Labda iwe ni kazi yako fulltime. Ili uweze kuingiza kiasi hicho cha pesa labda ufanye kazi 8 hours a day. Na kazi zile zinazohitaji skills kubwa. Watu wanaongelea urahisi sana kuhusu hizi freelancing lakini sio rahisi kihivyo.

1607242974965.png

Mkuu hii kitu inalipa kuliko kazi za watu wengi wanazolipwa huko makazini kwao. Hiyo project inafanyika week 2, lakini mimi uwa naweza fanya project yote siku moja ndani ya masaa mawili nikamaliza. Maana kukocoent na kuweka mifano tu.

Sasa hiyo ni kwa upande mmoja bado kuna project nyingine. Kwahiyo kukomaa ukatengeneza 1000 mpaka 2000 inawezekana. Mimi kuna mtu ninamfahamu yani nashindwa hata mkadilia anatengeneza kiasi gani kwa mwezi maana yeye daily kupokea dollar 100, 200 kawaida. Ila nasoma mbinu zake
 
Wabongo wengi ni waongo sina uhakika na ripoti zako mkuu
freeeln.jpg

Masasa mawili yaliyopita nimelipwa kiasi hicho actually inabidi anilipe jumla 280$ ya kazi ya wiki, ila kasha review kiasi hicho ndiyo kaachia alipo na ni kazi ya wiki na hapa anaongeza kazi ya wiki nyingine.

So si kwamba hailipi inalipa ila inabidi uwe kwenye your own lane, ujue wapi unafit siyo kisa umeona huyu anapata pesa huku nawe uvamie. Na hii ni sehemu moja nikianza kuonyesha kila ninacho earn kila eneo utashangaa
 
Mkuu mimi nimekuwa nikiitumia hii lakin kwa yule anaenza . Nilikuwa sifaham kama ukipewa project kuna pesa ambayo unaitoa then baadae wanasema wanairudisha.nkapatwa na wasiwasi kidogo imekaaje hii
 
Mkuu mimi nimekuwa nikiitumia hii lakin kwa yule anaenza . Nilikuwa sifaham kama ukipewa project kuna pesa ambayo unaitoa then baadae wanasema wanairudisha.nkapatwa na wasiwasi kidogo imekaaje hii
Kuwa makini hutakiwi utoe pesa yoyote.
 
Mkuu mimi nimekuwa nikiitumia hii lakin kwa yule anaenza . Nilikuwa sifaham kama ukipewa project kuna pesa ambayo unaitoa then baadae wanasema wanairudisha.nkapatwa na wasiwasi kidogo imekaaje hii
Ni Platform gani hiyo uliambiwa hayo mambo ya unatoa pesa halafu baadae wanairudisha?! Au sijakuelewa?!
 
Ni Platform gani hiyo uliambiwa hayo mambo ya unatoa pesa halafu baadae wanairudisha?! Au sijakuelewa?!
Hata freelancer gig nyingi unakuta kazi ndogo madola kibao.

Ukiichek akaunti imetengenezwa jana na location ni Nigeria.
 
Greetings JF massive!

Kama kawaida leo nimepata time nataka nikuonyeshe jinsi vile unavyoweza kufanya kazi kama Online Freelancer na kutengeneza kipato kizuri tu kwakutumia Skills ulizonazo + muda wako wa free.

Kama hufahamu kabisa freelance ni nini soma hapa Beginner Level : Je, Online Freelancing ni nini? Kazi zinatoka wapi? Ni Skills gani zinahitajika? Nitalipwaje pesa? Jifunze kila kitu hapa
Beginner Level : Je, Online Freelancing ni nini? Kazi zinatoka wapi? Ni Skills gani zinahitajika? Nitalipwaje pesa? Jifunze kila kitu hapa

Kwa wanaonifahamu wanajua nimeandika mambo mengi kuhusu Online Freelancing na vile nimekuwa nikionyesha kwa uwazi kabisa kazi ninazofanya na pia pesa ninazolipwa. Nasema hili kwasababu haitokuwa na maana kama nitajaribu kuwaelekeza wengine vitu nisivyovifanya. Mimi si guru. Mimi ni lifelong leaner na nimekuwa nikifanya vizuri Upwork kwa muda sasa.

Angalia hii screenshot.

View attachment 1592751

Ok,

Labda unaweza uliza kuwa Top Rated ni nini?

Maana yake UpWork wanatambua kazi nzuri ninazofanya. Na hiyo inamaanisha I will continue to land more offer and make more money.

Lakini si Upwork kama kampuni pekee inatambua kazi nzuri.

Hata clients wenyewe wanatoa maoni yao.

View attachment 1592752

Ok hiyo screenshot ya pili hapo juu ndiyo msingi wa hii sredi kwasababu kazi nimeipata hivi karibuni tu nikaona niwajulishe watu hapa inawezekana sana kutengeneza decent money tena kwa kazi moja tu.

Well, kwanza kabisa niseme ni rahisi sana kupata hizi pesa kama utakuwa unafanya kazi zako kwa quality ya juu na client kukukubali.

Hiyo kazi kwenye screenshot ni ya translation.

Nilifanya negotiations na client na ananilipa $20 kwa kila article moja nayofanyia translation. Kila mwezi nina articles 15.

Je, ninatumia saa ngapi kufanya kazi hizi?

Jibu ni saa 2 tu kila siku nimemaliza kila kitu.

Kwahiyo unaona natumia saa 2 * 15 (mara idadi ya articles) kutengeneza $300.

Kwa pesa ya Tz hiyo ni 700,000+

Pesa kama hizi natumia kulipia rent apartment ninayokaa hapa Arusha.

Kumbuka hii ni side hustle tu. Si kazi pekee nayotegemea.

Nipo na kazi nyingine nazotengeneza zaidi ya $300 kila mwezi.

Lengo ni kukuonyesha opportunity Online freelancing imetoa ili uweze kuongeza kipato.

Kwamfano Wewe ni mfanyakazi na jioni + weekends upo na muda mwingi wa free. Kwanini usiwe freelancer? Utengeneze pesa za ziada?

Kwasababu kila mtu anapenda kutengeneza pesa kwa muda wake wa free.

Kwasababu let say wewe ni muajiriwa baada ya makato ya mikopo unayobakiwa nayo ni Ts 900,000 sasa ukiwa na $400 unazozipata kwa kazi zako kama Freelancer hiyo ni kitu kizuri sana.

Kwahiyo kama ulikuwa hufahamu ni namna gani utajiongezea kipato basi Online Freelancing ni CHAGUO SAHIHI. Hands down. Ukijitaji nikupatie usaidizi wa aina yoyote ile just contact me.

Ngoja nikuonyeshe kazi nyingine nazoendelea nazo.

View attachment 1592753

Hiyo screenshot ya juu ni kazi ya sales.

Client alikuwa anatafuta sales representative from Tz atakayemsaidia kuuza e-commerce platform kwa wamiliki wa restaurants.

Sasa kila restaurant itakayokubali kutumia platform hii basi wewe utalipwa recurring income $18 kila mwezi.

Hiyo maana yake kama ukiweza kushawishi restaurants 50 basi hiyo ni $18 * 50 = $900

Na hizo pesa zitaingia kila mwezi bila wewe kuendelea kufanya kazi nyingine yoyote ile.

Hii ndiyo real passive income.

Na ndiyo maana nakomaa nayo.

View attachment 1592754

Hiyo screenshot ni kazi nimeshaifanya tayari.

Hii ilikuwa kazi ndogo $45.

Client alihitaji nimsaidie kufungua account ya AirBnB na kuweka kila kitu sawa.

Kwa wasiofahamu AirBnB ni nini nitaandikia uzi wake hapa JF.

Kazi nyingine nayoendelea kuifanya ni kufanya design za YouTube thumbnails.

View attachment 1592755

Hii kazi ilianza kama one time project lakini naona client ameamua kunipatia long term contract ya miezi 6+

Ninalipwa $10 kwa kila thumbnail moja ninayo-design.

Kazi nyingie ninazofanya ni kazi za Interpration na hii ni kazi nimekuwa nikifanya kwa miezi mingi. Hii kazi ya Interpretion inanipatia $150 kila wiki. $600 kila mwezi.

Ningependa niweke na screenshot yake but I need to go now.

Tuwasiliane makingmoneyonlinetz@gmail.com

Tukutane wakati mwingine.

Cheers
Nilikuwa natafuta kujua una lengo gani,kumbe unatafuta kazi nyingine ya kufundisha watu jinsi ya kupata online jobs.
 
Back
Top Bottom