The Fierce Urgency of Now: Tunahitaji vitendo sasa hivi na si kusubiri mpaka 2015! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The Fierce Urgency of Now: Tunahitaji vitendo sasa hivi na si kusubiri mpaka 2015!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Susuviri, Feb 27, 2011.

 1. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Naomba nianze kwa kumnukuu kinara wa haki za binadamu, mwanaharakati na shujaa Martin Luther King Jr:
  “We are faced with the fact, my friends, that tomorrow is today. We are confronted with the fierce urgency of now. In this unfolding conundrum of life and history there is such a thing as being too late. Procrastination is still the thief of time. Life often leaves us standing bare, naked and dejected with a lost opportunity. The ‘tide in the affairs of men’ does not remain at the flood; it ebbs. We may cry out desperately for time to pause in her passage, but time is deaf to every plea and rushes on. Over the bleached bones and jumbled residues of numerous civilizations are written the pathetic words: ‘Too late.’ “

  Mi naomba niwapatie kwa kifupi maelezo ya kwa nini sisi watanzania hatuna budi kushughulikia janga hili la taifa linalotukumba kiuchumi, kisiasa na kijamii

  1. 'It's the economy, stupid!' Hii ilikuwa ni slogan ya Bill Clinton alipokuwa anachuana katika uchaguzi mkuu wa rais na George Bush senior mwaka 1992. Hii ilikuwa ni njia ya kuwashtua wananchi wa Marekani kuwa uchumi wao ni muhimu na ni vyema wakiipa kipaumbele kwani chini ya miaka 8 ya Reagan na 4 ya Bush senior, uchumi wa nchi uliyumba. Je hii inahusika vipi na tanzania?
  Nadhani sina haja kuwaeleza kwa kiina matatizo ya kiuchumi tunayoyaona nchini ikiwa ni pamoja na: serikali kushindwa kulipa kwa muda na kikamilifu watumishi wake; madeni ya serikali kuongeza hususan madeni kwa wakandarasi, na wadeni wengine wa nje na ndani; kupanda kwa bei ya bidhaa mbalimbali na kuongezeka kwa gharama ya maisha kwa wananchi wote;
  Hivi sasa tunasikia kuwa serikali imeomba pesa ya dharura kutoka wahisani kwani inaonekana tusipopatiwa msaada shughuli zote za serikali na za kitaifa zitasimama kwani bajeti iliyopangwa haitimii. Sasa tukumbuke ya kuwa mwaka 2005 tulikuwa tuna akiba ya mabilioni (USD) hivi sasa akiba yetu ni 3.9 bilion USD ambayo inatutosha kwa miezi 6 tu.
  2. Misukosuko ya kijamii: matatizo haya tunayaona katika kuongezeka kwa udini ambayo wengi wanadai kuwa si tatizo halisi bali inakuzwa na watawala. hata hivyo tumeshaanza kushuhudia dini kupigana na uharibifu wa mali. Hii ni hali hatari na inaonyesha kuwa tusipoziba ufa sasa hivi tutajenga ukuta mwaka 2015!
  3. Matatizo ya kisiasa: hii ni pamoja na JK kukosa uhalali au legitimacy wa kutawala kutokana na uchakachuaji alioufanya na washirika wake. Hali hii inachangiwa na ukweli kuwa hata wanajeshi walimpigia kura kwa idadi kubwa Dr Slaa na mpaka sasa wananchi wengi bado wanasubiri kusikia Dr Slaa anasema nini na kumwona kama ndiye rais wao wa kweli au wanasema 'rais wa moyoni'. Suala hili ni lazima tulikubali kuwa lipo na tusitake kuipuuza hata kama wapo wanaoamini kuwa JK alishinda kihalali. Lakini zaidi ya hayo pia kuna suala la JK kukosa mwongozo na hivyo kubaki kuwa mtazamaji na siyo kiongozi wa kweli, mfano mzuri ni milipuko ya Gongo la Mboto ambapo ameonekana kuongelea juu juu suala hili na hata kabla wananchi hawajazika alikimbilia nchi za nje. Kiongozi huyu pia ameshindwa kutoa tamko la uhakika kuhusu matatizo mengine mengi ambayo naomba niwaachie myaorodheshe ikiwa ni pamoja na suala la nyongeza ya mshahara; ukosefu wa nidhamu jeshini; kampuni ya ufuaji wa umeme Dowans; nk

  Kama hitimisho naomba turudi hapo juu na kusoma upya maneno ya Martin Luther King Jr na kuiweka katika context ya sasa ya nchi yetu na tuseme kuwa sasa hivi ni muda wa kuweka pembeni chuki zetu binafsi, uhasama wa siasa, udini na ukabila, - TUKO KATIKA HALI MBAYA!
  Ila inaonekana kuwa hii failed state inaendelea kuwepo kwa kuwa wapo wenye maslahi yao wanaosukuma gurudumu kwani katikati ya hali hii wao wanaendelea kufaidika. Hata hivyo sisi kama watanzania inabidi tuungane na tuchukue hatua mapema na tulete mabadiliko na turekebishe hali hii.
  Njia pekee ni kumwomba Kikwete na chama chake wapumzike kwanza ili hali irudi kuwa ya kawaida. Hivyo basi hatuna muda tena wa kupoteza na kusema eti tunasubiri 2015 kwa sababu by then tutakuja kutimiza yale anayotuonya Martin Luther King: "Over the bleached bones and jumbled residues of numerous civilizations are written the pathetic words: ‘Too late.’"

  Ninakaribisha michango kutoka wanaJF wenzangu na niko tayari kupata mawazo yetu kwamba nini kifanyike kama wapo ambao wanaona maandamano na nguvu ya umma si njia sahihi. Ila naomba jibu lisiwe kusubiri mpaka uchaguzi ujao mwaka 2015, maana haileti maana kwa mantiki hii.
   
 2. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  You said it all!
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,599
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  we need initiator! time is up
   
 4. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  indeed we need change, and it has to be real change. Just hoping that we are not replacing the devel by another devel in a new outfit!
   
 5. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Unajua mkuu siku zote huwa nasema kuwa hata kama tutachagua bomu wacha tufanye makosa lakini ni makosa tuliyochagua sisi wenyewe kwa hiari. Lakini naamini kuwa watanzania tumepewa busara nyingi na Mwalimu Nyerere na pamoja na mapungufu yake, Mwalimu Nyerere alikuwa philosopher kama Martin Luther King na alituachia mwongozo mzuri kwamba nchi yetu inatakiwa iweje (nchi inayoheshimu dini na kabila y akila moja, yenye common identity) na pia uongozi gani unatakiwa. Kutokana na background hii, mi naamini tutambua mapema makosa yetu katika siku zijazo.
  Tatizo tuliyokuwa nayo sasa hivi ni kuwa bado wapo wanaodhani kuwa CCM ya sasa ni ile ya Nyerere na kumbukeni kuna generation iliyokua bila kujua uongozi mwingine isipokuwa ule wa CCM. Lakini pia vijana haohao wananipa matumaini kwani wanaonekana kutaka mabadiliko!
   
 6. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na wewe na sidhani kama ni wakati wa kusubiri Chadema au chama tu cha siasa kituongoze peke yao, bali inatakiwa sisi wananchi pia tujisukume na kuleta mabadiliko. Tatizo kutokana na mfumo huu tumekuwa suspicious of people and causes! Lakini nafikiri hatuna muda wa kupoteza, hivi sasa mtu yoyote anaetaka kuleta mabadiliko tuungane nao, tutakuja kuchambua baadae motives.
   
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kujikusanya kama ngogwe sio sahihi kwani ,kuna taratibu za kufuatwa,mfano uchapishaji ,na matangazo ambayo yanahitajika kuenezwa kama vumbi la jangwani ,na mfano unaweza kupanda daladala na kugawa karatasi za kuonyesha ukandamizaji uliojaa nchini ,na si lazima uandike makaratasi kibao,ni ujumbe mdogo tu pengine karatasi za bundle moja ya A4 na sio lazima kugawa hata kuzimwaga kariakoo au kuziweka nje ya msikiti au kanisa ,anaetoka anaokota halikadhalika kubandika kwenye magari au mabasi ,unajua basi linaelekea Mtwara unaikandamiza kwa super glue mradi unakuwa na tahadhari ,sehemu ambazo watu wanakatiza kwa wingi unaweza kubandika ,just unaanzia kwa kuandika,,,Wakati wa kujikomboa na makucha ya CCM ni huu ,hii inakuwa ni kampeni ,halafu unaongezea kwa kumalizia ,mimi nipo tayari je wewe ?
   
 8. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Mkuu Mwiba, mi naona wazo lako ni nzuri ajabu na ni rahisi sana kutekeleza. Maneno na maudhui ya kuweka katika makabrasha haya yanaweza kuandikwa humuhumu na kila mtu anaprint na kusambaza kivyake. Mpaka kesho tuweke mapendekezo hapa, mimi nitaanza nasubiri wenzangu tuugane. Hata kama uko nje ya nchi unaweza kuchangia kimawazo.
   
 9. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,959
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  Du hili jukwaa lingefikia hata 50% ya waTZ ya Misri yangetokea. Mkuu uko juu
   
 10. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #10
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Mkuu Nyakageni, tusaidie kuwafikia watanzania wengine, tusambaze ujumbe kupitia njia mbalimbali. Pamoja tutafikia malengo yetu kuwa nchi huru na uhuru wa kweli!
   
 11. n

  niweze JF-Expert Member

  #11
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  This is well said article. Thanks so much for clear elaboration of Tanzania current status. Watanzania haya majonzi na maumivu tunayoyapata hivi leo kwa kila familia in exception to viongozi wa ccm ni lazima tuyashughulikie sasa na sio kusubiri five years from now. Tukiangalia swala la uchumi, hakuna hata hatua yeyote ile tumesikia wanajua au waliofanya kuongeza ajira au kushughulikia hizi investments za migodi na vitu vingine viwe really profitable to Tanzanians. Hakuna efforts zozote zile kuleta "transparency" katika uendeshaji wa shughuli za serikali (serikali ya wananchi). Tangu lini tumeona discussions za policies zinazowahusu Watanzania zikiwa zinajadiliwa mbele ya wananchi au na wananchi wenyewe. Even decisions to allow investments bids for the governments (Tanzanians Assets), ccm is keeping out the Tanzanians. What kind of leadership allows its people to suffer and profit from it? (answer is none -except to Gadhaff and Mubarak)

  Viongozi wa upinzani na wananchi wanapigania "katiba" na mpaka sasa tunaona wazi Kikwete anataka kulikumbatia na kutueleza wananchi kwamba yeye ndie mtanzania pekee anaweza kubadilisha na kuandika katiba. Vitu gani hatuoni kwamba huyu si kiongozi wawatanzania? Kiongozi gani hata kama aliiba anaweza kufanya decisions za kinyama kuleta makampuni kama "downs" au "Richmond" au kuendesha watanzania kama wasio na akili? Hili swala la "Gongo la Mboto" au hapo nyuma "Mbagala" linatia hasira na kuumiza sana taifa letu. Kitu gani tuseme kuhusu Kikwete au lugha gani tutumie? Mbagala wamekufa wananchi na hii sio mara ya kwanza kupatwa na mauaji kama haya. Ripoti na uchunguzi kuhusu hili swala vinakwenda ofisi ya raisi na Kikwete anakaa navyo. Kinachomfanya yeye so special na kutopeleka kwa wananchi au discussion za bunge nini? Hili sio swala la kwanza kwa Kikwete kuweka ofisini kwake. Tunakumbuka List ya mafisadi na wafanya biashara ya madawa ya kulevya? Tumeona impacts yake? Mataifa mengine kiongozi kama Kikwete either yupo jela na ameshafukuzwa zamani sana, lakini cha kusikitisha tunachukua muda mrefu sana kumwondoa.

  ]Matokeo na Majanga Yalioletwa na CCM Itatuchukua Miaka 50 Kuyatatua. Tusisubiri na Nina Uhakika
  Mwezi Umebaki
   
 12. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #12
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kabisa coz people are ready since yesterday!
   
 13. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #13
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Mkuu Niweze, nashukuru sana kwa mchango wako kwani umedhihirisha uzalendo wako. Naamini watanzania wengi tuna uchungu na nchi yetu na tunajiuliza tufanye nini. Ni kweli itachukua miongo kadhaa kurkebisha lakini ni lazima tuanze mapema. Tuendelee kutoa mawazo na hatimaye tutakuwa na action plan.

  Mkuu RealMan, hata mi naamini watanzania tuko tayari kupokea mabadiliko!
   
Loading...