'The Economist' Takes Gloves off on Kikwete...

Rais aliingia kwa mbwembwe nyiingi lakini hakuna kilichotokea. Assessment ya 'the economist' ni sahihi kabisa. Hakuna uzushi wala kusingiziwa. Inawezekana Kikwete was promising kabla hajaingia na alionekana kama mtu ambaye angeweza kuleta mabadiliko. Bahati mbaya in terms of kuleta mabadiliko he has been worse than Mkapa, yes worse Mkapa.

Mifano iko kila mahali. Hakuna sehemu ambapo unaweza kusema efficiency ime-ongezeka. Kote kumevurugika na kuzidi kuharibika. Mifano michache hapa chini;

1/ Aliingia akiahidi kupunguza bei ya umeme. Lakini tokea alipoingia TANESCO imekuwa chafu zaidi. Rushwa za maofisa wa Tanesco kwa walalahoi wanaotaka umeme zinazidi kushamiri kila mahali. Tanesco yenyewe na wizara ya madini na nishati zimezidi kuchafuliwa na misururu ya scandals.

2/ Bandari ya Dar es Salaam inaweza kuwa one of the best economic tools kwa Tanzania yenye mipaka na nchi 6 ambazo ni landlocked (Eastern congo is like another landlocked country). Lakini mismanagement ya bandari imeendelea na performance is so poor, wizi wa mizigo (vifaa vya magari, n.k.) unaendelea kama ilivyokuwa miaka kumi iliyopita, uzembe na uvivu kila mahali, you only see mismanagement everywhere. Hakuna improvement yoyote kwenye bandari despite president kwenda pale on a number of occasion. Anachofanya ni kulalamika kama watanzania wengine tunavyolalamika.

3/TRA inakusanya kodi nyingi zaidi. Lakini rushwa na uzembe, wizi na form nyingine za corruption bado ni hallmark ya hawa watoza ushuru wa Tanzania. Rais Kikwete hajarekebisha chochote alichokikuta. Miradi yote ni ile iliyokuwa inaendelea toka enzi za Mkapa. Hapa hakuna improvement yoyote.

4/Matumizi mabaya serikalini. Serikali inaendelea kuongoza kwa kutofuata sheria za kodi. Maofisa wengi wa serikali na Taasisi zake wanaendelea kulipwa malipo mengi yasiyokuwa na msingi wowote na hayakatiwi kodi. Ofisa wa serikali anasafiri analipwa posho yote, bado analipiwa hoteli (full board), nk. Maofisa wakubwa wengi wa serikalini hukaa maofisini mwao less than 25% of the time, muda wote wako safarini, na safari zingine zina overlap, lakini zote wanalipiwa posho na marupurupu. Vikao vinavyofanyika maofisini wanalipwa posho nono nono za vikao ambazo hazikatwi kodi!!! Kwenye sekta binafsi malipo yote kwa wafanyakazi ni lazima yapitie kwenye payroll na TRA is always terrorizing entrepreneurs na milolongo ya kodi zisizo na kichwa wala miguu. Kikwete hajarekebisha chochote hapa.

5/Mashirika ya umma yaliyorithiwa: TTCL sasa hivi inaandaliwa kufirisika ili iuzwe bure (kumbuka wakati wa mkapa jinsi NBC ilivyoandaliwa kuuzwa bure). Serikali imeendelea kung'ang'ania mkataba mbovu kati ya TTCL na Celtel international ambao unaifanya TTCL iendelee kuwa mateka wa mshindani wake (Zain) na hivyo kushindwa kuimplement chochote kinachoeleweka na kuelekea kwenye kufilisika. Kikwete aliingia kwa ahadi ya kurekebisha lakini hakuna kilichorekebishwa na maisha yanaendelea as usual. Kinachoendelea ndani ya mashirika mengine yote ya umma makubwa; TRL, TANESCO, ATC, Bandari, etc. ni upuuzi ule ule. No change, ni kama hakuna serikali mpya iliyoingia madarakani.

6/Perfomance ya wizara kama utalii (TANAPA), Wizi wa magogo, vitalu vya uwindaji etc.....etc. Wizara ya Ardhi imerudi kwenye uozo wake wa zamani uzembe katika allocation ya viwanja, rushwa, utapeli na kila kitu vinaendelea. Ni wizara gani unaweza kusema imerekebisha mambo na ni more efficient?? Angalia mradi wa vitambulisho na jinsi ulivyokuwa embroilled katika scandals ambazo hazieleweki!!!! Where is efficiency ndani ya serikali?? Wapi kumebadilika?

Toka kuwe na presidential term limits inaonekana marais wote walijitahidi miaka mitano ya kwanza. Ile ya pili ikawa disaster. Kumbuka Mzee ruksa aliingia na fagio la chuma (kuleta efficiency serikalini), miaka mitano ya mwisho was full of scandals.

Mkapa miaka yake mitano alileta matumaini kwenye kudhibiti matumizi ya fedha na ukusanyaji wa kodi. Lakini miaka mitano ya mwisho was full of scandals za corruptions etc.

Sasa Kikwete on first 5 years hali imekuwa hivi. Miaka mitano ya mwisho itakuwaje??? Ni kweli kama wanavyosema economist atachaguliwa tu. Lakini ujue hiyo miaka mitano ataitumia kujenga network ya watakaomlinda atakapoondoka. kama hajafanya kitu sasa forget baadaye!!
 
Fundi Mchundo kila kitu kimeelezwa kwa kina. Takwimu zimetolewa. Mwelekeo upo. Tatizo ni je huo mwelekeo ni wa kwenda wapi - Egalite au Eliteville?

Hiki ndicho unachozungumzia?

Elimu
58. CCM katika kipindi cha 2005-2010 itazielekeza Serikali kuendelea kushirikiana na wahisani, mashirika ya dini, sekta binafsi na wananchi kwa jumla katika kuimarisha elimu katika ngazi mbali mbali.
Elimu ya Awali
59. Lengo la CCM kwa kipindi cha 2005-2010 ni kuongeza kasi ya upanuzi wa elimu ya awali kwa kuhamasisha sekta binafsi na kuhakikisha kwamba sera ya kila shule ya msingi kuwa na darasa la elimu ya awali inatekelezwa ipasavyo.
Elimu ya Msingi
60. Baada ya mafanikio makubwa yaliyopatikana katika utekelezaji wa MMEM, CCM katika kipindi cha 2005-2010 itazielekeza Serikali kuchukua hatua zifuatazo:-
(a) Kuongeza kiwango cha ubora wa elimu.
(b) Kuweka msukumo maalum wa uandikishaji wa watoto wote wa rika lengwa la watoto wa umri wa miaka 7-13 (NER) katika ngazi ya elimu ya msingi kufikia asilimia 100 mwaka 2010. Aidha, kuongeza uandikishaji wa watoto wenye ulemavu na wengine wenye matatizo maalumu.
(c) Kuendelea kujenga na kupanua miundombinu ikiwa ni pamoja na nyumba za walimu, madarasa, vyoo na huduma zinazohusika.
(d) Kuendelea kuhakikisha kwamba maslahi ya walimu yanaboreshwa na kulipwa kwa wakati.
(e) Kuendelea kuimarisha ukaguzi wa shule ili kuimarisha ubora wa elimu.
(f) Kuongeza idadi ya wanafunzi watakaoendelea na elimu ya sekondari kufikia asilimia 50 ya watahiniwa wa Darasa la Saba ifikapo mwaka 2010.

Imetoka:Chama Cha Mapinduzi - CCM - Ilani

Wapi wanazungumzia namna gani wataweza kuandikisha asilimia 100 ya watoto katika elimu ya NER ifikapo mwaka kesho?
Wapi wamezungumzia quality ya elimu na namna ya kuiboresha? Wapi wamezungumzia wataongezaje maslahi ya walimu na namna uchumi wetu utakavyoweza kugharimia?
Hata hayo maslahi hawajaelezea? Kama ni mshahara kutoka wapi kwenda wapi? kama ni makazi, ni makazi ya aina gani?
Na wapi wameongelea checkpoints za kuhakikisha yote haya yanafanikiwa?
Reviews za mpango zitafanyika wakati gani. Tunajua maendeleo ya elimu katika nchi yetu hayako sawasawa.
Ni wapi wameongelea ni sehemu zipi ziko nyuma na jitihada gani zitafanyika kuwakwamua?
Wanaongelea kuongeza uandikishaji wa watoto wenye ulemavu n.k. Wapi wameelezea mahitaji halisi ya watoto hao na ni juhudi gani zitafanywa kuhakikisha kuwa wanaweza kutumia madarasa yetu kama wanafunzi wengine? Na kadhalika , na kadhalika!

Na hii ni kwenye elimu tu? Huko kwengine si itakuwa balaa!

Najua hii ni ilani ya Chama na si serikali na pengine maswali yangu yangeelekezwa kwa serikali. Haya, serikali imeonyesha wapi namna itakavyotekeleza hii ilani? Kwa maneno mengine, majibu ya maswali yangu yanaweza kupatikana wapi?
 
Mwisho wetu ni mbaya kabisa tunakokwenda. Waliopigania uhuru walitumai leo hii 2009 tungekuwa mbali kimaendeleo, lakini tuko vibaya. Naamini tunakokwenda ni kubaya zaidi.
 
... even disturbing, is the fact that some prominent Wabunge are pushing ahead for remuneration hikes!!

... haki ya nani tena miaka thelathini ya CCM ni ya kuwekewa kikomo! Liwalo na liwe!
 
The Economist wamemaliza kila kitu. Matatizo yanayotutatiza yanajulikana, njia za kuyatatua zipo, kwa nini hayatatuliwi ? Hili gazeti ni very reliable on economic issues.Jirani zetu wakiandikwa possitively on economic issues inabidi tushtuke. What is wrong with Tanzania?
KUna matatizo mengi lakini kubwa ni kuwa hatujui hasa ni mfumo gani wa uchumi tunaoufuata. Katiba inasema tanzania inafuata mfumo wa ujamaa na kujitegemea, in the reality, mambo si hayo.
tatizo jingine ni kuwa tunashindwa kutengenisha kati ya siasa na uchumi. Wenzetu wanasifiwa kwa sababu kwanza wanajua wanafuata mfumo gani wa uchumi na wanapoamua kufanya mambo ya kiuchumi wanayafanya professionally na kuachana kabisa na siasa (ingawa wapo opportunist wachache wanao-take advantage ya situations fulani kujinufaisha). hapa kwetu, siasa ni uchumi na uchi=umi ni siasa, unadhani tutafika hivyo kweli???
 
Miafrika Miafrika Miafrika Ndivyo Tulivyo!! And deep down in your heart of hearts, you all know it's true.
 
Kenya, Uganda, Botswana, Rwanda... ndivyo isivyo?

Kwa taarifa yako, hao Kenya, Uganda, Botswana, Rwanda hawajatuzidi kihivyo. Nymba za udongo kila kona. Lishe duni. Rushwa kama kawa. Ukabila na mengineyo mengi. Kwa ujumla hali za nchi nyingi za Kiafrika kusini mwa jangwa la Sahara ziko similar. Kwa hiyo kujibu swali lako, hao iliowataja na wenyewe Ndivyo Walivyo
 
... even disturbing, is the fact that some prominent Wabunge are pushing ahead for remuneration hikes!!

... haki ya nani tena miaka thelathini ya CCM ni ya kuwekewa kikomo! Liwalo na liwe!

SteveD:

Ukweli wa mambo ni kuwa watanzania hatutaki kuukubali ukweli. Shughuli zote ambazo zingefanya kipindi hiki cha JK kiwe na maendeleo zilitakiwa kuwa na misingi ya miaka zaidi ya 30 iliyopita.

Technocrats waliopo Kenya au Uganda hawakwenda shule jana. Ni watu wenye zaidi ya miaka 45.

Hivi miaka yote toka tumepata uhuru tunafanya nini ???
 
I wonder what the president reads, if he reads that is. Hints zote hizi hapati message, I expected him to do something after Bob Geldof "unceremoniously" gave him hints at the IMF meting earlier this year. Does ikulu subscribe to any intellectual publications?
 
Viongozi tulionao hawako kwa ajili ya masilahi ya Taifa ila kwa ajili ya manufaa binafsi. Kwa ujumla kila kiongozi anaeingia madarakani kuanzia Rais hadi wale wa kada ya chini wamejawa na ubinafsi zaidi na hawana ile roho ya utaifa.

Angalia JK alivyoingia madarakani anataka kila kitu kibadilike; mathalani anataka bandari na uwanja wa ndege wa kisasa ujengwe Bagamoyo, makao makuu ya mkoa wa Pwani yahamie Chalinze, kijiji kikubwa na cha kisasa kiwe nyumbani kwake Msoga, barabara kuu ya kwenda mikoa ya kaskazini na nchi jirani ipitie Bagamoyo na mengineyo.

Swali la kujiuliza ni je! kama Taifa hatuna mambo ya kipaumbele?, hatuna mipango ya kitaifa ya muda mfupi na mrefu bila kujali ni chama gani ama kiongozi gani aliye madarakani?, kwa udogo wa uchumi/ama kwa kutegemea fedha za misaada tutaweza kujikwamua kutoka kwenye hali tuliyo nayo kama kila chama ama rais atakayeingia madarakani atapanga ama kuamua mambo yake yanayohusu uchumi wa Taifa jinsi atakavyo, ni lini miradi ama mipango tuliyonayo itakamilika?.

Mkapa aliweka mkazo kwenye barabara na akafanikiwa kujenga barabara ya Lindi - Mtwara, Lowasa aliweka mkazo kwenye elimu, Pinda yeye mapambano yake kwenye kilimo hususani ununuzi wa matrekta, akija WM mwingine atakuwa na msimamo wake, madarasa/shule za Lowasa kwa sasa hazina waalimu wala vifaa vinavyotakiwa kufanya hadhi ya shule ionekane. Leo tunaambiwa Tanzania ni kisiwa cha amani lakini wataalamu wanatuambia kupitia tafiti zao kuwa Tanzania ni moja ya nchi ambazo zina mazingira ambayo sio mazuri kwa kufanya biashara/uwekezaji ikiwa ni nchi ya 127 kati ya nchi 181 kwa mwaka 2009 ilhal mwaka 2008 ilikuwa nchi ya 124 hivyo tunazidi kudorora badala ya kuboresha.

Tunahitaji kizazi ambacho kiko serious na nchi yetu na ambacho kina dhamira ya dhati ya kuleta mabadiliko vinginevyo tuwe tayari kukabiliana na hali mbaya kila uchwao.
 
Kwa taarifa yako, hao Kenya, Uganda, Botswana, Rwanda hawajatuzidi kihivyo. Nymba za udongo kila kona. Lishe duni. Rushwa kama kawa. Ukabila na mengineyo mengi. Kwa ujumla hali za nchi nyingi za Kiafrika kusini mwa jangwa la Sahara ziko similar. Kwa hiyo kujibu swali lako, hao iliowataja na wenyewe Ndivyo Walivyo

...sawa Ngabu, jibu linatosheleza kiasi.

... lakini kama hawajatuzidi kihivyo, unakubali kuwa kuna ka-difference walau kadogo? Kanatokana na nini?

... kama unakubali kuna ka-difference, je kanabakia constant; ya kwamba -hakabadiliki (kuweza kupungua au kuongezeka) for good or worse? Can we ever build on that?
 
Ninafurahi kwamba watu wengi tunakubaliana na hii article. Ingekuwa miaka michache iliyopita tungesema hao ni mabeberu wanaoiangalia nchi yetu kwa jicho la husda. But i wonder what our decision makers think when they read news articles like this !! Wanaweza kuibuka na kusema gazeti hili linaharibu umoja na mshikamano.
 
Tusiwalaumu viongozi. Tujilaumu wenyewe kwa kuwarudisha madarakani kila chaguzi.

Wewe huoni hata huyo mwandishi wa hiyo makala kasema karibu kwa uhakika kuwa Kikwete atachaguliwa tena kuwa raisi? Viongozi wetu ni reflection yetu sisi wenyewe wananchi.
 
Tusiwalaumu viongozi. Tujilaumu wenyewe kwa kuwarudisha madarakani kila chaguzi.

Wewe huoni hata huyo mwandishi wa hiyo makala kasema karibu kwa uhakika kuwa Kikwete atachaguliwa tena kuwa raisi? Viongozi wetu ni reflection yetu sisi wenyewe wananchi.

NN,
Ukisoma mstari wa mwisho utanipata kwa undani zaidi.
 
Tusiwalaumu viongozi. Tujilaumu wenyewe kwa kuwarudisha madarakani kila chaguzi.

Wewe huoni hata huyo mwandishi wa hiyo makala kasema karibu kwa uhakika kuwa Kikwete atachaguliwa tena kuwa raisi? Viongozi wetu ni reflection yetu sisi wenyewe wananchi.

... Ngabu, Viongozi kwa namna moja ni kama walimu madarasani.

... Ukitokea kuwa mwanafunzi katika darasa la mwalimu mpenda maendeleo, ni dhahiri kuwa ataonesha mfano na kuwa chachu ya kukua kifikra za maendeleo kwa wanafunzi wake.

... Ndiyo viongozi tunawachagua. Tunawachagua tukiamini kuwa wako bold na capable enough kuweza kutuletea chachu za maendeleo. Kama wako sawa nasisi na wanahaki sawa na sisi katika maamuzi yao, basi hakuna haja ya kuwa na viongozi, maana yale wawezayo kuyafanya kama moja ya mandate zao hazitakuwa tofauti na sisi tusioviongozi.
 
...sawa Ngabu, jibu linatosheleza kiasi.

... lakini kama hawajatuzidi kihivyo, unakubali kuwa kuna ka-difference walau kadogo? Kanatokana na nini?

... kama unakubali kuna ka-difference, je kanabakia constant; ya kwamba -hakabadiliki (kuweza kupungua au kuongezeka) for good or worse? Can we ever build on that?

Kwa kweli hako ka difference mimi sikaoni. Kila kukicha wananchi wengi tu wa hizo nchi ulizozirejea wanajilipua majuu. Baadhi (some) ya ulizozitaja wana ukabila unaozidi wa kwetu. Hao Waganda wana li dikteta Li Museveni. Hao Wakenya hawana lolote...kiasi kikubwa cha miundombinu yao wamerithi kutoka kwa waliowatawala (Waingereza) kwa sababu watawala wao walijipa kutawala Kenya kwa miaka 999 (kama unakumbuka vizuri historia). Kwa hiyo Waingereza thought they were there to stay so they had to fix up the place...

Kwa hiyo tofauti zilizopo kwa kweli ni ndogo sana kiasi cha kutoleta tofauti yoyote ile. Huwezi kunitoa Tanzania na kunipeleka eti Kenya au Rwanda kwa sababu huko kuna fursa bwelele za mimi kufanikiwa.
 
Kwa taarifa yako, hao Kenya, Uganda, Botswana, Rwanda hawajatuzidi kihivyo.
Jidanganyane hivyo hivyo na ndio mnaomdanganya raisi wenu......Rwanda umefika kijana? nyie watz endelezi malumbano ya mengi na rostam wenzenu wanapiga hatua......

.....na huyo raisi wenu mwambieni ajionee aibu na familia yake..
 
Kwa kweli hako ka difference mimi sikaoni. Kila kukicha wananchi wengi tu wa hizo nchi ulizozirejea wanajilipua majuu. Baadhi (some) ya ulizozitaja wana ukabila unaozidi wa kwetu. Hao Waganda wana li dikteta Li Museveni. Hao Wakenya hawana lolote...kiasi kikubwa cha miundombinu yao wamerithi kutoka kwa waliowatawala (Waingereza) kwa sababu watawala wao walijipa kutawala Kenya kwa miaka 999 (kama unakumbuka vizuri historia). Kwa hiyo Waingereza thought they were there to stay so they had to fix up the place...

Kwa hiyo tofauti zilizopo kwa kweli ni ndogo sana kiasi cha kutoleta tofauti yoyote ile. Huwezi kunitoa Tanzania na kunipeleka eti Kenya au Rwanda kwa sababu huko kuna fursa bwelele za mimi kufanikiwa.

...can you ever buid on difference, should you know that there is? The Economist is reporting on that little difference... kama unanipata Ngabu.
 
Back
Top Bottom