The Economist na Mauongo Yao Kuihusu Tanzania: Waidanganya Dunia Tuna Torture Wakimbizi! Wanapata Faida Gani? Kwanini Tunanyamazia Uongo Huu?

Mkuu Chige, kwenye Refugee & Migration Law kuna kitu kinaitwa The Principle of Non-Refoulment, ambacho kinatakaza kwa namna yoyote ile serikali kuwarudisha kwa lazima wakimbizi ndani ya nchi ambayo wanaweza kupata mateso (Persecution) au kuuwawa. Tanzania imevunja sana hii kanuni dhidi ya wakimbizi tangu kipindi cha Mzee Mkapa.

Miaka ya 90 alikuja Raisi wa Burundi akafika hadi kwenye makambi ya wakimbizi na kuwahakikishia kwamba Burundi ni shwari na warudi. Lakini walivyorudi tu wakakutana na mtutu wa bunduki, maelfu na maelfu ya wakimbizi waliuwawa na serikali ya Tanzania ikajifanya haifahamu chochote kile.

Sasa tukija kwenye hilo lako, ni heri polisi kukutana nao ni ngumu: Wale majamaa wa Uhamiaji wamepewa nguvu kubwa ambayo wanaitumia vibaya hasa kufanya vitendo vya rushwa dhidi ya wakimbizi. Kibaya zaidi wanashindwa kufahamu tofauti kati ya Mhamiaji Haramu (Illegal Immigrant) na Mkimbizi (A Refugee/Asylum Seeker), wenyewe wakikukamata wanafanya kitu kinaitwa A Transfer of Burden of Proof ambapo wewe ndiyo unatakiwa ujitetee kwamba ni Mtanzania, Mhamiaji haramu au Mkimbizi na ukishindwa basi inakula kwako.

Sheria ya Uhamiaji imewapa hii nguvu, lakini ukishindwa kufanya hivyo wao ndiyo wenye mamlaka ya mwisho kukufanya lolote. Nadhani kisheria huu ni mwanya mbaya ambao unajenga mazingira ya matumizi mabaya ya madaraka hasahasa pale ambapo yanatumika kisiasa. Kubwa ni kwamba lazima tuwe na njia mbadala ya haraka ambayo itampa mkimbizi au raia haki ya rufaa endepo atahisi kuonewa na hizi mamlaka.

Tatizo hili limesababishwa na mianya kwenye Mikataba ya Kimataifa na Kikanda inayolinda haki za wakimbizi, ambapo haizibani sana serikali husika. Wao huishia kusema "A Grant of Asylum is strictly a state's prerogative" halafu huku kwingine wanasema "A host state must take all necessary precautions to ensure protection of refugee population residing in its territory". Hapa ndipo matatizo yanaanza, Serikali zinajiamulia kufanya lolote kwasasababu The Grant of Asylum is state's prerogative.

Kuna dada moja Mjerumani nlishawahi kufanya naye kazi, yeye anafanya kwenye shirika la wakimbizi kule kwao Ujerumani. Juzi ameniambia wakimbizi wanaudhi sana hasa hawa jamaa wa kiarabu kutoka Syria, maana ukiwapa moja wao watataka mbili: wanafanya ubakaji, wanataka kuhudumiwa kwa kodi za wajerumani na baadhi wanahusishwa na mitandao ya Ugaidi. Lakini kasema pamoja ya yote haya kuna cha kujifunza kuhusu utu na ubinadamu maana hawa watu hawana pakwenda.

Kiufupi ni kwamba wajerumani (mabeberu + wakristo) wameona ni vyema kukaa na waarabu (waislamu), ambao wametoka kilomita nyingi bara jingine kwenda kuomba hifadhi nchini kwao. Lakini sisi watanganyika tunahisi ni nongwa kuwapokea majirani wenzetu ambao ni weusi kama sisi, tena ambao baadhi yao wana maelfu ya ndugu nchini Tanganyika. Ukiangalia vizuri utatambua kwamba huu ni mkakati urioratibiwa vizuri na vyombo vya ulinzi na usalama, hasa baada ya mkuu wa nchi kusema wazi kabisa kwamba "Tanzania ilishawalea sasa inatosha, mrudi kwenu mkajenge nchi".
Ndugu yangu bandiko hili angepaswa kuliona Pascal Mayalla!!

Nikianza hilo la Wakimbizi kunyanyaswa sana, nadhani kila aliye timamu atakumbuka wakati fulani hata hapa JF tuliwahi kujadili hilo la Wakimbizi wa Burundi, na baada ya watu kupiga kelele sana, serikali ikahalalisha udhalimu wao kwa kutumia mwanya wa hicho hicho ulichosema... kwamba Wale ni Wahamiaji Haramu na sio Wakimbizi!

Dah! The burden of proof!!! Yaani sipati picha Uhamiaji wanavyotumia huyo mwanya kupiga pesa hata za Wakimbizi halali manake majority ya hao Wakimbizi sidhani kama wanaweza kutofautisha kati ya illegal na refugee!

Anyway, nilifuatilia sana hilo la Wakimbizi kutoka Syria hadi nikafikia kusema " a woman will always be a mother" huku nikimchukulia Angel Merkel jinsi alivyokuwa amewapambania Wakimbizi wa Syria ingawaje baadhi yao walikuwa wanaonesha ushenzi usiovumilika hata chembe!

Na moja ya mambo ambayo walinekera sana hawa Wakimbizi kutoka Syria ni pale vijana wawili au watatu (sikumbuki vizuri) walipombaka msichana mmoja huko ukimbizini!

Nikabaki kujiuliza, ikiwa Wazungu ambao kitamaduni na Waarabu ni kama mbingu na ardhi lakini bado wanawavumilia kwa sababu za kibinadamu, hivi watu kama sisi tunakosaje ubinadamu kwa watu ambao kimsingi "we're one and the same" almost in all aspects of life!! Yaani Wazungu ambao they've nothing to share culturally Arabs lakini ingawaje miongoni mwa hao Arabs ni total monsters wengi wao ni watu wema... kwanini tuhukumu wote at the cost of few monsters!!
 
Wew maneno yako hayo umefanyia research wap?, Ushawah kufika kambi ya wakimbizi yoyote, # mm hometown n kigoma# huwa tuanongea nao na sijawah sikia kitu Kama hichi na kinacuoendana na hiki, tatzo some black people they think that white people are Gods, kwamba walichosema hakuna kukichakata kichwan n kukiamin tuu na kukihubiri
Wakimbizi waliotendewa ukatili ni raia wa burundi na sio ambao wapo kwenye kambi ya wakimbizi kigoma, ukipata muda soma ile taarifa ya HRW unaweza kuelewa

Halafu kama haya hayana ukweli, serikalinyetu haijakanusha popote na haijajibu batua ya HRW ambayo imetaka wajibu hizo shutuma

La mwisho, ni kosa kumfukuza mkimbizi, ninachojiuliza ni kwa nini serikali ilikataa kuwapokea wakimbizi na mbaya zaidi jeshi letu limewatendea ukatili, kuna mambe mengi hapa ya kusikitisha na yanahitaji majibu na sio propaganda
 
Wanabodi,
Kila mara nasisitiza humu, uongo ukisemwa sana, na kuachwa kujirudia rudia bila kukanushwa, mwishowe uongo huo hugeuka ukweli. Na uongo ambao ni uongo mtupu, ukisemwa kuwa kitu fulani kitatokea, tusipo kanusha uongo huo, halafu hicho kitu kikaja kutokea kweli, then, kufuatia kuanuni ya matokeo, ule uongo utahesabika ndio ukweli, kwa sababu umetokea kweli. Hii ni kufuatia baadhi ya kauli, zinauwezo wa kuumba.

Mfano kuna huu uongo wa jarida hili kuhusu hili jambo la kuihusu Tanzania, ambao ulisemwa mwaka 2019. na kudaiwa kuwa litatokea Tanzania kwenye uchaguzi wa mwaka 2020. Hatukukanusha, tukanyama na kuwapuuza kwa hoja za uzushi huo ni upepo tuu na utapita.

Lakini kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2020, hilo jambo, hawa The Economist walilolizusha, likatokea kweli!, matokeo yake, sasa itaonekana kuwa kilichotokea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ni kweli kilipangwa kabla, na The Economist walikisema, wakati kiukweli, kile The Economist walichokisema, ilikuwa ni uongo na uzushi, lakini kwa vile, hatukukanusha uongo huo na uzushi huo, kisha ukaja kutokea kiukweli kabisa, dunia italiamini jarida la Economist kuwa walisema kweli, hata kama matokeo ya uchaguzi mkuu huu, ni Watanzania wenyewe, kwa ridhaa yao, wamewakataa wapinzani, na kuichagua CCM kwa mapenzi yao, katika uchaguzi huru na wa haki, licha ya dosari ndogo ndogo, no one will belive its peoples will! ya Watanzania!, watauamini uongo ule kuwa kilichotokea kilipangwa, kikasemwa kimepangwa, kikatekelezwa na ndicho kilichotokea!.

Kwenye toleo la la wiki hii, Jarida la The Economist limeendeleza mauongo yao kuihusu Tanzania, waidanganya dunia kuwa Tanzania, inaendelea kufanya mahojiano kwa kutumia njia haramu za mateso makubwa ya Torture, na njia hizo zinatumika kuwatesa wakimbizi wa Burundi, ili kuwalazimisha kurejea nchini kwao. Japo mimi sio mtu wa ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama, kuthibitisha au kukanusha tuhuma hizi, lakini. kwa vile ni mwandishi wa habari, niliyehudumu kwenye sekta ya habari kwa takriban miongo mitatu, hivyo ninakuwa na uwezo uitwa "insight", wa kubaini kitu cha uongo kwa kisikia au kukisoma. Hiyo insight ni uwezo unaotokana na long experiance ya uzoefu wa muda mrefu kwenye jambo fulani, hivyo mtu akisema jambo fulani la uongo, huhitaji a rocket science kumbaini anasema uongo, au ukisoma andiko la uongo, huchukui hata dakika mbili kubaini bandiko hilo ni la uongo!. Swali la kujiuliza ni hawa Jarida la The Economist, wanapata faida gani kutunga uongo wa mambo mabaya kuihusu Tanzania?, lakini pia, kwa kwanini sisi Tanzania, tunazushiwa uongo na tunanyamazia tuu uongo huu, bila kuukanusha?, au kwenye mamlaka zetu, kutokana na mauonga haya kuvurumishwa kwa ngeli, kwenye majarida na vyombo vya habari vya kimataifa, hivyo hatuna watu wenye ngeli na uwezo wa kukanusha maungo hayo kwa ngeli hizo hizo?. Sisi uwezo wetu ni kukanusha tuu maungo kwenye hivi vipeperushi vyetu vya kufungia maandazi na samaki?.

Naomba nikupeleke kwenye makala yenyenyewe nzima nzima kisha nikuchambulie, upi ni mchele, na zipi ni pumba!.

No haven​

Tanzania’s police are torturing refugees from Burundi​

Uchambuzi wangu wa taarifa hii ni kama ufuatavyo
  1. Msingi wa uchambuzi wangu ni kutumia kitu kinaitwa logical progression kwa kufuata formula ya tenga la samaki, samaki mmoja akioza, wote wameoza!. Ukivua samaki asubuhi, ukawaweka kwenye tenga, ukavua wengine mchana, ukawaweka kwenye tenga lilelile, kisha ukavua wengine jioni, nao ukawaweka tenga hilo hilo, ulipofika sokoni, ile unatoa samaki mmoja, ukamuona ameanza kuoza, usijifariji kuwa huyo samaki aliyeoza ni kati ya wale samaki waliovuliwa asubuhi, hivyo akaanza kuwapekua na kuwatafuta wale waliovuliwa jioni kwa kudhani, watakuwa bado ni fresh!, huo ni kujisumbua bure, kwenye tenga la samaki, samaki mmoja akioza, wote wameoza!.
  2. Kanuni hiyo ndio nimeitumia kwenye hii story, hata kama ni kweli, kuna baadhi ya mambo mabaya haya yametokea, kama kwenye kuripoti, meripoti mambo ya ukweli, asilimia 99%, na ili kuikoleza story yako, ukaweka jambo moja tuu la uongo, ule uongo mmoja, unabatilisha kweli zote 99, na kuonekana yote ni uongo mtupu, kama yule samaki mmoja, anavyoozesha, samaki wote kwenye tenga la samaki.
  3. Ili habari yoyote iwe ni habari kamilifu na timilifu, inapaswa kuwa na sifa kuu 4.
    1. Truthfulness
    2. Objectivity
    3. Impartiality
    4. Balancing
  4. Uongo wa Kwanza: Habari hiyo haina Truthfulness, ukweli, hivyo ni habari ya uongo!. Truthfulness ndio kanuni kuu ya uandishi wa habari, duniani kote, "tell nothing but the truth", yaani kusema kweli daima, na kuandika ukweli mtupu. Katika kuripoti habari yoyote, ili pia habari hiyo iweze kuaminika, ni kuripoti with pictures, visuals, or actualities ili msomaji aone, kuona ni kuamini, hivyo kwenye reporting, ukifanikiwa kupiga picha, video, au kufanya mahojiano, halafu ukaweka picha, video na interviews, msomaji au mtazamaji, akiona hizo picha au video, ataamini zaidi, kuliko maandishi pekee. Ili kujenga picha mbaya ya Tanzania kwa wasomaji wao, na kuuhadaa ulimwengu kuhusu Tanzania, habari hiyo imeandamana na picha ya kutishia amani ya vurugu na kuchomwa matairi barabarani,View attachment 1642222japo picha hiyo ni picha ya tukio la kweli, lakini sio Tanzania!, wameiweka bila kuandika maelezo yoyote ya hiyo picha ili wasomaji waone ni Tanzania!. Hivyo uongo huu mmoja tuu, wa kutumia picha ya uongo, kutoka nchi zenye vurugu, na kuiripoti as if ni Tanzania, inatosha kubatilisha story yote nzima nzima, hata kama yote yaliyosemwa ni kweli yalitokea!, kuutumia uongo kuhalalisha kitu cha kweli, kunachachua ukweli wote na kuonekana wote ni uongo!.
  5. Uandishi unaongozwa na misingi, taratibu na kanuni, uki publish picha yoyote kwenye gazeti lolote, lazima kwanza utoe kitu kinaitwa Photo credit, ya ni nani aliyepiga hiyo, imepigwa lini, imepigwa wapi na kutoa maelezo ni kwenye tukio gani!. Sasa kwa vile story ni negative kuhusu Tanzania, wakatafuta picha mbaya kutoka huko walikotafuta, wakaipachika kwa kutoa tuu photo credits kuwa ni picha ya Reuters, lakini bila maelezo yoyote, kusema hapo ni wapi, lini au ni tukio gani, ili msomaji akisoma tuu, aone ni Tanzania!, kitu ambacho sio kweli, hiyo picha sio Tanzania!. Unaweza kuni challenge, kwa hoja kuwa maadam mimi sio ripota wa hiyo story, nimejuaje hapo sio Tanzania?, hapo sasa ndipo matumizi ya ile logical progression yanapokuja. Watanzania ni watu pisi sana!, ukiangalia huo wingi wa hayo mawe barabarani, na ukumbwa wa mawe yenyewe, na wingi wa matairi yaliyochomwa, huo ni uthibitisho, hiyo picha ni ya kutoka nchi za watu wenye vurugu. Watanzania hatuko hivyo!. Wametumia picha ya vurugu, kuchafua tuu image ya taifa letu!. Watalii ni very sensitive people, unapozungumzia Tanzania na kuweka picha kama hiyo, bila kusema hapo ni wapi na ni lini, amini usiamini, hata kama ulipanga uje Tanzania, ukishaona tuu kitu kama hicho, unaghairi, huji!.
  6. Ili mwandishi kuandika habari yoyote, kitu cha kwanza ni unapata kitu kinachoitwa "news tip", hii ni kutoka kwa mtu anayekutonya habari fulani, kwa sisi waandishi experienced, unajikuta una "nose for news" yaani pua yako ina uwezo mkubwa wa kunusa habari, baada ya tip, unatafuta news lead, uanzie wapi. Yule mtoa habari wako anaitwa "source", katika kuandika habari yoyote yenye tuhuma nzito, kwanza inamtaka mwandishi kujiridhisha na ukweli wa huyo source wake. Ukiisha kamilisha kumhoji, unatakiwa kabla hujaichapisha hiyo habari, usitegemee just a single source, lazima ufanye verification, kuzithibitisha hizo tuhuma, kwa kufanya double checking na cross checking. Hii habari ya The Economist, imemtumia source mmoja tuu mwanzo mwisho!, hivyo kama source ni muongo, anakuingiza chaka, it's very unprofession kutumia just a single source kwa tuhuma nzito kama hii, hivyo habari hii imeegemea upande mmoja, sio impartial, haina impartiality!.
  7. Baada ya kuipata habari na mwandishi kuandika, anafanya kitu kinachoitwa, objectivity consideration, kwa mwandishi unajiuliza hii habari ina malengo gani?, msomaji akisoma atapata picha gani, kwa vile hili jarida, kila siku linaripoti taarifa negative tuu kuhusu Tanzania, na hili niliwahi kulizungumzia, https://www.jamiiforums.com/threads...-hakuna-mazuri-yotote-ya-kuyaangazia.1471986/ , hivyo mwandishi ameripoti with malice aforethought kwa kutafuta negative stories tuu kuhusu Tanzania, hivyo habari hiyo kukosa objectivity.
  8. Ukipata habari yoyote ya tuhuma za upande mmoja, maadili yanatufundisha usiripoti one sided story, lazima uutafute upande wa pili na kuusikia ili kuibalance story yako. Na kwa vile hii tuhuma, inahusu mambo nyeti ya kuhusisha vyombo vya usalama, then mwandishi alipaswa kuibalance story yake kwa kupata the authoritative source, wa kwanza ni mtu wa UNHCR kuthibitisha hizo tuhuma, wa pili ni RPC wa eneo husika kuthibitisha, hilo tukio limetokea. Hili halikufanyika, hivyo hiyo sio balanced story, imekosa balance, hivyo ku justify ile hoja ya malice aforethought.

Paskali
kwanini umeileta hiyo ripoti hapa?, Kua mzalendo kwa nchi yako ,ungeicha huko wala watu tusingeiona, hili jarida lina chuku na serekali yetu ila Raisi wetu Magufuli hatishiwi nyau na vijarida uchwara
 
Taifa linhitaji RECONCILIATION kwa matatizo yetu ya ndani kisiasa,wapinzania wamegeuzwa wkimbizi ndani ya nchi yao na wanatengwa bila ya kusikilizwa na kuhujumiwa kila kona.heri hao wakimbizi wao wanaye wa kuwasemea, Wapinzania ni kama yatima nchi hii.
 
Hili gazeti litakuwa linatumiwa na viongozi wa Chadema kuchafua taswira ya nchi yetu. Maana tokea aingie JPM madarakani na kufanya kazi nzuri,wanaisakama Tanzania. Na mengi wanayoandika yanaakisi kile wanachama na wafuasi wa Chadema huwa wanakisema dhidi ya taifa letu.
 
Back
Top Bottom