The Doomed flight: Boeing 777 [MH370] Malaysia Airlines

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,258
20,708
Kutokana na maombi ya baadhi ya wanachama wa Jamii Forums waliokuja PM kuniomba niandike kile ambacho ninakifahamu kuhusiana na kupotea kunakostaajabisha kwa dege la shirika la ndege la Malaysia,leo nimeamua niandike machache kuhusu ndege hii na namna ilivyopotea katikati ya rada chungu nzima za nchi kubwa na ndogo duniani....

Sikuwa na mpango wa kuandika lolote kuhusu tukio hili,lakini nimeandika kwa heshima ya member wenzangu waliokuja kuniomba niandike kuhusu tukio hili nami bila hiyana,baada yakukusanya taarifa chache nimefanikiwa kuandika....

Katika namna ya kustaajabisha na ya ajabu kabisa,dege hili kubwa kabisa lilitoweka katika mazingira yaliyoitwa "yasiyoeleweka" na hadi leo haijulikani iko wapi na ilikwenda wapi.Wengi wameshindwa kuamini kama katika ulimwengu na dunia hii tunayoambiwa kwamba ina maendeleo makubwa kabisa ya kisayansi ndege kubwa kama ile inaweza kupotelea kusikojulikana na hata kutokupatikana hadi leo.

Nini kilitokea siku ya tukio?Ilikuwaje? Twende pamoja katika makala hii ambayo itakuelezea mengi kwa kadiri ya mwandishi...

Karibu....

Ndege ya aina ya Boeng 777 iliyofahamika kama flght 370 kutoka katika shirika la ndege la Malaysia airline iliyotoweka katika mazingira ya kutatanisha dakika 94 baada ya kuondoka katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur International airport siku ya tarehe 8 mwezi march ya mwaka 2014.Ndege hii baada ya kutoweka harakati za kuitafuta zilianza na miaka kadhaa baadaye zilifungwa....

Wamiliki wa ndege hii ambayo ni shirika la ndege la nchi ya Malaysia,shirika ambalo lilianzishwa mwana 1972 baada ya kuparaganyika kwa umoja wa ushirikiano wa usafirishaji wa anga baina ya Malaysia na Singapore ulioanzishwa mwaka 1947.Makoa makuu ya shirika hili ni Kuala Lumpur katika uwanja wa Kuala Lumpur Internation Airport.Ndege hii ilikuwa inaendesha safari zake katika Asia ya kusini/magharibi na Mashariki ambapo ni katika nchi za Australia,New Zealand,Mashariki ya kati pia ilikuwa inafanya safari zake katika nchi za Ulaya na Amerika katika jiji la Los Angeles kupitia Tokyo,Japan ambapo shirika linalomiliki ndege hii lina ndege zingine pia lakini ndege hii ilikuwa inafanya safari hizi hadi kufikia kutoweka kwake mwaka 2014 tarehe 8 ya mwezi March...

nintchdbpict0002460783411.jpg

Baadhi ya ndege za shirika la ndege la Malaysia Airlines

Shirika la Ndege la Malaysia liliwahi kupata ajali tatu katika ndege zake zinazofanya safari katika maeneo tajwa hapo juu lakini ajali zote hazikuhusisha ndege hii aina ya boeng 777 iliyofahamika kama flight 370.....

Sept. 2,1992,ndege moja ya shirika hili ilipata ajali baada ya tairi zote za ndege hii kupasuka wakati ikijiandaa kuruka katika uwanja wa kimataifa wa Kuala Lumpur.Bahati nzuri hakukuwa na vifo wala majeruhi...

Sept. 15,1995,Ndege nyingine ya shirika hili ilipokuwa inajaribu kuruka katika uwanja wa ndege ulioko katika mji wa Kota Kinabalu ilishindwa na kwenda kuangukia katika nyumba zilizokuwa jirani na uwanja huo na kusababisha vifo vya watu 34 waliokuwa ndani ya ndege....

March 15, 2000,Mitungi yenye hewa ya sumu na vilainishi vya hatari kwenye ndege iliingizwa kimakosa kwenye moja ya ndege za shirika hili na kampuni moja ya ki-China na kusababisha hasara katika baadhi ya maeneo katika ndege hii ambayo ilikuwa ni Airbus A330 kitendo kilichopelekea kampuni hii ya ki-China kupigwa fain ya dola mil 65.....

Boeng 777:Flight 370

nintchdbpict000279248754.jpg

Boing 777 a.k.a MH 370 ikichanja mbuga kwenye moja ya safari zake

Aina hii ya ndege ilitengenezwa kubeba abiria 282.35 katika bussines class na 247 katika economic class.Engine zake ni aina ya Rolls royce trent 892 zilizowekwa chini kidogo ya mabawa yake yenye urefu wa futi 200 ambayo ni sawa na mita 61.Ndege hii ujazo wake wa makadirio wa mafuta [maximum fuel capacity] ni galoni 47,380 ambayo ni sawa na lita 179,400.Ina uwezo wa kukimbia kil 897 kwa saa.

Ndege hii ilifanyiwa ukarabati wa kawaida tarehe 23 feb,2014 na hakukuwa na jambo lolote la kustua au kuvuta hisia za mafundi wakati huo wa marekebisho madogo madogo ambao ni wa kawaida kila baada ya muda fulani wa ndege kutumika au kufanya shughuli zake.Ndege hii haikupata ajali yoyote kubwa kabla ya kupotea kwake isipokuwa iliwahi kuripotiwa ajali ndogo mwaka 2012 iliyopeleka kupata tatizo kidogo kwenye bawa lake moja....

March 8,2014,siku ya safari

Ndege hii ilikuwa ipo kwenye uwanja wake wa nyumbani na makao yake makuu ikisubiria wakati wake wa safari kuelekea China.Siku hii ambayo ndege hii ilikuwa inaendelea katika kutoa huduma kwa wahitaji ilikuwa ni siku ya kawaida tu na isiyokuwa na hali ya hewa ya hatari ya namna yoyote ile wala kitisho chochote kile.Abiria walikuwa wakiendelea kumalizia taratibu na kuanza kuingia kwenye ndege hii tayari kwa safari ya kila mmoja kuelekea anakokujua....

Mpaka kufikia siku hii,ndege hii ilikuwa imeshafanya safari kwa masaa 53,465 na mzunguko wa safari 7,525 ambapo huhesabiwa kwa kuanzia kuondoka hadi kutua mwisho wa safari ya ndege husika.Kiongozi wa ndege hii siku hii alikuwa anajulikana kama Capt. Zaharie Ahmad Shah.

nintchdbpict000074864535.jpg

Rubani Zaharie Ahmad Shah

Kiongozi huyu alikuwa na miaka 53 na alizaliwa katika mji wa Penang ambao uko kaskazini mwa nchi ya Malaysia.Kiongozi huyu alikuwa na mjukuu mmoja hadi kufikia siku hii na alikuwa na uzoefu wa angani wa masaa 18,000.Msaidizi wake aliyejulikana kama Fariq Abdul Hamid,aliyekuwa na umri wa miaka 27,alikuwa na uzoefu wa angani wa masaa 2,763.Kijana huyu alikuwa na mchumba na alikuwa katika mipango ya kufunga ndoa....

Siku hii dege hili la kuvutia kabisa la shirika la ndege la Malaysia lilikuwa limebeba watu ambao hufahamika kama abiria kutoka mataifa 14 ambao walikuwa wametimiza idadi ya watu 227 na wafanyakazi wa ndege 12 ambao wote walikuwa ni raia wa malaysia.Kati ya hao abiria,abiria 153 walikuwa ni raia wa China,abiria 3 walikuwa ni raia wa Marekani,abiria 6 raia wa Australia,abiria 2 raia wa Canada,abiria 4 raia wa Ufaransa,raia 1 kutoka Hong Kong,abiria 5 kutoka India,abiria 7 kutoka Indonesia,abiria 2 kutoka Iran,abiria 1 kutoka Uholanzi,abiria 1 kutoka Urusi,abiria 1 kutoka Taiwan na Ukraine 2....

Saa 12:41 A.M

Flight 370 iliondoka kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Malaysia saa 12:41 ikiwa na abiria hao kutoka mataifa hayo wakiwa na amani na furaha wakielekea maeneo tofauti ya dunia hii ilikokuwa inaelekea ndege hii.Kama zilivyo taratibu za safari za anga,kila ndege huwa ina utambulisho wake na eneo la kuruka.Ndege hii iliruka kama Boeing 777-2H6ER.Maneno ya siri "H6" kwa tafsiri ya "kawaida" naweza kusema kwamba neno hilo la siri linasimama kutambulisha eneo la kurukia ndege la shirika hilo la Malaysia na neno "ER" ni badala ya "Extended Range".....

Ndege hii ilitarajiwa kuwasili Beijing,China alfajiri ya saa 6:30 ikiwa imebeba watu hao 239 ndani.Mawasiliano ya mwisho kufanyika baina ya rubani msaidizi Fariq Abdul Hamid na wasimamizi wa ndege wa angani kutoka kiwanja cha kimataifa cha Malaysia ilikuwa ni saa 1:19 za usiku.

Baada ya mawasiliani hayo,dakika mbili baadaye kifaa kwaajili ya kuzipa msaada rada kuweza kuiona ndege hii kilizimwa na hii ilikuwa ni saa 1:21 za usiku.

Dakika kama 56 baadaye,yaani saa 2:15,jeshi la Malaysia liliona "kitu" [object] ambacho jeshi hilo halikukielewa kikiwa angani Kikiwa kinaelekea magharibi.Taarifa hii kutoka jeshini ilikuja kusemwa wiki moja baada ya ndege hii kutoweka."Kitu" hicho ambacho jeshi la Malaysia lilikiona angani kikiwa kinaelekea magharibi kilitoweka kwenye radar ya jeshi hilo baada ya kusafiri kwa kilomita 322 angani kwenye pwani ya Malaysia iliyoko kwenye mji wa Penang.

Kufikia saa 6:30 alfajiri ambapo ndege hii ilipaswa kuwasili China hakukuwa na taarifa yoyote kuihusu mahala ilipo.Ilipofika saa 8:30 asubuhi Satelite iliweza kupata signal kutoka kwenye antena ya ndege.Baada ya hapo hakukuwa na taarifa yoyote kuhusiana na ndege hiyo...

March 9,masaa 24 baadaye....

Baada ya kupita masaa 24 bila kujua ilipo ndege hii mamlaka zinazohusika nchini Malaysia zilianza kuisaka ndege hii maeneo ya pwani ambako signal ya mwisho kutoka kwenye ndege hii ilipatikana na waliona vitu kama mafuta kwenye maji ya jirani na eneo hilo baharini lakini baadaye walikuja kugundua kuwa mafuta yale yalitoka kutoka kwenye meli na siyo ndege.

March 10

Msako wa ndege hii unapanuliwa zaidi hadi kusini mwa pwani ya China baada ya kuonekana kuwa kuna uwezekano wa ajali ya ndege hii kutokea jirani na Hong Kong.Wasakaji wa ndege hii kutokea Vietnam wanaendesha msako huu na wanashindwa kupata chochote cha kuwaonesha mahali ambapo huenda ndege hii ilipata ajali....

Siku hii NASA nao wanaongeza nguvu katika kuisaka ndege hii iliyopotea kwa mazingira ya kushangaza kabisa.NASA wanatumia vifaa vya kisasa kabisa kuisaka ndege hii kuanzia siku hii...

March 11

Inadiwa kwamba kulikuwa na upotevu wa document ambazo zinahusishwa na ndege hii.Wapelelezi wanaingia kazini na baada ya muda mfupi inatoka taarifa kwamba upotevu wa nyaraka hizo haukuhusiana na magaidi kwa namna yoyote ile.

Baadaye maafisa wa anga wa Malaysia waliripoti kuwa,kutokana na ndege kusomeka kwenye rada inahisiwa kuwa ilibadili uelekeo na kurudi ilipokuwa inatokea nyakati za usiku manane.Mpaka hapa hakukuwa na taarifa iliyoeleweka juu ya uelekeo au ilipo ndege hii.Ndugu za abiria waliokuwa kwenye ndege hii walianza kuuliza maswali serikalini baada ya ndugu zao kutoonekana na ndege kutoonekana vile vile.Maafisa wa serikali waliendelea kuwapa matumaini ndugu hao kuwa bado hawajaelewa haswa ni wapi ndege ile ilikuwa lakini kutokana na ukimya mrefu uwezekano wa ndugu na ndege hiyo kupatikana katika hali ya kawaida ni ndogo sana...

Ndugu wa abiria walianza kuingiwa na kihoro baada ya taarifa hii na kila walipoangalia vyombo vya habari taarifa iliyokuwa inarushwa hewani kwa wakati huo ni kupotea kwa ndege iliyokuwa imewabeba ndugu zao...

March 12

Siku hii ilianza kwa maafisa wa serikali ya Malaysia kufungua jalada la uwezekano wa ndege hii kuwa imetekwa na watu ambao hadi wakati huo walikuwa hawajajulikana.Serikali ya China ilionesha picha zilizopigwa na satelaiti kuonesha kuwa ndizo za ndege iliyopotea kusini mwa China lakini baadaye maafisa wa serikali ya Malaysia walisema kwamba hizo picha hazikuwa za ndege hiyo.....

Hadi kufikia siku hii zilikuwa zimekatika siku nne bila kupatikana kwa ndege hii au hata hadithi tu inayohusiana na ndege hii....

March 14

Baadhi ya watu waliokuwa kwenye kuisaka ndege hii waliliambia gazeti la New York Times kwamba inawezekana ndege ile ilipoteza uelekeo baada ya kupoteza mawasiliano na uwanja wa Malaysia International Airport....

March 15

Makachero wa serikali ya Malaysia wanaripoti kwamba,wamepekua nyumbani kwa rubani wa ndege hii na wanahisia kwamba inawezekana kuna mtu aliweza kuingilia mawasiliano ya ndege na uwanja wa Malaysia muda mfupi baada ya ndege kuondoka uwanjani hapo na inadaiwa kuwa mtu huyo alikuwepo kwenye ndege ile.Makachero hao wanaendelea kusema kwamba kuna uwezekano mkubwa wa rubani kuhusika kwa namna ya kipekee katika kadhia hii....

Baadaye waziri mkuu wa Malaysia Najib Razak alidai kuwa mawasiliano ya ndege ile yalikatwa makusudi na mtu ambaye hakujulikana na ilibadilishwa uelekeo baada ya kutokuwa na mawasiliano na kwamba ndege ile ilikuwa imetekwa...

Timu ya kuisaka ndege hii inaendelea kufuatilia mawasiliano ya mwisho kabisa baina ya ndege hii na waongoza ndege wa uwanja wa kimataifa wa Malaysia....

March 16

Usakaji wa ndege hii unaendelea na wigo wa kuisaka unapanuliwa zaidi na taarifa inatolewa kuwa ndege hii iliendelea na safari ikiwa na mwendo usioeleweka kwa muda wa masaa saba baada ya kupoteza mawasiliano.

nintchdbpict000180323726.jpg

Ramani ikionesha namna ndege hii ilivyokuwa inasakwa kwenye bahari ya Hindi

March 17

Mamlaka za anga za Australia na Indonesia zinaamua kutumia ndege za patrol kuisaka ndege hii kusini mwa bahari ya Hindi.Wapelelezi wa Malaysia wanaendelea kufanya uchunguzi wao kwa kukagua taarifa za abiria mmoja baada ya mwingine waliokuwa kwenye ndege hii ili kupata angalu taarifa ambazo zitawasaidia kuelewa jambo ambalo litasaidia kuisaka ndege hii iliyoyeyuka mithili ya moshi angani....

Waziri mkuu wa Malaysia anawaomba wasakaji wa ndege hii kutoka Malaysia kuongoza timu za kuisaka ndege hii...

March 18

Inatolewa taarifa kwamba rada ya Thailand inaweza kuwa imeiona ndege hii.Lakini taarifa hii inakuwa ni siri baina ya serikali hizi mbili hadi leo na haikueleweka sababu ya kutotoa taarifa hii ni nini.....

March 19

Wataalam wa utafiti kutoka Marekani wanatua katika pwani ya bahari ya India kuongeza nguvu katika kuitafuta ndege hii ambayo hadi sasa hakukuwa na matumaini yoyote yale ya kuipata.Wataalam hawa wanaomba taarifa iliyopatikana nyumbani kwa rubani ili waweze kuifanyia kazi.Lakini katika hali ya kustaajabisha,waziri wa ulinzi wa Malaysia anawaambaia kuwa taarifa hizo zilifutwa kwenye tarakilishi [Computer] iliyokuwa imezihifadhi.

March 20

Taarifa inatoka katika serikali ya Australia kwamba wanadhani wameona mabaki ya yanayohisiwa kuwa ni ya ndege kusini mwa bahari ya Hindi.Picha zilizopigwa na Satelaiti zinonesha vitu visivyoeleweka baharini ambavyo vinadhaniwa kuwa ni mabaki ya ndege.Ndege maalum kwaajili ya kutafuta ndege hii zinatumwa eneo hili lakini hakukuwa na taarifa za kutia moyo hata baada ya utafiti huu kufanywa kwa kiwango kikubwa kabisa na upana wa maili 23,000...

March 21

Wataam wa anga kutoka Uingereza wanashangaa ni kwa namna gani ndege hii inaweza kupotea bila kuonekana kwenye rada wala Satelaiti na wanaendelea kusema kwamba haiwezekani jambo hili kutokea.Maswali yanaendelea kuulizwa kutoka kwa ndugu na jamaa lakini hakuna majibu ya kuridhisha.Kufikia hapa ndugu wa abiria waliokuwa kwenye ndege hii wanaanza kuamini wapendwa wao wameshapoteza maisha na uwezekano wa kupatikana hai unatoweka kabisa....

Kila mmoja anaanza kuomboleza kwa imani na taratibu zake na baadhi ya ndugu wanafanya taratatibu za kuwazika wapendwa wao angalau hata kwa kutumia picha.Simanzi inaendelea kutanda katika nchi aote ambazo raia wao walikuwa kwenye ndege hii haswa nchini China ambako ndiko kulikuwa na watu wengi waliokuwa kwenye ndege hii.....

March 22

Rada ya Australia inaona vitu kama mabati meusi yakielea baharini.Satelaitiya China nayo inaona vitu vya kufanana na hivyo kusini mwa bahari ya Hindi na wote kwa pamoja wanakubaliana kwamba hayo ni mabaki ya ndege hii ambayo imepotea kwa namna ya kustaajabisha kabisa.Vitu hivi ambavyo vilikuja kukadiriwa baadaye vilikuwa na urefu wa futi 72 kwa 43 havikuweza kupatikana kwenye eneo vilivyohisiwa kuonekana.Kila mmoja anaendelea kushangaa kwa tukio hili la ajabu kupata kutokea....

March 23

Satelite ya Ufaransa nayo inaona vitu vikielea baharini na vinadhaniwa kuwa ni mabaki ya ndege hii ya Shirika la Malaysia.Wahusika wanatuma picha za vitu hivi kwenye timu ya kusaka ndege hii ya Australia na mara moja wanaelekea vilipoonekana vitu hivi lakini baada ya kutafita kwa muda hakuna kilichopatikana...

Sintofahamu inazidi na watu wanashindwa kabisa kulielewa tukio hili....

March 24

Satelaiti ya Australia inaona tena vitu vikielea baharini na timu inakwenda eneo hili na kufanya utafiti wa kina kwa muda wa masaa kadhaa bila mafanikio yoyote yale...

Waziri mkuu wa Malaysia anaitisha kikao na waandishi wa habari na anawaeleza kwamba kufikia hapa wanaamini kwamba ndege hii ilipata ajali kusini mwa bahari ya Hindi.Waziri mkuu anaendelea kueleza kwamba wataalamu wa kutafiti ajali za ndege kutoka Uingereza wamesema kwamba wanaamini ndege hii ilipoteza muelekeo ikiwa katika eneo la mwisho kujulikana kabla haijapata ajali kusini mwa bahari hiyo ya Hindi...

Waziri Mkuu huyu anasema kwamba familia za wale abiria 239 waliokuwa ndani ya ndege hii zimejulishwa tayari....

March 25

Hali mbaya ya hewa inasababisha wataalam wa kuendelea kuisaka ndege hii kusitisha zoezi hili....

March 26

Waziri wa uchukuzi wa Malaysia Hishammuddin Hussein anasema kwamba satelaiti ya nchi hiyo imeona vitu vingi vipatavyo 122 vikielea baharini kweye eneo ambalo hapo kabla satelaiti ya Australia iliona vitu vya kufanana na hivyo siku ya jumapili ya tarehe 23

March 27

Satelaiti ya Thailand inaona vitu vingine vingi zaidi vikielea baharini na vilikadiriwa kuwa kama 300 hivi ambavyo wanavihusisha na ndege iliyodhaniwa kupata ajali kusini mwa Australia.....

March 31

Meli ya Kichina inafanikiwa kukusanya vitu vyote vilivyodhaniwa kuwa ni mabaki ya ndege hii lakini baada ya kuvifanyia utafiti wa kina vinagundulika havina uhusiano na ndege hii...

April 4

Meli ya Kichina inagundua signal ambayo inadaiwa ni signal kama inayoweza kutoka kwenye kisanduku cheusi cha kwenye ndege...

April 13

Meli ya Australia nayo inapata signal inayofanana na iliyopatwa na meli ya Kichina.....

April 17

Manowari moja inapewa jukumu la kutafiti chini ya bahari kama kutaonekana mabaki yoyote ya ndege au kitu kingine kitakachoweza kuleta matumaini juu ya kupotea kwa ndege hii ya shirika la ndege la Malaysia....

Bahati mbaya manowari hii inakosa chochote cha kutia matumaini....

April 29

Maofisa wa serikali ya Malaysia wanafanya uchunguzi juu ya taarifa kutoka kwenye kampuni moja ya nchini humo kwamba imeona mabaki na sauti kama za mabaki ndege kwenye maeneo ya kusini mwa bahari ya Hindi...

Hakuna chochote cha kutia moyo kilichoonwa na maofisa hawa wa serikali ya Malaysia....

Julai 29, 2015

Vinapatikana vitu ambavyo vinathibitika kuwa ni mabaki ya ndege lakini bila kuthibitishwa kuwa ni kutoka kwenye ndege iliyopotea ya Malaysia.Mabaki haya yanapatikana katika kisiwa cha Reunion....

Feb. 27, 2016

Mabaki mengine yanayothibitishwa kuwa ni ya boing 777 yanapatikana kwenye ufukwe wa Msumbiji.Ukaguzi wa mabaki haya unakamilika tarehe 24 March,2016 na inadaiwa kuwa mabaki hayo ya ndege yanakaribia kufanana na ya ndege iliyopotea ya Malaysia...

Waziri wa viwanda wa Australia Darren Cheste anasema kwamba kwa namna mabaki hayo ya ndege yanavyoonekana inaonesha kuwa ni ya ndege iliyopata ajali baharini,kwenye bahari ya Hindi na kuishia kupatikana kwenye pwani ya Msumbiji na hii inaonesha wazi kuwa ni mabaki ya ndege ya shirika la Malaysia,MH 370 iliyopotea....

nintchdbpict000272732594.jpg

Baadhi ya mabaki yanayodhaniwa kuwa ni ya ndege MH 370,Boeing 777

July 22, 2016

Australia, China na Malaysia zinakubaliana kwamba kama mabaki ya ndege hii hayatapatikana katika umbali wa maili za mraba 120,000 basi harakati za kuisaka ndege hii zitasitishwa rasmi....

July 30, 2016

Kunaonekana kitu kama bati kubwa sana kwenye kisiwa kimoja cha Tanzania ambalo linadaiwa kufanana kabisa na miongoni mwa mabaki ya ndege hii iliyopotea,hii ni kwa mujibu wa waziri wa usafirishaji wa Australia....

October 7, 2016

Kunapatikana bawa la ndege katika kisiwa cha Mauritius linalodaiwa kuwa ni la ndege iliyopotea....

January 17, 2017

Hatimaye harakati za kuisaka ndege hii zinasitishwa ramsi baada ya makubaliano kufikiwa baina ya nchi za China,Australia na Malaysia.....

Ukiangalia namna usakaji wa ndege hii ilivyokuwa na taarifa zilivyokuwa zinatoka kuna maswali mengi zaidi ya majibu.Hakuna aliyeweza kujibu maswali haya hadi leo.Hebu tuendelee kuangalia dondoo mbali mbali kuhusu usakwaji wa ndege hii kisha tuendelee....

Sayansi iliyotumika kuisaka ndege hii...

Kufikia hapa ni karibia miaka mitatu ya kuitafuta ndege hii bila mafanikio yoyote.Kila mmoja anaendelea kujiuliza kila aina ya maswali juu ya kutoweka kwa ndege hii kwa namna ya kustaajabisha klabisa.Hakuna anayejua kwa hakika ni nini kilichotokea ukiacha dhana mbali mbali kuihusu ndege hii...

Katika kuisaka ndege hii kulitumika vifaa vya teknologia ya hali ya juu kabuisa kama vile ndege kutoka katika kikosi cha maji cha Marekani maarufu kama US Navy,ndege inayojulikana kama P-8A Poseidon patrol plane.Ndege hii ina uwezo wa kuona hata kitu kidogo sana na kilicho mbali sana majini.lakini pamoja na kutumika bado haikuonekana ndege hii...

1493450518060.jpg

P-8A Poseidon patrol plane.

Ndege hizi ambazo zilikuwa mbili,moja ilitumika katika pwani ya Malaysia na nyingine katika pwani ya Australia ambako inaaminika ndiyo ilikuwa mwisho wa ndege hii.Pamoja na yote haya ndege hii bado haikupatikana....

Ilitumika radar maalum kwaajili ya kutafutia vyombo vilivyokwama chini kabisa majini,radar hii inajulikana kama Sonar.Radar hii ndiyo iliyoigundua ndege ya shirika la Ufaransa iliyopotea baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Rio De Jeneiro mwaka 2009 na baadaye kuja kuonekana na rada hii ikiwa imekwama chini baharini umbali wa kil 4 kutoka juu...

Pamoja na kutumika kwa kifaa hiki chenye uwezo mkubwa kabisa hakukupatikana chochote kinachohusiana na ndege hii ya Malaysia airline kitu kilichowashangaza sana watu wengi...

Sintofahamu...

Baada ya taarifa kuwa ndege hii ilipotea kwenye rada,kumekuwa na maswali mengi sana juu ya uwezekano wa ndege kama hii kufikia hatua isiweze kuonekana kwenye rada....

Profesa wa masuala ya anga wa chuo kikuu cha Florida huko nchini Marekani Sid McGuirk,anasema kwamba tukio hili ni la aina yake maana siyo la kawaida kabisa....

Mtaalam huyu anasema kwamba,kikawaida ndege huwa na rada mbili.Moja waajili ya kutoa mawasiliano juu ya eneo ndege ilipo na nyingine kwaajili ya kutuma taarifa maalum kwa kila ndege ambapo rada hii hutumia kifaa maalum kilichowekwa kwenye ndege kinachojulikana kama "transponder"...

Anaendelea kusema kwamba kimsingi vifaa vingi vinavyoisaidia rada hizi kufanya kazi vipo ardhini na ndiyo maana kuna wakati ndege inapotea kwenye rada kwa muda mfupi na baadaye kuonekana tena.Anasema kwamba kama transponder ikizimwa inakuwa ni ngumu sana ndege kufuatiliwa.Anasema kwamba magaidi hutumia njia hii wanapoteka ndege.Lakini hulazimika kuiwasha tena pale ambapo wanahitaji kutua au kuwajulisha wenzao waliopo chini kuwa wapo wapi....

Kama Flight 370 ilitekwa na magaidi basi ingeweza kujulikana haraka sana,lakini hata kama ilitekwa na magaidi ili iangamizwe bado mabaki yake yangepatikana kiurahisi au hata maada ya muda mrefu bada ya ajali lakini haijawa hivyo hata kwa kudhania tu....

Mtaalam huyu anaendelea kusema kwamba,ndege ya shirika la ndege la Ufaransa iliyopata ajali mwaka 2009 na baadaye kuja kugundulika eneo iliyopatia ajali na kisha kijisanduku cheusi kuja kupatikana miaka miwili baadaye sambamba na mabaki ya ndege ile ilikuwa ni tofauti kwasababu ndege ile ya shirika la Ufaransa iliruka juu sana na kisha kupata shida baada ya hali ya hewa kuwa mbaya na baadaye kuangukia baharini na kuja kuonekana miaka miwili baadaye chini kabisa ya bahati ya Atlantiki ni tofauti na hili maana ndege ya shirika la Malaysia ilikuwa inaruka umbali wa kawaida tu na ilionekana kwenye rada hadi muda mfupi ilipopotea na baadaye kuonekana tena...

Dhana mbali mbali khusiana na kutoweka kwa ndege hii....

Dhana ya Bermuda....

Kumekuwepo kwa dhana ya kugundulika bermuda nyingine kusini mwa Vietnam.Dhana hii ilipelekea watu wengine kufikiria kuwa inawezekana ndege hii ilikwenda kupotelea huko,lakini taarifa zinaeleza kwamba eneo hilo halijathibitishwa,na hata kama lingekuwa limethibitishwa bado safari ya ndege ya saa moja wasingekuwa wamefika eneo hilo na hatimaye kupotea kiajabu....

Dhana ya kumhusisha rais Putin...

Mwandishi wa masuala ya kisayansi wa Marekani Jeff Wise amehusisha kupotea kwa ndege hii na vita baridi inayoendelea baina ya Marekani na Urusi na alidai kuwa inawezekana rais Putin akawa ameidungua ndege hii kwasababu alidhani kuwa itaumiza nchi za magharibi..

Dhana ya kuihusisha Marekani...

Muongoza ndege wa zamani wa Ufaransa Marc Dugain anasema kwamba inawezekana kwamba ndege hii ilidunguliwa na Marekani kwa sababu walidhani kuwa imetekwa na wanaodhaniwa kuwa magaidi.Pia anasema kwamba inaweza kuwa ilidunguliwa kwa bahati mbaya na majeshi ya Marekani yakishirikiana na majeshi ya Thailand kwa bahati mbaya....

Dhana ya kujitoa mhanga

Afisa wa polisi wa Malaysia anayefahamika kama Tan Sri Khalid Abu Bakar anasema kwamba inawezekana kulikuwa na mtu ndani ya ndege aliyesababisha ndege hiyo kupata ajali ili afe kwasababu ambazo anazielewa yeye mwenyewe...

Dhana ya kumhusisha rubani

Inadaiwa kuwa siku chache kabla ya siku ya ajali,rubani wa ndege hii alikuwa ameachana na mkewe.Inadaiwa kuwa inawezekana kuwa aliamua kujiuwa kwa kuitosa ndege hii majini kutokana na tukio hili...

Midomo wazi...

Mpaka kufikia hapa,dhana hizo zote hakuna hata moja iliyosaidia chochote kwenye ajali hii ya kustajabisha kabisa bali zinaongeza maswali zaidi....

Hadi leo hakuna taarifa ya kueleweka kuhusu ndege hii.Kila aliyekuwa na ndugu kwenye ndege hii ameamua kuchukulia kwa namna ajuavyo maana hakuna chochote cha kueleweka kuhusu tukio hili...

Huenda kuna siku tutajua ni kitu gani haswa kilichotokea,lakini hadi kufikia leo hakuna taarifa yoyote ya kueleweka kuhusu Flight 370,ndege kutoka shirika la ndege la Malaysia.Ndani ya ndege hii kulikuwa na wanandoa waliokuwa wametoka honeymoon na wanandoa hao ni wa-China.Walikuwa wanarudi nyumbani kuanza maisha mazuri ya ndoa na maisha yao yameyeyuka na ndege hii ya ajabu.....

Tuwape pole wale wote walioguswa na ajali hii kwa namna yoyote ile....

Hii ndiyo dunia tuliyomo....

Tukutane tena wakati mwingine kunako majaaliwa....

Tchao....
 
Wakuu Moderator 's

Ninaamini ninyi ni wasikivu na mnajua shida inayolalamikiwa kwenye jukwaa hili kuhusu namna mnavyozishikilia mada zetu tunazoziweka hapa,naombeni muufanyie moderation uzi huu kisha muuachie mapema maana malalamiko ni mengi sana...

Najua muda huu Paw , Pruner , PainKiller , Reserved na Mhariri mpo online fanyeni yanayostahili wakuu....

Ahsanteni sana....
 
duuh hongera mkuu kwa. makala mzur me naamin hiyo ni ajal ambayo ni planned kabisa si rahis kihivyo kwa Dunia ya leo ipotee ndege afu isijulikane ilipo time will tell kila kitu kitakuwa wazi
Mkuu,hii ajali imeacha wengi midomo wazi kwakweli...

Ngoja tusubiri muda maana huwa hauongopi kabisa....
 
Kuna Watanzania wengi inasemekana lakini
kuwa wametajirika na ndege hiyo au ndege zingine zilizopata ajali na mabaki ya vitu
vya thamani kutoka kwenye mizigo yakawafikia kwenye visiwa vya mkoa wa lindi na pwani

habari hizo nilizipata kimbiji huko nikaoneshwa watu wanaodaiwa kupata mabegi huko baharini yenye vito....sijui ukweli wake zaidi ya kuwa nimesikia tu
 
Mkuu hiii ndege ilianguka na kuzama moja kwa moja baharini kama ilivyo. So far binadamu tunajua zaidi kuhusu space ambayo ni endless kuliko bahari ambayo ipo ndani ya sayari yetu. Tunajua approx 5% tu ya deep Sea, hivyo kitu kikienda chini kabisa sehemu ambazo bado ni unexplored basi tusahau. Hata hiyo ndege ya US Navy P-8A yenye uwezo wa juu katika kuchunguza vitu baharini kuna sehemu kibao za deep Sea haiwezi toboa.

Bado hatuna vyombo vinavyoweza kuwithstand extreme pressure na giza uvunguni mwa bahari.
 
Asante. Makala yako ni nzuri yenye mtiririko kwa mtu kuelewa. Ningeshauri saa ziwekwe kwa Kiswahili badala ya 6:00 asubuhi iwe saa 12:00 asubuhi.
 
Back
Top Bottom