The Dog Day Afternoon...CCM na Dola! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The Dog Day Afternoon...CCM na Dola!

Discussion in 'Great Thinkers' started by Rev. Kishoka, Oct 4, 2008.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  [​IMG]


  This is a best story coming out of Tarime. Nimeonelea nianzishe maada si kuongelea Uchaguzi wa Tarme bali ni kuhusu CCM, Dola na Wananchi.

  Nakumbuka enzi za enzi tulikuwa tunavisha Mbwa jezi za Simba wa Msimbazi. Hata siku moja sikuwahi kusikia kuwa Polisi pale Msimbazi, Polisi wilaya Ilala au Polisi mkoa Dar Es Salaam wakitafuta mchokozi aliyevisha mbwa fulana ya Simba!

  Sasa huyu mbwa kavishwa jezi ya CCM, Serikali (yes Polisi ni Serikali!) ya CCM kupitia vyombo vya dola vimemkamata mwenye mbwa asaidie upelelezi kuelewa ni kwa nini mbwa alivaa vazi "tukufu" la nchi!

  Mbwa huyu, masikini Bobi wa watu ameuawa, najiuliza kosa la Bobi lilikuwa nini wakati yeye alikuwa ni tarishi?

  Labda upande mmoja, nitaelewa kwa nini Polisi wamkamate Mwenye mbwa kwa kuwa kitendo cha Bobi kutembea na fulana ya CCM, kilihatarisha usalama kwa kuchochea fujo.

  Sasa swali langu ni hili kwenu ndugu Watanzania, inakuaje DOLA inafanya kazi kwa umakini kuilinda CCM au CCM ikiwa inahujumiwa lakini wengine na hata Taifa wakihujumiwa, DOLA hujivutavuta?

  Hiza Tambwe katamba kuwa CCM ndicho chama chenye dola, ikiwa na maana ya Serikali na vyombo vyake hasa Mahakama, Polisi na Jeshi. Si mara ya kwanza kusikia Viongozi wa CCM na Serikali yake hasa nyakati za uchaguzi wakitanguliza vitisho vya kulinadi Jeshi la Polisi au nguvu za Serikali kupitia CCM.

  Hivi Watanzania tu finyu wa upeo kudharau mambo na kuishia kughafilika kwa hasira za juu hata kutaka kutoa uhai? Hivi wangemvisha hiyo fulana kichaa, malaya au mwizi anayefahamika wakamtembeza barabarani kumtangaza kuwa CCM ni sawa na Kichaa, Malaya au Jambazi kama namna ya Fasihi, je wale wapenzi wa CCM wangefikia hatua ya kumuua bianadmu anayekidhalilisha Chama chao, badala ya kujibu mapigo ya ki itikadi hata kutunga taarabu au kumtumia John Komba aimbe angalau wimbo wenye kijembe kuwakebehi iwe Chadema, CUF au TLP?

  Ni lini Mtanzania atapevuka na kuachana na hizi hisia mbovu za kujibu kebehi kwa hasira n a kukimbilia kutoa uhai?

  Ni lini CCM wataacha kutishia kila mtu kuwa wao wanamiliki Polisi?

  Je ilikuwa ni sahihi kwa Tambwe Hiza kutamka waziwazi kwenye jimbo la Marehemu Chacha Wangwe kuwa viongozi wakuu wa Chadema ndio watuhumiwa wa kifo cha Wangwe ambacho tuliambiwa ni ajali, lakini Hiza anatamkia umma kuwa kilikuw ani mauaji na wahusika (suspects) ni Viongozi wa Chadema?

  Mbona yeye hakamatwi na Polisi kwa uchochezi? Polisi mko wapi kumkamata Tambwe kwa kuchochea vurugu?

  Hivyo ni sahihi, kwa Tambwe na CCM kutoa kebehi na tuhuma chafu zisizo za kweli wala kuwa na ushahidi na za kichochezi, lakini kwa Wapinzani kuikebehi au kuituhumu CCM na serikali yake, rungu la dola linafanya kazi kwa mwendokasi wa mwanga na umahiri wa hali ya juu!

  Tuliyaona Pemba, Kiteto na kweingineko, sasa yanajirudia Tarime!
   
 2. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Kwanini Mbwa wadhalilishwe?
  Kwani mbwa si rafiki wa binadamu tena?
  Haa mambo ya kinazi ya zamani na kweli ccm wamechokonolewa.
  Utamaduni wetu sisi mwafrika umechanganywa saana na wavamizi wakoloni...
  Na ndio maana mbwa akioanekana mtaani mara nyingine ni mawe tuu!
  Jamani...Hii haijakaa sawa ndugu zangu..Mimi naona badala ya kusema ccm imedhalilishwa...Hapa ni mbwa kadhalilishwa kwani maisha yangekuwa mazuri na utajiri wetu basi hata mbwa nao wangepata chakula na kupewa upendo wanao satahili kama rafiki na walinzi wa wanadamu.
  NB:Wenzetu mbwa hata wale wanaoenda vitani huwa wanabeba bendera na wanafanya kazi za hatari sana huko kwa nusa nusa zao za mabomu nk.
   
 3. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2008
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  on this showing,we still have a long way to go,at first mimi nilidhani CCM wamemvesha mbwa,ili wajipatie kura,silly me,kumbe tanzania yetu mbwa is a non entity.well perhaps with time we will catch up with the world
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
   
 5. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
   
 6. S

  Sam JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2008
  Joined: Jun 6, 2006
  Messages: 416
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
   
 7. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
   
 8. M

  Mkuu Senior Member

  #8
  Oct 4, 2008
  Joined: Jan 1, 2007
  Messages: 127
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wazee mbona haya sio mageni kutokea katika nchi yetu au kwa vile yametokea dhidi ya ccm?kule zaznzibar ni mara nyingi sana watu wa cccm wanazitumia bendera za chama pinzani na kuwavisha mbwa hata fulana zenye picha za mgombea pia na wala sija sikia mtu kakamatwa au mbwa kukamatwa sio kuuwawa hayo kwa upande mwengine wa shilingi ni halali kwa hiyo ni lazima tufahamu katika masuala haya bado kuna mipaka ambayo kuna wenzetu haiwahusu.
   
 9. Black Jesus

  Black Jesus JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2008
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  katika macho ya wahisani wanaoipa misada TZ ni ukatili kutowa roho ya mnyama bilakuwa na sababu na hasa ukiangalia huyo mbwa ni mnyama ambae hakuwa na kosa lolote ni vizuri tukafanya taratibu tukapela kule ili kuonesha jinsi gani Viogozi wa tz walivyokuwa makatiti hata inapofika kwa wanyama wasiokuwa na hatia wacha raia wa kawaida
   
 10. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Tukumbuke pia kuwa mbwa yule hakuvaa ile fulana, alivalishwa! Na matokeo yake ati kauawa! Pengine labda kuna ushirikina, kuna mtu kaaminishwa kuwa mbwa yule kavishwa fulana ili kufanikisha lengo la kichawi!
   
 11. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #11
  Oct 5, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Dah!! Hii nayo kali jamani, yaani mbwa kauwawa na POLISI kwa vile alivaa jezi ya CCM? Hilo linaacha maswali kadhaa:
  1. Kwani mbwa yule alifanya kosa gani la jinai lililosababisha POLISI wamshughulikie?
  2. Je alifikishwa mahakamani akahukumiwa na mahakama kuwa atanyongwa? Tunafahamu kuwa kazi ya polisi ni kukamata na kudhibiti uharifu lakini kazi ya kuadhibu wahalifu ni ya mahakama.
  3. ...............

  On the other note,

  Rev Kishoka unaweza usiamini lakini nadhani bado ni kweli. Kule Australia kulikuwa na sheria au pendekezo la sheria kuwaadhibu watu watu wote wanaowavisha wanyama wao nguo za binadamu kwa sababu kufanya hivyo ni kuwadhalilisha wanyama wale ambao naturally hawavai nguo za binadamu!!!!!!!!!!!!!!

  Kwa sheria ya namna hiyo, miliki wa mbwa ndiye angeadhibiwa huku mbwa akidunda ndani ya jezi ya CCM.
   
 12. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #12
  Oct 5, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Na hasa inapokua ni t-shirt ya CCM maanke hata hao binadamu wanaovaa hilo gwanda la CCM nawashangaa.Mbwa nadhani ndiye aliyedhalilishwa,ni sawa na uende ujerumani leo hii uvalishe mbwa wa watu T-shirt yenye Nembo ya chama cha Nazi na picha ya Hitler.Mkuu utakua umendhalilisha mbwa halikadhalika hapa Nyumbani Mbwa kuvaa t-shirt ya CCm ni udhalilishaji.

  Mbwa alidhalilishwa.
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Oct 5, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Sisi tunafanya vitu kinyume nyume, mbwa aliyevaa jezi ya CCM anauawa kwa kuvaa jezi na siyo kwa kuwa mbwa; lakini mafisadi wanaovaa suti nzuri na kuiba toka Benki Kuu kwa jina la CCM wamepewa siku kadhaa kurudisha fedha. Ilikuwa ni vigumu mno kumvua mbwa jezi na kumpa bobi supu na kutokana na ugumu huo akaadhibiwa kuuawa. Lakini wezi wetu wa CCM wameendelea kudunda na fulana zao za kinga ya Chama huku wakinywa misupu inayotokana na fedha zetu; nani atawavua magwanda yao ya kifisadi?
   
 14. Mkanya

  Mkanya JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 600
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0


  umeona eeeh! yaani hiki ni kituko,ila mapolis walivyo muona huyo mbwa nao walicheka sana (walifurai mno) sasa nashangaa iweje auwawe huyo mbwa asiye na akili.
   
 15. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  kwa nini walimvalisha mbwa tisheti? ni katika kufikisha ujumbe, ujumbe umefika, thamani ya ccm imepungua mno, thamani ya ccm ni sawa ni mnyama kwa sasa, ccm haina utashi, wanaccm wameishiwa utashi, kwa hiyo kama huna utashi thamani yako ni kama mnyama mathalani mbwa.

  ccm wanajua fika hilo, ubinadamu uliwaishia zamani, walipotunga azmio la zanzibar, walipoanza kuiba kura kule zamnzibar 1995! walipoamua kuwa kama mbwa mbele ya chatu, kwa kuwakumbatia mafisadi, kwa kukomba hazina benki kuu, wakati huo leo kuna chuo kikuu kimefungwa zaidi ya wanafunzi 200 wameshindwa kulipa karo zao!ardhi university.

  wakati huo ccm wamechukua chakula cha watoto wakatupia mbwa, yaani wakauza migodi yote, mashirika yote nk

  sasa mwanachi wa tarime atakibeba chama hiki kwa mbeleko gani? chama kisicho na utashi? ni sawa na mbwa

  ccm wanavyokumbatia mafisadi ni kama mbwa na chatu, mbwa hana ujeuri mbele ya chatu, humkimbilia chatu ili akamezwe? ccm ina ujeuri gani mbele ya rostam azizi? manj? etc

  CCM NI KAMA MBWA MBELE YA CHATU, MBWA KUVIKWA TISHETI YA CCM NI SAWA KABISAAAAA, NA UJUMBE UWAFIKIE
   
 16. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #16
  Oct 6, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Jamani inasikitisha huyo mbwa kauwawa kwa kuvalishwa sale ya CCM na mwenye mbwa kufunguliwa mashtaka.Kunawatu wangapi wanaovaa sale za CCM ambao matendo yao hayalingani na sale hiyo?(Ingawa CCM kwa matendo yao ni Mafisadi,Wezi wakuu hawana tofauti)Mkapa,Lowassa Rostam,Change, Viongozi wengi wangazi za juu akiwemo Rais mwenyewe n.k !!!!!!! Wangaeanzia kwa hao sio kuwaua angalau kuwafikisha katika vyombo vya sheria.Ni mara ngapi tumeshuhudia bendera yetu inakanyagwa katika viwanja vya ndege na hata katika jengo la bunge (mbona wanaotembea katika bendera hizo wasikatwe miguu au kuuawa.MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
 17. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #17
  Oct 6, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Cha kusikitisha hapa na kama huyo mbwa aliuwawa kwa sababu hakuwa na kosa basi bila kuzungunga zunguka hicho kitendo ni cha kulaaniwa kabisa. Ila kwa CCM wangepaswa kujisafishwa kwanza kabla hawajaanza kutetea kwa nini mbwa avalishwe jezi yao, ukweli ni kwamba hata mbwa ni msafi kuliko uchafu wa mafisadi wa CCM ambao kwa kinadharia wanafanya chama chao kionekane kichafu japo sio wote!
   
Loading...