The Deceptive Manipulation of "Delilah"

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Nalazimika kurudi nyuma kuanzia mwezi May mpaka August ya 2015, wakati wa mchakato wa kutafuta wagombea Urais kwa vyama vya siasa, hususan Chama "Tawala" Chama cha Mapinduzi.

Nikitafakari hali ya leo hii, giza tororo la ukimya wa sauti zenye kujenga mantiki, kutetea Amani, Utulivu na Mshikamano na hata kutumia busara na hekima kuleta ufahamu na mwelekeo sahihi wa Taifa, najiuliza kama haya tunayoyashuhudia leo ni ubunifu wa makusudi kulifikisha Taifa mahali hapa ambapo imani na amani kati yetu inadorora na kumeguka?

Nimesoma barua ya Hussein Bashe, kuwasilisha hoja binafsi Bungeni ya kuundwa kamati ya bunge kupitia hali ya uvunjifu wa haki na amani unaoonekana kufanywa bila woga na Dola kutuhumiwa.

Najiuliza vitendo vyote vya kuanzia Alphonce Mawazo, Ben Saanane, miili kwenye viroba Coco beach, Uharamia na mauaji MKIRU, uvamizi clouds, kutekwa Roma, shambulio la Lissu, kutekwa Mwandishi Makambako, Akwilina, Luena wa morogoro na sasa Nondo... ongezea kauli za Musiba na hata mengine mengi yenye kunyooshea dola na utawala vidole, je haya yanatokea kwa kuundwa makusudi (by design)?

Najiuliza kama katika kurudisha imani ya WaTZ kwa CCM, WaTZ na hasa watu wa Upinzani tumeingizwa mkenge na kulishwa chuya kutusahaulisha Tatizo letu kuu kuwa ni mfumo na katiba dhaifu na sasa hivi tangu January 2016 tumewekeza nguvu za upinzani kumpinga mtu na kikundi kidogo cha watu na si mfumo mzima ambao umeruhusu uwepo wa watu ambao wamejengewa chuki na sasa kwa umoja tuko tayari kuwaona wakiondolewa?

Upinzani ukajiunga kujenga Ukawa, ukajitutumua kuvunja UKUTA, asasi za jamii na Raia kila mmoja akiongelea ya Udikteta na vyuma kukaza na yote yakielekeza vidole kwa kiuhalisia watu kama wanne au watano wenye madaraka ya kiutawala nchini.

Swali linakuja je, hawa tano wakiondolewa na jamii ikashangilia anguko lao, je safari ya mabadiliko ndio itarudi tena nyuma badala ya kusonga mbele? je kama jamii na Taifa tutaridhika na matokeo ya kuwaondoa hawa wachache ambao kwa sasa wana mamlaka na wanatuudhi?

Je tumejiuliza kama haya tuyaonayo ya kufikia mahali Amani, Utulivuna Mshikamano viko kwenye hatari ni danganya toto iliyojificha na kisha ushujaa wa "wachache" wa Chama Tawala wenye uthubutu wa "kujikosoa na kujisahihisha" kutuletea "mapinduzi baridi" yasiyo na umwagaji damu wala vurugu kama ilivyotokea Zimbabwe na hata Afrika ya Kusini na kwa ujumla wetu tukasifia na kushangilia hatua hizo za "busara na hekima"hata tukasahau na kutupilia mbali azma ya Tanzania mpya kama sauti na mawazo yetu walivyoandaa Rasimu ya Warioba ya katiba mpya?

Je leo azma ya Ukawa kuubomoa UKUTA ukifanikiwa kwa "ushujaa" ndani ya CCM kuubomoa UKUTA, upinzani utakuwa na hoja na sera gani kujiuza kwa Watanzania kuwa wao ni mbadala ya CCM?

Je Ukawa na Upinzani kwa ujumla ulibugi stepu tangu 2015 na kukimbilia kuangalia sura na fursa ya kushinda uchaguzi badala ya kujiuliza fursa ya kubadilisha walau mfumo ambao umezalisha na kulelea "Udikteta Uchwara" walioipoteza kwenye Bunge la Katiba kutokana na kutabirika kwao (predictable to be reactionary)?

Nahisi kama tumejifunga goli wenyewe, tena goli la tobo....na hofu yangu ni jamii nzima kukaa "Mguu Pande! mwili legeza" !
 
Hii ni hoja ambayo inahitaji kuangaliwa kwa karibu. Mpaka upinzani utakapojihoji ni kwanini uliwezesha Magufuli juibgia madarakani malalamiko yake yatapuuzwa. Sisi wengine tuliunga mkono chaguo pekee lililokuwa la lazima kulinganisha na chaguo lile jingine. Hili halikupaswa kuwa hivyo.
 
Acha kujitoa ufahamu kiasi hicho Mkuu!!!! Kama Chakubanga Pori pori analijua hili wewe unashindwaje kulifahamu!? Dah!!!!



Hii ni hoja ambayo inahitaji kuangaliwa kwa karibu. Mpaka upinzani utakapojihoji ni kwanini uliwezesha Magufuli juibgia madarakani malalamiko yake yatapuuzwa. Sisi wengine tuliunga mkono chaguo pekee lililokuwa la lazima kulinganisha na chaguo lile jingine. Hili halikupaswa kuwa hivyo.
 
Back
Top Bottom