Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
Kama kuna kitu cha wazi ambacho ni funzo kubwa kwetu Watanzania katika miaka minne hii ya Awamu ya Tano na "Utawala" (maksudi kabisa badala ya kutumia uongozi) wa Magufuli ni UTHUBUTU!
Uthubutu, ni uwezo wa kufanya mambo bila kuwa na kigugumizi au kujishuku. Ni kufanya mambo, kusimamia unaloliamini bila kujali au bila woga. Sasa kwa Magufuli ambaye tulijua akiwa waziri alikuwa ni mchapakazi mpaka kuitwa bulldozer, ilimaanisha alifanya mambo jinsi alivyoona ni sawa kwa nafasi yake na sasa kwa kupata Urais n kuwa Rais wa Jamhuri, basi Ari, Kasi na Nguvu zake za kuwa Bulldozer na uthubutu zimeongezeka maradufu.
Uthubutu si lazima tuutazame kwa matokeo chanya pekee, hata matokeo hasi yanaweza kutokea kutokana na mtu kuwa na uthubutu, kudhamiria na kufanya lile alilokusidia.
Rais Magufuli ametusaidia sana kutuonyesha kwa vitendo, na si semi, kauli au porojo kuwa kwenye nia pana njia.
Naam, kuna maamuzi mengi yaliyotokana na Uthubutu huu yameleta maswali mengi na hata matokeo ya "uthubutu" kuonekana kama hatua ambazo zilikosa weledi, busara, uhakika au hata hekima. Lakini cha msingi kwa andiko langu hili si kukosoa au kusifia mafanikio au kushindwa kwa maamuzi aliyoyafanya, la hasha... naangalia silika ya kibinadamu ya kuwa na uthubutu, Daring!
Nakumbuka miaka 10 ya Rais Kikwete, uongozi au utawala wake ulionekana umepwaya kwa kukosa Uthubuu wa ukali na kusimamia mambo yafanyike, bila kujali matokeo. Nakumbuka mgombea wa Urais 2015 Bwana Lowassa alinukuliwa mara kadhaa akisema Tanzania inahitaji mtu mwenye kufanya maamuzi magumu, na Watanzania ule u-soft soft wa awamu ya nne, ulitufanya tutake kupata mtu "Dikteta" kauli na nadharia ambazo kwa umoja wa Kitaifa bila hata chembe ya tofauti za kisiasa ai itikadi, ilikuwa ni "natural" kukubali uhitaji wa kuwa na Rais Mkali, Dikteta!
Magufuli kathibitisha katika uanadamu kuwa Uthubutu si jambo la kusadikika, bali li jambo la kweli, lina uhai na kila mtu akikusudia na kujiamini, anaweza kuwa na Uthubutu!
Nikiiangalia Tanzania ilipo leo hii, miaka 58 tangu tupate Uhuru ambapo bado tuko kwenye hatua za mwanzo za kujaribu kupiga vita Ujinga, Umasikini, Maradhi, Unyonge na Utegemezi (UUMUU)pamoja na kutamka kwa vinywa vyetu mahitaji ya maendeleo ya taifa kuwa ni Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora, sifa, hulka na wajihi wa kuwa na Uthubutu bado ni mchanga sana na ndio chimbuko la kukosa kujiamini, kuwa wanyonge na waoga kufanya maamuzi magumu.
Kuna dhana na falsafa inayosema fanya jambo, lisipozaa matunda chanya au uliyotegemea-matokeo hasi yanakupa fursa kurudia mchakato na kujifunza pale ulipokosea na kurudia jambo kwa ubora na umakini zaidi. Cha msingi ni kujiamini na kuwa na uthububu wa kufanya mambo.
Sasa kwa Tanzania yetu ya leo "Ya Magufuli" ya "MATAGA" na "CCM Mpya" utegemezi wa mwenye kujiamini na mwenye kuthubutu kumebakia kuegemea na kumtegemea mtu mmoja, Rais Magufuli. Wengine wote wamekaa kando wakishangilia na kusifia lakini hawana Uthubutu wa kwao wa kujitegemea na kwa nafsi zao bila kutegemea na kuzengea Uthubutu wa magufuli ambao sasa umeambatana na mamlaka na dhama kubwa kama Rais wa nchi.
Tumeshuhudia watendaji wa Serikali na Wanasiasa ambao wana majukumu ya kuongoza nchi, wakigeuka kuwa Wanyapara, wasiojiamini, wakitegemea sana UDola wa Kimamlaka na zaidi turufu yao kubwa ni kusema "maagizo kutoka juu" wakimaanisha ni maelekezo na maagizo ya Magufuli, wakikimbilia kuutegemea Uthubutu wa Magufuli kama ngao na nguzo.
Nasi wananchi ambao hatuna mamlaka au dhamana ya kiuongozi au madaraka, nasi tumekaa kando kwa unyonge au kuachia kila kitu kifanywe na kuamini na kutegemea "ah Magufuli ni kiboko".
Leo haki ya mwananchi inakanyagwa na kupuuzwa, tunakosa Uthubutu wa kudai haki na kusimama imara kukataa kuburuzwa. Ndio kuna hofu na mazingira ya kutishiana ambayo yanatufanya kukosa kujiamini, lakini kwa nini hatumtazami Magufuli yule aliyekuwa Waziri ambaye alisimama na kupata alichotaka na kudhamiria mpaka tukamsifia kwa ujenzi wa miundo mbinu Tanzania?
Nimesema awali, Uthubutu si lazima uzae matoke chanya (ambayo yanaweza kuwa ni mtazamo wa mtu, kikundi au wa aina moja au nyingine) au matendo yanayotikana na Uthubutu yapokelewe kwa mikono miwili na kila mtu. Lakini laiti kama kila mmoja wetu kwa miaka 58 tangu tupate Uhuru wetu tungekuwa na utashi, uimara, ujeuri, kujiamini na uthubutu hata kwa asilimia 50% a uthubutu wa Magufuli, si ajabu Tanzania ingekuwa mbali sana kwenye maendeleo yake ya uchumi, kupanuka na kukomaa kwa haki za watu na yote ambayo tunanung'unikia leo, si ajabu yasingekuwa manung'uniko au kero za kutukosesha raha.
Nikiangalia na kupima Uthubutu wa Magufuli, kuna mengi kafanya (kutenda si lazima kuwe ni sifa ya kufanikiwa jambo) kwa kuamua. Ama ni kutoa maagizo, kuamrisha na kusimamia kikafanyika bila kujali matokeo (consequences or final result) au kuangalia hisia za watu. Mfano, aliazimia kupanuliwa kwa barabara, kukafanyika ubomoaji ili kupisha upanuzi wa barabara hata njia ya reli ya SGR. Hakusubiri majadiliano ingawa yawezekana kukawa na gharama kubwa kwa maamuzi hayo hasa pale penye malalamiko ya fidia.
Akaamua kununua ndege kwa fedha taslimu, zimenunuliwa ndege 5 kwa mkupuo tena kwa fedha taslimu bila kuwa na ukiritimba ambao Serikali na ATCL walifanya kwa miaka 20 kabla ya Magufuli kuboresha au kuwezesha Shirika la ndege kuwa na ndege za kutosha (wengi mtakumbuka ndege za Mattaka). Akasitisha mazoea ya kusafirisafiri ya viongozi na watendaji wa Serikali bila kujali kama kulikuwa na umuhimu wa uwepo na uwakilishi wetu au la, lakini amri yake ilisikilizwa kwa kuwa alisema atatumbua. Leo tumeona Chato inajengwa kwa kasi kubwa; iwe ni maagizo, amri au watu "kujituma" kuhakikisha Chato inakuwa na hadhi kubwa na sasa inageuka kuwa kivutio cha biashara na utalii. Akasema kufanyike uhakiki wa vyeti, wa wafanyakazi wa Serikali, nayo yakatimia. Akasema lazima kila mtu apate stakabadhi akinunua bidhaa ili Serikali ipate mapato... leo kila mtu anahangaika kuwa na stakabadhi! Akasema lazima tuhamie Dodoma, iwe kumekamilika au la, watu wakahamia Dodoma, wengine ofisi ziko kwenye vibanda na wanakaa vyumba vya kupanga.. lakini Serikali imehamia Dodoma.
Sasa najiuliza, sisi kilitushinda nini miaka yote kufanya maamuzi kama haya?ni kigugumizi gani kilitushika kwa muda mrefu kufanya mambo na kuwa na uthubutu, bila kuwa na woga au kujiumauma? kwa nini tuliamini hatuna uwezo wa kufanya mambo kwa hiari lakini tunafanya sasa kwa kuamrishwa na ni sawa na kwamaba tunachapwa mijeledi, tunazinduka na kufanya?
Leo nina uhakika Magufuli akisema tunarasimisha Katiba ya Wananchi iliyotokana na Rasimu ya Warioba, litafanyika bila kupingwa au miguno. Sheria kadhaa na miswaada imepelekwa bungeni na "Chama tawala" ama kwa woga, unafiki au labda ukweli halisi kimepigia kura na kupitisha kila kilichopelekwa na Serikali ya awamu ya tano. Rais Magufuli leo akisema ni marufuku kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya siasa, hakuna atakayebisha.
Sasa ni rahisi kusema yeye ana mamlaka makubwa na anatumia cheo chake, lakini ukweli unabakia kuwa anayafanya kutokana na Uthubutu, daring.. hata kama mara nyingine ni kiholela (reckless) au ni kishari (mercilessly), but he gets shit done regardless.
Je sisi wote tungeanza kujiamini na kuanza kuwa na uthubutu bila woga kufanya mambo tunayoamini ni haki yetu kikatiba, ni wajibu wetu kusimama kuyapigania. Iwe ni nyumbani, makazini, kwenye masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi, kiuzalishaji na kila jambo, uwe ni mfanyakazi, mwajiri, mfanyabiashara, mwanasiasa.. tukiwa wote na uthubutu, na tukafanya maamuzi kwa umakini lakini tukisimama imara kwa uthubutu, basi Tanzania ya Viwanda na Gurudumu letu la maendelo litapiga hatua kubwa na za haraka sana.
Lakini tukiendelea kwua Wategemezi wa magufuli, siku anaondoka tutarudi kule kule, kukwama matopeni na hata kuwa na mawazo potofu ambayo yanajengwa sasa hivi kusema tunahitaji Magufuli akae zaidi ya muda ulioko kwenye katiba.
Namshukuru sana kwa kutuonyesha Uthubutu, tuungane, tusimame imara tufanye mambo kwa uthubutu kupata haki zetu na maedneleo ya kweli na endelevu.
Ahsante Rais Magufuli kwa kutufundisha Uthubutu! Daring, Boldness.. Get Shit Done attitude!