The criminal mind; Kagasheki case,wanasiasa wananunulika.

ray jay

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
1,084
1,500
Katika miaka ya nyuma kidogo niliwahi kusoma kitabu maarufu ambacho kimeandikwa na Mmarekani mwenye asili na mzaliwa wa Italia Mario Puzzo kinachoitwa The Godfather. Kitabu hicho kimeeleza kwa ufasaha wa hali ya juu kuhusu mtandao wa maharamia, mafia na majangili ulivyo imara katika kushirikiana na kuwatumia wanasiasa katika kuhakikisha kuwa mtandao wao wa kuendesha matendo ya uvunjaji sheria na kuimarisha mtandao wao wa kihalifu.

Nikirudi katika suala lililojitokeza hivi punde ni wazi kuwa mtandao wa wahalifu upo Tanzania na una nguvu isiyokuwa na kifani. Kwan kwa namna ya uchangiaji na uwasilishaji wa ripoti ya tume iliyoundwa kufuatilia operesheni tokomeza ni wazi kuwa mtandao umefanya kazi yake na hakika wanasiasa wanaendelea kudhihirisha kuwa wanabei na wananunulika.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom