The Citizen: JK alilishinikiza Bunge kumpa Zitto ulaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The Citizen: JK alilishinikiza Bunge kumpa Zitto ulaji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Mar 20, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Gazeti la The Citizen limeripoti kwamba JK aliingilia kati mchakato wa Bunge wakati lilipokuwa linachagua wenyeviti wa Kamati za kudumu za Mahesabu (parliamentary Oversight Committees) kwa kushinikiza Mbunge Zitto Kabwe wa Chadema apate uenyekiti wa ile kamati ya Mahesabu ya Mashirika ya Umma (POC).

  Likinukuu habari za kutoka vyanzo vyake vya uhakika, gazeti hilo limeandika kwamba baada ya kuona jinsi CCM wakishirikiana na CUF wakila njama za kuhakikisha Chadema isipate uenyekiti wa kamati hata kimoja katika zile tatu za mahesabu ambazo kikanuni ni lazima ziongozwe na Upinzani (yaani PAC, LAAC na POC) Zitto alimpigia simu JK kumwomba aokoe jahazi ili apate uwenyekiti wa hiyo kamati moja (POC) ambayo ndiyo alikuwa akiiongoza wakati wa uhai wa Bunge lililopita.

  Na kweli, JK akatumia uwezo wake ili Chadema wapate hiyo kamati moja.

  Mwenye soft copy in full ya habari hii ya The Citizen tunaomba aiweke hapa.
   
 2. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #2
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  taarifa zilizopo ni kwamba lowassa ndie alie lobby ili yeye na wafuasi wake wapewe nafasi za uenyekiti wa kamati za bunge ili kufanikisha njia kuelekea uchaguzi wa 2015.chunguza kwa umakini utagundua wengi wa wenyeviti wa kamati za bunge ni wafuasi wa huyu fisadi.
   
 3. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Sishangai
   
 4. C

  Chesty JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 2,348
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Sio kitu cha kushangaza hata kidogo kwa TZ. Na ndio maana mwelekeo wa Zitto upo obvious, for everyone to see.
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Heh!

  Siri sasa zaanza kufichka, nami nili-suspect hivyo all along.

  Hata hivyo ninaweza kusema ni JK ndiye aliikuwa behind move yote ile ya kupindisha tafsiri ya kanuni za bunge ili kuhakikisha CDM inyimwe kuongoza kamati hizo nyeti za mahesabu ya umma.

  Sababu kubwa ni kuweka watu ambao watasaidia kuwafichia CCM ufisadi wao katika serikali na Zitto ni mtu muafaka katika kazi hiyo ingawa anataka aonekane mbele ya umma kwamba ni mpmbanaji wa ufisadi.

  Hata hivyo kinachijitokeza zaidi ni jinsi CUF ilivyojidhihirisha mbele ya umma kwamba ni CCM-B maana iliweza kushirikiana na CCM katika njama hizi za kichinichini dhidi ya CDM.

  Mojawapo wa matokeo ya hiyo ni jinsi CDM ilivyokwenda kwa wananchi kuwaamsha kuyabaini madhambi mengi ya CCM, kitu ambacho CCM (na CUF) wanakuja juu kuwaambia eti CDM ni wachochezi etc etc.
   
 6. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  What a shame to JK and Zitto!!

  Pls Confirm the news before we do a tough confrontation to the whole issue!!
   
 7. Magogwajr

  Magogwajr JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hilo gazeti la lini mzee? toa source vizuri tulitafute hata internet.......nasita ku-comment chochote kuhusu hiyo habari hadi nisome source...
   
 8. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mama yangu weeee!!!!!

  Yaani Mkwere ndiye alikuwa akiongoza njama hizo Bungeni huku akiwa Ikulu. Kwa CUF nasema hili: Wananchi walishaanza kuwashitukia tangu Oktoba 31 na sasa watahakikisha mnapotea kabisa huku bara na wala nguvu za CCM mnaowategemea kuwakweza itashindwa!

  That is the truth.

  Yaani CUF mnakubali kamati ya mahesabu ya umma yaangaliwe na watu kama akina Mrema na Cheyo, wa kutoka vyama vya upinzani visiyokuwa na Wabunge isipokuwa wao wenyewe tu? Usaliti mkubwa huu!!

  Kwa hivyo sasa chini ya akina Mrema CCM sasa wako raha mustarehe kwani hao vibaraka wao hawatathubutu kuibua EPA nyingine -- ambazo tunasikia ziko nyingi tu zinazongojewa kuibuliwa.

  Tunaomba Mkwere amalize ngwe yake kwa amani, asiipeleke nchi katika machafuko kutokana na njama zake za kichinichini.
   
 9. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Gazeti ni The Citizen on Sunday la leo tarehe 20 Machi 2011 ukurasa wa mbele ambayo ndiyo habari kuu. Kichwa cha habri cha stori hiyo ni: 'How Kikwete saved the Day for Chadema'
   
 10. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Mmhhh ZITTO ZITTO mbona unatutia aibu kaka!!!!!!!!!!!
   
 11. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  I cant find it on the Citizen website, IT-holic mtusaidie, kama uzushi tujui. Meanwhile ngoja ntafute hardcopy
   
 12. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Nunua hard copy naona bado hawaja-update website yao kama upo nje ya nchi sorry brother
   
 13. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #13
  Mar 20, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  hakuna cha aibu zto baba usisikie mamneno ya watu,we kamuwa tuuuuu,kwani bwana zito kusaidiwa na kikwete kuna shida yeyote ile?
  mimi sioni kama kuna tatizo
   
 14. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #14
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  nimeitafuta hii habari kwenye http://www.thecitizen.co.tz/news sijaipata!! au kuna gazeti la citizens la kiswahili? maana mada ya citizens lakini imeletwa kwa kiswahili au ndio fruits za shule ya kata...
   
 15. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #15
  Mar 20, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
 16. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #16
  Mar 20, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni kwamba JK anaongoza genge la mafisadi katika serikali na Zitto anafahamu hivyo fika.

  Na kama wewe huoni hilo tatizo basi ni mmoja wa genge hilo au unanufaika nalo au ni mbumbumbu tu katika jamii.
   
 17. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #17
  Mar 20, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,846
  Likes Received: 11,965
  Trophy Points: 280
  Mchawi mpe mtoto akulelee atajiuliza mara mbilimbili kabla ya kumuua.
   
 18. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #18
  Mar 20, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mkuu, Heshima mbele!
  Habari tamu sana lakini hukutoa chanzo na Wana JF wameitafuta kwenye The Citizen hawaioni. Unaweza kutuwekea chanzo cha habari ikiwa haitoki "Redio Kifua"?
   
 19. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #19
  Mar 20, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ni rahisi sasa kujumlisha mbili na mbili kupata nne! Sasa akiwa kama M'kiti wa POC tunaona jinsi Zitto anavyohaha kuiokoa serikali ya CCM kuhusu suala la umeme, na hasa kuhusu Dowans suala ambalo linaitikisa CCM ki-kwelikweli, na pia suala la mradi wa Kiwira.

  Lakini kwa upande wa kiwira naona anajiingiza tu kwani halihusu sana kamati yake ya POC -- liko katika kamati ya January Makamba. Ana kiherehere sana kijana huyu, namtabiria mwisho wake kuwa hovyo. Tukumbuke ya Lamwai jamani -- CCM haina rafiki wa kudumu, bali ina masilahi yake ya kudumu -- ambayo ni ufisadi.
   
 20. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #20
  Mar 20, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tunamwomba Zitto aingie humu JF na atujibu masuala haya:

  1. Je ni kweli aliwasiliana na JK kuomba ulaji katika POC?

  2. Kwa nini alifanya hivyo?

  3. Je hakuona kwamba kwa yeye kupewa Uwenyekiti wa POC na JK kunamaananisha kwamba atakuwa anafanya majukumu yake kwa masilahi ya JK (aliyefanikisha kuipata nafasi hiyo) na serikali ya CCM kwa ujumla -- na siyo kwa masilahi ya umma wa Watanzania kwa ujumla?
   
Loading...