Punguza hasira na Belo mkuu.

Kwa kweli Belo ni man utd lakini ni kati ya mashabiki ambao kama hafanyi mzaha anatoaga mchanganuo unbiased.

Ni kweli MPAKA SASA Matic ameonesha ni bora kuliko Bakayoko. Haimaanishi Bakayoko ni mbovu. Waliomnunua Bakayoko nadhani waliangalia zaidi future kwa maana ya umri wao na potential aliyonayo Bakayoko. Huenda Matic hakutaka kugombania namba ndiyo akashinikiza kuondoka lakini wangekuwa pamoja msimu huu angemfundisha Bakayoko a thing or two.
Hilo si katai mkuu lakini huwezi kusema Bakayoko mbovu ni baadhi ya vitu wanazidiana Bakayoko kuna vitu mzuri zaidi ya Matic na Matic kuna vitu ni mzuri hivyo hivyo plus Matic ana expierence na ile ligi for almost misimu mitano sasa kwahiyo anaijua in out lakini pia ni mchezaji mzuri hilo halipingiki sioni tofauti katika Matic ni yule yule aliyekuwa Chelsea ndo yule yule aliyopo United anaperform vizuri vile vile bado.
 
Mtazamo wangu juu ya mechi:

- Playing too defensive kwa kuendelea kumuweka Azpilicueta kama right wing kulisababisha tukafungwa goli mbili leo. Shida ya hii system inampunguzia nguvu ya kushambulia maana anakuwa too defensive na inampunguzia nguvu ya kudefend maana anajua kuna Rudiger nyuma yake.

- Kocha alifanya vyema kumtoa Morata maana aidha bado ana majeruhi hivyo anacheza kwa uoga ama hana nguvu bado za kuhimili mikiki ya Premier League (hapa ndipo wapenzi wa Lukaku wanapopata point kwa nini wanadhani ni bora kuliko Morata). Hata hivyo bado naamini Morata ni chaguo sahihi kama ataweza kubadilika kuendana na physical demands za game za EPL.

- Baada ya kumtoa Morata, kulibaki pengo la kati - kuzuia mipira isivuke kati na ndipo alipomtoa Alonso ambaye alikuwa anazidiwa defensively upande ule. Akamuingiza Willian ambaye Alikuja kucheza nafasi ya Pedro zaidi. Azpilicueta akaenda kushoto.

- Pedro na Willian walicheza wote kama wing back na attacking kwa kupokezana ingawa Pedro alionesha kurudi nyuma zaidi na kumuacha Willian atambae mbele. Hii iliwachanganya Watford kutokujua yupi hasa ni wing back na nani atapanda.

- Kuna moves kadhaa pia zilionesha kama Willian alikuja kati alipokuwa akicheza Fabregas kisha Fabregas akapanda juu. Yote hii iliamsha sana nguvu ya midfield na kuanzia dakika ya 70 hadi mpira unaisha, tuliweza kudominate midfield.

- Kwa kutambua kuwa Willian, Pedro na Fabregas sasa wanaingiliana nafasi na kutaka kusogeza mashambulizi mbele, akaingia Zappacosta kudhibiti ulinzi na Willian akapanda mbele nafasi ya Pedro. Na goli la nne ndivyo lilivyopatikana.

- Kwa kuangalia tu jinsi tulivyocheza dakika 25 za mwisho ni dhahiri kuwa mechi nyingi tulizonazo kocha akiweza kukpanga kikosi hikihiki chembamba vizuri tuna uwezo wa kushinda. Nadhani msimu huu kutokana na kununua wachezaji wengi wageni na kutafuta hasa wapi wanacheza kocha anajikuta anabadili kikosi mara kwa mara lakini akibahatisha chemistry nzuri bado naamini tuna kikosi kizuri sana kulinganisha na timu nyingine kwenye ligi.
Mkuu umeongea point almost kila kitu lakini nadhani kwanini Conte asibadilishe mfumo turudi Kucheza 4-3-3 au 4-2-3-1 maana naona kama wapinzani wameshausoma mfumo wetu wa 3-4-3 na tunakuwa exposed sana wanapofanya counter attack ni vyema tucheze na mabeki wanne(Rüdiger,Luiz,Cahill,Azpilicueta)
 
Quna tetesi qwamba hichi qipindi cha qiangazi qocha anataqa qumtoa Batsman ..ila qazuiliwa; ni qweli waquu..??
Duh mkuu, ni kwamba simu yako haina kitufe cha 'K' ama?

Mpaka napata ukakasi kukujibu kwa uandishi huu aisee. Samahani lakini.
 
Mkuu umeongea point almost kila kitu lakini nadhani kwanini Conte asibadilishe mfumo turudi Kucheza 4-3-3 au 4-2-3-1 maana naona kama wapinzani wameshausoma mfumo wetu wa 3-4-3 na tunakuwa exposed sana wanapofanta counter attack ni vyema tucheze na mabeki wanne(Rüdiger,Luiz,Cahill,Azpilicueta)
Kwa Conte nadhani ni vyema kuongelea kutafuta winger wazuri zaidi. Sidhani kama atabadili nfumo wake hivi karibuni.

Cha maana kutafuta wings wazuri na kuendelea kuomba Kante asiumie tena.
 
Kwa Conte nadhani ni vyema kuongelea kutafuta winger wazuri zaidi. Sidhani kama atabadili nfumo wake hivi karibuni.

Cha maana kutafuta wings wazuri na kuendelea kuomba Kante asiumie tena.
Kante na Drinkwater tunawamiss sana sababu kwa sasa timu haina namba sita tunalazimisha tu maana Bakayoko na Fabregas wote siyo namba sita halisi
 
Hilo si katai mkuu lakini huwezi kusema Bakayoko mbovu ni baadhi ya vitu wanazidiana Bakayoko kuna vitu mzuri zaidi ya Matic na Matic kuna vitu ni mzuri hivyo hivyo plus Matic ana expierence na ile ligi for almost misimu mitano sasa kwahiyo anaijua in out lakini pia ni mchezaji mzuri hilo halipingiki sioni tofauti katika Matic ni yule yule aliyekuwa Chelsea ndo yule yule aliyopo United anaperform vizuri vile vile bado.
Hapa najua nitazusha ugomvi ila wacha niiseme tu hii sentensi:

- Kwa mechi ambazo tumecheza msimu huu. Matic amemzidi Bakayoko kila kitu.

- Kuna siku mchezaji anaharibu tu. Haimaanishi generally kuwa ni mchezaji mbaya. La hasha, huwezi kuwa on top kila siku.

- Mfano mzuri ni game za jana. Bakayoko hakucheza vizuri kama tulivyomzoea ila kwa yeye naweza kumtetea kuwa, sawa na Morata, wanacheza kiuoga kuepusha kutonesha majeraha yao. Kwa jana wote Matic na Bakayoko waliboronga kwenye timu zao. Matic katika tackles sita, alifanikisha mbili tu. Bakayoko kwa upande wake alizidiwa kabisa ubora na Doucoure.
 
Kante na Drinkwater tunawamiss sana sababu kwa sasa timu haina namba sita tunalazimisha tu maana Bakayoko na Fabregas wote siyo namba sita halisi
Na Drinkwater akiwa fit na partnership yake na Kante ikakubali kama walivyokuwa Leicester basi Bakayoko ajue benchi litamhusu sana.

Kwa mtazamo wangu kwa jinsi alivyochezesha kikosi mechi hizi za mwanzo atatumia 3-5-2 maana atamtumia Fabregas zaidi na mbele itakuwa Hazard na Morata.

Mara chache atakazowatumia Willian na Pedro napo pia hakutakuwa na nafasi ya Bakayoko.
 
IMG_2605.jpg
IMG_2607.jpg
IMG_2606.jpg
Hapa najua nitazusha ugomvi ila wacha niiseme tu hii sentensi:

- Kwa mechi ambazo tumecheza msimu huu. Matic amemzidi Bakayoko kila kitu.

- Kuna siku mchezaji anaharibu tu. Haimaanishi generally kuwa ni mchezaji mbaya. La hasha, huwezi kuwa on top kila siku.

- Mfano mzuri ni game za jana. Bakayoko hakucheza vizuri kama tulivyomzoea ila kwa yeye naweza kumtetea kuwa, sawa na Morata, wanacheza kiuoga kuepusha kutonesha majeraha yao. Kwa jana wote Matic na Bakayoko waliboronga kwenye timu zao. Matic katika tackles sita, alifanikisha mbili tu. Bakayoko kwa upande wake alizidiwa kabisa ubora na Doucoure.
Matic kamzidi Bakayoko defensively na siyo kwenye kushambulia mkuu.Bakayoko anaperform vizuri kwenda mbele siyo kurudi nyuma vivyo hivyo kwa Fabregas ndiyo maana hawa wote wanashine vizuri wanapocheza na Kante kwasababu mzigo wa kukaba unapungua kuliko wanapocheza pamoja mkuu.
 
  • Thanks
Reactions: SIM
Na Drinkwater akiwa fit na partnership yake na Kante ikakubali kama walivyokuwa Leicester basi Bakayoko ajue benchi litamhusu sana.

Kwa mtazamo wangu kwa jinsi alivyochezesha kikosi mechi hizi za mwanzo atatumia 3-5-2 maana atamtumia Fabregas zaidi na mbele itakuwa Hazard na Morata.

Mara chache atakazowatumia Willian na Pedro napo pia hakutakuwa na nafasi ya Bakayoko.
Tusubiri tuone kitachofuata
 
458ACCB300000578-5003497-image-a-174_1508592775094.jpg

The All Season Man of the Match for Chelsea...We call him DAVE!

458ACE6E00000578-5003497-image-a-177_1508592872930.jpg

Sina lengo la kumponda Cahill, ila huyu alistahili kuwa Captain wa timu yetu..mbele ya Hazard na Luiz!
Nafurahi siku hizi unaanza kunielewa kwa nini cahill hastahili kuwa capten
Na ukabaji wake ndio siupendi kabisa toka misimu mitatu nyuma
 
Hapa najua nitazusha ugomvi ila wacha niiseme tu hii sentensi:

- Kwa mechi ambazo tumecheza msimu huu. Matic amemzidi Bakayoko kila kitu.

- Kuna siku mchezaji anaharibu tu. Haimaanishi generally kuwa ni mchezaji mbaya. La hasha, huwezi kuwa on top kila siku.

- Mfano mzuri ni game za jana. Bakayoko hakucheza vizuri kama tulivyomzoea ila kwa yeye naweza kumtetea kuwa, sawa na Morata, wanacheza kiuoga kuepusha kutonesha majeraha yao. Kwa jana wote Matic na Bakayoko waliboronga kwenye timu zao. Matic katika tackles sita, alifanikisha mbili tu. Bakayoko kwa upande wake alizidiwa kabisa ubora na Doucoure.
Ni kweli mkuu ila ndio amefika tu nafikiri msimu ujao atakuwa fiti zaidi na tutampenda tu jamaa namfurahia kwa kuwa ni mtu wa kwenda mbele japo ni wa kukaba zaidi
Bao alilofunga batman la nne ni juhudi zake za kupenda kwenda mbele
 
Back
Top Bottom