The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Dau,

Mimi nauliza tu maana kila niliposoma sioni hayo mambo.

Naona hili lilikupita ukiangalia hii thread kutoka mwanzo mwandishi wa VOA ambaye alikuwa katika msafara huo na JK alitoa hizi habari kwa VOA ambao walikuwa wanatangaza jana. Tembelea VOA huenda wakawa na hiyo habari ya Jana wakati JK alipoona JOTO YA JIWE.

Vile vile kuna member amenukuu yale yaliyoripotiwa.
 
Dau,

Imebidi nisikilize tena lakini sijafanikiwa kusikia hicho alichoandika Mwanakijiji. Mimi naona Mwananchi, Tanzania Daima na VOA wameongelea kitu kimoja ambacho ni wananchi kulalamikia maisha yao duni. Rudia maandishi ya Mwanakijiji:

"nasikia msafara wake umekwamishwa kuingia Buzwagi wananchi wanataka wapewe maelezo... mbona mbunge wao hakuambiwa kuwa mkataba umesainiwa?"

Mimi sijaona hilo jambo linapoongelewa.
 
Dau,

Imebidi nisikilize tena lakini sijafanikiwa kusikia hicho alichoandika Mwanakijiji. Mimi naona Mwananchi, Tanzania Daima na VOA wameongelea kitu kimoja ambacho ni wananchi kulalamikia maisha yao duni. Rudia maandishi ya Mwanakijiji:

"nasikia msafara wake umekwamishwa kuingia Buzwagi wananchi wanataka wapewe maelezo... mbona mbunge wao hakuambiwa kuwa mkataba umesainiwa?"

Mimi sijaona hilo jambo linapoongelewa.


Mtanzania

Wananchi walikuwa wameshika mabango yenye ujumbe mbalimbali; kwa mujibu wa VOA Rais alishuka na kuongea na wananchi akiwa njiani kuelekea Buzwagi...lakini mwishoni yule ripota akaulizwa na mtangazaji wa studia; Je raisi alifanikiwa kwenda Buzwagi? Ripota akasema Rais badala yake alielekea Kahama.

Ni maoni yangu kuwa hilo la kwamba wananchi "specific" wamehoji mbona mbunge wao hakuambiwa yalikuwa mawazo ya Mkjj...I could be wrong...ila ni Kweli kuwa Mbunge alisema bungeni yeye hakuwa na taarifa za kusainiwa mkataba.
 
Yebo yebo,

Nakubaliana na wewe 100% ulichoandika hapo juu na ndicho nilichokisikia na kukisoma hata mimi. Ni hatua kwenda mbele
kwamba wananchi wanaanza kulalamika. Lakini pia inabidi kuwa makini ili tusiwe tuna spin stories

Kuhusu Anna Kilango nafikiri tulijadili suala lake hapa:
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=3339

Ingawaje michango ghafla ilibadilika na kwenda kwa yule balozi mjasirimali.
 
kutoka kwa maggid : http://mjengwa.blogspot.com/

CCM kufanya maandamano Jumamosi kuunga mkono uamuzi wa
bunge.

Hivi kweli CCM wako arrogant kiasi hicho mpaka kudiriki hata kuitisha maandamano kuunga mkono ujinga kama ule?

Tanzania tumefika pabaya sana ambapo baadhi ya watu wanajiona kama miungu watu. Hivi JK kweli anashika hatamu kule CCM?
 
Dua,

"nasikia msafara wake umekwamishwa kuingia Buzwagi wananchi wanataka wapewe maelezo... mbona mbunge wao hakuambiwa kuwa mkataba umesainiwa?"

Mimi sijaona hilo jambo linapoongelewa.

Hilo jambo liliongelewa bungeni na mbunge mwenyewe lipo kwenye hansard za bunge.
Debating the 2007/08 budget estimates of the Prime Minister's Office, the CCM legislator declared in parliament his dismay at reports that the government had entered into the mining contract with Barrick Gold for the Buzwagi area, with residents of surrounding villages including himself as their MP being told nothing by the authorities.

This was a good six weeks-plus before Kabwe, the Kigoma North MP representing the opposition CHADEMA party, raised his own private motion on the issue at which point it was turned into an unwholesome, political partisanship affair culminating in the bizarre suspension of Kabwe from all parliamentary activity for the rest of the year.
Soma Hapa

Vile vile kuna maelezo kutoka kwa Barrick wenyewe jinsi walivyokurupushwa kwenda London mara moja kusaini mkataba kwenye hotel wakati wao wenyewe hawana ofisi UK.
 
Dua,

Basi mzee yameisha maana naona tunaongelea vitu tofauti kabisa. labda mimi sikuelewi na wewe hunielewi. Soma maelezo ya Yebo Yebo, ynatoa ufafanuzi wa kutosha.
 
[
QUOTE=Mtanzania;61129]Yebo yebo,

Nakubaliana na wewe 100% ... Ni hatua kwenda mbele
kwamba wananchi wanaanza kulalamika. /QUOTE
]

Mtz,

Unadai kuwa ni hatua kwenda mbele kwamba wananchi wanaanza kulalamika. Wewe unadhani kuwa kwa kumpa ujumbe Rais kupitia walichokifanya maana yake nini? Kuwa wanafurahia?
 
Ndugu Mtanzania tufikie mahali tuangalie Tanzania na si vyama vyetu.Naona michango inavyo changanya nia nk.Umewavaa sana Chadema lakini kumbuka hata CCM sasa wanataka kuandamana kama ni kweli kuhalalisha wizi wa Karamagi na wewe ni Chama chako ? Mimi nadhani tuongelee siasa za Tanzania kulingana na hali iliyopo ama kulingana na muda na matukio yanayo jiri.Kabla ya issue ya Zitto Siasa zilikuwa zimelala na Mzee Ndesa alisha zimwa kwa Malima kupewa msamaha.We need kupambana tu bila ya kujali .Kama ni umoja basi Chadema nadhani wako na wenzao wote wa upinzani kwa kila hali .Ushahidi upo lakini mwisho wa siku Zitto kama Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na mhusika mkuu kwenye hii issue lazima apite na Chama chake kuelezea yanayo tokea kabla ya upotoshwaji hauja anza kupitia Usalama wa Taifa na magazeti yenye ubia na CCM
 
Ibrah,

Sikuelewi una maana gani hapo maana kwa ueleo wangu hakuna nilipoandika kumaanisha wanafurahia walichokifanya.

Maana yangu ni kwamba kwa nchi, raia ana haki ya kulalamika anapoonewa na mambo mengi ndio yanapoanzia hapo.

Huko nyuma watu walikuwa hawatoi malalamiko yao nje na wanaishia kulalamika pembeni. Kama sasa wameamka na kuweza kumkabili JK na kumweleza kukwerwa kwao, hiyo kwa watu wanaothamini utawala wa haki ni hatua mbele.

Kushindwa kusimama imara na kudai haki zetu ndiko kunakotufanywa Watanzania tunyanyaswe. Sasa kama hao wananchi wamepata courage ya kulalamika, mimi naamini ni jambo zuri kwahiyo ni hatua mbele.
 
Nimegundua sasa Majeshi yetu yote na watu wa Usalama wana enjoy mapesa ya walipa Kodi. Juzi Mwanza nimeona wale FFU wamepewa special kofia nyekundu wanatamba njiani eti wanatafuta waingizaji wa mirungi lakini mbele ikaja gari ina wasomali wakakata mapesa mengi wakaachiwa kuingia na mirungi Mwanza , sasa my point ni kwamba JK anaongoza Nchi akiwa amejawa sana na hofu huu ndiyo ukweli wa mambo .Nimemuona kuanzia Tarime majuzi CCM walikuja na 40m kuwahonga wale madiwani ili CCM ichukue Halmashauri lakini Mbowe akawapiga bao .JK alienda huko Mugumu nk akiwa kajawa na hasira .Yeye anafanya kazi kimya kimya huku akijionyesha kwamba ni mtu wa watu .Swala la wananchi kuandamana na kumzuia kuto ingia Buzwagi Polisi wa CCM walikuwa wapi ? Maana wamewezeshwa sana siku hizi .
 
Ndugu Mtanzania tufikie mahali tuangalie Tanzania na si vyama vyetu.Naona michango inavyo changanya nia nk.Umewavaa sana Chadema CCM

Chifu,

Ungesaidia kama ungeeleza ni michango gani inachanganya ili nifafanue na pia kwanini unadhani ninawavaa CHADEMA? Kwanini husemi ninawavaa CCM?

Kwa uzoefu wangu hapa mambo yanayoongelewa kwasehemu kubwa yanahusu CHADEMA na CCM, kuna mengine pia lakini sehemu kubwa ni juu ya hivyo vyama viwili.

Siko hapa kuwafundisha CHADEMA wafanye nini, kwanza uwezo huo sina na CHADEMA wana wetu wengi wenye uwezo kuliko mimi juu ya siasa. Ninachofanya ni kutoa maoni yangu juu ya ninavyoona mimi
kama mwana JF na Mtanzania.

Binafsi sioni kama matatizo ni CCM au CHADEMA au TLP. Ninaamini matatizo ni watu, ni viongozi wa hivi vyama. Aidha ninaamini
viongozi wengi wa CCM ya leo wanatuwakilisha sisi Watanzania tulio wengi, yaani matendo yao ni reflection ya mawazo, fikra na matendo ya Watanzania walio wengi wa leo.

Ni rahisi kuiondoa CCM madarakani kuliko kuondoa hii culture ya ubinafsi, uwizi,uroho, uvivu na uongozi wa mabavu ambayo imetukumba watanzania.

Sasa kama hatusemi haya mambo leo kwasababu CHADEMA ni chama chetu, au hawako madarakani, basi tujiandae kupata akina Mwai Kibaki wengine, akina Muluzi na kale kajamaa ka Zambia nk.

Sasa kama kuyasema hayo ni kuwavaa CHADEMA? basi ni jambo zuri kuwavaa kama tunavyowavaa CCM. Maneno ya Mzee ES yana maana sana hasa "kumkoma Nyani giladi"

Wengine tunaamini hapa hatuogopi mtu wala chama, tutaendelea kuwavaa tu. CCM wakikosea tutasema, CHADEMA wakikosea tutasema lakini pia CCM wakifanya mema tutasema na hivyo hivyo CHADEMA wakifanya mema tutasema.
 
Dau,

Imebidi nisikilize tena lakini sijafanikiwa kusikia hicho alichoandika Mwanakijiji. Mimi naona Mwananchi, Tanzania Daima na VOA wameongelea kitu kimoja ambacho ni wananchi kulalamikia maisha yao duni. Rudia maandishi ya Mwanakijiji:

"nasikia msafara wake umekwamishwa kuingia Buzwagi wananchi wanataka wapewe maelezo... mbona mbunge wao hakuambiwa kuwa mkataba umesainiwa?"

Mimi sijaona hilo jambo linapoongelewa.

Mtanzania, Mkjj hakuwepo mahali pa tukio kushuhudia hayo aliyoyaandika. Inawezekana vyanzo vyake vyenye ushabika viliangalia mambo kwa mawani ya mbao na kuongeza chumvi kidogo. Wekea mkazo neno alilotumia 'nasikia'

Unajua, wananchi wetu wengi vijijini bado wanao ustaarabu wa kiungwana sana, wa kuwaheshimu wageni na hasa viongozi wakuu kama rais wa nchi. Nina hakika, muda si mwingi na kama mambo ya kiserikali yakiendelea kama yanavyokwenda sasa hivi, hali itageuka haraka sana.
 
Jamani, naomba muwe mnaangilia sana maneno ninayotumia. Najitahidi kuqualify vitu vingi ninavyosema ili kuondoa utata wowote ule sasa isije kuwa ya mambo ya mtu kunianzishia mada na kusema "mwanakijiji alisema hivi"! Mara nyingi details zinakuwa sketchy inapotokea breaking news. Kumbuka kuwa taarifa yangu niliiweka kabla ya VOA so source yangu siyo VOA niliwaambia sikilizeni VOA kwa vile Source yangu on the ground iliniambia kuwa kulikuwa na mtu wa VOA kwenye msafara.
 
Jana JK alikwenda kwenye dinner ya usiku hapa kahama kwenye ukumbi wa lake house na alishindwa kuongea na pia hakusalimia .anaonekana kuchanganywa sana na labda ni kuwa ni juu ya yale majibu ya mkurugenzi wa barrick kuwa Karamagi na Kikwete ndio waliwaita wande london kusaini mkataba husika na hili nafikiri liwekewe tread yake kwani hili linaibvua hoja mpya kuwa kumbe waziri ndio alidanganya zaidi kuwa alikuwa anawahgi kumbve yeye ndio aliwaita kwenda bar kusaini mkataba husika.
 
MOJA ya wabunge makini nimrod MKONO Alipata kugoma kwenye sherehe ya kukabidhi dola laki mbili kwa halmashauri yake ya musoma zilizotolewa na barrick akisema hicho kiwango ni kama tusi .....

Una maana makini katika style yake ya KULADAU la walalahoi nchini?

Tanzanianjema
 
Jana JK alikwenda kwenye dinner ya usiku hapa kahama kwenye ukumbi wa lake house na alishindwa kuongea na pia hakusalimia .anaonekana kuchanganywa sana na labda ni kuwa ni juu ya yale majibu ya mkurugenzi wa barrick kuwa Karamagi na Kikwete ndio waliwaita wande london kusaini mkataba husika na hili nafikiri liwekewe tread yake kwani hili linaibvua hoja mpya kuwa kumbe waziri ndio alidanganya zaidi kuwa alikuwa anawahgi kumbve yeye ndio aliwaita kwenda bar kusaini mkataba husika.

The buck stops with JK. Huyu jamaa ni kilaza na limbukeni huwezi kuongoza nchi kwa mishen town. Inflation inapanda kwa kasi wakati yeye na EL wanagawa pesa kama njugu ambazo hawajui zilitoka wapi. Wako busy kuchuma utajiri kwa sababu ya matumbo yao. Hii ndio sababu mnaweza kuelewa tangu ashike madaraka angalie safari alizopiga za huko Mwanza kwenye share zake halafu trip za Uarabuni.

Hivi sasa ana kiwewe maana wabongo wamekwisha mjulia janja yake .............................na bado tutaona mengi subirini.
 
Katika pita pita yangu nimekutana na presentation hii ya Marehemu Prof. Chachage ... its a very nice read hasa katika mwanga wa kile kinachoendelea Buzwagi na sehemu nyingine zenye madini.
 

Attachments

  • chachage.pdf
    200.2 KB · Views: 42
Back
Top Bottom