The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Zito akichangia bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, amesema kwamba Waziri Karamagi alikwenda kusaini mkataba wa Mgodi wa Buzwagi, London kwa kutumia mfumo wa mikataba wa zamani wakati serikali ikiwa inajadiliana na wawekezaji kurekebisha mikataba hiyo.
 
AMEKIRI KUSAINI Mkataba wa Buzwagi huko London, lakini anasema kwamba hauna mapungufu yaliyokuwapo katika mikataba ya zamani.

Anasema kabla ya mkataba kukamilika inabidi kufauata
Kwanza wataalamu wizarani. Then mwanasheria wa serikali
Lakini mpaka hapo hauwezi kusainiwa mpaka upitie na kamati ya ushauri ya madini.

Akasema Mkataba huu wa Buzwagi umepitia taratibu hizo zote lakini wakati mkataba huo unajadiliwa, ndio kulikua na kikao cha bodi ya Barrick na Wakati ule yeye alikua amesafiri na Rais nchi za nje na mkataba huo wataalamu walikuwa wanamalizia kuandika.

Wakaniambia kuhusu tatizo la bodi, nikaawaambia waniletee na aliyeleta ni mwanaseria na Wizara si wa kampuni ya Barrick,na wakati huo yeye kwa kuwa ametokea sekta binafsi alitumia hiyo kasi ya Private sector katika kuharakisha huo mkataba ili asiwacheleweshe wamiliki wa Barrick

Pia akadai kwamba mgodi wa Buzwagi hauna rasilimali kubwa na hivyo ni mgodi mdogo.

Haya kazi kwenu Watanzania
 
Zito kawasilisha hoja akitaka kuwasilisha bungeni hoja ya kutaka kuundwa kwa kamati teule kuhusu kauli ya Karamagi akijibu tuhuma za kwenda kusaini mkataba London. Amesema Waziri kadanganya BUNGE
 
Wabunge wamjia juu Waziri Karamagi mkataba mpya London
*Washangaa uzembe wa serikali kuruhusu mchanga
*Wataka Stamico kurejeshewa meno

Na Daniel Mjema, Dodoma

WABUNGE wamedai kuwa suala la kupanda kwa mafuta na migodi mikubwa kumilikiwa na wageni kuwa ni ushauri mbovu na uzembe wa watendaji serikalini.

Masuala ya madini, kupanda holela kwa bei ya mafuta na kutopelekwa kwa umeme vijijini ndio mambo makuu yaliyozua mjadala mzito bungeni mjini hapa jana wakati wabunge wakichangia bajeti ya Wizara ya Madini na Nishati.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA) alihoji hatua ya Waziri wa Madini na Nishati, Nazir Karamagi, kusaini mkataba mpya wa madini na Kampuni ya Barrick wakati serikali haijamaliza kupitia mikataba ya zamani.

Zitto alisema inashangaza kwamba wakati agizo la Rais Jakaya Kikwete la kupitiwa upya kwa mikataba halijafikia tamati, Waziri Karamagi ametia saini mkataba na kampuni hiyo kufungua mgodi mpya wa Buzwagi.

"Kinachosikitisha ni kuwa mkataba huo umetiwa saini kwa niaba ya Serikali na Waziri wa sasa wa Madini na Nishati tena utiaji saini mkataba huo umefanyika London (Uingereza) na sio Tanzania," alisema Kabwe.

Kabwe aliongeza kuhoji: "Ni kwa nini mkataba mpya umesainiwa wakati taifa linapitia mikataba. Vitu kama hivi ndio mwanzo wa rushwa…tunataka kufahamu vipengele vya mkataba huu."

Pia, alitaka serikali itoe maelezo ni kwa nini iliuza hisa ilizokuwa ikimiliki katika migodi nchini na sasa inataka kumiliki tena hisa na akatahadharisha kuwa dhahabu inayochimbwa na kampuni ya Barrick itamalizika baada ya miaka 18.

Kwa upande wake, Mbunge wa Nzega, Lucas Selelii (CCM), alisema kukamatwa kwa mchanga wa dhahabu uliosombwa Kahama na baadaye kukamatwa jijini Dar es Salaam ni uzembe wa serikali.

"Wizara imejiondoa mno katika usimamizi wa uchimbaji madini kwa makampuni makubwa kiasi kwamba wanachimba wenyewe, kufunga madini wenyewe na kusafirisha wenyewe halafu watuletee taarifa, hii haifai," alisema Selelii.

Selelii alisema, makampuni hayo yanachukua mchanga wenye dhahabu kutoka kwenye mashimo na kuupakia moja kwa moja kwenye malori na kupeleka nje ya nchi bila kupitia kwenye mitambo ya uchekechaji.

Mbunge wa Rufiji (CCM), Profesa Idriss Mtulia, alitaka Shirika la Madini (Stamico) lirudishiwe jukumu lake la kusimamia uchimbaji wa madini nchini na akataka linunue mitambo ya uchimbaji na kuikodisha kwa wachimbaji wadogo.

Kuhusu suala la kupanda kwa bei ya mafuta nchini, Mbunge wa Viti maalumu, Mhonga Ruhwanya (Chadema), alitaka wabunge wa CCM kutosikitikia hali hiyo wakati wao ndio waliounga mkono kupitishwa kwa bajeti hiyo kwa mbwembwe nyingi.

"Nimeletewa ujumbe na wananchi wa Kigoma wananiambia niwaulize wabunge wa CCM walikuwa wapi mafuta yakipanda na wao ndio walioshabikia bajeti…wananiambia niwaulize wanasikitika nini sasa," alisema Ruhwanya.

Mbunge huyo alipendekeza serikali iliwezeshe Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), kiwe chombo pekee cha kuingiza na kusambaza mafuta nchini kwani, kwa kufanya hivyo inaweza kudhibiti biashara ya mafuta nchini.

Kwa upande wake, Mbunge wa Bukene, Teddy Kasella-Bantu (CCM) alitaka serikali iyabadili magari ya kifahari aina ya Toyota Land Cruiser, maarufu kama mashangingi ili yatumie gesi asilia kama njia ya kubana matumzi.

"Kuwepo na utashi wa kisiasa ili serikali iyabadilishe magari yote ya serikali na mabasi ya abiria ili yatumie gesi asilia kwa kuwa matumizi ya nishati hiyo ni nafuu mara dufu kulinganisha na mafuta ya petroli," alisema Kasell-Bantu.

Alitoa mfano kuwa, Land Cruiser likitoka Dar es Salaam kwenda Dodoma litatumia gesi asilia yenye thamani ya Sh18,000 tu wakati kwa hali ilivyo sasa magari hayo hutumia zaidi ya Sh100,000 kwa umbali huo huo. Umbali wa kutoka Dar es Salaam mpaka Dodoma ni kilomita 453.

Kuhusu hoja ya kupanda kwa bei ya mafuta, Selelii alisema matatizo yanayolikumba taifa hivi sasa yanatokana na ushauri mbaya ambao serikali ilipewa na watendaji wake na kufikia uamuzi wa kuitelekeza TPDC.

Mbunge wa Viti maalum, Josephine Genzabuke(CCM), alisema kutokana na tamaa ya utajiri wa haraka, baadhi ya makampuni ya mafuta yamekuwa yakichanganya mafuta ya ndege na dizeli na kuyauza kama mafuta ya taa.

Genzabuke alisema matumizi ya mafuta hayo yamekuwa na madhara makubwa hasa kwa wananchi wa eneo analotoka la Kigoma ambako watu watano wameshapoteza maisha kwa kulipukiwa na mafuta hayo.

Wabunge karibu wote waliochangia bajeti hiyo, kilio chao kikubwa kilikuwa ni umeme vijijini, huku Ruhwanya akisema maendeleo ya Kigoma yanachelewa kusonga mbele kutokana na kukosekana kwa umeme.

Baadhi ya Wabunge ambao maeneo yao hayajafikiwa na gridi ya taifa, waliiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kupeleka jenereta ili wananchi wa maeneo hayo waweze kushiriki katika kukuza uchumi.
 
...ni ya msingi.

...ila baadhi ya issues wanazichukulia juujuu bila kupata details ambazo zingewafanya wasizishikilie bango kiasi hicho!

...kama ni chakula kina chimvi nyingi!ila kinalika hivyo hivyo!
 
na Schola Athanas

WAZIRI wa Nishati na Madini, Nazir Mustafa Karamagi, jana alidai kwamba aliokolewa na Spika wa Bunge, Samuel Sitta kutoka katika kibano cha wabunge wakati wa kuchangia hotuba ya bajeti ya makadirio ya wizara yake.
Akizungumza katika kipindi cha Bunge Wiki Hii, kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TvT) na kuongozwa na Tido Mhando ambaye ni mkurugenzi wa kituo hicho, Karamagi alisema Sitta alimuokoa baada ya kuvunja baadhi ya vipengele katika kanuni za Bunge, vinavyowawezesha wabunge wengi kuchangia.

“Mjadala ulikuwa mkali kidogo, si kwa nia mbaya, ni kwa nia ya kuboresha, ni kweli, vyombo vya habari viliandika kuwa niliokolewa na Spika, hii ni kutokana na Spika kuvunja baadhi ya vipengele katika kanuni za Bunge, vinavyowawezesha wabunge wengi kuchangia,” alisema Karamagi.

Alisema wabunge wengi walikuwa na hamasa ya kuchangia ili wapate umeme katika maeneo yao, hivyo kulikuwa na maswali mengi.

Akizungumzia baadhi ya hoja za wabunge zilizotolewa katika mjadala wa wizara yake, alisema suala la wageni pekee kufanya utafiti wa awali wa madini si la kweli kwa kuwa kuna Watanzania 5,800 wanaofanya utafiti huo na wamekwishapewa leseni za kazi ya kuchimba madini.

“Bado wizara inaendelea kutoa leseni kwa Watanzania ambao waliingia katika maeneo ya wachimbaji wenye leseni kubwa, hawa tunawaondoa katika maeneo hayo na kuwatafutia maeneo mengine ilimradi wafuate sheria,” alisema Karamagi.

Kuhusu mikataba kuharakishwa na kubadilishwa, alisema huwa inabadilishwa na inatofautiana kati ya mikataba ya zamani na ya sasa.

Akizungumzia agizo la rais la kupitia upya mikataba ya madini, alisema si jambo rahisi kuiondoa haraka kwa sababu mikataba ina taratibu zake, hivyo inapaswa kuwasiliana na wenye kampuni ili kuwaomba wakubali kuibadili kwa hiari yao.

“Mikataba ya mwanzo ilikuwa kwa ajili ya kuwavutia wawekezaji, hivyo kwa kuwa soko la madini la Tanzania limeishajulikana, tutabadilisha vipengele kwenye mikataba ambavyo tuliviweka kwa ajili ya kuwavutia.

“Na hata mafuta na gesi, kuna kampuni 19 ambazo zinafuatilia, nishati hizi zimeshagundulika katika maeneo ya Songosongo, Mnazi Bay, Mkuranga na Kigoma Bay,” alisema Karamagi.

Akizungumza katika kipindi hicho, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), alisema serikali iliahidi kuwa mikataba ya madini itabadilishwa na kamati itaundwa, cha kushangaza bado mikataba inaendelea kusainiwa kinyume cha azma ya serikali na rais mwenyewe.

“Mikataba inatakiwa kubadilishwa haraka kwani kuchelewa kunasababisha kampuni kushindwa kulipa kodi haraka ambayo ni asilimia 30, kutokana na kuondolewa kwa vipengele katika sheria ya mwaka 2001-2002, kuna kampuni ambazo zilitakiwa kuanza kulipa kodi ikiwemo Barrick, lakini inashangaza kuona wakisaini mkataba mwingine,” alisema Kabwe.

Gema Akilimali kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), alisema wawekezaji wanaokuja kuchimba madini wanakuja kunyang’anya maeneo kwa sababu wanawakuta wananchi wanachimba madini katika sehemu hizo, hivyo hawafanyi utafiti kama inavyodaiwa katika mikataba hiyo.

“Nashauri wavune madini, lakini badala ya kuyauza nje kama madini, vitengenezwe vito vya thamani na viuzwe ili taifa lipate faida zaidi,” alisitiza Akilimali.

Katika mjadala wa makadirio ya wizara yake, Waziri Karamagi ambaye ni Mbunge wa Bukoba Vijijini, alibanwa kwa kiasi kikubwa na wabunge, wengi wakitaka maelezo ya kina juu ya kero ya umeme, mikataba ya madini na mambo mengine kadha wa kadha.

Hata hivyo, kutokana na idadi kubwa ya wachangiaji ambao kila mmoja alionekana kuwa na hoja nzito, Spika alilazimika kuingilia kati mara kwa mara na hatimaye kufanikisha kupita kwa mbinde kwa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.
 
Bravo Karamagi kwa kuweka ukweli hadharani kuwa spika alikuokoa

Hatuwezi kujenga taifa kwa mawaziri wetu kusema uongo na kumtegemea spika kuwakingia kifua..
 
Jamani hii mada mbona inakosa nyama nyama... Karamagi alisema nini na Zitto alikuwa anataka nini kifanyike? Ni wapi Karamagi amekosea?
 
Jamani hii mada mbona inakosa nyama nyama... Karamagi alisema nini na Zitto alikuwa anataka nini kifanyike? Ni wapi Karamagi amekosea?

Mzee Mwanakijiji ... hoja ya kwanza ya Mh. Zitto ni kwamba imekuwaje Mh. Karamagi amesaini mkataba mpya wa uchimbaji dhahabu kule Buzwagi wakati zoezi la kupitia mikataba ya zamani bado halijakamilika? Kusaini mkataba mpya ni kukiuka agizo la rais aliyeagiza kwamba mikataba yote ya madini ipitiwe upya na ifanyiwe marekebisho.

Hoja ya pili, ni kwanini alisaini huo mkataba akiwa London badala ya kusaini akiwa Dar? Hali hiyo inapelekea harufu ya rushwa au mazingira ya kusaini mikataba ya aina ile iliyosainiwa zama za BWM.
 
admn.. tafadhali unganisha hii na ile ya hapo juu ya Halisi kuhusu Karamagi kwenda kusign mikataba nje...
 
Anybody head of the below statement? Let me paste it here, taken from somewhere else, with apologies...

"You have 1000 cows, you don't want to milk them, you are too lazy even to think about them. You request investors to milk them for you, they milk the cows and take all the milk, your children suffers malnutrition, investors pay you 30 Tshillings, you sign an agreement with them in their countries - abroad, they give you some money as bribery and you buy a litter of milk from the same investors! but for your concubine!"

It is becoming a coincidence?
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom