The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

hata Kampuni kubwa la Enron kabla ya viongozi wake kuiba mamilioni ya pesa za wafanyakazi na wateja lilisifiwa na wall street?

Barrick itasifiwa tena sana mwaka huu
 
CCM NI MUFILIS! Kama walivyosema wadau wengine, hawa jamaa wawili ni makapi ya vyama vya upinzani na ndio hao leo waonekana ni wakamanda wa kutumainiwa katika mapambano ya CCM ya kutaka kujisafisha. Unajua, kama mkono wako una matope halafu ukautumia mkono huo huo kujifuta uso kinachotokea hapo ni kujichafua uso wako. Sasa hivyo ndio SiSiMafisadi wachofanya. Wapo hoi hawa wendazimu.
 
siku chache tu baada hao mafisadi kuumbuliwa mbele ya kadamnasi naona imekuwa tabia ya kila fisadi wakipishana kwenye korido za maofisi yao wanakofanyia upuuzi wao ili kuita waandishi wa habari kwa madai ya kujisafisha.Kinachoshangaza zaidi hao watu wanajikanyaga zaidi nakuzidi kutupa full data maana kitendo cha karamagi kukana kuwa hajasaini mkataba london kuna maanisha nini? au amesha sahau alipolotwambia? halafu kwanini akatae kulizwa maswali? huko ndiyo kujisafisha au kujichafua? hivi shilling ina thamani ikiwa na sura ngapi? mimi nafikiri kama lengo lake lilikuwa kuongea bila kulizwa bora angeitisha injili ambapo hupashwi kuhoji maneno ya padri. naje kwanini waandishi wa habari mkakubali kuandika wakati yeye amekataa msimuulize? Namshauri karamagi bora anyamaze tu kama Mkono, maana kadri tukiona sura yake kwenye lunginga wengine tunatapika. akimpeleka Dr.Slaa mahakamani ataumbuka zaidi maana mpaka sasa sisi tunaamini mtumishi wa mungu Dr.Slaa nimkweli mpaka hapo karamagi atakapotueleza tena mabilioni aliyotudanganya kutokana na mkataba aliosini yatatoka kwenye biashara zake za makontena au lah!
 
Waziri Karamagi atetea mkataba wa Buzwagi
Stella Nyemenohi
HabariLeo; Friday,September 28, 2007 @00:02
WIZARA ya Nishati na Madini imeeleza kushangazwa kwake na mjadala unaoendelea juu ya mradi wa Buzwagi. Imesema huo ni mkataba ulioboreshwa kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na mingine iliyowahi kusainiwa.

Katika kile ambacho Waziri Nazir Karamagi alikieleza jana kuwa wapinzani wameamua kutumia mradi huo kama hoja ya kujiegemeza katika siasa, alisema mkataba huo una maeneo mengi yaliyofanyiwa maboresho kwa maslahi ya nchi.

“Mkataba huu hauna tofauti na ile ya zamani; labda upya wake ni kwamba huu ni mkataba bora uliofanyiwa marekebisho makubwa….. wapinzani hawana hoja, wanatafuta mahali pa kuegemea,” alisema Karamagi.

Karamagi, ambaye hata hivyo hakuweza kubainisha kama nakala ya mkataba iliyosambazwa juzi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ni sahihi au la, alisema hakuna kitu kigeni kilichojitokeza katika mkataba huo. “Huo mkataba waliosema watasambaza sijauona kwa hiyo siwezi kufahamu kama ndiyo wenyewe au la,” alisema Karamagi alipozungumza na HabariLeo kwa simu.

Hata hivyo, alisisitiza kuwa ipo taarifa rasmi ya serikali itakayotolewa wiki ijayo kuelezea uwazi wa mkataba huo na vipengele mbalimbali vilivyoboreshwa ikilinganishwa na mikataba iliyopita ya namna hiyo. Miongoni mwa vipengele vilivyomo katika mkataba huo ni kipengele cha urudishaji wa mitaji ya uwekezaji.

Wakati awali gharama ilikuwa ni asilimia 100 kwa mwaka wa kwanza, mkataba wa sasa unaonyesha kuwa urudishwaji huo utakuwa ni asilimia 80 kwa mwaka wa kwanza na baadaye, miaka inayofuata ni asilimia 50. Vile vile, ndani ya mkataba huo, yapo masharti kuhusu kununua bidhaa na huduma mbalimbali, kwa wawekezaji kutakiwa kuzingatia hilo kwa kununua bidhaa za hapa nchini. Kipengele kingine ni masharti kuhusu kuchangia Mfuko wa Uwezeshaji kupitia Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwezeshaji wa dola za Marekani 125,000 kwa mwaka.

Wakizungumza na gazeti hili, baadhi ya maofisa wa serikali walisema viongozi wa upinzani wametumia udhaifu wa serikali wa kutokuweka bayana sera mbalimbali zinazotengenezwa kwa ajili ya wananchi.

“Ukikaa na kuchunguza madai ya wapinzani, hupati hoja ya msingi. Cha zaidi, wamewateka wananchi kwa mawazo kwa kutumia udhaifu wao wa kutokuelewa sera na michakato mbalimbali inayoandaliwa kwa ajili yao,” alisema ofisa mwandamizi wa serikali ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Ofisa huyo alishauri badala ya serikali kujibizana na wapinzani hao, iandae utaratibu wa kuwashirikisha wananchi kufahamu sera mbalimbali zilizotengenezwa kwa ajili yao kuepusha kutekwa na watu wenye ajenda binafsi za kutafuta madaraka.
 
Waungwana kama mnavyofahamu Karamagi atafanya mkutano na waandishi wa habari hapo Jumamosi, Sept 29, 2007. Tuweke maswali yetu hapa ndugu zetu waandishi wa habari waliokuwepo hapa wanaweza kuyatumia baadhi ya maswali hayo hiyo Jumamosi.

1. Mh. Baada ya kuvuja kwa mkataba wa Buzwagi kati ya serikali ya Tanzania na Barrick je, serikali ina mpango wowote wa kuweka bayana mikataba ya mwanzo kati yake na Barrick ambayo hadi hii leo bado ni siri?

2. Kwa maoni yako unaona huu mkataba wa Buzwagi una maslahi yoyote kwa Tanzania na Watanzania?
 
Hiza, Akwilombe watumika kummaliza Zitto

Na Patrick Mabula, Kahama


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewatumia wanasiasa waliojiunga kutoka Upinzani kuzima hoja za mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe, kuhusu mgodi wa Buzwagi wilayani hapa, kuhusu mkataba wa madini kusainiwa Uingereza.

Wakihutubia mkutano wa hadhara juzi wanasiasa hao Bw. Tambwe Hiza aliyetoka CUF na Bw. Shaibu Akwilombe aliyetoka CHADEMA, walisema Bw.Zitto alitunga uongo na anatafuta umaarufu wa kisiasa.

Awali, Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusufu Makamba, aliyeanza kuhutubia, aliwaeleza wananchi wa hapa kuwa madai ya Bw. Zitto ni ya uongo yenye lengo la kukwamisha uwekezaji na maendeleo ya wananchi wilayani hapa.

Alisema wananchi wanapaswa kumpuuza, kwani ana lengo la kukwamisha ajira ya vijana wapatao 600 watakaoajiriwa na mwekezaji wa Kampuni ya Barrick wakati mgodi wa Buzwagi utakapoanza kazi.

Bw. Makamba alisema anashangazwa na baadhi ya wananchi wa Kanda ya Ziwa kumpokea Bw. Zitto kama shujaa wakati hoja zake zilikuwa si za kweli na kuwataka watu wa hapa, atakapokuja wasimpokee kwa namna hiyo wakati wa ziara yake.

Bw. Akwilombe alisema yeye anamfahamu vizuri Bw. Zitto kuliko watu wa hapa, na kwamba hoja zake zilikuwa za kutunga ili kutafuta umaarufu, kwa kuwa hakuna sheria yoyote inayozuia mkataba kusainiwa nje ya nchi.

Alidai yeye akiwa CHADEMA walipanga mbinu za kutengeneza uongo ili wapate umaarufu na kuongeza kuwa hata mkataba wa Reli yaTAZARA ulisainiwa China, lakini reli ilijengwa nchini, hivyo akawataka wananchi wampuuze Bw. Zitto.

Bw. Akwilombe alisema akija kuhutubia masuala ya mgodi wa Buzwagi, kama anavyohutubia sehemu zingine za Kanda ya Ziwa na kupokewa kishujaa wampuuze.

Naye Bw. Hiza alisema CHADEMA wanatumia kigezo cha mgogoro wa mkataba wa Buzwagi kuzunguka nchi nzima kutafuta umaarufu na kujipatia wanachama.

Alisema lengo kuu la Bw. Zitto kuzusha hoja hiyo bungeni ni kutaka iundwe tume ya kuchunguza utiwaji saini mkataba huo ili yeye awe Mwenyekiti wa Tume hiyo ili ajipatie posho wakati wa uchunguzi.

Alisema mbunge anapoanzisha hoja ikifanikiwa kuundiwa tume yeye anakuwa ndiye Mwenyekiti, hivyo mgogoro wa Buzwagi lengo lake lilikuwa kutafuta fedha za Tume hiyo ambayo ingefanya uchunguzi hadi Uingereza ulikofungiwa mkataba.

Bw. Hiza alisema kama Tume ya Malima ilitumia sh. milioni 100 uchunguzi wa uwekaji mkataba wa Buzwagi ungegharimu zaidi ya kiasi cha pesa, kutokana na uchunguzi wake kufika Uingereza.

Alisema mkataba uliowekwa ni halali na taratibu zote zilifuata sheria za nchi na kuwataka wananchi wasiyumbishwe na hoja za wapinzani ambao alidai yeye anawafahamu.

Watanzania wa leo si wale wa mwaka 47! Nani atakayeaamini hawa waganga njaa ambao waliokimbilia CCM ili wakaukwae ungunge!? Watanzania wanaijua vizuri sana hakuna jipya hapa wanajibaraguza tu, Watanzania wameshasonga mbele, kama hakuna mabadiliko ya kweli yatakayowaridhisha wananchi basi nyie MRIE tu juhudi zenu zote zitagonga ukuta.
 
Kila wakijaribu kukaa kimya wanashindwa.

Eti hajapata nakala!
Sasa ni vipi waziri mzima kujibu hoja bila kuona mkataba ulio sambazwa?

Serikali inaandaa hoja?

Yaani ninyi washenzi akina Karamagi mnapika data nyingine mpya? Angalieni msijikanyage zaidi na baadaye zikatuma dhidi yenu wenyewe?

SISIEMU wanatushangaza kweli wanakaa kidete kutetea Uoza mnuko ili wasiondoke madarakani? Sasa mwenye tamaa ya madaraka ni nani?

Karamagi ananipa kicheko cha hasira!

Sasa huu kama ni mkataba mzuri hiyo waliyodai wanarekebisah ikoje?

Pengine humo kuna kipengere cha Akina Barick kutembea na wake na dada zetu kwa mtindo wa SANDWICH wakati wowote wakijisikia!!!

Mwe!!

Kabla ya uchaguzi wa 2010 nitasikia mengi.
 
hawa wapuuzi kweli kweli eti anaongelea 125,000$ eti kama mchango wa maendeleo,huku wakichukua billions yaani tumejaza vilaza tuu ,si bora hata wasichimbe wasubiri tuchimbe wenyewe tukipata uwezo..maana hiyo 3% is a big joke,na wanasema sheria za madini ni copycat from Australia lakini wamesahau wachimbaji wa Australia ni wenyewe wananchi na mtu wa nje huwezi pata more than 25% kwa hiyo pesa yote inabaki Australia....wapuuzi kweli kweli hawa wanauza nchi.
 
Zitto kiboko yao hata wakimwondoa ukweli umesha kuwa bayana sio kama alivyoondoka AC. Tumeshindwa kumpa tano kwa sababu hakutuachia urithi mkononi isipokuwa Usia ambao kutokana na mazingira umesha zimwa. Zitto hakulala katupa urithi na tutauenzi kwa hali na mali zetu.
 
Hamna lolote, muuaji ni mmoja na hahusiani na Zitto, Muuaji wa Ipyana na Amina ni mmoja tu na nyie mnalifahamu hilo.

Kwahiyo acheni FIX.
 
Back
Top Bottom