Ujasusi Sebuleni Kwetu

Something is wrong somewhere!

kila nikijaribu kufungua threads za the bold kupitia app ya JF zinagoma. nimeuninstall app nikadownload tena lakini tatizo bado lipo.

Tatizo hili ni kwa threads zilizoanzishwa na the bold pekee, hususan "the richest man in Africa" na huu mpya wa "ujasusi sebuleni kwetu".

Slim thug sio mtu wa mchezo mchezo!
Mkuu mimi kwangu imekua nzito kufunguka yaani inaload hatari
 
Mkuu Habibu B. Anga Kuna gharama yeyote kujiunga kwenye group la whatsapp?
kuna gharama buku tano labda kama kashusha. jamaa anakuja kuvuna walevi wa simulizi zake na kuwapeleka wassup. hivi sasa mimi nishabiki wa humble africa dogo ana andika story inaisha. kama ile michael angelo duuu kuna mtu nilimpa akaisoma akajiunga jf siku hiyo hiyo
 
kuna gharama buku tano labda kama kashusha. jamaa anakuja kuvuna walevi wa simulizi zake na kuwapeleka wassup. hivi sasa mimi nishabiki wa humble africa dogo ana andika story inaisha. kama ile michael angelo duuu kuna mtu nilimpa akaisoma akajiunga jf siku hiyo hiyo
Mtu anafanya anachokipenda na mwishowe hicho ndo fursa kwake..hiyo sio dhuluma ni kazi ya mikono yake,tuambie wewe kitu gani unapoteza mda wako kuandaa halafu una share humu bure?usiwe na akili za kimaskini...heshimu professional za watu kwani eric shigongo kafanikiwa kwa kazi gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna gharama buku tano labda kama kashusha. jamaa anakuja kuvuna walevi wa simulizi zake na kuwapeleka wassup. hivi sasa mimi nishabiki wa humble africa dogo ana andika story inaisha. kama ile michael angelo duuu kuna mtu nilimpa akaisoma akajiunga jf siku hiyo hiyo
Gharama za kujiunga na Humble African?
 
NEXT EPSODE:itakua samahani kwa usumbufu siwezi endelea na hii makala sababu familia ya Ghailani kule zanzibar wameona inawadisturb maisha yao kwahyo basi sitaendelea nayo na sababu zilizo nje ya uwezo wangu nimeambiwa nisiendelee.😀😀😀 hii makala nayo haiishi na nilijua tu ukikatisha ile ya kagame basi itafuata hii ya 1998 balozi kulipuliwa halafu nayo itakatishwa next epsode.
akimaliza hii utavua nguo dk ngapi?
 
NEXT EPSODE:itakua samahani kwa usumbufu siwezi endelea na hii makala sababu familia ya Ghailani kule zanzibar wameona inawadisturb maisha yao kwahyo basi sitaendelea nayo na sababu zilizo nje ya uwezo wangu nimeambiwa nisiendelee. hii makala nayo haiishi na nilijua tu ukikatisha ile ya kagame basi itafuata hii ya 1998 balozi kulipuliwa halafu nayo itakatishwa next epsode.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
UJASUSI SEBULENI KWETU




SEHEMU YA PILI



Nilieleza namna ambavyo Hamis kijana wa Kitanzania alivyobadilika kutoka kwenye kuuza duka la kaka yake pale kariakoo mpaka kuanza safari za ughaibuni ambazo wengi hawakujua alikwenda kufanya nini hasa. Nimeeleza pia namna ambavyo Hamis alijiunga na kikundi cha Al-Qaida na kupatiwa mafunzo ya kijeshi huko Afghanistan na pia namna ambavyo alishiriki kwenye kutoa mafunzo kwa vijana wa Mohamed Farrah Aidid pale Somalia walipokuwa wanapambana na vikosi vya Umoja wa Mataifa vikiongozwa na Marekani.

Lakini nilieleza kuwa mtu ambaye alimuingiza kijana huyu wa kutoka kijijini cha Mdimuni pale Zanzibar kwenye mtandao wa Al-Qaida alikuwa ni bwana Mohammed Odeh au 'Bwana Somba' kama ambavyo maswahiba wake wengi na waumini wenzake katika msikiti uliopo katikati ya jiji hili la Dar es Salaam walipendelea kumuita.

Kabla sijaendelea mbele sana na simulizi hii, wacha niwamegee uhondo wa jikoni kabisa tuelewe ni namna gani ambavyo Odeh alisaidia sana kuupenyeza mtandao wa Al-Qaida hapa Afrika Mashariki na hususani hapa kwenye jiji hili la Dar.


Watu wengi sana ambao walikuwa wanamfahamu Odeh au hata kama umewahi kumsikia wazee wakisimulia kwenye vijiwe vyetu vya kahawa kuhusu Odeh na genge lake watakwambia kwamba Odeh alikuwa ni 'mwarabu koko' wa kariakoo hapo au kule Mombasa… wengi wanaamini hivyo. Na Odeh kwa kutumia ucheshi wake na uzoefu wake wa 'kijasusi' na kwa ustadi na umahiri mkubwa alifanikiwa kuwaaminisha watu jambo hili ili aweze kuficha hasa ukweli wa yeye ni nani.

Ukweli ni kwamba 'bwana somba' alikiwa ni mzaliwa wa nchini Saudi Arabia japo familia yake baadae ilihamia nchini Jordan ambako alikulia huko na kumalizia huko masomo yake ya shule ya upili. Mwaka 1986 alienda nchini Ufilipino kujiunga na chuo kikuu cha Far Eastern kilichopo mjini Manila ambako alisomea masuala ya uhandisi. Akiwa chuoni hapo Odeh alikuwa akijihusisha sana na shughuli za umoja wa wanafunzi wa kiislamu na ni katika masuala haya ya vikundi vya dini chuoni ndipo alikutana na baadhi ya wanafunzi wenzake wafia dini haswa ambao walikuwa na mikanda ya rekodi za mihadhara ya Sheikh Abdallah Azzam. Kwa wale wafuatiliaji wa makala zangu kwa muda mrefu mtakuwa mnamkumbuka huyu Sheikh, nilimuongelea kiasi katika makala ya "September 11: Behind The Curtain".
Sheikh Abdallah Azzam ni 'legend' katika ulimwengu wa vikundi vya dini vya misimamo mikali. Huyu bwana ndiye ambaye alikuwa 'mentor' wa kwanza kabisa wa Osama Bin Laden kipindi anaingia kwenye harakati za mapigano ya kidini. Inaaminika pia ni yeye Sheikh Azzam ndiye ambaye alitoa hili jina la 'Al-Qaida' akimaanisha 'msingi'.

Katika mwaka wake wa mwisho pale chuoni Odeh alikuwa anatumia muda mwingi sana kusikiliza mawaidha ya Abdallah Azzam kiasi kwamba yalimuingia mno mpaka akafikia uamuzi wa kuacha chuo na kufunga safari kwenda Afghanistan kujiunga na Mujahedeen ambao kipindi kile walikuwa wanapambana na serikali ya Afghanistan chini ya Rais Mohammad Najibullah ambayo ilikuwa kama kibaraka wa nchi ya Urusi.


Taarifa za intelijensia zinaonyesha kwamba Odeh aliwasili nchini Afghanistan mwezi octoba, 1990. Alipokelewa katika kambi ya Mujahedeen ambayo iliitwa Farouq Camp. Akiwa kwenye kambi hii alipatiwa mafunzo ya awali ambayo yalihusisha hasa utumiaji wa silaha nyepesi.
Baada ya kumaliza mafunzo ya awali Odeh alipelekwa kwenye kambi nyingine kwa ajili ya kupatiwa mafunzo ya ngazi ya kati ambayo haya yanahusisha usomaji wa ramani na masuala ya milipuko.

Baada ya kumaliza mafunzo ya ngazi ya kati akiwa hapo hapo Afghanistan chini ya mikoni ya Mujahedeen Odeh alipatiwa mafunzo ya ngazi ya weledi (Advanced Trainings) ambayo yenyewe hasa yalihusisha matumizi ya silaha nzito kama vile vifaru, rocket launchers, surface to air missiles n.k. akiwa hapa hapa Afghanistan, Odeh alijifunza masuala ya udaktari katika medani ya vita.

Ujuzi wake huu aliojifunza wa udaktari katika medani za vita ndio ambao ulimfanya mwaka 1991 apelekwe mjini Jalalabad ambako kulikuwa na kituo maalumu cha matubabu wa Mujahedeen ambao wamejeruhiwa katika mapambano dhidi ya serikali ya Afghanistan na Warusi. Akiwa huko huko Jalalabad kuna siku kituo chao cha matibabu kilishambuliwa kwa bomu na Odeh alipata majeraha makubwa kichwani. Odeh aliuguza majeraha yake kwa wiki kadhaa na alipopona tu alirejea tena kwenye kambi ya mafunzo za mujahedeen. Safari hii alipatiwa mafunzo ya namna ya kuteka kambi ya adui pamoja na majengo ya balozi.

Inakadiriwa kwamba mnamo mwezi March, 1992 ndipo ambapo Odeh alifanya Bayat kwa Osama bin Laden. Bayat ni kiapo cha kidini ambapo mtu anayekifanya anaweka nia kwa kutumia vitabu vya dini ambapo anaahidi kwa nadhiri kumtii huyo mwenzie na kufuata uongozi wake kwa kila ambacho atamtuma. Yaani ni sawa sawa na huku uswahilini tunavyosema 'kula yamini'.
Kwa hiyo ndio kusema kwamba Odeh alikuwa ni mmoja wa wanachama wa mwanzo kabisa wa Al-Qaida ambao walikuwa na weledi wa juu kabisa.

Kudhihirisha kwamba Osama alikuwa na mipango mikubwa kabisa na Odeh bila hata mwenyewe Odeh kujua… mara tu baada ya kufanya bayat kwa Osama, Odeh alipelekwa kwenye kambi ya mafunzo iitwayo Sadeek Camp ambapo alipatiwa mafunzo adhimu mno na ya hali ya juu kuhusu milipuko na namna ya kuiunda. Mafunzo haya yalikuwa yanatolewa na nguli wa masuala hayo ya uundaji mabomu na kiungo muhimu mno ndani ya Al-Qaida mtaalamu mwenye asili ya Misri aliyejulikana kama Abdel Rahmen Yasin.
Naweza kuthubutu kusema kwamba Abdel Rahmen Yasin anabakia kuwa moja ya manguli hodari zaidi wa uundaji mabomu kuwahi kutokea duniani na pengo lake ndani ya Al-Qaida itachukua muda mrefu mno kufanikiwa kuliziba kwa kumpata mtu wa weledi wake tena.
Akiwa kwenye kambi hii Odeh alifundishwa na Abdel Rahmen njia adhimu zaidi za uundaji mabomu kama vite ukokotozi wa hesabu za kikompyuta ili ku-configure detonator cords pamoja na blasting caps. Odeh alifundhishwa pia uyeyushaji wa TNT mpaka kupata 'shape charges' ambazo zinawa kuelekezwa kwa 'target' mahususi. Pia Odeh alifundishwa kuhusu uunganishaji wa bomu na vilipuzi vya kimahesabu na vya umeme.

Odeh aliiva. Daraja la Odeh lilipanda ndani ya Al-Qaida. Umuhimu wake kwa Al-Qaida ukatukuka.

Baada ya vita ya Mujahedeen dhidi ya serikali ya Afghanistan kuisha kutokana na kumuilondoa madarakani kibaraka wa urusi Rais Najibullah, Al-Qaida walijikuta wanahitaji mahala kwingine kwa kwenda "kumpiga shetani".
Ni katika kaipindi hiki ambapo majeshi ya Marekani yalikuwa yameingia nchini Somalia kuongoza vikosi vya Umoja wa Mataifa vya 'kulinda amani'. Suala hili la Marekani kuingia Somalia nimelieleza kwa undani sana kwenye makala yangu ya "Operstion Gothic Serpent" kwa wale ambao wamepata fursa ya kuisoma watakumbuka. Somalia ilikuwa kwenye vita na kila ukoo ukitamani wao ndio waitawale Somalia na hivyo kuzua machafuko mabaya ya vita ya wenyewe kwa wenyewe. Lakini Marekani na washirika wake walipoingiza majeshi yao ndani ya Somalia kulifanya koo nyingi ziache kupambana wenyewe kwa wenyewe na hatimaye kuungana kumpinga adui mmoja, Marekani.
Osama Bin Laden pia alichukulia kitendo hicho cha Marekani kuingiza majeshi Somalia kama uonevu kwa 'ndugu zake' wa imani hapi Somalia.


Mohamed Farah Aidid aliibuka kuwa ndiye mwenye nguvu zaidi pamoja na vikosi vya ukoo wake vya koo ya Um Rehan.

Osama bin Laden akamteua Odeh pamoja na komando mwingine ndani ya Al-Qiada aliyeitwa Saif al-Adel ambaye kabla ya kujiunga na Al-Qaida alikuwa ni 'Special Force' ndani ya jeshi la Misri na kuwatuma kwenda kusaidia vikosi vya Mohamed Farah Adid na kazi yao kubwa ilikuwa ni kufundisha wapiganaji wa Aidid.
Tukumbuke kwamba hii ilikuwa ni mwanzoni kabisa mwa vita kabla hata ya yule kijana wa kizanzibar niliyemuelezea kwenye sehemu ya kwanza ya makala kwenda kule Somalia.

Japokuwa Odeh na Saif-al-Adel ndio ambao walihusika kufundisha vikosi vya Aidid nchini Somalia lakini jambo moja ambalo wengi hawalifahamu ni kwamba Osama aliingiza karibia waarabu wengine wapiganaji wapatao 250 nchini Somalia ambao walikuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya Majeshi ya Marekani na washirika wake.

Odeh alikaa Somalia kwa miezi saba akifundisha wapiganaji wa Aidid.

Baada ya hapo alihamia nchini Kenya akiwa na wenzake wengine wawili ambao alikutana nao Somalia na kujenga urafiki. Wenzake hao wawili walikuwa ni Mustafa Mohamed Fadhil ambaye ni raia wa Misri pamoja na Fadhili Ally raia wa Kenya.
Wakiwa Kenya wakatafutiwa 'connection' na kuajiriwa kwenye kampuni fulani ya Kitanzania ambayo sitaitaja kwa jina kwa sababu za kimaadili lakini kampuni hii inahusika na uaguzaji mizigo kutoka uarabuni kupitia bandari ya Mombasa na bandari ya Dar es Salaam.
Kuna kipindi fulani cha karibia miaka miwili Odeh akiwa kama mwajiriwa wa kampuni hiyo alikuja kukaa hapa Tanzania na alipangishiwa flat pale maeneo ya Ilala. Ni katika kipindi hiki Odeh alipata kufahamu vyema mji wa Dar na kujenga urafiki na watu kwenye mitaa ya katikati ya jiji na hata kuzoeleka sana kwenye msikiti fulani maarufu ambao nao pia uko katikati ya jiji.

Baadae Odeh alirejea nchini Kenya na kumuoa mwanamke wa Kikenya na kuanzisha familia kabisa pale Nairobi.
Lakini mwishoni mwa mwaka 1995 Odeh aliitwa tena nchini Somalia na Osama bin Laden. Ni vyema kufahamu kwamba katika kipindi hiki Bin Laden alikuwa anaishi nchini Sudan kwa kificho kikubwa.
Bin Laden alimuita Odeh nchini Somalia kwa sababu maalumu… alikuwa anahitaji ampe uchambuzi wa intelijensia kwa muda wote huu wa karibia miaka minne aliyokaa Afrika Mashariki ameona mwanya gani ambao wanaweza kuutumia kuwashikisha adabu Wamarekani.

Odeh akatoe uchambuzi wake wa intelijensia. Akawapa mapendekezo yake. Osama akamruhusu arudi Nairobi kwa ahadi kwamba ndani ya wiki chache atampa maelezo juu ya oparesheni adhimu zaidi dhidi ya Marekani kuwahi kutokea.

Odeh akarejea Nairobi.

Wiki chache baadae mlinzi binafsi wa Bin Laden alimtembelea Odeh nyumbani kwake jijini Nairobi. Akampa maelezo ya Awali juu ya Oparesheni ambayo Bin Laden anataka itekelezwe. Zilikuwa ni Oparesheni mbili… ya kwanza iliitwa 'Operation Kaaba' ambayo ilipangwa itekelezwe Nairobi Kenya pamoja na 'Operation Al-Aqsa' ambayo ilitakiwa kutekelezwa hapa Tanzania jijini Dar es Salaam.

Mlinzi huyo wa Osama alimuachia Odeh kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kununua boti ya kisasa ambayo Odeh ataitumia kufanyia shughuli ya uvuvi ili kujipatia kipato aweze kutunza familia yake lakini pia boti hiyo itakuja kutumika kwa kazi maalumu wakati wa utekelezaji wa oparesheni.
Mwisho mlinzi yule wa Osama alimtaka Odeh ahame jijini Nairobi ili kulinda 'cover' yake.

Tofauti na wengi ambao walikuwa wanamfahamu Odeh kipindi kile na hata sasa wazee wetu wa Ilala na Kariakoo ambao walikuwa maswahiba wake wakiamini kwamba Odeh alikuwa 'mshua' fulani mwenye pesa na pengine walidhani hata anaishi kifahari sana huko Kenya, lakini ukweli ni kwamba Odeh alihama jijini Nairobi na kuhamia Mombasa ndani ndani kwenye kijiji kinaitwa Witu na alijenga nyumba yake ya udongo isiyo na maji ya bomba wala umeme na aliishi hapo na familia yake. Sio kwamba aliishi kwenye nyumba ya udongo kwa sababu ya umasikini, hapana… alifanya hivyo kulinda 'cover' yake pale Mombasa.

Odeh alitumia boti yake ya kisasa kwa shughuli za uvuvi katika ukanda huu wa bahari ya hindi ya Afrika Mashariki na mara nyingi sana alikuwa akija tena hapa Dar es Salaam kama uvuvi kuuza samaki zake. Ukienda pale bagamoyo ukiwauliza wavuvi wa siku nyingi, naam wanamfahamu Odeh. Vivyo hivyo ukienda pale kunduchi wavuvi wanamfahamu Odeh kwa uzuri kabisa.
Na alikuwa akishatia nanga na boti yake basi lazima abebe misamaki yake kuwapelekea zawadi maswahiba zake wazee wa Kariakoo na wazee wa Ilala pale na msikitini hapo katikati ya jiji. Mizawadi hii kedekede ya kufululiza ndiyo ambayo ilifanya watu wake wa karibu wamuite jina la "Bwana somba".

Ndipo hapa ambapo katika sehemu ya kwanza nilieleza namna ambavyo alijenga mazoea na kijana Hamis kutoka Mdimuni Zanzibar ambaye walikuta msikitini pale katikati ya jiji na kufanikiwa kumuingiza katika mtandao wa Al-Qaida. Na huyu Hamis naye alitumika ku-recruit 'fupi'. Kama bado haujang'amua huyu bwana anayeitwa fupi ni nani basi nikuarifu huyu ni Ahmed Ghailani… kijana ambaye habari yake yawezekana uliwahi kuisikia miaka kadhaa iliyopita alipokuwa Mtanzania wa kwanza kushikiliwa kwenye gereza la Guatanamo Bay.

Kazi ya uvuvi iliendelea… wakivuliwa samaki na binadamu. Odeh alichanja mbuga.

Kila akiingia jijini Dar maswahiba walifurahia mizawadi ya samaki.. mijodari, vibua, tasi kwa kolekole… mwenzao alikuwa anakusanya intelijensia. Wao walifurahia ucheshi wake na ukarimu.. mwenzao alikuwa anaangaza jicho kufanya 'recruitment' ya vijana wa kusaidiana nao kwenye kutekeleza Operesheni Kaaba na Operesheni Al-Aqsa.


Stay here…



Habib
To Infinity and Beyond

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SEHEMU YA PILI COMMENT # 158

Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi @Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM @Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij addenbwii ONTARIO Kobe The Vein Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya Sitaki ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo mgumu2 troublemaker Linamo shedede kamtu33 SteveMollel ngushi Donald stewart Mshuza2 Glycel mnonje Ochuanilove SingleFather Santi DEOD 360 ngushi anatory antony ukhuty chris van chicha auxillius Goma Son Hubeb pes KING DUBU VILLAIN mwayena donbeny Aleppo JipuKubwa shoo61 BOMBAY John mungo Nyakageni bato Dogo 1 sufra chamlungu painscott wegman Bravo Engliash MOSELBAY wa stendi FaizaFoxy bigmind cadabraa Internal Kelvin mwalukas mnonje Kelvin X Somoche Wgr30 Miiku Poise Jabman kalamuyamwalimu BOMBAY the say juxhb witnessj Gide MK Mmanyema mgogoone Mnongane Mandingo koncho77 afsa ngaboru Paradoxer Heavy Metal KIMBURU 06 Raaj kichekoh ngumba njeche kikale DullahTza Goodluck Mshana julius Darcy Denis Kasekenya mashonga kitalembwa Khaleed Shaban middle east SirChief jiwe jeusi Mkambarani mansakankanmusa gambada ynwa ney kush mossad 03 white wizard xtaper Mzigua90 Ollachuga Oc Gidbang Mateja M.G Yango jipu abaa4all DIBAJI Agenda1 Grahnman The MaskmaN Slim5 Xubzero agprogrammer JoJiPoJi Architectus blance86 Mamtolo monde arabe Ngao Ya Imani stardust JK naiman64 Dharra seledunga ABB SHAMMA Richard Waziri wa Kaskazini Mwinjuma1 Kanungila Karim baracuda Mwamba028 besaro Pyepyepye Bilionea Asigwa ibn Kiti Chema Tugas Royal Warrior mederii mmangO manzi james LIKUD adrenaline Royal Son Mhadzabe salaniatz Natasha Ismail jiwe jeusi chibalangunamchezo
John Mloy conjuget Van Pauser great G Mtoto wa nzi Zeus1 hindustan Sci-Fi MAN OF PEACE kashata emnly danny baraka bb MTOTELA kbosho TEMLO DA VINCA


Sent using Jamii Forums mobile app


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom