Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,533
Maji yanapoanza kukolea joto, msuguano wa chembe chembe zinazounda maji huanza kusuguana na kuanza kutoa mvuke. Kadri jinsi moto unavyoendelea kwa kiwango kile kile au kuongezeka, msuguano wa chembe chembe hizi huongezeka, mvuke huongezeka na kama chombo ambacho maji haya yanachemshiwa kina mfuniko, mluzi mwepesi na fukuto la mvuke huanza kuinua ule mfuniko.
Hitimisho la kupata joto huku kwa maji, ni maji kuchemka, yakiwa na joto la hadi nyuzi 100 sentigredi. Inapofikia hatua hiyo, maji haya pamoja ni salama kiafya kwa kunywa, lakini ni hatari maana huweza unguza na hata kuhatarisha maisha ya mwanadamu.
Mfano huu wa maji kuchemka, ni kuoanisha hali iliyofikia mchemko kwa kupitia Wanafunzi tangu shule za msingi, sekondari mpaka ngazi ya vyuo hususan Chuo Kikuu Dar Es Salaam.
Katika kipindi cha miezi minne iliyopita, kumekuwa na wimbi la wanafunzi kufanya fujo ambazo zimefikia hatua ya kuharibu mali na hata kupotea kwa maisha.
Pamoja na kuwa sikubaliani na njia walizotumia Wanafunzi hawa, anzia wa kule Mtwara au Lindi waliochoma shule kwa ajili ya Sukari, Kantalamba ambao walikasirikana kuvunja vunja mali za shule na magari kisa kufungwa kwenye mechi ya mpira na mwenzao kuchapwa viboko, Green Acres ya Dar ambao wamefanya uharibifu wa karibu Shillingi 100 Millioni kisa Muziki na kupewa pasi za kwenda kutembea na mwisho Baba lao UDSM ambao wamefanya vurugu na migomo kutokana na kukosekana maji, umeme, calculator, kusimamishwa uchaguzi wa serikali ya wanafunzi na sababu nyingine nyingi, lakini naelewa chimbuko la hasira zao na kamwe si jambo la kupuuzia.
Ninachojiuliza, Serikali inajifunza nini kutokana na hili? Je jamii yetu inajifunza nini kutokana na haya mambo yaliyotokea?
Wanafunzi hawa wanachofanya ni active resistance, na wamekimbilia kufanya fujo na kuharibu mali kama tamati ya hasira na kuchoshwa kwao kwa kuendelea kutokusikilizwa au maombi na matakwa yao kutokufanyiwa kazi.
Sisi hapa JF, tunatumia passive resistance, ingawa si kwa nguvu zote, ila mazungumzo yetu ya kuuchambua mfumo wa kiutawala na maswala yanayohusu jamii na athari zake, ndiyo yanatufanya tuwe kwenye kundi la passive resistance, non violent resistance.
Hata walioandamana majuzi kule Buzwagi, waliomzomea Mkapa na wale wa Morogoro walimzomea Ngasongwa ni sehemu ya civil disobidience kudai haki.
Maji yameanza kuchemka, sehemu moja ya jamii yetu imefika ngazi ya juu ya kusubiri haki itumike ili mahitaji na vilio visikilizwe.
Ukiangalia kesi zote za hawa wanafunzi, chimbuko la fujo zao ni UONGOZI wa shule na vyuo vyao.
Sisi hapa JF, magazetini na sehemu nyingine, chimbuko la vilio vyetu ni UONGOZI na VIONGOZI.
Swali linabakia, je Taifa na Jumuia zetu zina matatizo gani ya Uongozi? Inakuwaje kunakuwa na msukumo mkubwa wa Jamii kutokuridhika na Uongozi?
Kilichoshtua zaidi ni vijana wa Green Acres, shule binafsi ambao wanalipia ada kwenda kwenye hiyo shule. Nikajiuliza, kawaida ya migomo na vurugu katika Shule hutokea kwenye Shule za Serikali. Sasa kama hata kwenye Shule binafsi kunaanza kuwa na vurugu, je ni ugonjwa gani katika ngazi za uongozi Taifa letu inalikosa?
Sizungumzii Ufisadi au Uhujumu, bali ni Upeo wa Uongozi Mahiri ulioambatana na Hekima, Busara, Uwajibikaji, Ufanisi na Unyenyekevu.
Inaelekea viongozi wengi wa Tanzania wa ngazi mbali mbali tangia mitaa, kijiji, taasisi, shule, mashirika na hata serikali kuu na Kiongozi Mkuu, Rais, ni vipofu, viziwi na pua zao hazi fanyi kazi vizuri kung'amua kuwa kuna fukuto la Jamii na Taifa lililochoshwa na adha, mahangaiko na kukosa amani kwa kutokujua Kesho wataamka wakiwa katika hali gani.
Tulipoandamana kulienzi Azimio la Arusha, Viongozi na Wananchi walikuwa bega kwa bega wakiungana Kulijenga Taifa linalojitegemea, lenye watu wenye juhudi na maarifa katika kupiga vita Ujinga, Umasikini na Maradhi.
Lakini sasa inaelekea Mwananchi anachapwa mjeledi na kiongozi wake, kushurtishwa avumilie machungu na makali ya maisha kama kukosekana kwa huduma nzuri za elimu kwa watoto, kinga ya afya, ajira, bei punjifu ya mazao, mishahara midogo, kukosekana kwa miundo mbinu mizuri kwa sekta kama za umeme, maji, usafiri wa matata anzia reli hata barabara na kutwa kuchwa akiambiwa "vumilia kidogo" lakini kukiwa hakuna tumaini.
Mwananchi anaambiwa "Vumilia Kidogo" huku akikamuliwa na serikali yake na Viongozi wake, kuchangia kila kitu kwa kipato haba, kushurtishwa kufanya mambo yanayokidhi matakwa ya Viongozi na si ya Jamii au Taifa.
Tumekosa viongozi wasikivu, wenye kung'amua haraka kuwa maji yakikaa kwenye moto kwa muda mrefu, hufukuta na katika safari yake ya kubadilika kutoka kuwa kimiminika kuwa hewa, mvuke huleta msukumo ambao hufanya maji yachemke.
Asilani tusikimbilie kusema eti ni mbegu mbaya tuliyoipanda kutoka tupate uhuru, au ni mipango mibovu ya viongozi wa kwanza. Kuendelea kulaumu ya kale na kuyafanya kuwa ndiyo sababu kuu ya udhaifu wa viongozi wa sasa, ni kuwapa viongozi hawa sababu za kukwepa uwajibikaji kwa kuwa watakimbilia kusema kuwa wao ni "Walevi" kwa kuwa Baba na Bau zao walikuwa ni "Walevi".
Taifa sasa hivi liko njia panda na kwenye ncha ya kuangukia kwenye vurugu mithili ya wanafunzi. Kila mtu anajifunza kutokana na fujo hizi na mwishowe kila mmoja wetu atasema imetosha, ngoja nami nichukue "kitofa" na kufanya vurugu.
Ikiwa Viongozi walishindwa kusoma mambo ya nyakati wakati Shamba la Ballali alilolipata halali liligawanywa na wananchi wenye hasira kama vazi la Yesu, basi tuendako ni hatari na kunanikumbusha nilichokiona na kusikia pale Kariakoo nyuma ya CCM Lumumba.
Ilikuwa ni November ya 2004, nimetoka Kanisani nikiwa na Mzee Kishoka na wake zetu, tukaenda kununua nyama. Kulikuwa na vikundi vya watu wakibarizi asubuhi kusugoa.
Nilichokisikia kutoka kwa hawa ndugu na nilichokiona kutoka machoni mwao, kimenikaa mpaka leo, na ikawa ndio ongezo la hasira zangu kwa ugoigoi wa Serikali.
Tuliposhuka kwenye gari, jamaa wakatutazama, kisha wakaanza kusema, "Ruksa hiyo, Ruksa hiyo", nikaangalia nyuma sikuona mtu, ila kelele hizo zilielekezwa kwetu. Nikawaangalia na kuwakazia macho mithili Bush alivyomkazia macho Putin, nikaona hasira tupu zilizotokana na kushindwa kusikilizwa kwa kero zao ambazo zimeendeleza wao kuwa wanyonge na kuhisi kuwa ni masikini wasio na haki au sehemu katika nchi yao.
Nikasema, ikiwa kuvalia kwa utanashati kunatoa tafsiri ya "Ruksa" wakati huo, basi tunapoenda na kubaya sana ikiwa Serikali na Viongozi hawatafanya juhudi kufanya kazi zao ili kuondoa hizi zana potofu kuwa kila mwenye tai ni "Ruksa" au kwa leo "Fisadi".
Kwa nyie wapambe wa viongozi, kina Salva, Balile na wenginewe, mkisoma maandiko haya, nendeni mkawaamshe mnaowasaidia.
Waambieni maji yameanza kuchemka na hatari yake ni kuungua. Watuepushie balaa na kufanya kazi kwa umakini ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua kuondoa kero kwa wananchi na kushughulikia uzembe,dhuluma, hujuma na ufisadi. Waambieni kama hawawezi kazi za uongozi, ni heri wang'atuke na si kuendelea kutulaghai na miezi 18 ijayo watuambie wanataka kura zetu waendelee kuwa Viongozi (Watawala).
Nawatakia wiki njema.