Mwanakijiji swala langu kubwa ni kuwa kwanini unajadiliwa? je ni watu wachache au wengi wanaoleta haya mazungumzo wakiwa na nia zao binafsi au ni majority?
Juzi wawakilishi wetu, wabunge, walizima kabisa issue za Richmond. Mimi na wewe leo ni mashahidi kuwa kuna mambo mengi sana ndani ya bunge hatukubaliani nayo.Kwa hiyo kwa nchi zetu hizi kusema kuwa kuna wawakilishi hakuufanyi muungano kuwa halali. wawakilishi is just a paint kusema wananchi wote walihusika.
Swala la pili ni kuwa lets say nikakubaliana na wewe kuwa wawakilishi wanafanya kitu kuwa halali, then, swali la pili je waliwasiliana na wananchi kwa kiasi gani?
Umeona Obama aklivyohangaika kutoka meeting moja kwenda nyingine, kutoka chuo hiki kwenda kile kuinadi policy yake ya health care. Je wawakilishi walifanya hivyo waliwaelimisha wananchi kiasi cha kutosha na hata kupata maoni yao? If not so then wananchi walifanywa wanyama wasio na value yoyote??, na serikali za kiafrika nyingi kiwamo ya Nyerere ambaye unajaribu kutaka kumtetea walitufanya hivi ni bahati mbaya sana kuwa wengine hawajaliona hili
Kama nchi yetu sote kwanini maamuzi hayawi ya sisi wote? na kama kuna wawakilishi then kwanini hawawasiliani na wapiga kura wao? najua unaweza kusema wawakilishi "si mliwachagua wenyewe" no matter mlimchagua au hamkumchagua swala ni kuwa wananchi wengi hawakujua kuhusu hii issue, that alone is a big mistake, swala la kwa kwanini mliwachagua is another long agenda yenye sababu nyingi, moja wapo kubwa ni nini nguvu ya wawakilishi? akina Kilango bungeni yes wanasema kwa nguvu; kiasi gani as individual ana nguvu kufanya vitu viende au visiende?
Hoja yangu ni kuwa Up to this point (kwa Imani) muungano ni halali, ninachofanya ni kupata nguvu na supportive argument ya kujiaminisha ninachokiamini, na ninashtuka ninapoona watanzania wenzangu tulioungana nao wanasema kuwa muungano si halali, lazima nishtuke, nini kinaendelea , kama sote tu family, why on earth other people questioning our union? mpaka sasa hizi bado sijapata strong reasons za kufanya imani yangu iwe thabiti.
Note that I do believe our union is genuine,but believing is not necessary the truth!!
Akija mtu na hoja na kuthibitisha kuwa ni halali, then wanaopiga kelele kuhusu muungano ni wangapi? kama wachache leave them! kama wengi then something must be wrong somewhere?
kama wawakilishi hao wakitunga sheria (pamoja na ufisadi au madhaifu yao) sheria hizo zinakuwa halali na tunatakiwa kuzitii kwanini basi linapokuja suala la muungano tusione kuwa ni halali? As a matter of fact, it can easily be argued kwamba bunge la wakati ule lilikuwa na uhalali zaidi na uzalendo zaidi kuliko hawa wenzetu wa sasa.
kwa kiasi chochote kile wao ni wawakilishi; hakuna ulazima wa kuhamisha magoli kwa wakati huu. Kwamba Muungano ni halali kisheria hilo sina shaka nalo. Kwamba baadhi ya vitu vingefanywa tofauti hilo linaweza kujadilika lakini haliondoi uhalali wa muungano. Kwa mfano watu wawili wanapofunga ndoa kwa hiari yao uhalali wa ndoa yao haufutiki ati kwa sababu wazazi hawajaulizwa au kutoa baraka zao! Lakini vile vile tunajua ni vizuri kama pande mbili za familia zinahusishwa katika harusi n.k Hata hivyo, uhalali wa ndoa upo.
Jamani kuna mambo ni lazima tuyaangalia in historical context; hivi wakoloni walipokuja kututawala walijipitisha kwa kiasi gani kwa wananchi ili tuwaelewe na kuwakubalia? Waliomba maoni ya nani juu ya kuundwa kwa nchi ya Tanganyika? Wajerumaini walipofanya Berlin Conference na kuigawa Afrika kama kugawana pizza ni mwafrika gani aliulizwa? Lakini tumekubali kuwa mipaka waliyoiweka na miundo mbinu yake ilikuwa halali na hatuihoji? Gavana wa Mwingireza alipoigawa Tanganyika au Wajerumani walipoinunua Mafia au Bagamoyo toka kwa Sultani tunasema ni halali.. Nyerere kukaa na Karume na kuamua kuunganisha wananchi wao, tunasema "it was wrong!!"..
Demokrasia ni pamoja na kuamini kuwa wawakilishi wamechaguliwa na wananchi kuwakilisha wananchi. Kama wananchi wanaona wawakilishi wao wanafanya kitu ambacho hawakubaliani nacho demokrasia inawaita wananchi kuwaondoa wawakilishi hao kwenye sanduku la kura. Lakini, haiwezekani kila jambo moja basi wabunge waende kuuliza. Jambo moja tunalosahau ni kuwa TAnganyika na suala la Muungano lilikuwa halina utata. Tanganyika na hata Zanzibar (ASP na TANU) viliamini katika Umoja wa Afrika.
Sisi Tanganyika hatukuwa na tatizo lolote katika masuala ya Muungano tuliamini katika Muungano, itikadi yetu ilijengwa katika kuunganisha bara la Afrika. Hata kama wangewauliza watu, wakati ule kura nyingi ingekubaliana na sentiments za wakati ule. Kilichofanyika kilikuwa ni natural progression of an ideological trajectory of pan-africanism.
Waberoya, tatizo hapa kuna hoja mbili ambazo wengi wetu hawajakaa chini kuzifikiria kwa makini. Kuna suala la uhalali wa Muungano, na kuna suala la utekelezaji wa Muungano. Umetolea mfano Obama; Juzi Gavana wa Arizona ametia sahihi sheria ya kuharamisha uwepo wa wahamiaji haramu na kuruhusu polisi wa Arizona kuweza kuwakatia mbaroni wahamiaji haramu. Hata hivyo suala la uhamiaji ni suala la Federal Gvt; Obama ameagiza Justice dept kupitia sheria hiyo na nina uhakika itapelekwa kwenye mahakama kuu (supreme court) na kuonekana ni kinyume cha Katiba na kufutwa! Baada ya kupitisha sheria ya mambo ya afya, serikali zaidi ya 30 za majimbo zimeamua kushtaki sheria hiyo kuwa inaingilia haki za Majimbo. Yote hayo yataamuliwa mahakamani lakini hayahoji uhalali wa Muungano wa Marekani.
Sisi katika ufinyu wetu wa kufikiria tunapokutana na matatizo yautekelezaji wa Muungano tunakimbilia "tuvunje tu yaishe".. tukisema kwanini tunaambiwa " kwa sababu una kero"!! Haya ni majibu ya watu wasiofikiria. Inanisikitisha wakati mwingine kwa sababu our collective reasoning as I've mentioned somewhere else is mediocre and pathetic to say the least. NI lazima kwanza tukubali principle kuwa:
. Muungano ni halali
. Muungano ni wa nchi uliounda taifa moja
. Muungano ni wa kulindwa na kutetewa dhidi ya maadui wa ndani na wa nje (tukumbuke kuwa hakuna kitu kitakachowafurahisha mahasimu wa waafrika kama kuona jaribio pekee la kuunganisha afrika likivunjika wakati wao Europe na kwingine wanajitahidi kuungana zaidi na zaidi)
. Matatizo ya Muungano yanatatulika kirahisi tu (kama tungepata watu wenye akili timamu za kutatua matatizo zaidi ya porojo!)
The truths stands objectively alone; it doesn't matter whether u believe it or not.
Labda tatizo haliko "somewhere".. may be what is wrong is with the many people wanaopiga kelele kwa sababu hawajafikiria kiundani na kiakili. Kupiga kelele kwa watu wengi hakufanyi hoja zao kuwa ni halali au zina maslahi ya ukweli. Sometimes the minority hold the key to the defense of truth. I'm not a follower of many who shouts but the silent majority who think before they speak.
Thanks, now as the heat is high,
unasemaje wazanzibar wakisema wajiondoe kwenye muungano?
hawawezi!! kwa sababu tukikubali wanaweza itakuwaje kama Kilimanjaro nao wanataka watoke kwenye Muungano (kumbuka kabla ya Tanganyika Kilimanjaro ilikuwa tayari kuwa taifa peke yake!); nini kitazuia haki ya wananchi wa Kagera kujitenga au Mtwara na Lini? Wawaulize wenzao wa Marekani ya kusini ambao walitaka kuvunja muungano wa US!!
Kwani sultan aliwauliza wazenj kabla ya kuweka mipaka? Kabla ya mapinduz ya Jan 12, 1964i wazenj walipiga kura za maoni?[/QUOTE
Kwani ufisadi unaofanywa sasa uliwahi kuibiwa kutoka nyumbani mwako, mbona unaulani? Si uwache tu?]
hawawezi!! kwa sababu tukikubali wanaweza itakuwaje kama Kilimanjaro nao wanataka watoke kwenye Muungano (kumbuka kabla ya Tanganyika Kilimanjaro ilikuwa tayari kuwa taifa peke yake!); nini kitazuia haki ya wananchi wa Kagera kujitenga au Mtwara na Lini? Wawaulize wenzao wa Marekani ya kusini ambao walitaka kuvunja muungano wa US!!
hawawezi!! kwa sababu tukikubali wanaweza itakuwaje kama Kilimanjaro nao wanataka watoke kwenye Muungano (kumbuka kabla ya Tanganyika Kilimanjaro ilikuwa tayari kuwa taifa peke yake!); nini kitazuia haki ya wananchi wa Kagera kujitenga au Mtwara na Lini? Wawaulize wenzao wa Marekani ya kusini ambao walitaka kuvunja muungano wa US!!
"WALE WOTE WANAOPIGANIA HAKI WANAPIGANIA VITA VYA HAKI NA WALE WANAOPIGANA VITA KWA LENGO LA KUKANDAMIZA WENZAO,KUWANYANYASA NA KUWATAWALA HAWAPIGANI VITA VYA HAKI" DR Kikwete (tAREHE 25/04/2010)
Si wanasema kuwa hizi articles hazipo? Mwiba alizipata wapi?