The Article of Union between the Republic of Tanganyika and the Peoples’ Republic of | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The Article of Union between the Republic of Tanganyika and the Peoples’ Republic of

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Jan 30, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  The Article of Union between the Republic of Tanganyika and the Peoples’ Republic of Zanzibar

  WHEREAS the Governments of the Republic of Tanganyika and of the Peoples’ Republic of Zanzibar, being mindful of the long association of the peoples’ of these lands and of their ties of kinship and amity; and being desirous of furthering the unity of African peoples, have met and consider the union of the Republic of Tanganyika with the Peoples’ Republic of Zanzibar:

  AND WHEREAS the Governments of the Republic of Tanganyika and of the Peoples’ Republic of Zanzibar are desirous that the two Republics shall be united in one Sovereign Republic in accordance with the Articles hereinafter contained:

  (i) The Republic of Tanganyika and the Peoples’ Republic of Zanzibar shall be united in one Sovereign Republic.

  (ii) During the period from the commencement of the union until the Constituent Assembly provided for in Article (vii) shall have met and adopted a Constitution for the United Republic (hereinafter referred to as the interim period ), the United Republic shall be governed in accordance with the provisions of Articles (iii) to (vi)

  (iii) During the interim period the Constitution of the united Republic shall be the Constitution of Tanganyika so modified as to provide for –

  (a) a separate legislature and executive in and for Zanzibar from time to time constituted in accordance with the exiting law of Zanzibar and having exclusive authority within Zanzibar for matters other than those reserved to the parliament and executive of the united Republic;

  (b) the offices of two Vice-Presidents one of whom (being a person normally resident in Zanzibar) shall be the head of the aforesaid executive in and for Zanzibar and shall be the principal assistant of the President of the united Republic in the discharge of his executive functions in relation to Zanzibar;

  (c) the representation of Zanzibar in the Parliament of the united Republic;

  (d) such other matters as may be expedient or desirable to give effect to the united Republic and to these Articles.

  (iv) There shall reserved [sic] to the Parliament and Executive of the united Republic the following matters -

  1.External Affairs
  2.Internal Affairs
  3.Defence
  4.Police
  5.Emergency Powers
  6.Citizenship
  7.Immigration
  8.External Trade and Borrowing
  9.The Public Service of the United Republic
  10.Income Tax, Corporation Tax, Customs and Excise
  11.Harbours, Civil Aviation, Posts and Telegraphs

  And the said parliament and executive shall have exclusive authority in such matters throughout and for the purposes of the united Republic and in addition exclusive authority in respect of all other matters in and for Tanganyika.

  (v) The existing low of Tanganyika and of Zanzibar shall remain in force in their respective territories subject –

  (a) to any provision made hereafter by a competent legislature;

  (b) to such provision as may be made by order of the President of the united Republic of the extension to Zanzibar of any low relating to any of the matters set out in Article (iv) and the revocation of any corresponding law of Zanzibar;

  (c) to such amendments as may be expedient or desirable to give effect to the union and to these Articles.

  (vii) (a) The first President of the united Republic shall be Mwalimu Julius K. Nyerere and he shall carry on the government of the united in accordance with the provisions of these Articles and with assistance of the Vice-Presidents aforesaid and of such other ministers and officers as he may appoint from Tanganyika and Zanzibar and their respective public services.

  (b) The first Vice-President from Zanzibar to be appointed in accordance with the modifications provide for in Articles (iii) shall be Sheikh Abeid Karume.

  (vii) The President of the united Republic in agreement with the Vice-President who is head of the executive in Zanzibar shall -

  (a) Appoint a Commission to make proposals for a Constitution for the united Republic.

  (b) Summon a Constituent Assembly composed of representatives from Tanganyika and from Zanzibar such numbers as they may determine to meet within one years of the commencement of the union for the purpose of considering the proposals of the Commission aforesaid and to adopt a Constitution for the united Republic.

  (viii) These Articles shall be subject to the enactment of laws by the Parliament of Tanganyika and by the Revolutionary Council of the Peoples’ Republic of Zanzibar in conjunction with the Cabinet of Ministers thereof, ratifying the same and providing for the Government of the united Republic and of Zanzibar in accordance therewith.

  IN WITNESS WHEREOF Julius K. Nyerere, the President of the Republic of Tanganyika and Abeid Karume, the President of the Peoples’ Republic of Zanzibar, have signed these Articles, in duplicate, at Zanzibar, on this twenty-second day of April,1964.
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Na Salma Said,
  JUMLA ya Wazanzibari 12 waliowahi kumshitaki mwanasheria mkuu wakidai kutaka hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar juzi wamekwenda ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) ziliyopo Zanzibar na kuwasilisha malalamiko yao hayo.
  Akizungumza na waandishi wa habari katiak ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) Mjini Unguja, Naibu Katibu wa kikundi hicho kiitwacho Zanzibar People of Representatives, Rashid Yusuf alisema suala la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar limegubikwa na utata mtupu na linafaa kushughulikiwa ipasavyo na sio kuandaa kamati ambazo hazina nguvu kisheria.
  Alisema hivi karibuni wamekwenda katika ofisi za UN na kuwasilisha malalamiko yao juu ya suala hilo na kutaka hatua za dharaura kuchukuliwa kwani Muungano uliopo haupo kisheria hasa kwa kuwa Mwanasheria mkuu wa serikali ya mapinduzi Zanzibar kusema mahakamani kwamba hana hati za makubaliano ya muungano huo.
  Naibu huyo alisema awali walikuwa wajumbe 10 na ambao wawawakilishi wazanzibari zaidi ya millioni moja katika kudai haki yao ya kutaka muungano uwepo kisheria alisema kikundi chake kilikwend amahakamani kumshitajki mwanasheria mkuu atoe hati ya muungano lakini bahati mbaya amesema hana hati hiyo.
  Alisema kutokana na mwanasheria mkuu wa Zanzibar kudai kwamba hana hati ya muungano hivyo muungano uliopo haupo kihalali na wazanzibari wanapaswa kujua makubaliano ya muungano yamekuwaje hasa hadi serikali ambaye amekula kiapo kusema hakuna mkataba wa muungano jambo ambalo ni kosa kisheria.
  Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliasisiwa na viongozi wakuu wan chi mbili rais wa Zanzibar Mzee Abedi Amani Karume na rais wa Tanganyika, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.ambao walikuwa wanalengo la kuunganisha umoja na ushirikiano.
  “Mwanasheria Mkuu yeye ni taasisi ya serikali na akisimama hasemi kama ni yeye anasema anaisemea serikali kwa hivyo amekula kiapo na kusema mkataba huo haupo ndio maana tukasema haupo kitaifa na Kimataifa hivyo muungano huu sio halali”Alisema Yusuf.
  Aidha amesema Muungano huu uliopo hivi sasa una mapungufu zikiwa zimeungana nchi mbili ni vyema kukawa na usawa mapungufu hayo yameonekana kutokuwepo kwa mkataba wa muungano ,tatizo hilo limefikishwa umoja wa mataifa ili kupata ufafanuzi zadi.
  Nae katika mkutano huo Mshiriki ambae ni Mzee Amour Bamba alisema Muungano ni mzuri lakini uwe ule unaotakiwa, Zanzibar haijaelezewa itafaidika vipi na Muungano huu.
  Aidha alisema tokea mapinduzi ya mwaka 1964 hadi hii leo zinazungumzwa kero za muungano lakini haionekani ni namna gani zinaondoshwa kero hizo na badala ya kuondoshwa kero zimekwua zikizidi kila kukicha bila ya kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu.
  Alisema Sasa ni wakati muafaka wa rais Amani na rais Kikwete kuwa wawazi kwa kuweka usawa wananchi ili kudumisha Muungano huu kwa kufanya hivyo kero hizo zitaondoka
  Wazanzibari wanapenda Muungano lakini haijapatikana haki ya kila upande ni upi katika Muungano huu hilo ndio suali ambalo wazanziabri wengi au watangaika wengi wanajiuliza na wanapaswa kupewa jibu la suali hilo“alisema na kuongeza kwamba jibu la hilo linaweza kupatikana iwapo marais wawili hawa waliopo sasa kabla ya kumaliza muda wao madarakani kutoa jibu kwa watanzania wote.
  Mzee huyo ambaye anakisi cha miaka 80 amesema nchi hizi mbili hazipaswi kutawaliwa kiimla hivi sasa kwa kuwa zama hizo zimeshapitwa na wakati na wakati uliopo hivi sasa ni ule unaokwenda na utandawazi ambazo unakwenda sambamba na utawala bora na utandawazi.
  Kero za muungano wa Tanganyika na Zanzibar zimekwua zikiibuka mara kwa mara kutokana na baadhi ya tume zinazoundwa kushughulikia kero za muungano hutotatua matatizo yaliopo na kusababisha malalmiko makubwa ya kiuchumi na kisiasa has upende wa Zanzibar.
  Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umepiga katika kipindi kigumu sana kufuatia kutikisika kila baada ya kipindi Fulani kutokana na wanasiasa kudai mambo kadhaa ambayo kutaka kutolewa ndani ya orodha ya muungano ambapo kwa mujibu wa mkataba wa muungano mambo yake yalikuwa 11 ya awali na sasa kufikia hadi 23.
  Akizungumza na waandishi katika mkutano huo, Rashid Hemed (Joe) amesema anashangazwa na mambo ya muungano yanavyokwenda na hatua zinavyochukuliwa kiutaratibu huku wanasehria wakiwa wapo kimya hali ya kuwa wanajua muungano huu sio halali kwa mujibu wa sheria.
  Amesema tokea kuasisiwa kwa muungano huo ambao waanzilishi wake ni Mwalimu Nyerere na Mzee Karume mambo yalikwenda vyema lakini alipokufa tu Mzee karume viongozi wote waliotawala Zanzibar wameshindwa kuendeleza muongozo wake aliouwacha na badala yake kufuata mkondo wa maji jambo ambalo sio sahihi katika nchi.
  Joe amesema wazanzibari wanataka muungano wa Afrika na hawataki muungano huu ambao sio halali wenye kuendeleza ukoloni ambao Zanzibar imevamiwa na Tanganyika na sio wameungana.
  “Tumevamiwa sio tumeungana Tanganyika imeivamia Zanzibar na ndio ukaona hivi sasa hakuna utamaduni hakuna chochote mila silka na utamaduni wetu wote umepotea watu wanaingia tu ovyo na kuzidi vitendo vya ujambazi, umalaya kila kitu kibaya kimeenea Zanzibar…tumevamiwa” amesema Joe.
  Amesema Rais Amani baada ya kutafakari ameona anataka kufuata nyayo za baba yake na kutaka kuirejeshea hadhi Zanzibar ndio maana akataka suala la mafuta na gesi asilia litolewe katika orodha ya mambo ya muungano.
  Kauli hizo zimekuja wakati Serikali ikijitayarisha na maadhimisho ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutimiza miaka 46 ya Muungano huo ambapo sherehe hizo zitafanyika Tanzania April 26 mwaka huu.

  Source: zanzibar yetu web blog.
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Nakubaliana nao.
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Apr 24, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
  domino failure!

  Inaonekana vitu vingi sana walivyovianzisha waasisi wa taifa hili bila consent ya wananchi vitakuja kuanguka siku moja. Na hizi failures zinaweza zikawa zina suggest failure ya vitu vingi sana. Build it when they start to fall/collapse........

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. M

  Magezi JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hivi yule mzanzibari al qaeda anayeshikiliwa kwenye jela za USA haja hukumiwa?
   
 6. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #6
  Apr 24, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Wako sahihi...
   
 7. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2010
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Magenzi utapatwa na Taminala Kensa ya Tumbo bure kwa kujishughulisha na yasio kuhusu .
   
 8. Tambara Bovu

  Tambara Bovu JF-Expert Member

  #8
  Apr 24, 2010
  Joined: Dec 19, 2007
  Messages: 586
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ni batili kabisaaaaa
   
 9. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #9
  Apr 24, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Una haraka ya nini? Kwanza hebu tushughulikie jamaaa zako wanaouwa Maalbino!
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Apr 25, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Je Tanganyika ilikuwa halali?
  Je Zanzibar ilikuwa halali?

  Kabla ya Muungano?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #11
  Apr 25, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
  Ndiyo zilikuwa halali kaka kabisa.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Apr 25, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kwanini zilikuwa halali?
   
 13. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #13
  Apr 25, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Somethings are not worth commenting about.
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Apr 25, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Jasusi.. unajua wakati mwingine fikra fulani zinaachwa kukua kwa sababu hazipewi changamoto: Kwa mfano, watu wanasema kwa haraka kuwa Muungano wetu siyo halali kwa sababu wananchi hawakuulizwa! Tukiwaambia kuwa mbona Bunge la Tanganyika na lile la Zanzibar yote yalikutana na kupiga kura kuridhia mkataba wa Muungano ndiyo baadaye Karume akaenda Dar kukamilisha taratibu za kuunganisha nchi (baada ya mabunge kuridhia Muungano) wakosoaji wa Muungano watasema kwanini haikupigwa kura ya maoni!

  Wanataka tuamini kuwa uhalali wa Muungano unahitaji kura za maoni! Tukiwauliza mbona Muungano wa US, UK, hawakupiga kura lakini ni muungano halali? Makoloni ya kwanza 13 ya US yalipojiunga na kuwa umoja kwenye vita vya mapinduzi na baadaye kuungana kama taifa hawakupiga kura za maoni kuwauliza wananchi ila wawakilishi wao.

  Sasa leo hii baadhi yetu wanataka tuamini kuwa Muungano wetu siyo halali ati kwa sababu hakuna kura ya maoni iliyofanyika. Lakini hawa hawa wanaamini mipaka iliyojengwa na Mjerumani na Mwingireza kuunda Tanganyika na Zanzibar kuwa ni mipaka halali na kuwa mataifa yaliyoundwa na wakoloni yalikuwa ni halali! Hawajiulizi uhalali wa mataifa ya wakoloni ulitoka wapi wakati babu zetu waliwakataa? Kwanini Tanganyika ilikuwa ni nchi halali na watu wanaililia wakati haikuundwa na Watanganyika bali na wakoloni? kwanini Tanganyika ya mkoloni ikumbatiwe wakati Tanzania ya wazalendo ikataliwe!? Labda tunaamini wakoloni walikuwa sahihi zaidi walipotuundia Tanganyika bila hata kumshirikisha Mtanganyika mmoja, lakini Tanzania iliyoundwa kwa kushirikisha watanganyika na wazanzibari inaonekana haifai.

  Kwa hiyo, wakati mwingine naamini ni vizuri tu kuwajibu ili kuonesha mantiki inapoanzia au inapoishia.
   
 15. D

  Dotori JF-Expert Member

  #15
  Apr 25, 2010
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 547
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Safi sana! Nimeipenda hii Mwanakijiji
   
 16. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #16
  Apr 25, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Ni sawa na hoja na kasumba nyengine kujazwa katika vichwa vya watu wasiofikiri vizuri. Si kweli na kama ushahidi unao tuletee hapa nitakuwa wa Mzanzibari wa mwanzo kukubali uhalali wa Muungano huu batili, kuwa bunge la Zanzibar (kwanza lipi?), limeridhia mkataba (upi?) wa muungano na baadae Karume akenda Dar kukamilsha taratibu (twambie zipi?) za kuunganisha nchi, hizi ni kasumba na porpaganda za uwongo, ambaye hakuna anayeziamini huku kwetu hata hao viongozi wa CCM Zanzibar, ni mara ngapi Mh. Aman Karume amekuwa akilalamika kuwa baba yake "anasingiziwa" mambo wala hajafanya.

  Baraza la Mapinduzi Zanzibar, wakati huo ndo chombo cha maamuzi ya amri (military commission) na halikuwa na hadhi ya bunge au chombo cha kutunga sheria, halikuwa na ridhaa ya Wazanzibar, kwa kuwa lili ji-impose lenyewe madarakani. Lakini tuseme hivyo unavyotaka wewe kuwa kilikuwa chombo kilichokuwapo kupitisha maamuzi makuu ya nchi, bado uhalali wa Muungano utahojiwa kwa kuwa hakuna ushahidi wowote wa kimaandishi(hansard or minutes) za kukutana chombo hicho, mahala popote pale ndani na nje ya Zanzibar kupitisha maamuzi ya kuunganisha Zanzibar na Tanganyika.
  Huo unaouita "mkataba wa Muungano", kule Zanzibar na wazanzibar wote, ikiwemo SMZ hawakijuwi hata kilivyokaa...Mwanasheria MKuu wa Zanzibar alipoitwa Mahakama Kuu ya Zanzibar na kuulizwa huo ulipo "mkataba" wa muungano, alijibu "...hajuwi..." na jibu lipo katika rekodi za Mahakama ya Zanzibar kama jibu la serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambayo wewe unasema Baraza lake la Mapinduzi lilikutana kupitisha mkataba wa muungano...kwa jibu la Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, huo ni uwongo...!
  Pengine haya yasikutwange, hata waasisi wa ASP, Mzee Aboud Jumbe, alishaeleza kuwa yeye ndiye aliyekuwa mshauri nambari moja wa Mzee Karume,katika hilo Baraza la Mapinduzi...hakifanyiki kitu bila yeye kuarifiwa mapema, hata kama hayupo, kwa maneno yake mwenyewe Mzee Jumbe...anasema kuwa aliyemshawishi Karume kuunganisha nchi ni Nyerere...na yeye wakati anarudi ziara ya kikazi Pemba...alikwenda Kiswandui kuripoti kwa bosi wake(Mzee Karume) na kumkuta ndiyo kwanza anamaliza mazungumzo na ujumbe wa serikali ya Tanganyika ulioongozwa na Mzee Kawawa, Bhoke Munanka n.k...waliotumwa na Nyerere kuja kumshawishi Karume akubaliane na mpango wake wa kuunganisha nchi. Baada ya ugeni huo kuondoka, Karume akamueleza Jumbe kuwa ameshakubali kuunganisha Zanzibar na Tanganyika na kumtaka yeye Jumbe akubali. Au hili ndo unaliita baraza la mapinduzi Mwanakijiji?(refer kitabu cha Aboud Jumbe...Partner-ship...) kwa maelezo zaidi ya unafiki na ubatili wa huu Muungano.
  Mipaka ya nchi ya kikoloni, kwanza Zanziabar haikuwahi kuwa koloni, kwakuwa ilikuwa ni nchi kabla ya Sultan na ikaendelea kuwa hivyo hata baada ya Berlin conference...mabadiliko ya tawala ni jambo la kawaida kwa nchi zote duniani, kwa hiyo ilikuwa na haki ya kuamua mustakbali wake, wakati wowote ule na si kulazimishwa kuungana kwa njia za kijanja janja za Karume na Nyerere tu!
  Bado nasisitiza, kama wanavyosisitiza wazanzibari wote, mfano wangu, kuwa Wazanzibar walikuwa na haki ya kuulizwa kwa njia yoyete ile, mustakabli wa jambo lolote linalohusu nchi yao...Karume na Nyerere hawakuwa mitume wa mungu kuwa walivyotaka wao ndo wanavyotaka wananchi hata wa kizazi hiki.
  Kinyume cha mambo, kwa kuonyesha kuwa Muungano huu ulikuwa ni batili na kwa nia ya kuimeza Zanzibar, wananchi wake hawakupewa fursa ya kuulizwa kama wanataka au la, lakini yale mambo ambayo hayakuwa na haja ya kuulizwa kama wanataka au la ndiyo serikali ya Muungano inawauliza wananchi. Mfano Kura ya maoni ya serikali ya umoja wa kitaifa, umeona wapi wewe suala la umoja na mshikamano watu wakaulizwa kama wanalitaka au hawalitaki kama si upuuzi wa ki-CCM huu? si wangetumia fomula ile ile,unayodai wewe kuwa ilifanywa na BLM, kuamua tu, sasa iundwe serilkali ya umoja wa kitaifa, kwa nia ya kuleta umoja na mshikamano. Kwa kiasi hiki cha unafiki wa SMT,SMZ na CCM, huoni kuwa kina akisi unafiki ule ule wa Nyerere na Karume, wao wawili tu, kuamua jambo la haki za mamilioni ya wananchi?
  Na je, si kwa kiasi hiki hiki tunaweza kuhoji ukweli wa kauli kuwa Muungano huu ulikuwa wa ridhaa, huku kukiwa na kauli na matendo yaliyojaa shaka?
  Watu wanaogopa nini kurudi kwa wananchi kuwauliza wanancho taka, kwa nini serikali ya Muungano inalazimisha lazima Muungano huu udumu...kwanini wanashikilia Zanzibar tu...Zanziabar tu...Zanzibar tu...mbona EAC member states hazikulazimishwa kubaki katika shirikisho zilipoona mambo hayendi vizuri...kila mmoja akashika njia yake...kwanini Tanganyika inaishikilia Zanzibar tu, imekuwa haina khiyari, haina sauti....bado tukae tuamini kuwa tuliungana kwa ridhaa...?
  Kwanini Nyerere, hakuzilazimisha Kenya na Uganda kubaki kwenye shirikisho...wakati "...uwezo, nia na sababu alikuwa nayo...hata nguvu..." kama kweli alikuwa na dhamira ya umoja wa Kiafrika na badala yake kuishikilia Zanzibar kama ya baba yake na mama yake...! bado mnataka kuamini tuliungana kwa ridhaa...?
  Wanaoungana kwa ridhaa, kama ilivyokuwa kwa AEC ya mwanzo wanakuwa na haki sawa na maamuzi...na ndiyo maana walipoona ujinga wa Nyerere wakamuacha mkono,kwa kuwa walikuwa na khiyari...waliungana kwa khiyari...mbona hili halipo kwa Muungano huu wa Tanzania kuna nini....? bado mnataka tuamini kuwa muungano huu ni halali...?
  Tufanyeni kura ya maoni ya haki, kuamua, kama SMT ni majasiri kweli na wafanye, mimi nawapa changamoto hiyo, kuwa itakuwa ni kipimo cha uhalali wa muungano huu, na sisi wazanzibar hatutakuwa na matatizo nao hata kidogo.
  Hili si jambo geni, Eritrea walifanya na Ethiopia 1990s, Serbia-Montenegro walifanya, serbia-kosovo walifanya, E. Timor na Indonesia walifanya...na maeneo yote hayo walipewa fursa wananchi kuamua mustakbali wa nchi zao kwenye muungano...kwa nini sisi isiwezekane...?
  Muungano huu utabakia ni batili kwa maoni ya Wazanzibar wengi iwapo hautawekwa katika mizani ya haki ya kupima uhalali wake.
   
 17. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #17
  Apr 25, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280

  Mwanakiji unachosema ninakubaliana nacho kabisa na mifano unayoisema ya huko nje nayo ni halali. Swala zima hapa ni kuwa tunaweza kuhalalisha muungano kwa sababu ulizozisema, kuwa bunge lilipiga kura. Kwangu mimi kura za maoni sioni kama zina ulazima kama wawakilishi wa wananchi walihusika. On the other hand kuhusu mipaka hiyo ipo dunia nzima haijalishi nani aliweka au la.

  The question here ni kuwa kama wananchi wanaelewa umuhimu wa muungano haya malalamiko yasingekuwepo! Mwanakijiji watu washindwe kuona documents za muungano kisa kwa sababu waliwakilishwa na wabunge? what does that make difference na kuhusu mikataba ya madini,ambayo ngasongwa anasema ni siri ya serikali?

  Personaly labda ujue msimamo wangu, I do believe muungano ni halali, ila uhalali wa muungano kama hautahalalishwa na wananchi (social licence)wenyewe basi kuna tatizo somewhere, ndio wabunge walipiga kura je waliongea na wananchi wao? kwa mfano huku bara hatuna tatizo na muungano, kitu gani kinapelekea hawa zanzibar na uchache wao kutotaka muungano? Mwanakijiji serikali inaweza ikawa sahihi kwa vitu vingi sana, ila isipokuwa wazi kwa wananchi husika, vitu vingi vinakuwa nullified.

  Mfano issue ya Kakobe na Tanesco unaona wazi kabisa serikali iko sahihi, lakini mpaka inapokuja kumwelekeza mwananchi hasara imeshatokea, why our governments are not open? hii hali tete ya sasa kwenye muungano ni failure yenyewe! mbaya zaidi wanaposema watu ambao ni wazee

  kwani nini tuliungana, faida, nyaraka ziko wapi n.k viwe wazi.

  Hii issue haitakiwi hata kujadiliwa in first place! tangu 1964 hakuna elimu au habari au namna yoyote ya kuwaelimisha hao watu wa visiwani? Ukijivika vazi la uongozi zaidi utaona failure ya hii issue , ukijivika vazi la utawala, hutaona tatizo na hasa unapokuwa na sababu za msingi.

  Hata leo wanaweza kuwa convinced wakaelezwa umuhimu wa Muungano!, leo tutajaribu kuulinda, just one generation tu tangu muungano maswali yako hivi!!! je miaka 100 ijayo hali itakuwaje? au mlioshuhudia muungano mtaona fahari leo muungano ukiwa intact, ila baada ya miaka 50 ukavunjika simply kwa sababu serikali inaendekeza ubabe wa kuficha documents! documents halali, zisizo na mawaa wala madoa?

  Mtu anasema bila woga Tanganyika iliivamia Zanzibar? is this not a joke? failure ya hizi statement siyo wananchi ni serikali, ina maana they know nothing about muungano! hawajashawishiwa kuuona umuhimu wa muungano! hakuna utaratibu wa kurithisha elimu hii ya muungano ieleweke hata na vizazi vijavyo, hamna huu utaratibu!

  Wananchi wana nguvu jamani tena hasa wanapokuwa wajinga!!!
   
 18. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #18
  Apr 25, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  HASWAA!! Sasa jambo lililowekwa kisheria na baadae kukiukwa Sheria tunasemaje kisheria kitu hicho???
   
 19. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #19
  Apr 25, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,571
  Likes Received: 18,544
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, ni bahati mbaya sana, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, hauna mkataba wowote in a real sense ya mkataba wa kimataifa kati ya mataifa mawili huru. Tukishakubaliana kwamba hakuna mkataba kabisa, hapo ndipo ilegitimacy ya muungano ilipoanzia. Kilichopo sio mkataba wa Muungano bali ni makubaliano ya muungano, not a contract but only agreement just like MOU.Pamoja na kutokuwepo huo mkataba, mimi ni muumini wa Pan-Africanism kuwa Waafrika ni wamoja ila ni wakoloni ndio wamekuja kutuwekea mipaka. Hakuna ubishi Wahaya wanabelong chini ya Kabaka Empire enzi za Interlucustrine Kingdom ambapo kina Mkama Rumanyika were part and parcel, bali ni mkoloni ndiye aliyekuja kupiga mipaka wahaya kujikuta wako huku na Waganda kule, sawasawa na Wamasai wa Kenya na Uganda ni wale wale.Hatuhitaji paperwork documents be it hati au mkataba kuonyesha tumeungana, kama yalivyo mapenzi ya kweli toka enzi za mababu, hatukuhitaji hati/cheti cha ndoa kuthibitisha mapenzi na ndoa ni mpaka waipokuja wazungu na macheti yao.Hivyo Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulizaa Tanzania, hauhitaji paper work be it hati/mkataba ili kuuhalalisha, hata pale Nyerere na Karume waliposemezana tuu wao kwa wao ilitosha bila kuandika chochote popote. Tatizo hizi zote mbili zilishakuwa nchi huru kwa mujibu wa wazungu, mambo yanakwenda kwa hati na maandishi na ikibidi wananchi washirikishwe kitu ambacho hakikufanyika kwa mujibu wa taratibu.Kwa maoni yangu, Wanzanzibari ni wanafiki wa hali ya juu sana, kama waliukubali Muungano bila kuleta fyoko fyoko yoyote, iweje leo wakapitisha kura ya maoni kuulizia jambo dogo jema la kuwaletea umoja miongoni mwao, na wasitake kutumia fursa hiyo ya kura ya maoni kuwauliza Wanzanzibari jambo kubwa kama hili la Muungano na nchi nyingine?!.
   
 20. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #20
  Apr 25, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145

  Kama ni hivyo basi hojaji za uhalali wa mambo isiwe kwa Muungano tu. Mbona hilo baraza lilipitisha mambo mengine mengi lakini hayo hayahojiwi?
   
Loading...