The Arab & Western Spring - Nguvu ya Umma?

Mr.Toyo

JF-Expert Member
Feb 9, 2007
433
117
Tumekuwa tukishudia matokeo mengi ya watawala walokuwa thabiti katika madaraka wakiangushwa kwa kianzio cha maandamano ya raia wao
chicago-egypt-protest-2011-1-29-16-42-25.jpg

Miongoni mwao ni Tunisia, Egypt, Libya na nyinginezo ambazo kwa sasa ziko katika hatihati ya kuangushwa tawala zilizopo..
images

On the other hand naamini kwa wafuatiliaji si geni suala la maandamano yanayoendelea huko USA waandamanaji ikiwemo moja ya madai yao “End financial aid to Israel, end occupation of Gaza,”
end_aid_to_israel.jpg

Nini mawazo yako juu ya kinachoendelea katika nchi hizo...?
 
Kwa habari zilizonifikia jana ni kwamba Turkey imo mbioni kutumika na NATO kuishambulia Syria..

Am following up on that, will post it here with SOURCE.
 
JUMANNE, 11 OKTOBA 2011 09:54
Mwamko wa wananchi wa Marekani waenea katika miji mingi zaidi
wall_street_march_04907.jpg
Maandamano ya wananchi wa Marekani yanayopinga mfumo wa kibepari nchini humo yamepamba moto na kuenea katika miji zaidi ya elfu moja ya nchi hiyo.
Mwamko huo wa wananchi wa Marekani dhidi ya watu wanaohodhi kila kitu nchini Marekani umepata nguvu kutokana na kuongezeka ubadhirifu, umaskini na ukosefu wa uadilifu katika jamii ya nchi hiyo.
Waandaaji wa maandamano hayo yaliyopata ilhamu kutokana na mapinduzi ya wananchi wa nchi za Kiarabu wamesema kuwa wataendelea na harakati zao hadi ushindi.
Maria All-wine ambaye pia ni mwanaharakati wa haki za binaadamu amesema kuwa wataendelea kukusanyika kwenye eneo la Freedom Plaza karibu na Ikulu ya Marekani White House kwa muda usiojulikana.
Wananchi wa Marekani wanalalamikia pia siasa za nchi yao za kupoteza fedha nyingi kugharamia vita nje ya Marekani kama vile Afghanistan katika hali ambayo wananchi wa nchi hiyo wanakufa kwa njaa.
Wananchi wa Marekani aidha wanalalamika kuwa, utajiri wa nchi hiyo umehodhiwa na asilimia moja tu ya watu, huku asilimia 99 ya wananchi wengine wa Marekani wakisumbuliwa na matatizo mbalimbali.

CHANZO:
Mwamko wa wananchi wa Marekani waenea katika miji mingi zaidi
 
Back
Top Bottom