THE ACCIDENTAL BILLIONAIRES- The founding of facebook: a tale of money,genius and betrayal

Hii JF siyo ya GT anymore watu wana IQ ndogo sana, akili yako imekuw messed sana na mademu hamna kingine akl inawaza poor guy whoever you are, Link iko hapo juu in pdf form anaeielewa lugha ya malkia ajisomee asieelewa asubir mwana amalizie kama wewe una link ya kiswahil wape watu.
Unashindia magazeti ya udaku unajiita great thinker? What was the name of the last book yo read wewe unajiita great thinker...
 
Unashindia magazeti ya udaku unajiita great thinker? What was the name of the last book yo read wewe unajiita great thinker...
Anyway, kuna kitu utakuw una-miss in ur life which gives you so much stress na pia kuna stage haukuipitia vzur during ur childhood so psychologically u're nt okay, na it shows una ulimbuken na u-much knw in yu, yu need some counseling little guy, ulishaisoma hyo story hukuisoma has nothing to do with us, hajaanzsha hyo thread for argumentation, weng tunaijua hyo story bt mtu anapojtolea ku-type vtu vyte hvo on his time hatakama vna-miss something we appreciate coz,
Watu wata-refresh their brains na mwngne ataweza kuokota ktu in that story hence life wll go on.
Mwanaume kuwa na wivu wa dizain hyo inatia ukakas kidogo, am sure utakuw n mwanamke coz mwanaume huwez kuwa hvo.
Na it seems vtabu umeanza kuvisoma juzi, vitabu tulivovisoma wengne huenda hamna hata kwenye ukoo wenu aliyewah kuvisoma na hautakuja kuvisoma mpaka unakufa, vya story kama hz huwa tunapga story tu only weekend days.
 
Kila movie lazima antagonist aplay part yake

I'm not trying to make you understand, ila:-

Moja: I'm not a man

Mbili: Hujalazimishwa kusoma

Tatu: Hata ningetoa link direct bila kusimulia, na imani kati ya watu kumi mmoja pekee ndo angeweza kusoma

Nne: Link imo humu ndani wenzio wameshaitoa, siju kwa nini wewe sasa hujaenda kuisoma, naimani hujasoma comments

Tano: Don't pretend to act smart


Haters.! Hatin for no godamn reason,link imewekwa uko juu hajasoma n' yet analalamika.

Sina mood ya kuongea sana acha niishie hapa kwa leo aiseee
 
Story iendelee, kiukweli ile original story haieleweki co tu kwa lugha iliyotumika bali mpangalio wa story kwa ufupi haivutii kuisoma. So shusha vitu mpaka mwsho.
 
Screenshot (140).png


Sehemu ya 5


Kitendo cha Eduardo kufunga akaunti ya bank kilikuwa ni kama kitendo cha kuwakaata koo Mark na Dustin, kilikuwa ni kama kitendo cha kuiondolea uhai kampuni kitendo ambacho kingeharibu kazi yote aliyofanya Mark kwani bila pesa kampuni isingefanya chochote kile, kama server zingezima hata kwa siku moja, ingeharibu sifa ya thefacebook na kusababisha watu kuhama katika mtandao huo. Eduardo alikuwa amevuka mpaka, huenda hakuelewa alichokifanya, huenda alifanya vile kwa sababu ya hasira au la lakini Sean aliona kitendo kile kilikuwa ni cha kitoto na si cha kibiashara kama ambavyo Eduardo alifikiria, Sean aliona Eduardo anamatatizo makubwa ya kutojielewa ambayo alitakiwa ayashughulikie, kwanza kitendo cha yeye kusema anafanya shughuli za kampuni akiwa Newyork huku wenzake wakiwa California aliona kuwa kilikuwa ni kitendo cha kijeuri kisichokuwa na sababu, halafu pili kutumia umiliki wake wa asilimia 30 kuipelekesha kampuni, kwamba anaishinikiza kampuni kufuata anavyotaka yeye! Sean aliona kuna sababu ya kumchukia Eduardo

Pamoja na yote hayo Mark hakutaka kumchukia Eduardo, Mark hakuwa na moyo wa kumchukia mtu wala hakuvutiwa kutaka kumchukia Eduardo, alikubaliana na hali halisi kama ilivyokuwa, lakini bado alitaka kuendelea kuwa na sababu ya kuamua alichokiamua.
Kwanza, chini ya usimamizi wa Sean aliamua kuibadilisha kampuni kuwa 'limited liability company' yaani wamiliki wa kampuni hawahusiki na madeni ya kampuni, ili kuweza kuilinda kampuni dhidi ya vitisho vya Eduardo, kisha alichukua fedha zake za chuo alizowekeza ikiwemo fedha za ada na kuziweka kwenye kampuni ili zikute zikisaidia kampuni kwa muda mpaka mambo yatakapokaa sawa. Na kwa kuwa katika kipindi hicho alikuwa amepokea barua kutoka kwa mwanasheria wa ConnectU alieajiriwa na Winklevoss twin ili aweze kushughulikia mashtaka yao dhidi ya Mark, basi Mark angehitaji pesa kwa ajili ya kujitetea
Na hivyo basi, alihitaji mwekezaji ili aweze kupata pesa za kampuni na za kuendesha kesi yake ambapo Sean alimwambia kuwa asiwe na hofu kwani mapacha hao hawakuwa hatari yoyote ile kwa kampuni kama ambavyo alivyokuwa Eduardo.
Sean alijithidi kwa kadri ya uwezo wake na kuweza kutafta connection sehemu ambayo alijua lazima itakuwa funguo wa kile kitakachoenda kutokea mbeleni, sehemu ambayo itaifanya thefacebook kuwa kama ambavyo alijua itakuwa

Sean alimpeleka Mark kuonana na mwekezaji, Mmiliki wa Paypal, Peter Thiel ambae hapo mwanzo Sean aliwahi kumsogelea na kumletea kampuni nyingine ya mtandao ili aweze kuwekeza na kuweza kuwekeza na tangu siku hiyo Sean alimweka Peter Thiel akilini kwake kama iwapo itatokea fursa nyingine ya uwekezaji

"Nafikiri atakupenda" Sean alimwambia Mark ili kumfariji wakati ambao walikuwa ndani ya lift kuelekea kwenye office ya Peter Thiel na Mark akionekana kuwa kimya sana " Ni muda wa dakika kumi na tano tu utakuwa tayari umeshatoka" Sean aliongeza

Kikao kile cha dakika kumi na tano, Peter Thiel alikigeuza na kwenda mpaka launch kisha Mark na Sean kuchukuliwa kwenda kutembezwa sehemu mbalimbali ili kumpa nafasi ya kujadili Peter Thiel na wenzake

Peter Thiel alikuwa kama ambavyo Sean alitarajia
Peter Thiel alikubali kuwekeza thefacebook, alikubali kutoa dollar laki tano kama pesa ya kuanzia
Dollar laki tano kwa Mark hazikuwa pesa nyingi,Mark hakuwahi kujali pesa lakini kwa pesa hizo hakuwa tayari kuzipuuza kwani alichotaka ni kampuni yake, alichotaka ni kampuni yake aliyoianzisha bwenini iweze kuendelea kwa kuwa hakuwa tayari kurudi nyuma na alimwambia Peter Thiel kuwa asingeweza kurudi chuoni ili aweze kuendelea na uvumbuzi wa thefacebook ila kama thefacebook isingefanikiwa basi angekuwa tayari kurudi chuoni

Peter Thiel aliziita fedda zile kama mbegu, ambazo aliona zingetosha kuwafikisha miezi ya mbele na kusema kuwa atatoa tena endapo hitaji litajitokeza
Na sasa kampuni ilikuwa inaenda kubadilika, kwanza Peter Thiel ataenda kuwa mmiliki wa asilimia 7 za kampuni na atakuwa na nafasi katika board ya madirector watano ambao wataiongoza kampuni kusonga mbele huku Mark akiendelea kuwa katika nafasi mbalimbali ikiwemo kuwa mkuu wa kampuni yenyewe. Na kingine 'thefacebook' ilikuwa inaenda kubadilika jina na kuwa ni 'Facebook' pekee kama ambvyo Sean aliomba kila siku iwe hivyo
Kampuni ilikuwa lazima iandikwe na kuainishwa upya kama ambavyo wamekubaliana na Thiel, ilitakiwa kutoka kwenye uzamani wake na kuwa kampuni mpya ambapo share zitatolewa upya kuashiria mpangilio mpya huku akijumuishwa Thiel na Sean Parker pia ambae amekuwa akifanya kazi kama partner wa Mark tangu ahamie sehemu wanayoishi
Suala lililobaki lilikuwa ni la Eduardo, Mark aliamua kuwa Eduardo bado aendelee kuwa na asilimia 30 zake ili kwamba waweze kumjumuisha na kumuhusisha kwa kadri ambavyo angetaka japo kampuni jipya litakuwa na sheria mpya, sheria ambazo ni tofauti, haikuwa kampuni ya bwenini tena bali kampuni halisi yenye mwekezaji halisi
Kampuni halisi ambayo walitakiwa kwendana nayo ili kuweza kuthamanishwa na kile kilichopatikana, kwamba share zitakuwa kulingana na nguvu kazi, kama Eduardo atakuwa huko New York akitafuta wawekezaji atapata share inavyotakiwa lakini kama asipozalisha share zitapunguzwa kama ambavyo itakuwa kwa kila mtu. Sean aikubaliana na hilo lakini alijua kuwa bado kuna kikwazo mbele, kazi kubwa bado ilikuwa inahitajika kufanyika
Kikubwa kilichokuwepo ni Mark alitakiwa amfuatishe Eduardo,Eduardo akubali kuhusu sheria na maamuzi yale ya kampuni ili kuweka kila kitu sawa, atatakiwa aelewe kwamba yale sio mambo ya kibinafsi tena na bali ni biashara na Eduardo mwenyewe alijiona kuwa ni mfanyabiashara, alitakiwa aelewe kuwa pia hayakuwa mambo yaliyohusisha watu wawili bwenini tena, Sean Parker aliona kama Eduardo hataelewa basi hatakuwa anaijali Facebook kama ambavyo wanaijali
Na Sean na Thiel walikuwa wamemwelewesha Mark kuwa hakuna mwekezaji ambae ataenda kuwapatia pesa waakiwa na mtu ambae anakimbia kimbia New York akidai kuwa anamiliki asilimia 30 za kampuni ambazo anazitumia kushinikiza akiwa tayari kwa lolote lile, kusimamisha akaunti, kuwatishia wao na kuitishia kampuni pia
Kama Eduardo hataelewa basi hatakuwa na faida tena, atakuwa hayupo tena

***

Mark hakufurahishwa na tukio lile la bank na kuamua kufanya kikao na Thiel na kuweza kupata fedha za kampuni japo ilikuwa ni kinyume na matakwa ya Eduardo
Walikuwa wamebishana mara kwa mara kwenye simu kama ambavyo marafiki wa kawaida wangeweza kubishania kitu ambacho kimekuwa kama ambavyo hawakutarajia kiwe
Ndio, Eduardo alitenda ndivyo sivyo kwa kitendo kile cha bank, lakini Mark amekewa mbinafsi kwa kutomhusisha Eduardo katika maamuzi yale.
Mpaka hapo Mark alimwambia Eduardo kuwa asogee nyuma kidogo ili aweze kuwa huru na kujali zaidi masomo yake, alimshawishi kuwa, kampuni ilikuwa inakuwa kubwa kwa yeye kuweza kuendesha masuala ya kibiashara peke yake kitu ambacho kilikuwa hakiwezekani kama ambavyo Eduardo alikuwa anadai inawezekana
Kampuni ilikuwa inaendelea kukua na kwamba yeye na Dustin walikuwa hawarudi chuo, inawezekana kwa semister moja au hata zaidi ya hapo na kwamba walikwa wanapanga kuajiri mtu ambae atachukua nafasi ya Eduardo kwa muda
Pia walikuwa wanaendelea kuboresha zaidi site kwa namna ya kupendeza ikiwemo kuwepo kwa magroup mbalimbali ambayo watu wangeweza kujiunga, wazo ambalo Eduardo aliwahi kuzungumza nae kipindi wanaanza kutengeneza website hiyo

Zilikuwa zimepita takribani wiki nane tangu chuo kifunguliwe,Eduardo kuwa chuoni na kusahau kama kuliwahi kuwa na likizo. Katika mwaka wake huo wa mwisho, kitu ambacho kilimfurahisha zaidi Eduardo ni kumskia Raisi wa chuo akitangaza kuwa wanafunzi wote wanaoingia mwaka wa kwanza ameshawaangalia kwenye Facebook, Eduardo alifurahi kwamba Raisi alikuwa anatumia website yao kuwafahamu wanafunzi wake wakati miezi kadhaa nyuma yeye na Mark hawakuwa chochote kile chuoni hapo na sasa Raisi anaangalia walichokifanya!

Mpaka mwisho, Eduardo alikuwa amepoa na hasira zake alizokuwa nazo ziliisha, alikuwa amekuja na suluhisho kwamba, siku zote Mark atafanya vitu kama Mark, kitu cha muhimu kilikuwa ni kwamba kampuni ilikuwa inasonga mbele, kwa pesa za Thiel ,hakuwa anahatarisha fedha zake tena. Thiel sasa alikuwa ni kila kitu hivyo hakuna kitu kwa wakati huo ambacho kampuni ingeshindwa kukikabili.
Kila kitu kilikuwa kinalipiwa na fedha alizowekeza Peter Thiel kuanzia nyumba mpya ambayo walihamia baada ya kufukuzwa kwenye nyumba ya kwanza kutokana na fujo walizokuwa wakizifanya zikiwemo kufungulia mziki kwa sauti ya juu, kupanda juu ya paa na kujitupia kwenye swimming pool, kurushia vitu ndani ya swimming pool na kuharibu badhi ya vitu pia,
Server zaidi ziliweza kuongezwa na kompyuta nyingi zaidi ziliweza kununuliwa zaidi ya ambavyo Eduardo angeweza kutegemea

Malumbano ya yeye na Mark yalikuwa na haja ya kuwepo tena? Na kwa wakati huo Mark alikuwa amemwita California ili aweze kusign documents za muundo mpya wa kampuni mpya, Eduardo alinyanyua mabega kuashiria kuwa yote yalikuwa ni kwa ajili ya kheri

Akiwa ameketi kwenye kiti katika nyumba ile mpya California akiiangaza jinsi ilivyokuwa, kila mmoja akiwa bussy na kompyuta na headphones sikioni akiwemo Mark ambae wamesalimiana kwa kutikisa kichwa tu na kuongea maneno mawili matatu basi na hawajazungumza chochote tena tangu awasili ambapo alipokelewa na mwanasheria wa kampuni ambae alimsalimia kwa kumshika mkono huku akitabasamu
Akiwa ameketi pale, mwanasheria alie pembeni yake alimkabidhi document za kampuni
Eduardo alianza kuzipitia document zile za kuunda kampuni jipya huku akionekana kutozielewa hivyo aliomba kueleweshwa, mwanasheria alimsogelea na kuanza kumwelewesha kwamba kulikuwa na mabadiliko ya shares za kampuni, shares za kampuni jipya zikichukua nafasi ya zile za zamani, kulingana na mwanasheria na Mark ambae alisogea ili kusaidia kuelezea muundo mpya wa kampuni, walimwelezea Eduardo kuwa, sasa atakuwa na asilimia 34.4 ya umiliki wa facebook, share ambazo zimeongezeka kutoka zile asilimia 30 za mwanzo, Mark umiliki wake umepungua mpaka asilimia 51, Dustin sasa ana asilimia 6.81 ya umiliki wa kampuni, Sean Parker anaumiliki wa kampuni kwa asilimia 6.71 ambapo Eduardo aliona ni nyingi kuliko alivyostahili, na Peter Thiel alikuwa na umiliki wa kampuni kwa asilimia 7
Eduardo alichokiona kwenye document kingine ni kuwa hataruhusiwa kuuza share zake kwani umiliki wake bado upo kwenye karatasi, alihashumu pia ni hivyohivyo kwa Mark Dustin na Sean

Eduardo alizisoma document zile tena na tena akijua kuwa ni za muhimu, kwamba zilikuwa ni documents halali na hivyo kuzisign ilikuwa ni hatua kubwa ya kampuni, lakini mpaka hapo alihisi kuwa yupo salama kutokana na sababu Kwanza, kulikuwa na wanasheria pale, wanasheria wa facebook ambapo ilimaanisha akilini kwake kuwa ni wanasheria wake pia, na kingine Mark rafiki yake alikuwepo pale na alimwambia kuwa documents zile zilikuwa ni nzuri na za muhimu, na pia Sean Parker alikuwa sehemu ndani mle na kwa sasa akiwa ni sehemu halali ya facebook
Kitu cha muhimu ni kwamba bado angeendelea kuwa na asilimia zake zilezile.
Kitu alichojiuliza ni kwamba, ndio kutakuwa na mchujo wa share, kwani hawatakuwa wakichujwa wote kwa pamaoja? haijalishi kuwa sio thefacebook tena, je hatakuwa na cheo kilekile kwenye hii facebook? Aliwaza mazungumzo ya nyuma aliyokuwa amezungumza na Mark karibuni, Eduardo kama hakuelewa vizuri vile, akilini mwake aliona kama Mark alikuwa akimwambia kuwa-hakuhitaji kufanya sana kazi kwa kampuni wakati akiwa chuoni, kwamba wanaenda kuajiri mtu, kwamba asogee nyuma- wakati yeye alisema kuwa bado atakuwa na muda wa kufanya kazi thefacebook

Zile documents aliziona akilini mwake zikisema kuwa alikuwa ni mtu mkubwa katika kampuni kwa namna ambayo hajapata kuona. Vitu vitaweza badilika kwa kadri pesa zitakavyozidi kuingia na kadri watu watakapozidi kuajiriwa lakini documents zile zilikuwa ni muhimu katika kuunda kampuni

Na Mark alikuwa amemwambia kuwa kutakuwa na party, party ya kusherehekea kipindi watakapofikisha watu million moja, part ambayo Peter Thiel ataifanyia katika mgahawa wake hivyo Eduardo atatakiwa kusafiri tena kuja kuhudhuria party hio

Eduardo alitabasamu huku akichukua kalamu na kusign documents zile, na kwa kuwa sasa alimiliki asilimia 34 ya facebook aliona kuwa kulikuwa na haja ya kusherehekea.

***

December 8 2004
Eduardo aliingia ndani ya mgahawa ule ambao sherehe ilikuwa ikifanyika, sherehe ya kufikisha wanachama million moja wanaotumia facebook
Eduardo aliangaza huku na kule ndani ya ukumbi ule uliojaa watu mbalimbali na kuweza kuwaona Sean, Mark na Peter wakiwa wameketi sehemu moja, na kwa bahati nzuri siku hiyo iligongana na siku ya Sean ya kuzaliwa hivyo kila mmoja alikuwa na furaha
Sean alikuwa ameketi akiwasikiliza Mark na Peter wakipanga mipango mbalimbali ya kuipanua facebook na kuiboresha zaidi na pengine kutengeneza application ya watu kuweza kushare picha na hivyo facebook ingeendelea kuboreka kila siku na kila siku
Sean aliwatazama Mark na Peter wakizungumza na kuona kuwa wame match kama ambavyo alihisi itakuwa na kuona kuwa mpaka hapo kila mmoja alikuwa na furaha

Eduardo tangu aingie ndani mle amekuwa akiwaambia watu kuwa yeye,Mark na Dustin wamegundua facebook pamoja, baadhi walicheka na baadhi walimtazama kama kichaa, hakuna aliejua alichokifanya, kila mtu alikuwa anamwangalia Mark- Mark pekee
Eduardo hakujali kubakia nyuma alichojua ni kwamba amehusika kiasi kikubwa kwa hao wanachama mailion moja kupatikana, na zaidi ya yote alikuwa anamiliki asilimia 34 ya kampuni na alikuwa na furaha kwa kisign documents za kampuni ambapo pia Peter Thiel ameweza kuwapatia pesa walizozihitaji ili kuendelea mbele na kampuni na hivyo Facebook itaendelea kukua zaidi na zaidi

***

april 3 2005
Eduardo alikuwa akiwaza safarai ya kuelekea California ambayo angetakiwa kuifanya kesho yake.
Ilikuwa imepita miezi miwili bila kuwa na mawasiliano na Mark ambapo kwa kipindi hicho amekuwa akijali masomo yake kwani karibu alikuwa amalize chuo na hivyo alihitaji kufalu mitihani michache iliyobakia. Kwa kipindi hicho cha miezi miwili alichokuwa hana mawasiliano na Mark, Eduardo aliweza kuaachia website yake iliyoitwa Joboozle ambayo ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya kutafuta kazi, aliendelea na website yake huku akimsubiri Mark arudishe mawasiliano ambapo mara ya mwisho kuwasiliana nae, Mark alimwambia kuwa, office mpya zilikuwa zikimalizika kujengwa na hivyo wangeweza kuhamia katika ofisi hizo

Mark aliporudisha mawasiliano nae kwa njia ya e-mail, siku chache nyuma, aliwambia kuwa asafiri kwenda California kwani kuna kikao muhimu cha biashara na kuna mwajiriwa mpya ambae anatakiwa akampe mafunzo
Mark aliweza kutaja vitu vingine ambavyo vilishika akili ya Eduardo, Mark alitaja baadhi ya wawekezaji ambao walikuwa wakivutiwa na kuwekeza kwenye kampuni yao na hivyo wataweza kumpatia nafasi mwekezaji mmoja.
Kitu kingine Mark alichotaja ni kwamba, yeye Mark, Sean na Dustin wanafikiria kuhusu kuuza baadhi ya share zao kwa hela kama dollaar million mbilia mbazo Mark alimtajia
Eduardo alishangazwa zaidi na hicho, kwanza documents alizosaini zilisema kuwa haruhusiwi kuuza share kwa sababu umiliki wake bado ulikuwa kwenye karatasi, sasa kwa nini Mark Sean na Dustin wao waweze kuuza hizo share zao? kwani hawakusaini documents kama alizosaini yeye?
Pili kwa nini Mark auze share? tangu lini Mark anajali pesa? na Sean Parker kwa nini aweze kutengeneza dollar milion mbili wakati amekuwa sehemu ya facebook kama wiki kumi tu zilizopita halafu yeye asiweze wakati amekuwepo kuanzia mwanzo?!

Eduardo aliona haikuwa sawa kabisa

Labda alielewa vibaya, au labda Mark atamwelezea vizuri atakapofika California. Kwa vyovyote vile hakutaka hisia zake na hasira zake zimtawale tena kama mwanzo kwani aliona hazikumsaidia chochote kipindi kile

Hivyo kesho angeweza kusafiri mpaka California , kuangalia office mpya ambazo zilikuwa zimemalizika kujengwa, kuhudhuria vikao vya biashara, kumfunza mwajiriwa mpya, pia kwa matumaini ya kuwa utakuwa ni mwanzo wa kurudisha sawa uhusiano wake yeye na Mark na kama kawaida akihitimu ataweza kurudi kwenye nafasi yake ya kwanza kama mwanzilishi mwenza wa kampuni wa Mark

***

April 4 2005
Eduardo ataikumbuka siku hii maisha yake yote

Alikuwa akizitazama karatasi ambazo mwanasheria amempatia dakika tu aliyoingia mlangoni ofisini mle. Alikuwa ni mwanasheria tofauti na wa mwanzoni, ilikuwa ni office tofauti, haikuwa tena office ile ya nyumba kama bweni, bali ni office halisi na mwanasheria mwingine halisi ambae alikuwa amesimama sehemu ofisini mle

Kwanza Eduardo alifikiri jamaa anatania kumsalimia na karatasi za mikataba zaidi ili aweze kusign, hata kabla hajapata nafasi ya kuiangalia office ile mpya, wala kabla hajamwuliza Mark kuhusu mwajiriwa mpya na ilikuwa hata kabla hajauliza kuhusu share zile ambazo walitaka kuziuza, ila baada ya kuanza kusoma documents zile aligundua kuwa hiyo safari ya California haikuwa kuhusu kikao cha kibiashara wala nini

Ilimchukua dakika chache kuelewa ni nini alikuwa akikisoma katika documents zile.
Kuelewa kule ilikuwa ni kama kupigwa risasi kifuani, hakuna kitu ambacho kingeweza kuelezea ilikuwa ni kama kuhisi namna gani, tena ni afadhali angekuwa amejua ni nini kitatokea, angejua ni nini kinakuja, angejua ni nini kinafuata, angalau angeona hata dalili. Hakuona chochote, amekuwa kipofu wa hali ya juu tena na mjinga wa hali ya juu
Hakutegemea kitu kama hicho kutoka kwa Mark, rafiki yake, waliekutana kipindi kile katika mazingira yale wakijaribu kufaa katika mazingira yale ya Harvard
Kwa Eduardo huu ulikuwa ni usaliti, halisi na dhahiri. Mark amemsaliti, amemharibu, amechukua kila kitu, kila kitu kimejieleza kwenye karatasi alizoshikilia mkononi

Kwanza document iliyokuwa na tarehe 14 january 2005 imeandikwa kwamba: makubaliano ya wamiliki wa share Thefacebook kuongeza idadi ya share ambazo kampuni inatakiwa kuzigawa kuwa mpaka share million19 kwa pamoja.
Pili, document nyingine iliyoandikwa tarehe 28 march 2005 kuhusu kugawa share zaidi ya million 20. Na kisha kulikuwa na document iliyoonesha utoaji wa share milion 3 nyongeza ya share kwa Mark Zuckerberg, share million 2 nyongeza kwa Dustin Moskovitz, na zaidi ya share million 2 nyongeza kwa Sean Parker
Eduardo aliziangalia idadi ya share zile huku akifanya mahesabu kichwani kwake pamoja na share hizo mpya, Umiliki wake wa facebook wa asilimia 34 haukuwa popote pale, kwamba kama share zote zimetolewa kwa Mark, Sean na Dustin inamaanisha share zake zilikuwa chini ya asilimia kumi na kama share zote mpya zimetolewa inamaanisha hakuna share zozote za kwake zilizobakia

Walikuwa wanamwondoa katika kampuni

Mwanasheria alijaribu kuongea nae huku yeye bado akizitazama karatasi zile, Eduardo alistaajabu kuwa Mark alitegemea ataichukulia vipi hali ile. Au labda Mark alifikiri Eduardo hatafanya chochote kile, laabda Mark alifikiri Eduardo ameshajitoa kwenye kampuni kitambo, kipindi aliposaini documents za mara ya kwanza ambazo zimefanya haya yote yawezekane, au labda kipindi alipofunga akaunti ya bank
Mwanasheria alimwambia Eduardo kuwa, share zote mpya zimeshatolewa kwa wawekezaji hivyo sahihi yake ni kama ilitakiwa tu kama umuhimu katika kampuni, kwamba ulikuwa ni uamuzi ambao tayari umeshafanywa

"NO"
Eduardo alikataa kusign
Amekuwepo tangu mwanzo, alikuwepo katika chumba kile bwenini, alikuwa ni mwanzilishi wa facebook, alistahili hizo asilimia 30, yeye na Mark walikuwa na makubaliano

Jibu la mwanasheria lilikuwa moja kwa moja
Eduardo hakuwa sehemu ya facebook tena, hakuwa sehemu ya wasimamizi, hakuwa mwajiriwa na wala hakuhusika na facebook kwa namna yoyote ile tena na hii inamaana atafutwa kwenye historia ya facebook

Kwa Mark Zuckerberg na facebook, Eduado Saverin hakuwepo tena.

Eduardo aliona kama ukuta unamsogelea kumzonga
Alihitaji kuondoka mle ofisini
Arudi Harvard

Hakuamini alichokiskia. Hakuamini usaliti ule
Lakini alikuwa hana uchaguzi, aliambiwa uamzi umefanywa, umefanywa na Mark Zuckerberg mwanzilishi na CEO, na kupitia raisi mpya wa facebook

Eduardo alibakiwa na wazo moja wakati mawazo mengine yakimwondoka kichwani

Nani alikuwa raisi mpya wa Facebook?

Alipojiuliza swali hilo,alitambua kuwa tayari alilifahamu jibu (Sean Parker)

***

Siku ya Sean ya kulipiza kisasi ilifika. Watu wa kampuni ya plaxo walikuwa wakipiga simu kila siku wakitaka kuzungumza na Mark, kila siku simu zilikuwa zikipigwa na majina makubwa makubwa kutoka kwenye kampuni ya Plaxo wakitaka Sean amweke Mark kwenye simu, wamekuwa hata wakimvizia sehemu mbalimbali ili waonane nae angalau hata wapate muda wa kufanya nae mkutano, kila siku walitamka offer za mamillion ya pessa wakitaka share facebook.
Kamwe Sean Parker asingeruhusu kitu kama hicho kitokee hata kama wangekuja na pesa kiasi gani asingewapa nafasi kwani makampuni mengi sana yaliitaka facebook, kila mmoja alitaka kipande cha facebook na kila mmoja alitaka kuwa facebook.
Hatimae Sean alikubali kupanga mkutano kati ya Plaxo na Mark, alimwambia Mark kamwe asikubali chochote kile watakachomwambia ila awasikilize tu na kuwachora mpaka kikao kitakapoisha

Sean alishuka ndani ya gari nje ya office ya Plaxo, zilikuwa ni dakika ishirini nyuma kwa muda ambao kikao kilitakiwa kuanza
Alimtazama Mark ambae alikuwa akishuka ndani ya gari lake
"Yesu mpendwa" Sean alijisemea kisha akatoa kicheko. Mark alikuwa amevaa pajama nyepesi, laptop kwapani kwake, nywele zake zikiwa kama za kichaa na huku akionekana kuwa serious

"Unauhakika na hiki" Mark aliuliza
Sean alicheka kwa sauti zaidi. Ndio alikuwa na uhakika wa hicho kuliko vitu vingine ambavyo amewahi kuvifanya
" Asilimia mia" Sean alijibu na kisha kutazama saa yake

Sio kwamba tu Mark alikuwa amechelewa dakika ishirini kwenye kikao na kampuni kubwa silicon Valley ila alikuwa anaingia kwenye kikao kama kituko flani wa mtaani, kitu ambacho ndo kilimchekesha sana Sean. Sean alikuwa haingii kwenye mkutano na Mark,na Mark alisema kuwa atakuwa sawa, kwanza angeomba msamaha kwa kusema kuwa alipitiwa na usingizi na hivyo hakupata hata muda wa kuvaa na kisha mkutano ungeendelea kama kawaida

"Mkutano utakuwa mzuri" Sean alimwambia Mark maneno ya mwisho ya kumfariji na kuitazama tena pajama yake na kucheka kwa sauti

***

June 2005
Siku ya mahafali ilifika, siku ya Eduardo kuhitimu chuo, Eduardo akiwa ndani ya joho na kofia na kuketi katikati ya wahitimu wengine akiangalia sherehe za mahafali zilivyokuwa zikienda katika eneo ambalo lilikuwa limejaa watu na wageni mbalimbali wakiwemo ndugu zake ambao hakujua ni sehemu ipi hasa walikuwa

Tangu Eduardo arudi kutoka California, tangu wakati ambao kwa sasa anauita kama wakati wa usaliti wa Mark, amekuwa akitumia muda wake mwingi chumbani akifikiria, akitafakari na kupanga maisha yake ya mbele

Chuo kilikuwa kimeisha sasa na alikuwa anaondoka chuoni hapo ambapo hakujua ni wapi hasa ataelekea ila alijua kuwa hakuwa mtoto tena na hakujihisi kama mtoto tena
Kitu kimoja tayari alikuwa ameanza, harakati za kisheria, za kwenda kwa kile alichoona kuwa kilikuwa ni chakwake. Aliajiri wanasheria, alituma barua, aliweka wazi lengo lake kwa Mark na team ya Facebook kwamba alidhamiria kuwafikisha mahakamani, hakupenda wazo la mahakama, la kwenda dhidi ya rafiki yake mbele ya jaji au jopo la sheria lakini alijua hakukuwa na njia nyingine na haikuwa kati yake na Mark tena

Edurdo alistaajabu kama Mark alikuwa na majuto yoyote yale kwa jinsi mambo yalivyogeuka kuwa.
Huenda hapana, Mark huenda hakutambua kama amefanya kosa lolote lile
Katika mtazamo wa Mark, amefanya kile ambacho ameona kilikuwa ni muhimu kwa biashara.
Facebook ilikuwa ni wazo lake la tangu mwanzo, yeye ndie aliepoteza muda wake kutengeneza, alitumia nguvu zake kuitengeneza, aliitengeneza akiwa kwenye chumba cha bwenini kwake, aliandika code, aliiachia web site, ameenda California, ameahirisha masomo yake, ametafuta msaada wa pesa. kwake yeye imekuwa ni Mark Zuckerberg production kuanzia siku ya kwanza, na mwingine yeyote alikuwa ni kama anajaribu kuning'inia tu, Winklevoss twins, Eduardo, labda hata Sean Parker

Kiuhalisia katika mtazamo wa Mark, ilikuwa, huenda Eduardo ndie aliye enda kinyume, ndie ambae ameusaliti urafiki wao. Katika mtazamo wa Mark- Eduardo alijaribu kuiumiza kampuni kwa kufunga akaunti ya bank, Eduardo alijaribu kuweka ugumu katika kupata pesa ya mtaji akijisisitizia nafasi yake kama cheo cha ukuu wa biashara, Eduardo amefanya vitu vingine ambavyo vingeweza kuihatarisha facebook, kama vile, kuanzisha website yake tofauti, joboozle, na kisha kwenda kwa watangazaji walewale ambapo Mark aliona kuwa ilitakiwa kuwa kama siri za biashara za facebook. Mark alikuwa na sababu ya kujiona kuwa amekosewa kama ambavyo Eduardo aliona kuwa amekosewa
Eduardo hakuona namna hiyo, aliamini kabisa na vilivyo kuwa amekuwepo tokea mwanzoni, aliamini kuwa amekuwa msingi wa mafanikio ya facebook, aliweka fedha za kuanzia, aliweka muda wake na alistahili ambacho walikuwa wamekubaliana mwanzoni
Ambapo aliwahi kukubaliana na Mark kuwa haikuwa kuhusu urafiki tena bali ilikuwa ni biashara tena biashara halisi

Hivyo atafuata ambacho aliamini alistahili, atampeleka Mark mahakamani ili akajielezee, ili akafanye ambacho kilikuwa ni sahihi

Alistaajabu hata kama Mark allikumbuka ni wapi walikotoka, kila kitu kilianza vipi, jinsi walivyokuwa wakijaribu kufanya kitu special ili angalau watambulike. Alistaajabu kama Mark alitambua kwa kiasi gani vitu vilibadilika
Au labda Mark hakuwahi kubadilika kamwe hata kidogo, labda alimsoma vibaya tangu mwanzo kama ilivyokuwa kwa Winklevoss twins
Eduardo alichora mawazo yake hewani.

Labda kamwe hakuwahi kumfahamu Mark Zuckerberg
Alistaajabu kama hata Mark Zuckerberg mwenyewe alijifahamu kwa kina.
Na Sean Parker? Sean Parker pia huenda alifikiri alimfahamu Mark Zuckerberg
Eduardo alikuwa na uhakika vilevile kuwa haitachukua muda kwa Sean Parker kuwa na Mark
Akilini mwa Eduardo aliona kuwa Sean alikuwa kam mtu anaebadilisha hali ya hewa tu, tayari alikuwa ameondolewa kwenye makampuni mawili, swali halikuwa kama pia ataondolewa facebook bali swali lilikuwa ni lini ataondolewa?

***

Baada ya miezi mitatu
Sean Parker alikuwa ndani ya party. Party iliyojazwa na watoto wa chuo ambayo ilikuwa ikienda vizuri na kila mtu alikuwa akifurahia

Mara mlango ulisukumwa na kelele zikaskika, hakuna alieskia king'ora cha tahadhari wala nini. Police walimiminika ndani mle bila watu kujua wamefikaje
Wazo la kwanza alilowaza Sean Parker ni kuwa huenda kulikuwa na mtu amefanya kosa kwani mle ndani kulikuwa na party pekee, party ambayo alienda na msichana mmoja mwajiriwa wa facebook, wakifurahia wenyewe kama kawaida ya ambavyo party zingine huwa, lakini sasa sijui ni kitu gani kimetokea katika party hii
Labda kulikuwa na pombe mle ndani au labda mziki kuwa wa sauti ya juu au labda kulikuwa na watu wanavuta unga, Sean Parker hakujua sababu ni nini hasa kwani tangu aingie ndani mle muda mwingi ameutumia kuwa sehemu moja na zaidi mfukoni mwake akiwa na inhalera kwa ajili ya asthma yake

Police walioneka kuwa serious bila kujali mazingira au kama ile ilikuwa ni party maeneo ya chuo.
Kama ilivyokuwa Sean Parker kuwa sehemu isiyo sahihi muda usio sahihi, lakini huenda hiii haikuwa bahati mbaya, labda haikuwa kutokuwa muda usio sahihi mahala pasipo sahihi, huenda haikuwa ni party tu ila huenda ilikuwa ni target tena kwa mara nyingine

Sean allijua kuwa Facebook haikuwa kampuni rafu tena, haikuwa kampuni ya bwenini tena bali ilikuwa ni kampuni iliyobadilika, iliyoendelea na kila siku ikizidi kukua na kuingiza pesa na kuelekea kuwa ya mabillion na huenda kuweza kupanua mipaka yake mpaka kwa watu wa kawaida na huenda kwenda mpaka kimataifa na hivyo Facebook kuweza kuwa zaidi ya kampuni kubwa duniani
Sean Parker alijua vyema jinsi ambavyo huwa vitu vikishakuwa vikubwa, Watu hubadilika na kuanza kuwa tofauti, urafiki hufa, matatizo hunyanyuka bila kujua ni wapi hasa yametokea
Na labda Facebook inavyozidi kuwa kubwa, na kadri pesa zinavyozidi kumiminika na wawekezaji kuanza kufiiria pesa katika mabillion huenda kuna watu waliohisi kuwa hakuna uhitaji wa Sean Parker tena
Imeshatokea hapo nyuma, mara mbili. Inaweza kuwa inatokea tena?
Au labda ni hofu yake tu lakini hali ni halisi kama inavyoonekana kuwa party imeharibika na yeye akiwa katikati yake, na kuwa ni kweli ilikuwa ni bahati mbaya na muda mbaya yeye kuwepo pale?

Sean Parker alipokamatwa kitu cha kwanza aliwaza kupiga simu, haijalishi alikuwa na hatia au hana lakini haikuwa picha nzuri kwa raisi wa kampuni iliyobadilika na kusonga mbele kuwa ya mabillion, kukamatwa tena akiwa na mfanyakazi wa kampuni,kwenye party
Hakuwaza kama ataishia jela lakini alikuwa na uhakika kuwa lazima Mark Zuckerberg angekereka na kitendo hicho hata kama alikuwa na hatia au hakuwa na hatia


***

Mark alikuwa kwenye office za Facebook muda aliopokea simu, huenda simu ilitoka kwa Sean mwenyewe au ilitoka kwa mwanasheria na hakujua ilikuwa ni saa ngapi hasa muda huo, huenda ulikuwa ni usiku wa manane au palikuwa pamekaribia kukucha,muda haukuwahi kuwa concept nzuri kwake, habari alizozipokea zilikuwa za muhimu sana kwake na ni habari ambazo zilitakiwa kushughulikiwa haraka na kwa ufanisi mkubwa

Sean Parker alikuwa ni genius na alikuwa ni nyenzo katika kuifikisha Facebook mahali ilipokuwa kwa wakati huo. Sean Parker alikuwa ni mmoja kati ya mashujaa wa Mark, na siku zote atabaki kuwa ni mkufunzi, mshauri na labda hata rafiki. Lakini kwa habari alizoziskia juu ya kilichotokea kwenye party, Sean Parker anatakiwa kuondoka.

Kwa sababu yoyote ile, ingawa Sean hataenda kupatikana na hatia kwa chochote alichokifanya, lakini katika macho ya watu, kwa hali ile, Sean Parker atakuwa hatari kwa Facebook, hata kama ilikuwa ni bahati mbaya au sio lakini matokeo yaliyotokea yalikuwa ni dhahiri

Sean Parker anatakiwa kuondoka

Kama ilivyokuwa kwa Eduardo, kwa Winklevoss twins, kitu chochote kinachokuwa shinikizo, haijalishi lengo ni lipi, kinatakiwa kushughulikiwa kwa sababu mwisho wa siku kitu kilichokuwa cha muhimu ni Facebook. Facebook ilikuwa ni kama mtoto kwa Mark na facebook ilikuwa ndio sehemu ambayo Mark aliweka maisha yake

na hivyo Mark hataacha kitu chochote kile au yeyote yule aweze kusimama katika njia ya Facebook

Mark alibaki na kampuni, aliona ni kama utani lakini ni zaidi ya utani, kwa jinsi alivyokuwa akichukulia mambo kwa namna ya kufurahisha, alitengeneza business card ambayo angekuwa akitemba nayo kila sehemu, juu ya Card aliandika maneno ambayo alikuwa akijitania mwenyewe kwa namna ya kufurahisha pengine hakuwahi kufikiria kama atakuja kuwa na kampuni ambayo anaimiliki yeye mwenyewe, aliandika maneno yaliyosomeka

"I'm CEO, Bitch"

Screenshot (139).png


***

Eduardo hakuwa na uhakika ni club gani alikuwa lakini alichojua ni kuwa alikuwa New York. Alikuwa peke yake akiwa amekunywa japo hakuwa amelewa sana, vitu mbalimbali vilikuwa vimechanganyika kichwani kwake na kuwa kama haoni vizuri vile.
Alikuwa amechoshwa na shughuli zake za kila siku ikiwemo maswala yake ya mashtaka na huku maisha yake akiyagawa mara Boston (ambapo alikuwa akienda kwa ajili ya kutembea kwenye club yake ya the phoenix), mara New York na wakati mwingine California na kuwa alikuwa na wiki kadhaa bila kupata usingizi vizuri

Akiwa kwenye dance floor, alitupia macho yake huku na kule,mara alimtambua mtu ambae alikuwa amesimama pembeni ya club akitazama uelekeo wake
Eduardo alimtambua alikuwa ni nani, aliwahi kumwona mara nyingi sana chuoni akiwa na kaka'ke, pacha wake, Eduardo hakuwa na uhakika huyo anaemtazama muda huo ni pacha yupi, ye alichojua tu ni mmoja kati ya mapacha wa Winklevoss ndie ambae alikuwa mbele yake kwa wakati huo ikiwa ni hatua chache kutoka mahali alipokuwa ndani ya club ile

Eduardo alitembea mpaka kwake na kumshika mkono pacha yule ambae alimkodolea macho ya kumshangaa, Eduardo aliruhusu maneno kutoka mdomoni mwake

"Samahani, amenitenda kama alivyowatenda ninyi"

Bila kuongeza neno jingine lolote aligeuka na kutowekea kwenye dance floor.

MWISHO.

WAKO WAPI KWA SASA

SEAN PARKER: Baada ya Sean Parker kuondoka facebook, Mwaka 2006 Sean Parker alikuwa msimamizi msaidizi wa 'Founders Fund' mfuko wa uwekezaji ulioanzishwa na Peter Thiel ukiwa umejikita San Fransisco ukiwa umelenga kuwekeza kwenye makumpuni yanayoanza ya teknolojia.
Mwaka 2014 aliachia ngazi ili aweze kujikita zaidi kwenye project zake zingine
Mwaka 2015 alitangaza mchango wa dollar million 600 kuanzisha 'Parker foundation' ambayo itakuwa ikishughulika na maeneo matatu-Science, Afya ya umma kwa dunia nzima na shughuli za kuleta maendeleo katika jamii.
tangu 2005 Sean Parker amekuwa ni surpoter mzuri wa harakati mbalimbali za kupambana na cancer na hata kuchangia pesa ili kuweza kusaidia research mbalimbali zinazohusu cancer. Amekuwa akitoa michango pia katika vyama vyote vya siasa Marekani
(Ana mke na watoto wawili)

TYLER NA CAMERON WINKLEVOSS: Tangu mwaka 2004 walifuatilia mashtaka yao dhidi ya Mark Zuckerberg na hatimae mwaka 2008 maamuzi yaliweza kupatikana,maamuzi ambayo yalitakiwa kuwa siri kama ilivyoamrishwa na judge lakini kampuni ya sheria iliyokuwa ikiwasimamia ilivujisha siri na kujulikana kuwa maamuzi yaliyoamriwa ni kulipwa dollar million 65 ambapo Tyler na Cameron hawakuridhika nayo na kuamua kukata rufaa lakini mwaka 2011 waliamua kuitupilia mbali kesi hiyo.
Mwaka 2008 walifanikiwa kuingia katika mashindano ya olympic yaliyofanyika Beijing nchini China na kuweza kumaliza mashindano katika nafasi ya sita

EDUARDO SAVERIN: Alifuatilia mashtaka yake dhidi ya facebook na mwaka 2008 jina lake liliweza kurudishwa facebook na kutambuliwa kama mmoja kati ya waanzilish wa facebook na hivyo uwepo wake ukawekwa kwenye historia ya kampuni na kuwa wazi kuwa mahakama ndio iliyoamua ili kuweza kumpatia credit kwa kazi yake katika uanzilishi wa facebook, pia kulikuwa na maamuzi mengine mbayo hakuruhusiwa kuyasema na huku ikijulikana kuwa alipewa asilimia 5 ya umiliki wa facebook.
Eduardo aliishi nchini Singapore kuanzia mwaka 2009 na mwaka 2011 alitangaza kuwa yeye si raia wa marekani tena kutokana na kwamba alivutiwa kufanya kazi na kuishi nchini Singapore.(Alikuwa raia wa Marekani toka mwaka 1998 akitokea nchini Brazil)

MARK ZUCKERBERG: Mmiliki halali wa facebook. Tajiri namba tano duniani akiwa na utajiri wa dollar billion 56. Katika topten ya watu tajiri duniani Mark ndie billionare mdogo zaidi duniani akiwa na miaka chini ya 35
Alimwoa mchumba wake Priscilla Chan ambae walikutana Harvard mwaka 2003.

THE SOCIAL NETWORK
Movie inayomwelezea Mark na uanzishaji wa facebook, ilitoka october mwaka 2010

Mark Zuckerberg- alipoelezwa kuhusu movie hiyo alisema kuwa " Nilitamani mtu yeyote asitengeneze movie kunihusu mimi wakati bado nipo hai". Lakini alitoa support yake katika kufanikisha movie hiyo ambayo nafasi yake iliweza kuwakilishwa na mwigizaji Jesse Einsenberg
David Kirkpatrick mhariri na mwandishi wa kitabu cha Facebook:the inside story of the company that connect the world alisema kuwa "Filamu inaukweli asilimia 40 tu.......matukio mengi yako sahihi lakini matukio mengi yamebadilishwa na kupindishwa, hata impression yake yote sio sahihi kabisa"

Sean Parker- aliiwakilishwa kwenye filamu na Justin Timberlake, japo alimsifia director wa movie lakini zaidi alichokaririwa akikisema Parker ni kuhusu yeye kuwa tofauti na uhusika uliowakilishwa kwenye filamu hiyo huku akilalamika kwa tabia isiyopendeza ambayo iliwakilishwa katika filamu hiyo
Parker pia aliikosoa filamu katika sehemu ya Eduardo Saverin kutoka facebook akisema kuwa ilikuwa sivyo bali ni kinyume cha jinsi yeye alivyotoka plaxo
 

Attachments

  • The Social Network Official Trailer -In theatres Oct 1 2010.mp4
    17.4 MB · Views: 72
Story yetu ndo imefikia mwisho hapo

Shukrani kwa kuisupport, kwa aliesoma na kuandika comment ya maana, tupo pamoja, wote japo sijaweza mtag mtu kutokana na nilivyokuwa nikiandika lakini naimani story itaweza kuonekana
Nilipoisoma story hii niliipenda hivyo nikatamani kushare na wana JF nikijua kuwa wapo watakao kuwa wakiifahamu lakini sio wote watakuwa wakiifahamu.
Ndio, kiasi flani inapoteza muda katika kuandika na kwa kuzingatia kuwa original story inampangilio wa ajabu kidogo hivyo katika lugha yetu nilijaribu ili angalau hata kidogo iweze kuleta maana huku nikijaribu kuacha baadhi ya vitu na vitu vya muhimu vyote nikijaribu kuviweka, lakini Yeah, hii yote ni kwa sababu napenda mambo ya uandishi na ndo maana nikaamua kujitolea kuandika story hii.

Shukran.
 
Aisee nimeifatilia mwanzo mwisho
Inavutia sana
Nimejifunza nguvu ya wazo
Wazo ni kitu chenye nguvu sana,ni muhimu kuchukua hati miliki ya wazo lako
Shukran mkuu
 
Back
Top Bottom