THE ACCIDENTAL BILLIONAIRES- The founding of facebook: a tale of money,genius and betrayal

Screenshot (126).png
Screenshot (100).png


Tyler na Cameron walikuwa wameketi wakisubiri kuonana na Raisi wa chuo, Tyler alikuwa amechoka na kupuuzwa kwani alikuwa ameshafika sehemu mbali mbali za uongozi mpaka kenye board ya chuo ambayo ilisema kuwa kesi hiyo ipo juu ya uwezo wao, Mark mwenyewe alikuwa amepuuzia amri yao waliyomtaka kuwa afunge website ile, ila badala yake Mark aliwajibu barua waliyokuwa wamemwandikia, alijibu majibu ambayo Tyler aliona kuwa ni pumba kwani Mark alisema kuwa alianza kutengeneza thefacebook baada ya kuonana na wao mara ya mwisho tarehe 15 january wakati Tyler akizingatia ukweli kuwa the facebook ilisajiliwa tar 13 january, walijaribu kutaka kuonana na Mark lakini Mark hakutaka kuonana nao

Hatimaye waliingia Ofisni kwa Raisi ambae tayari alikuwa na barua ya malalamiko yao na maelezo yote kuhusu kile kilichotokea
Raisi aliwauliza ni kwa nini wako pale, Tyler alimsontea barua ile ambayo kichwa cha habari killikuwa kinajieleza, Raisi aliisoma barua ile
"Nafikiri inajieleza yenyewe kuwa Mark aliiba idea yetu" aliongea Tyler
"Kwa hiyo mnataka mimi nifanye nini kuhusu hilo?" aliuliza Raisi
Tyler alimtazama Raisi kwa kustaajabu na kisha kumtazama kaka'ke, walibaki mdogo wazi kwa muda huku Tyler akihisi hasira inamwijia moyoni mwake kisha alisonta kitabu cha sheria za chuo kilichukuwapo ofisini pale
"Ni kinyume cha sheria za chuo kwa mwanafunzi kumwibia mwanafunzi mwenzake" Tyler alisema kisha akaquote baadhi ya maelezo ya kwenye kitabu kuwa 'Chuo kinategemea kuwa wanafunzi wote watakuwa waaminifu kwa wenzao: wanafunzi wote wanatakiwa kuheshimu mali za umma na mali za binafsi, hali yoyote ile ya wizi au uharibifu itachukuliwa kama ni utovu wa nidhamu na itasbabisha mwanafunzi kufukuzwa chuo'

Kisha Tyler aliongea kuwa " Kama mark angeingia bwenini kwetu na kuiba kompyuta mngemfukuza chuo lakini amefanya kitu kibaya zaaidi ya hicho, amechukua wazo letu na kazi yetu, Chuo kinatakiwa kiingilie na kufuata sheria zake za maaadili"

"Vizuri, nimesoma barua yenu ya malalamiko lakini sioni kama hili ni suala la chuo" Alijibu Raisi

"Lakini kuna sheria na kanuni za chuo" aliingilia Cameron na kuendelea kuwa "Kuna maadili ya heshima, kipi ni chema kama sheria haina meno yoyote yale"

"Mliingia katika sheria za maadili na chuo na sio na kila mmoja wenu, hili suala ni kati yenu nyie na Mark Zuckerberg"

Tyler alihisi anaelea juu ya siti, alihisi kama Raisi amewasaliti, chuo kimewasaliti, siku zote alijiona kama miongoni mwa jamii ya Harvard ila sasa aliona hakuna jamii
"Lakini sheria inawajibu wa kufuata kanuni za maadili" Aliongea Tyler
"Chuo hakipo kushughulikia suala kama hili. Hili ni kesi kati ya wanafunzi" Alijibu President
"Unashauri tufanye nini kuhusu hili suala" Tyler aliuliza
Raisi alinyanyua mabega kuashiria kuwa hajui kisha akasema " Kalitatueni suala hili na yeye mwenyewe au tafuteni njia nyingine ya kulishughulikia, kama suala halali"

Tyler alijua ni nini Raisi alimaanisha, kwamba wakaongee na Mark uso kwa uso wakati isingesaidia chochote kile akizingatia kuwa Mark alikuwa tayari kuwadanganya mbele ya macho yao. Au labda waende mahakamani ambapo ilionekana ni uchaguzi wa kuogofya kuuchukua
Ilikuwa inaleta msongo wa mawazo, Raisi wa chuo alikuwa anawaambia wajijue wenyewe, uongozi wa chuo ulikuwa umelinawia mikono suala hilo ambapo thefacebook ilikuwa maarufu chuoni na Mark alizidi kupata umaarufu, website ilikuwa inakuwa kila siku halafu Raisi anaonekana kabisa kupitisha mafanikio ya Mark
Tyler alijiuliza kuwa huenda Raisi aliamini alichokiandika Mark kuwa website ile ilikuwa tofauti na yao na hivyo hakukuwa na case dhidi ya Mark ila walikuwa na hasira kuwa hawakuwa wa kwanza kuachia website yao.

Waliondoka ofisini mle huku Tyler akiona kuwa kitu kilichobaki ni wao wenyewe kukabiliana na Mark.
Tyler alijua kuwa ataikumbuka siku hiyo kwani alihisi kuwa hiyo ndio ilikuwa siku yake ya mwisho ya kuwa mwaminifu
Iwe ni sahihi au sio sahihi Tyler aliona kuwa mtoto yule 'mpumbavu' alikuwa amewaibia wazo lao na kulifanya lake.


***

Mark na Eduardo walikuwa wameketi wakiangaza huku na kule, ilikuwa ni ndani ya hotel moja jijini New york ambapo walikuwa wameketi wakisubiri kuonana na mtu, Mark alikuwa amevaa aina ya masweta yake yale aliyozoea kuvaa pia alivaa aina ya sandel zake zile zile ambazo alizoea kuzivaa kila siku, hawakuwa pale kuonana na mwekezaji lakini Eduardo aliona bado lilikuwa ni suala la kibiashara hivyo angalau Mark angejaribu kuonekana fashionable kwani alivaa tofauti na mtu mwingine mle hotelini

Safari ile yote Mark alikuwepo kuwepo tu akiichukulia kama utani huku Eduardo alikuwa akiwajibika kwa kila kitu, gharama zote kuanzia usafiri, chakula na tax alilipa yeye huku sehemu ya kulala wakifikia kwa marafiki zao. Eduardo alizichukulia gharama zile kama ni gharama za kibiashara hivyo alitaka angalau Mark aichukulie serious safari ile.
Mark alikuwa hajafanya chochote kile lakini Eduardo kwa upande wake alikuwa amefanikiwa kuweka mikutano mingi na watangazaji wenye uwezo mkubwa japo hakuna mkutano uliokuwa umeenda vizuri,na huku katika mikutano yote, nusu ya mikutano Mark alisinzia na nusu mingine alikaa kimya bila kuzungumza chochote kile na Eduardo pekee akichukua jukumu lote la kuzungumza na kuelezea

Japo kila mtu waliekutana nae alionekana kupendezwa na facebook na idadi ya watumiaji wake bado hakukuwa na aliekuwa tayari kuweka order na kutoa pesa kwa ajili ya kutangaza kwani bado walikuwa hawana uhakika zaidi na hawakuelewa zaidi ni kwa jinsi gani facebook ilikuwa tofauti na mitandao mingine ambapo ukweli ulikuwa kwamba mtu aliekuwa akiingia facebook alikuwa akikaa muda mrefu zaidi kuliko mitandao mingine na bado tena angetamani kurudi mtandaoni mle. kama Mark angejribu kuwa serious kidogo huenda mambo yangeenda vyema kidogo.

Muda ulikuwa umeenda, mtu waliemsubiria alikuwa amechelewa, Sean Parker alichelewa kiasi kwani walikuwa wameagiza chakula na kumaliza kula bila kutokea. Eduardo hakujua mengi kumhusu Sean Parker lakini kile alichokikuta kwenye internent kwa kumsearch hakikumpendeza Eduardo, Eduardo aliona kuwa Sean Parker hakuwa mtu mzuri, mjasriamali aliyekwama katika makampuni mawili makubwa ya mtandao ilionekana kama ni kitu cha kukiangalia vizuri, Kwa Eduardo Sean Parker alionekana kama ni mtu jeuri na asiejali na labda hata ni hatari kidogo. Eduardo hakujua ni kwa nini Sean Parker alitaka kuzungumza nao au ni nini Parker alikitaka kutoka kwao ila Eduardo alikuwa na uhakika kuwa yeye hakutaka kitu chochote kutoka kwa Sean Parker

Eduardo akiwa anaangaza angaza alimwona Sean Parker akiingia hotelini mle, jinsi alivyoingia tu ilikuwa ni rahisi kumtambua, Sean Parker alionekana kumfahamu kila mtu hotelini mle, kwanza alikuwa akisalimiana na wakaribishaji huku akimkumbatia mhudumu kisha alisimama kwenye meza iliyo karibu na kusalimiana na mwanaume aliekuwa ameketi pale huku akichezea nywele za mtoto wa mwanaume huyo utafikiri alikuwa family friend na pia alisalimia watu njiani alipokuwa akielekea kwenye meza waliyokuwa wameketi. Eduardo alistaajabu 'huyu mtu ni wa aina gani?'

Sean Parker aliifikia meza yao na kutabasamu kidogo

"Sean Parker. Lazima utakuwa Eduardo na Kelly. Na ndio, Mark" (Kelly alikuwa ni girlfriend wa Eduardo, sikutaka kugusia upande huo mwingine)

Sean alienda kuketi pembeni ya Mark, Eduardo alimwona Mark akifurahi kumwona Sean Parker, ilikuwa ni kama kumwabudu muungu aliempenda, katika macho ya Eduardo aliona kuwa kwa Mark Sean Parker alikuwa ni muungu.
Sean Parker aliwaagizia vinywaji kisha akaanza kuwapa story moja baada ya nyingine, kuhusu nguvu za ajabu alizokuwa nazo, kuhusu Napster na mapambano aliyopigana, kuhusu Plaxto na vita ambayo alifanikiwa kidogo,Sean alikuwa muwazi karibia kwa kila kitu, alielezea maisha ya Sillicon Valley (jina mbadala la sehemu ya kusini mwa San Fransisco Bay katika sehemu ya kaskazini mwa jimbo la California, jina likiwa limeitwa kutokana na sehemu ile kuwa na idadi kubwa ya wavumbuzi, wazalishaji na kuwepo kwa makampuni makubwa ya technolojia)
Sean Parker alielezea pia maisha yake ya kupart Stanford na Los Angeles, alielezea marafiki zake waliokuwa mabillionaire na marafiki zake ambao bado walikuwa wanapigana kuwa mabillionaire, Eduardo aliweza kuona Mark akiviingiza vitu vyote vile kichwani,
Baada ya Sean kumaliza story zake aliwauliza ni maendeleo gani ambayo tayari wamefikia katika thefacebook.
Eduardo alianza kuelezea kuwa tayari walikuwa wamefikia shule ishirini na tisa, kabla hajamaliza, Sean alimgeukia Mark na kumuuliza ni mipango gani ambayo walikuwa wakiitumia kuwezesha shule zingine kujiunga
Eduardo aliketi pale akiwa amekereka kipindi Mark akielezea mbinu walizozitumia kuzifikia shule mbalimbali huku akitoa mfano wa jinsi ambavyo uongozi wa chuo cha Texan kilivyokataa kuipokea the facebook wakisema kuwa wao wana social network yao, Walichofanya kina Mark ilikuwa ni kuipeleka thefacebook kwenye shule zote jirani na chuo hicho na baada ya wanafunzi wa chuo hicho kuona marafiki zao wapo facebook waliuomba uongozi wa chuo uwaletee thefacebook hivyo thefacebook ikaingia chuo hicho

Sean alifurahishwa na story ile na kuquote sehemu ya habari aliyoisoma kwenye gazeti la Havard kuwa 'wanafunzi wamekuwa watoro wa darasani, kazi zimekuwa hazifanyiki, kinachofanyika ni wanafunzi kushinda mbele ya kompyuta zao wakitumia thefacebook.com ambayo imewafanya wawe kama vichaa'
Mark alionekana kufurahi na kutoamini kwamba Sean amekuwa akisoma habari zake, Sean kwa upande wake alionekana kufurahi kuona kuwa Mark ni shabiki yake, pale pale kulionekana kuwa na muunganiko wa hao wawili na Eduardo aliona kuwa huenda Sean hakumpuuza maksudi ila alijikita zaidi kwa Mark kwa kuwa wote walikuwa ni watu wa kompyuta

Muda ulienda, Sean aliondoka akimwahidi Mark kuwa watawasiliana na kuweza kuonana tena.

Baada ya Mark na Eduardo kuondoka pale hotelini Eduardo alimwambia Mark kuwa Sean sio mjasiriamali mzuri hivyo hawamuhitaji, Mark alinyanyua mabega bila kujibu chochote, Eduardo alikunja sura kuashiria kuwa maneno yake yalikuwa yanaingia sikioni mwa kiziwi kwani tayari Mark alikuwa amempenda Parker
Eduardo aliona kuwa haikujalisha, sio kwa wakati huo, haikuwa kwamba Parker ataenda kuwapa pesa kwani alikuwa hana pesa za kuwapa na thefacebook ilihitaji pesa kutokana na kuwa ilikuwa inakuwa kila siku na kuhitaji servers zaidi na ilikuwa imefikia hatua sasa walihitaji watu wengine wa kufanya kazi kwenye upande wa programming hivyo walihitaji interns ambao ni lazima wangewalipa kitu

Eduardo alipanga kuwa wakafungue account ya kampuni bank na kuweka fedha za kutumika na kampuni, na kwa kuwa Mark alikuwa hana pesa zozote zile ilibidi kutegemea fedha za Eduardo ambazo ndo zimekuwa zikitumika toka mwanzo

Sean Parker
Screenshot (97).png


***

Eduardo alikuwa ameketi kwenye moja ya general lectures, aliangaza macho na kumwona mwanaume aliekuwa amevaa suti na briefcase mkononi, alikuwa ni moja kati ya capital investors 'jesus christ' alijisemea Eduardo, kwani walikuwa wakimvizia Mark mpaka darasani, hakua wa kwanza kufanya vile kulikuwa na baadhi wakiwemo wawakilishi wa makampuni mbalimbali ya software na internent walikuwa wakimfuata Mark chuoni pale, kuna kipindi walimfuata Mark na Eduardo wakiwa dinning, kuna siku wakiwa library na kuna mwingine aliwahi mpaka kwenda bwenini kwa Mark, wawekezaji wengi walionekana kuvutiwa lakini tatizo walikuwa hawatoi fedha halisi au offer halisi, hivyo wote Eduardo na Mark hawakuwachukulia serious

Thefacebook ilikuwa inakuwa, ilikuwa na zaidi ya watu laki moja sasa, Eduardo alikuwa amefanya maendeleo kidogo na ya kutafuta watangazaji wa biashara, alienda pote kitaifa na maeneo ya karibu na chuo na baadhi ya makumpuni jirani yalikuwa yameanza kutangaza katika website ile japo fedha hazikuwa nyingi za kutosha kumudu gharama za kuiendesha kampuni ambayo uhitaji wa server ulikuwa unaongezeka kila kukicha
Kila mtu aliweka jitihada, hata Dustin na Chris walifanya kazi kwa bidii na thefacebook kuanza kuonekana kama ni kazi ya fulltime kiasi kwamba ilikuwa ngumu kubalance muda wa kuwa darasani na wakati huo huo thefacebook, lakini sasa chuo kilikuwa kinaelekea kufungwa hivyo wangepata muda mzuri wa kuwa na thefacebook
Mark pia alikuwa amefanya baadhi ya maamuzi muhimu kwenye kampuni, yeye na Eduardo waliamua rasmi kuisajili kampuni kisheria na kuwa na documents zote zinazohitajika kuwa nazo kama kampuni, kuwa na zile document kulifanya kampuni kuonekana kama halisi japo bado ilikuwa haijaanza kutengeneza faida yoyote ile

Pamoja na hayo yote, maamuzi ya nini cha kufanya chuo kitakapofungwa yalikuwa magumu, wote Mark na Eduardo walikuwa wametafuta kazi za kufanya kipindi cha likizo, Mark hakuweza kupata lakini Eduardo alikuwa amepata internship katika bank moja jijini New York japo haikuleta mantiki kwenda kufanya internship na wakati huo huo kufanya kazi na thefacebook. Kabla hajapeleka wazo hilo kwa Mark, Mark yeye aliamua kujitaftia cha kufanya, japo pia thefacebook ilikuwa ni chaguo lake lakini kwanza aliamua kuandaa project iliyoitwa Wirehog, program ya kushare files mbalimbali kama nyimbo video na picha ikiwa kama free software ambayo ingewza kupakuliwa na mtumiaji ambapo Mark alipanga baadae angeiunganisha na thefacebook, project ile alifanya yeye na rafiki zake akiwemo Andrew McCollum ambae alikuwa ni classmate wake, haikuwa kazi nyepesi kuifanya lakini Mark alikuwa tayari kuifanya na hivyo kugawa muda wake wa kufanya project hiyo na huku akifanya thefacebook ambapo kitendo kile kilimrahisishia Eduardo pia katika uamzi wake wa kuchukua internship huku akiifanyia kazi thefacebook.

Mark alikuwa amewaelezea wenzake kwamba amekuja na uamuzi kuwa kwa muda wa miezi hiyo ya likizo California ndo sehemu ambayo alitaka kuwa, alitaka kufanya kazi kwenye project yake ya Wirehog pamoja na kufanya kazi thefacebook akiwa Silicon Valley sehemu yenye historia kwa kompyuta programmers kama yeye na pakiwa ni ardhi ya mashujaa wake wote, Mark alitaka kwenda kule yeye na rafiki zake akiwemo Dustin na Andrew ambae bahati nzuri alikuwa amepata kazi maene yaleyale, tayari Mark na rafiki zake walikuwa wamepata eneo la kupanga, walipata nyumba ya kupanga ambayo ilikuwa karibu na maeneo ya chuo cha Stanford, ilikuwa ni nyumba ambayo wangeweza kuunganisha vitu vyao vyote walivyokuwa wakitaka kufanya

Eduardo hakuingiwa akilini na suala hilo aliloamua Mark, hakupenda kabisa kwani licha ya kuona kwamba New York ilikuwa mbali na California,pia aliona kuwa Silicon Valley lilikuwa ni eneo hatari na lenye ushawishi, aliona kuwa kipindi atakapokuwa New York, watu,wawekezaji kama jamaa waliomvizia chuo watakuwa wakimvizia, na kibaya zaidi aliona watu wabaya zaidi wa aina ya Sean Parker pia wangeweza kumvizia, katika kampuni Mark na Dustin walikuwa ni programmers na Eduardo alikuwa ni mtu wa biashara, sasa kama watagawanyika Eduardo angewezaje kuwaongoza kibiashara kama walivyokubaliana?
Mark alisema hakukuwa na muda wa kujadili suala hilo kwani hakukuwa na sababu ya kufanya wasiweze kufanya kazi kwenye majiji mawili kwa wakati mmoja, Yeye na Dustin wataendelea kuwa programmers huku yeye Eduardo akiendelee kutafuta advertisers na kushughulikia masuala ya fedha, kwa kuwa ameshaamua na Eduardo tayari anaenda kwenye internship hivyo watatafuta namna ya kufanya kazi wakiwa mbalimbali
Eduardo hakupenda wazo hilo lakini aliona ni baadhi ya miezi michache tu kisha wangerudi chuoni na kuendelea kufanya kazi pamoja.

Mle darasani Eduardo alimwambia Mark kuwa waende wakazungumze na jamaa yule mwenye suti waliemwona, Mark alimwambia Eduardo kuwa aende yeye kwani yeye alikuwa anaenda kuwafanyia interns interview
Eduardo alikumbuka kuwa walihitaji interns wengine wawili ambao watasaidia katika programming na ambapo itahitajika kuwalipwa mshahara hivyo pesa itahitajika
Siku chache Eduardo alikuwa amezungumza kuhusu suala la kufungua akaunti ya kampuni hivyo alienda akafungua akaunti kwenye bank of America na kuweza kuweka pesa ambazo zitaendesha kampuni na pesa za kusaidia kipindi cha kuendesha shughuli huko California ikiwemo mshahara wa kuwalipa interns, alimpatia Mark cheque ambayo angeweza kuitumia kufanya transactions zote za kifedha za kampuni kwa account aliyoifungua.

Mark na Dustin waliweza kuinterview interns kwa kuwashindanisha kuhack codes ambazo walizitengeneza wao, walikuwa programmers watano na waliohitajika ni wawili hivyo ambao wangekuwa wa mwanzo kumaliza ndio wangepata nafasi hiyo ya internship
darasa lilikuwa limejaa likishangilia kipindi programmers wakishindana kuandika codes kwa nguvu zote huku Mark akiwa amesimama pembeni yao, programmers walikuwa na hamasa na shauku ya kwenda na Mark California, na sio tu California, walikuwa tayari kumfuata popote pale kwani walimwona kama muungu wao
Hatimae wawili waliweza kuwahi na kumaliza kwa pamoja na kuweza kushangiliwa kwa makelele na mziki ukiachiwa kwa sauti kubwa, Mark aliwatangaza kuwa ndio washindi na kuwakaribisha kwenye thefacebook.


***

Hatimae Tyler, Cameron na Divya waliamua kuachia website yao baada ya kuifanyia kazi na kuwa ilikuwa ni karibia miaka miwili sasa tangu mara ya kwanza walipoanza kuitengeneza website hiyo ambapo sasa waliamua kuibadili jina na kuiita 'ConnectU'
Wakati huo walikuwa wamejiandaa kwa ajili ya kuondoka kwani tayari chuo walikuwa ndo wamemaliza hivyo, waliamua kuachia website yao wakiwa na matumaini ya kupata watumiaji kutoka sehemu mbalimbali pengine labda kushindana na mitandao mingine
Tyler alijua kuwa walikuwa wanaanza na hasara kubwa kwani alijua concept ya biashara ni 'kuwa mtu wa kwanza' kama ambavyo Mark amewaonesha, Tyler aliwaza huenda leo ConnectU ndiyo ambayo ingekuwa inazungumziwa kila mahali
Ilikuwa inawachanganya akili kila siku kusikia watu wakiiongelea thefacebook, haikuwa sio tu chuoni pale bali karibia kila sehemu, kwenye TV taarifa ya habari ilikuwa ni karibia kila siku, kwenye magazeti pia ilikuwa ni karibia kila siku

Mark Zuckerberg. Mark Zuckerberg. Mark fucking Zuckerberg

Tyler haikumtoka kichwani

***
Sean Parker alikuwa amesimama kimya pembeni ya gari yake akimsubiri girlfriend wake, ulikuwa ni mtaa tulivu ambao ulikuwa sio rahisi kuwaona watu wakitembea.
Mara Sean Parker alisikia jina lake likiitwa nyuma yake, haikuwa kawaida, aligeuka na kutazama, aliona kundi la wavulana likija, hakuweza kuwatambua, lakini waliposogea karibu aliweza kumtambua mmoja wao kuwa ni Mark Zuckerberg, Sean Parker alioneka kustaajabu kama ambavyo Mark alistaajabu kwani ilikuwa ni coincidence ya ajabu kutokana na kuwa tangu Sean Parker aonane na Mark hotelini alijaribu kumtafuta tena na hata kumvizia sehemu mbalimbali lakini hakufanikiwa kumpata pamoja na kuwasiliana kwa email kuwa waonane hawakufanikiwa kuonana

Ilikuwa ni bahati kwa Sean Parker kwani muda huo alikuwa akimsubiri girfriend wake ambae amefunga chuo ili ampeleke nyumbani kwao ambako Sean angekaa nae kwa siku chache na baada ya hapo angeondoka na kutokuwa na sehemu maalumu ya kuishi.

Mark alifurahi kumwona Sean Parker,akilinganisha kuwa ameenda silicon valley ambapo aliona ni sehemu sahihi ya kujenga kampuni ya mtandao hivyo ni nini kingekuwa bora zaidi ya kumfanya kuwa mshauri wake mtu ambae amewahi kuwa na makampuni makubwa ya mtandao? Mark alimwuliza Sean kama ataweza kujihusisha na thefacebook iwapo atavutiwa nayo, Sean hakuweza kusita kwani ndio, alikuwa amevutiwa na thefacebook tangu siku aliyoiona na alitaka kujihusisha nayo tangu siku ya kwanza, ndio alikuwa tayari kuchagua kujihusisha nayo kwani pia angeenda kuishi na mtu alieitengeneza the facebook

Sean aliweza kuikagua nyumba ile ambayo Mark na wenzake walikuwa wamepanga, aliangalia kila kitu walivyokuwa wameset, kulikuwa na vitu mbalimbali walivyokuwa wameongeza ndani ya nyumba ile huku wakifunga nyaya mbalimbali, nyumba ilikuwa rafu kiasi flani kwani vitu mbali mbali vilizagaa chini yakiwemo maboksi tupu ya vyakula, chupa za beer, na vifaa mbalimbali vya kompyuta pia vilikuwa vimezagaa ndani mle huku chumba kikubwa kikionekana kama bweni na kompyuta lab ambapo masaa ishirini na nne lazima kulikuwa na mtu bize na kumpyuta mbali mbali au laptop mbali mbali zilizokuwamo ndani mle

Sean alifurahi kuona team ambayo Mark ameikusanya ikiwa na bidii ya kazi , yenye ushindani na yenye akili kuanzia Dustin, Andrew na interns, maadili ya kazi yalikuwa ni kufanya kazi usiku na mchana akiwemo Mark mwenyewe, walipokuwa hawajalala hawali au kuogelea kwenye swimming pool basi walikuwa kwenye kompyuta wakizidi kupanua zaidi wigo wa thefacebook pia huku wakiendelea na kutengeneza Wirehog, kiukweli lilikuwa ni kundi bora katika mwanzo wa kutengeneza kampuni ambalo Sean hajawahi kuona
Mtu pekee ambae Sean hakumwona alikuwa ni Eduardo, kidogo ilimchanganya kichwa, mtu ambae alijitambulisha kwa cheo cha mkuu wa biashara wa thefacebook na alikuwa amethibitisha mara nyingi kwamba yeye ndie anaendesha mambo yote ya kibiashara ya website ile, na Sean sasa aliona ni dhahiri kuwa Eduardo alikuwa hashughuliki na shughuli za kila siku za the facebook

Mark alimwambia Sean kuwa Eduardo alikuwa ameenda Newyork ambako alikuwa na internship bank. Hapo hapo kengele ya alarm ililia kichwani mwa Sean, kwa yeye kuwahi kuwa sehemu ya makampuni mawili na kushudia mafanikio na kushindwa alijua kuwa sehemu kubwa na ya muhimu sana katika kuanza basi ni nguvu na nia ya waanzilishi, kama mtu alikuwa anaenda kufanya kitu kama hiki, kukifanya halisi, kifanikiwe halisi basi ilitakiwa kuiishi na kuipumua project kila siku na kila dakika

Mark alikuwa aki iishi project, alikuwa na msukumo, alikuwa na uwezo alikuwa ni genius, alikuwa ameweka nguvu zake zote kwenye kampuni ile, Mark kuamka alfajiri kila siku na kuwa mbele ya kompyuta yake akifanya kazi, Sean aliona kuwa Mark alikuwa anaenda kutengeneza moja kati ya historia kubwa ya mafanikio pale Silicon Valley, lakini Eduardo yuko wapi? Au kwa uhalisia aliouona Eduardo alikuwa bado ni sehemu ya uhusika kweli?
Ndio Eduardo ameonekana kama mtu mwema, amekuwa pale tangu mwanzo, ameweka kiasi flani cha fedha kulingana na Mark alivyomsimulia, hata mpaka hapo walikuwa wakitumia fedha za Eduardo ambapo imempa uzito kama mwekezaji wa kwanza kwenye kampuni, lakini zaidi ya hapo?
Eduardo alijiona yeye kama mfanya biashara lakini hiyo inamaanisha nini? Pale Silicon Valley haikuwa kuhusu biashara, ilikuwa ni vita, ilitakiwa kuwa pale na kufanya vitu ili kufanikiwa, kufanya vitu ambavyo havifundishwi kwenye darasa lolote lile la biashara, Yeye mwenyewe Sean hakusoma chuo lakini aliweza kuanzisha kampuni, watu mbalimbali waliokuwa wamefanikiwa pale hawakusoma vyuo akiwemo Bill Gates lakini waliweza kufanikiwa kwa kuwa pale na kufanya vitu katika uhalisia

Sasa Eduardo yeye hakuwa pale, Sean aliona kuwa Eduardo alikuwa havutiwi kuwa pale hivyo Sean alimtoa mawazoni, Sean aliona yupo na Mark na yupo na team ya Mark hivyo yupo na thefacebook, kwa msaada wake aliamini kuwa wataingeneza kampuni ile kuwa ya mabillion ya dolla kama project ambayo ndo alikuwa akiitafuta, aliona kuwa bahati imemweka pale kwa mara ya tatu sasa, kwanza alitaka awaoneshe watoto wale ni nini maana ya kuwa sehemu ya uvumbuzi ule.


ITAENDELEA........

 
Binadamu hatuna shukrani kabisa, mtu anatumia muda wake kuandaa habari, anatumia resources zake mwenyewe kutuletea habari bure kabisa, lakini bado kuna watu wana guts za kumwita Pumbavu!

Jirekebishe mkuu.
Kabisa, ila mpumbavu anaonekana ni yupi
 
mkuu ntaisoma baadae,sema nini hii sehemu ya 3 ungeipachika kwenye ile thread ya kwanza
 
People are freaking out bila kujua, ila story nishaipost toka jana lakini status yake ni kwamba bado inasubiri moderation ili iweze kuwa displayed publicly, as you know mods are bussy that's why hata wanachelewa kuifanyia moderation

Mkuu with all due respect, this is one of the best piece of work I've read hapa JF.

Natamani iishe lakini pia sitamani iishe, I feel like nahitaji kukaa naisoma muda wote.

BIG UP MAN!
 
Back
Top Bottom