The 60 meter exclusion zone rule is outdated and impractical for our cities

Kama lugha ya yai inapanda, utamuelewa Ali Mfuruki, mimi nimemsoma huku nimetulia nimemuelewa sana. Kwanza ameunga mkono bomoa bomoa zote katika road reserve, open spaces, unplanned areas na risky buildings.

Amesema anatatizwa ule umbali wa mita 60 toka kwenye njia za maji, tangu DSM City Master Plan ya mwaka 1968-1979 haijatekelezwa, na Master plan mpya ya 2012-2032 ambayo mpaka sasa haijapitishwa na huu ni mwaka wa 6!, hakuna popote ufafanuzi hizi mita 60 ni kwenye njia zipi za maji?. Amesema kama sheria hiyo ingekuwepo, tusingekuwa na beach hotel hata moja!, amesisitiza anatatizo na tishio la kuwabomolea watu mahekali yao kule beach na kuuliza, kwa kuyabomoa, serikali inataka kupata nini?, ametolea mfano mji wa Amsterdam, usingekuwepo, akatolea mfano jiji la London na majijini mengine, mto unapita katikati ya mji na hakuna tatizo. Hoja yake ni waliojenga beach, wapewe jukumu la kujenga miundo mbunu rafiki ya kuhifadhi mazingira ya maeneo yao na kutolea mfano Kunduchi Beach, Bahari Beach na Africana hotels, au kitu kinachofanyika barabara ya Ocean Road.

Mimi sina nyumba beach area lakini naungana kabisa na logic ya Ali Mfuruki. unawabomea watu mahekalu yao ili uhifadhi nini, wakati hayo mahekalu yanaweza kuwepo na mazingira kulindwa!.

Paskali
Hiki ndicho anachokisema haswa and its totally true.. Ukisikia watu wanaendeleza water front wanagusa maji kabisa. Mbali na kuupamba mji pia unaongeza Kodi na thamani ya mji huku ikipunguza gharama za utunzaji zisizokuwa na tija ..

Mfano kuna mradi wa wacanada ulikuwa unaitwa Toronto water front areas.. Umefanyika kwa kuingia baharini kabisa .. Kuongeza mita za mraba zenye thamani katika mji wa Toronto ..

Mr Mafuruki hata kama anatetea Mali yake lakini anayepoteza zaidi kwenye zoezi la kuyabomoa majengo haya ghali karibu na mito au kando mwa bahari ni serikali.. Inaondoa chanzo cha mapato.

Sheria nyingi tu zinahitaji kuangaliwa upya.. Hasa kushindana na tatizo la miji kukua holela. Narudia kila siku tatizo hili ni tatizo la kiutamaduni. Mpaka tutakabadilika kwa kuinfluence utamaduni wetu ndio tutafanikiwa.

Kwann nasema ni tatizo la kitamaduni.. Vijijini ambako ndio chimbuko la sehemu kubwa na watu wanaokimbilia mjini hakuna uataratibu au utamaduni wa kujenga kwa kuheshimu sheria na kanuni..

Hawa wanakijini ...ndio tumekuja tukajaa mjini rural- urban migration.. Tunataka kujenga kila tunapoona kipande cha Ardhi.. Utakuta wakati mwingine msimamizi wa taasisi hizi hata wizarani naye anafanya haya maana sio utamaduni wake ila analazimika kuyahubiri sio kufanya... kwa sababu ya kazi.

Kuongezea kwa Ally Mafuruki.. Nasema pamoja na kuzibadili sheria hebu zifanyike jitihada zitafsiriwe kwenye mitaala ya elimu. Zisomwe mashuleni na watoto wakiwa wadogo (indoctrination).

Pili Vijijini wawekewe sheria za uendelezaji Wa makazi.. Ikiwa ni pamoja na kuwa na mipango na kuiheshimu. Iwe ni marufuku kujenga bila kuwa na mpango Wa uendelezaji tudefine specification hats za majengo yawe ya tope au sio.. Ila watu wajue mbali na kujisitiri wewe unayo kazi ya kusitiri sura ya kijiji na taiga kwa ujumla.

Hawa wanavijiji watakapofika wakati wa kuja mjini natumaini watafika wakiwa na mtazamo wa kimipango ..sio kwenda kujenga hovyo hovyo.. Watauliza mamlaka na watelekezwa. Hata kama Ardhi inakuwa ya kwao wao..bado watafuata sheria.

Note: mjini tupo weeeengi sana ambao tunazo tabia za kijijini bado.. Tumejenga kwenye squatters na hatuna mpango wowote wa kuyarasimisha maeneo yetu.. Tunapenda maviwanja makubwa yasiyokuwa na barabara ni aibu kwa mfumo mzima wa elimu yetu na ustaarabu wa taifa.

Kamu.
 
Back
Top Bottom