Thank you so much, Beatrice. Ulichokifanya ni zaidi ya Upendo. Nitakuheshimu Daima

puker

JF-Expert Member
Nov 22, 2018
940
1,847
Habar za muda huu wa JF.

Kwenye haya, maisha yapo mambo mengi unaweza kukutana nayo pengine ukajihisi wewe ni mwenye bahati na thamani ya pekee kuliko yoyote katika huu ulimwengu.

Kifupi miezi kadhaa iliyopita nilikutana na huyu binti Beatrice (Fake name), tulianza kama marafiki...baadae tukawa wapenzi.

Kiukweli huyu binti alikuwa wa tofauti sana...na wanawake wengi niliyowahi kuwa nao kabla. Kwanza M/Mungu amemjalia uzuri wa kipekee, she is very beautiful, ni mpole, anampenda Mungu..hamuwezi mkazungumza sentensi tano bila kusikia neno Mungu...ni mtu anaemtegemea Mungu kwenye kila kitu.

Kiukweli niliona kabisa anasifa za kumfanya kuwa mke...tulipendana sana...aliniheshimu na mm nilimheshimu ....muda mwingi nilipokuwa free nilitumia kuwa nae, nilifurahi sana hakika nilijisi mwenye bahati kwa kukutana na mwanamke wa ndoto zangu.

Beatrice, hakuwa na tamaa kama ilivyo kwa wanawake wengine...mara kadhaa nimekuwa nikimpa fedha na zawadi mbali mbali kila nilipokuwa tunakutana lakini alionesha dhahiri hafurahishwi na jambo hilo...kwani akidai hayupo na mimi kwa ajili ya fedha bali ni mapenzi ya dhati na si vinginevyo. Kama atakuwa na shida ya fedha itakayo hitaji msaada wangu ataniambia lakini si vinginevyo.

Hali hii ilinishangaza, ni jambo LA tofauti sana kwa wanawake wengi wa dunia ya leo. Hivyo upendo ukazidi kuwa maradufu na kuona kabisa huyu ndie mwanamke wa maisha yangu.

CHANGAMOTO MPYA.

Jambo ambalo amekuwa akinishangaza huyu binti kila nilipokuwa nikihitaji penzi (sex) hakuwa tayari. Nikimuuliza sababu anasema ni maamuzi aliyojiwekea mpaka niwe mume wake halali ndio tutafanya hilo jambo.
Kuna siku nilimuuliza Kuwa yeye ni bikra? Akasema hapana...amewahi kushiriki hilo tendo mara kadhaa katika mahusiano yake yakiyopita huko nyuma but kwa sasa hayuko tayari. (Jambo hili lilinishangaza na kujiuliza sana why?)

Cha ajabu kila tulipokuwa tunazungumza hizo habari...alikuwa akitokwa na machozi na kuniambia ananipenda sana anaomba niwe mvumilivu hayuko tayari kunipoteza. Kiukweli kama mwanaume jambo hili lilikuwa linanipa wakati mgumu sana, pengine kufikia hatua ya kuanza kuwaza mambo mengi kumuhusu huyu binti.

MTEGO KABAMBE WA KULA TUNDA

Kutokana na tamaa zangu za kimwili ikabidi niandae mtego kabambe ili niweze kula tunda kwa huyu binti mrembo...siku tukapanga kwenda diner sehemu fulani hivi kwamba kuna maongezi muhimu. Tulipofika tukala na kunywa...nikamwomba tuchukue room ila nikampromise siwezi kumfanya chochote kwa Kuwa hayuko tayari. Ilikuwa ngumu lakini baadae alikubali.
Kiukweli niliona hii ndio nafasi adhimu ya mm kupata tunda la huyu bibie, tulipofika chumbani alipovua nguo kwenda bafuni kuoga...ndio alizidi kunishangaza...Ana uzuri wa ajabu..nikajiapiza siwezi kumuacha salama siku hiyo...baada ya kulala kitandani ...mm nikiwa na boksa yeye yupo na pichu tu na kanga moko...nikaanza uchokozi wa hapa na pale. Hakuonesha ushirikiano alijaribu sana kunisihi nisije nikamfanyia kitu ambacho amekikataa nitakuwa nime m dissapoint sana.

Uzalendo ukanishinda nikawa natumia nguvu sasa nili nipate tunda ukizingatia jogoo kashawika haelewi somo.

Mwishoni akakubali kushindwa ila akaniambia kabla sijamfanya chochote kuna jambo anataka kuniambia, nikamwambia bila shaka niko tayari lakini si kukosa penzi lake.

Beatrice, aliniambia ananipenda sana na sio kwamba hajui ni jinsi gani napata shida kutokana na msimamo wake, ila hawezi kufanya hivyo kwani atakuwa ameniingiza kwenye matatizo ambayo hakutamani yanikute kwa kuwa ananipenda sana...zaidi ya ninavyofikiria.

TAARIFA ZA KUSHTUSHA KUTOKA KWA BEATRICE.

Beatrice, akaniomba kuwa mstahimilivu na utulivu kwa atakachoniambia. Nikamwambia sawa. Aliniambia yeye ni muathirika wa V.V.U miaka zaidi ya kumi anaishi na maambuki...hataki kuniambukiza nikaja kukatisha ndoto zangu.
Kiukweli baada taarifa hiyo mwili wote ulikufa ganzi na hamu yote kuniisha..kiukweli sikuamini ninachokisikia. Beatrice aliniomba sana nisimwache ghafla anaweza fanya lolote kujidhuru hajui ataishije bila mm ananipenda sana. Anatamani niendelee kuwa katika maisha yake.

Sasa ndugu zangu...kiukweli nampenda sana huyu binti na sijui kama itakuwa rahisi hivyo kumtoa kwenye moyo wangu. Hivi inawezekana kuishi na mwathirika na ukabaki kuwa salama? Kiukweli nipo kwenye wakati mgumu sana kufanya maamuzi....

Niwaombe radhi kwa mtiririko mbaya ila lengo nikufikisha ujumbe huu. Nawasilisha.
 
Inawezekana mkuu..cha msingi muwaone wataalam wa afya kwa ushauri na mazingatio Ya namna ya kuishi pamoja.

Kama ni kweli,,hongera sana kwa beatrice anaupendo wa ajabu.

Ikitokea imeshindikana kuwa pamoja kama wapenzi,tafadhali usimpige chini ghafla utamsababishia matatizo.

Jiulize ingekuwa ni wewe umepata hayo maambukiza(hatuombei kabisa)ungeweza kumwambia mwanamke ukweli ikiwa tayari matamanio ya kupiga game yako 5g,au ungepiga nae game tena dry ili kuendeleza kisasi kwa aliyekuambukiza?!!

Beatrice anahofu ya Mungu sana haijalishi aliupataje lkni hofu ya Mungu ipo ndani yake
 
Ummenda naye kupima na kujihakikishia kweli ana maambukizi ya virusi vya UKIMWI? Maana isije ikiwa mchezo wa kukunyima tunda.

Ila kama umejihakikishia ana maambukizi siyo sababu ya kumuacha, kama mnapendana bado mnaweza kuishi pamoja na kuchukua tahadhari zote kujikinga na maambukizi. Ngono salama ndiyo njia pekee ya wewe kubaki salama. Tumia kinga, japokuwa ni jambo gumu sana ila imagine kama asingekuambia ulikuwa tayari kutumia kinga au ulikuwa unapiga kavukavu? Kama ungeingia kichwakichwa si bado ungeuvaa tu!

Uwaminifu wake kwako ndio umekuokoa, maamuzi ya mwisho yatatoka kwako, uendelee naye au umuache. Jambo la ujasiri itakuwa ni kuendeleza mahusiano yenu itakuwa ni ngumu kwa siku za mwanzoni ila utazoea na kuona kawaida. Chukua maamuzi magumu, fuata taratibu za kiafya na ngono salama au usiwe risk taker na ukubali kutafuta uelekeo mwingine.
 
Hivi inawezekana kuishi na mwathirika na ukabaki kuwa salama?

Ichi ndo kichwa cha Habari
 
Inawezekana ndiyo..kikubwa kufuata ushauri wa wataalamu wa afya.
 
Sema nayeye ana majaribu,yaani hataki kutoa ua lakini kavua mbele yako kwenda kuoga na akabaki na chupi

Mimi tayari saa hii ningekuwa naandika uzi wa kujisikitikia.
 
Hii story nadhani ilishawahi kuwepo humu kama hivyo japo hii imeeditiwa kidogo....


Naomba chapati mbili mama naniliii
 
Hata kama ni uongo..hii story inafikirisha.
Kuna la kujifunza hapa.
Kujifunza nini boss? Mnatufundisha vijana wenu kumhudumia mtu kwa nguvu, anakataa kujamiiana na anakubali siyo bikra kashajamiiana sana. Hiki ndiyo cha kujifunza?
 
Back
Top Bottom